Adui mwingine wa Bwana wa Mashahidi (a.s.) alikuwa ni Abdullah bin Hani Azdi. Mtu huyu alikuwa ni askari wa jeshi la Hajjaj bin Yusuf. Alikuwa kila mara akisema: "Ninazo sifa nyingi ambazo hakuna yeyote yule aliye nazo. Kwanza, katu, hatujawahi kumsema kwa ubaya Khalifa Abdul Malk ibn Marwan; pili, wanawake wetu wameapa kwamba iwapo Husayn bin Ali atauawa, kila mmoja wao atatoa sadaka ngamia warefu kumi. Hivyo wote wakafanya hivyo (alipouawa Husayn), tatu, hakuna hata mtu mmoja miongoni mwetu ambaye, alipoambiwa kumtukana Abu Turab (Ali a.s.) hakufanya hivyo, na katika kufanya hivyo asiwajumlishe Fatima, Hassan, Husayn nao". (Taarifa hii inatoka kwenye : "Sharh Ibn Abil Hadid, Juzuu 1, ukurasa wa 195). Adui wa Ahlul Bayt (a.s.) wa aina hii na mchochezi dhidi ya Imamu Husayn (a.s.) anathi-bitishwa uaminifu. Tahdhib imeandikwa hivi: ("Abdullah bin Hani Azdi) yu mfuasi mwaminifu wa Hajjaj bin Yusuf Thaqafi; amethibitishwa na 'Ijli kuwa yu mtu mwaminifu na wa kutegemeka".
|