Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
KULELEWA KWAKE

Alikaa na baba yake kwa muda usio pungua miaka kumi na moja katika sehemu ya kwao. Muda huu unaweza kuitwa muda wa amani. Baada ya hapo ilimbidi Ali Naqi (a.s.) aende Iraq na Imamu Hasan Askari (a.s.) alifika Samarrah na baba yake baada ya taabu zote za safari ndefu. Huko aliishi na baba yake jela chini ya uchunguzi na wakati mwingine aliishi katika uhuru kidogo. Lakini kila wakati aliishi na baba yake akijifunza kwa makini tabia yake katika hali za kila aina ambayo, pamoja na Mwanga alioupewa na Mwenyezi Mungu, alikuwa kamili kabisa kwa kazi ambazo alitazamiwa kuzishika.