Huyu ndie aliyekuwa amiri jeshi wa majeshi ya Yazid. Baada ya Yazid na Ibn Ziad, yeye anahusika moja kwa moja na matendo maovu mno yaliyotendwa dhidi ya Imamu Husayn (a.s.). Aliviambia vikosi vyake vishuhudie kwamba yeye anamtupia Imamu Husayn (a.s.) mshale wa kwanza. Mwandishi wa kitabu kiitwacho "Tahdhi'b al-Tahdhib" anamwelezea mtu huyu kama ifuatavyo:- "Yeye (Umar Ibn Sa'd) alizipokea Ahadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kutoka kwa baba yake na kutoka kwa Abu Sa'id al-Khudri, masahaba wawili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na mapokezi yake yalitolewa na mwanawe (aliyeitwa) Ibrahim na mjukuu wake aliyeitwa Abu Bakr Ibn Hafs Ibn Hurith, na Yazid Ibn Abi Maryam, na Qatadah, na Zuhri, na Yazid Ibn Habib na wengineo." "Mwana wa mtu huyu aitwaye Ijli amehadithia kwamba alikuwa na kawaida ya kuzihadithia Ahadith alizozipokea kutoka kwa baba yake na watu wengi wamezihadithia Hadithi walizozipokea kutoka kwake na yeye yu "Tabi'i" (Mwanafunzi wa Sahaba) na Thiqah (mwaminifu)". Kwenye kitabu kiitwacho Taqribul Tahdhib imeelezwa hivi:- "Umar Ibn Sa'd Ibn Abi Waqqas wa Madina, mkazi wa mjini Kufah, alikuwa ni Saduq (Mkweli). Lakini watu walimtweza kwa sababu alikuwa amiri jeshi wa jeshi lililomwua Husayn." Kumbuka kwa, hii ni kauli ya Shaikhul Islam wa mawahhabiya, Ibn Hajar. Ifuatayo hapa chini ni orodha ya wale waliozihadithia Ahadith zilizopokewa na 'Umar Ibn Sa'd:
Hawa ndio wale watu watatu ambao Mawahhabiya huwategemea kwa Ahadith zao na huwahesabu kuwa ni mabwana wa uhadithiaji wa Ahadith. Kutokana na hawa watu wote watatu kuyakubali mapokezi ya 'Umar Ibn Sa'd, kunamfanya mtu huyu kuwa msema kweli na mwenye madaraka. Zaidi ya hapo, uthibitisho zaidi unaotolewa ni kwamba Imamu Nasai, Ibn Majah na Bukhari wamezihukumu Ahadithi alizozihadithia. Kwenye hali hii, hakuna umuhimu wowote uwezao kupewa wale watu wa kawaida wanaojificha au yale maneno ya Ibn Mu'in pale aliposema: "Ni vipi mwuaji wa Husayn aweza kuwa mwaminifu?" Kwenye Sharhi yake ya kitabu kiitwacho "Mishkat", Mullah Ali Qari anayehesabiwa kuwa yu miongoni mwa waandishi wakweli juu ya tabia za wapokeaji wa Ahadithi) anafafanua, akisema: "'Umar Ibn Sa'd yeye mwenyewe hakumwua Husayn na inawezekana kwamba kushiriki kwake kwenye jeshi lile kulitokana na ujuzi wake halisi (ijtihad) na inawezekana kutokana na kuteleza au kutenda dhambi? Hivyo basi, iwapo malango ya lawama yanafunguliwa kwa hasira, kwa ajili ya vitu kama hivi, basi wanachuoni watajikuta kwenye mashaka". Kwetiye kitabu kingine kiitwacho "Mizanul-I'tidal" zaidi ya kuyaandika hayo kuwa Umar alishiriki kwenye vita dhidi ya Imamu Husayn (a.s.), aliongezea kusema: "Utu wake ni mwema kiasi cha kutokana kabisa na lawama. Mpokeaji wa Ahadithi (aitwaye) Su'ba (kwa kutokana na mabwana wake) amepokea Ahadithi kutoka kwake na wamefanya vivyo hivyo watu wengineo nao."
|