Imam Ali (a.s.) ni; "Ndugu ya Mtume na Wasii wake na Khalifa wake kwa Waislamu wote". Taz: Tarikhut Tabari J.2 Uk. 63 Maana ya "WASII" ni mtu anayesimamia kuendesha mambo ya mtu. Kwa kuwa Ali ni Wasii wa Mtume (s.a.w.) maana yake Ali atasimamia na kuendesha mambo ya Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.). Maana ya 'KHALIFA" ni mtu anayekuja kukaa mahala pa mtu baada yake. Kwa kuwa Ali ni Khalifa wa Mtume (s.a.w.) manna yake Ali atashika mahala pa Mtume (s.a.w.) baada yake. Mtume (s.a.w.) amesema: "Wewe (Ali) nafasi yako uliyonayo kwangu mimi, ni (kama) Haruna (nafasi aliyonayo) kwa Musa, isipokuwa hakuna Utume baada yangu". Taz: Sahih Bukhari Kitabu Maghazy Ujumbe uliomo katika Hadithi hii ni kwamba "Ali ni Haruna wa Muhammad isipokuwa hakuna Utume baada yake. Haruna mbali ya kuwa ni Khalifa wa Musa, lakini pia ni Nabji, hii ndiyo manna ya Hadithi kusema kwamba: "Ali na Haruna ni kwa kila kitu isipokuwa Unabii". Mtume (s.a.w.) amesema, "Mimi ninakuachieni vizito viwili ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea baada yangu, Quran na Ahlul Bait, viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh" Taz: Tafsir Ibn Kathir J.4 Uk. 122 Ahlul Bait ni cha pili katika vitu viwili ambavyo Mtume (s.a.w.) ameacha katika umma huu. lliposemwa: "Viwili hivi havitaachana mpaka vitakaponifikia katika Haudh" Maana yake, Quran na Ahlul Bait viko pamoja na vitakuwa pamoja mpaka siku ya mwisho. Kwa maneno mengine, uongozi wa Ahlul Bait uko sambamba na uongozi wa Quran. Kwa kuwa Ali ni Imam wa kwanza katika AhIul Bait, basi Waislamu kama watashikamana naye (kwa kufuata uongozi wake) hawatapotea baada ya Mtume. |