Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
KUFARIKI KWAKE

Baada ya maisha yenye shughuli namna hiyo kuna uwezekano wa kupatikana wakati wo wote ule kwa ajili ya fitina za kisiasa au lo lote lile lifananalo na hilo? Lakini kuongezeka kwa mvuto wake kwa watu katika mambo ya Kiroho na kuwa kwake chanzo cha Elimu ya Kidini vilikua ndiyo sababu kubwa ya watawala kutaka kuyaondoa maisha yake. Kwa maana dola ya Bani Abbas ingeliweza kusimama iwapo tu, Uislamu wa kweli usingelifahamika; au kwa ujumla hakukuwepo nafasi kwa wafalme wa ukoo huo, na matendo yao yote hayawezi kupata kibali cho chote kile cha raia isipokuwa tu, kama raia hao wakiwekwa gizani kuhusu kuwepo kwa Falsafia yo yote ile ya maisha yaliyo mazuri kuliko yale yanayofuatwa na serikali. Maimamu wa ukoo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) walikuwa ni mifano halisi ya mafundisho ya Mtume (s.a.w.) ambayo yalipinga kabisa desturi za Waarabu, zilizothibitika au yo yote kati ya madhehebu zilizoamini aina yo yote ile ubora wa taifa au yo yote kati ya zana nyingi za kimataifa ambazo hubadilika kila siku kulingana na matakwa ya watawala.

Hivyo, kutaka kuyaondoa maisha ya Imamu lilikuwa jambo muhimu sana kwa kuendeleza maisha ya serikali kama ilivyokuwa kabla hivyo mwishowe walifikiria hivyo.

Imamu alifariki (kwa kupewa sumu na Mu'tamad) mnamo tarehe 8 Rabi-ul-Awwal (Mfunguo Sita) mwaka 260 Hijiriya. Alizikwa huko Samarrah (Iraq) karibu na kaburi la baba yake, ambako, licha ya hali mbaya msikiti wa kaburi hilo bado umesimame, ambao ni moja ya sehemu kadhaa zilizo takatifu kwa watu wote.