Huyu alikuwa ni mwana wa nduguye Khalifa Abu Bakr na mwana wa Munafiq (mnafiki) mkuu aliyeitwa Ash'ath bin Qais na ni umbu lake Ju'dah binti Ash'ath mwuuaji wa Imamu Hassan (a.s.). Ibn Ziad alimtuma mtu huyu kwenye kupigana na Hadhrat Muslim bin Aqil, na huko Karbala, aliongoza kikosi cha askari elfu nne. Yeye naye anahesabiwa kuwa yu mpokeaji wa Ahadith, mkweli wa Ahlul Sunnah. Kwenye Tahdhibut Tahdhib anaelezwa hivi: "Muhammad ibn Ash'ath ibn Qais Kindi Abul Qasim alikuwa yu mkazi wa mjini Kufah. Mama yake alikuwa ni umbu lake Abu Bakr Siddiq. Ibn Ash'ath amepokea Ahadith kutoka kwa babayake na 'Umar na 'Uthman na Ibn Mas'ud na Ayisha; na kutoka kwake amezipokea Ahadith hizo mwanawe (aitwaye) Qais na Shu 'bi na Mujahid na Zuhri n.k. Ibn Habban amemwingiza miongoni mwa watu waaminifu. Mwenye Sunnan ya Ibn Dawuud liko moja miongoni mwa mapokezi yake juu ya Abdul Rahman ibn Qais na iko Hadith moja kwenye Sunnan ya Nasa'i izungumziayo juu ya Funga. Abu Zubair Razi ameeleza kwa Ibn Zubair alimpa mtu huyu ugavana wa Mosul". Kwenye kile kitabu kiitwacho Tahdhibut Tahdhib imeelezwa hivi:- "Muhammad ibn Ash'ath ibn Qais Kindi ambaye jina lake la utoto ni Abul Qasim, ni mpokeaji (wa Ahadith) anayekubalika - yeye yumo kwenye kundi la pili (yaani yu miongoni mwa Tabi'in)." Baadae Muhammad Ibn Ash'ath alidai Ukhalifa na Ulama wa Kiwahhabiya wanasema: "Yeye yu miongoni mwa wale ambao watu waliwapa Ukhalifa kwa makubaliano ya pamoja". Ukweli ni kuwa, hata sahaba maarufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Anas ibn Malik alikula kiapo cha utii kwake na akamtii. (Soma kitabu kiitwacho Hayatul Hayawan, Juzuu 2. ukurasa wa 48.)
|