 |
NYONGEZA
Mifano ya Maandishi na Hadithi za Imamu (a.s.)
- Jiepushe na kuwa pamoja na mjinga hata kama yu akutakiaye kila Ia kheri na usijiepushe na mtu mwenye hekima hata kama ni adui yako. Kwani mjinga atakuumiza uhitajipo msaada ambapo utu wa mtu mwenye hekima utamzuia kufanya jambo lililo chanzo cha uadui.
- Waraka wake kwa watu wa Qum, Iran: Mwenyezi Mungu aliudhihirisha wema wake kwa viumbe wake kwa kumleta Mtume wake Muhammad (s.a.w.) na ahadi zake na maonyo yake na kakubarikini kwa Rehema zake kwa kukuwezesheni mkubali dini yake ya kweli na kukutukuzeni kwa kukuangazeni na akapanda mbegu ya imani katika mioyo ya wahenga wenu na kuwabariki wale watu miongoni mwenu ambao wanaishi maisha marefu na kawabariki kwa kuwepo kwa Dhuria wa Mtume wake (a.s.) kuwa ndiyo viongozi wao.
Hivyo, wale waifuatao njia ya Haki watafaulu na kufaidi yale matunda waliyochuma kabla.Tunastarehe kwa sababu ya maarifa yenu mazuri na uhusiano wetu ni wa kuaminika. Shikaneni na amri zile ambazo wahenga wetu waliwapa vijana wenu na muwe na uhakika na zile ambazo vijana wetu waliwaahidi baba zenu. Mwenyezi Mungu awabarikini nyote.
- Barua yake kwa Bwana Ibn Babawaihi Qummi: Ewe Hasan bin Ali bin Husain bin Babawaihi Al-Qummi, kuwa mvumilivu ili kungojea nyakati nzuri. Marafiki zetu wataendelea kuwepo kila wakati katika hali hii ya hatari mpaka aje mwanangu ambaye Mtukufu Mtume wa Mungu (s.a.w.) alimbashiri kuwa ataijaza dunia kwa haki na usawa kama vile ambavyo ingelijaa mateso na dhuluma.
Hivyo, Ewe Sheikh, muwe wavumilivu wewe mwenyewe na wale marafiki zetu wote. Mwenyezi Mungu humpa hii dunia yake ye yote yule amuonaye kuwa anafaa katika viumbe wake. Na hakika mwishilizo mwema utakuwa na wale wamchao Mwenyezi Mungu. Amani ya Mwenyezi Mungu na Baraka zake na ziwe juu yako na juu ya marafiki zetu. Neema Zake na ziwe juu ya Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) na Dhuria wake (a.s.).
|