Mu'tazz Billah Abbasi alikuwa Mfalme wakati Imamu Hasan Askari (a.s.) alipopata Uimamu. Baada ya Mu'tazz kupinduliwa, Muhtadi alitawala kwa muda wa miezi kumi na moja na siku chache naye alirithiwa na Mu'tamad. Hakuna hata mmoja wa hao Wafalme aliyemwacha Imamu (a.s.) akae kwa amani. lngawaje Serikali ya ukoo wa Bani Abbas ilikuwa katika machafuko, licha ya matatizo hayo yote wote waliona afadhali kumwacha Imamu (a.s.) abaki humo jela. Sababu muhimu ilikuwa ni ile hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) ibashiriyo kuwa atafuatiwa na Maimamu kumi na wawili, wa mwisho wao akiwa ni Mahdi Akhirul Zaman (Imamu wa Zama hizi) na Qaim-i-Al-i Muhammad (endelezo la Ukoo wa Mtukufu Mtume s.a.w.). Hadithi hii ilienea kote katika ulimwengu wa Kiislamu. Watawala wa ukoo wa Bani Abbas walijua sana kuwa hao ndiyo makhalifa halali wa Mtukufu Mtume (s.a.w.) na katika hao Imamu Hasan Askari (a.s.) alikuwa wa kumi na moja, kwa hiyo mwanawe atakuwa ni kutimia kwa ubashiri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.). Kwa hiyo kila wakati walikuwa wakizuia kuwepo kwa Khalifa wake. Ndiyo maana hawakuacha kumchunguza Imamu Hasan Askari (a.s.) kama ilivyokuwa kwa baba yake, hivyo waliona kuwa ni lazima kumfungia katika jela ya peke yake. Lilikuwa jambo tofauti kabisa wakati mapinduzi ya kisiasa yameacha pengo katika nyakati za ufungwa wake, Iakini kila Mtawala aliyetawala alifuata shauri la watawala wa kabla yake la kumfunga Imamu tena. Hivyo karibuni muda wake mfupi wote wa Uimamu aliumalizia jela. Kuchungwa kwake kulifikia kilele wakati wa utawala wa Mu'tamad, ingawaje naye, kama wale wengine wa nyuma wote, alikijua vizuri cheo cha Imamu (a.s.). Kwani, wakati mmoja njaa iliingia nchini na mtawa mmoja wa Kikristo alidai kuwa anaweza kufanya mvua inyeshe na alifaulu kufanya hivyo. Hivyo kulikuwepo mlegolego katika imani ya Waislamu. Mu'tamad alihofia kuwa serikali yake itaangushwa hivyo aIimwita Imamu Hasan Askari (a.s.) kutoka jela. Imamu (a.s.) alimwomba mfalme amruhusu mtawa huyo kuja hadharani na kufanya muujiza wake mbele ya Imamu mwenyewe na alimtuma mtu fulani amwendee haraka yule mtawa wakati alipoinua mikono yake kuomba mvua na kuchukua cho chote kile alichokuwa nacho mikononi mwake. Wakati mambo haya yanafanika yule mtawa alionekana akionyesha mfupa kwenye jua na mvua zilianza kunyesha. Imamu alimwambia kuwa mfupa ule ulitoka katika mwili wa Mtume fulani na kwamba ilikuwa ni tabia ya mifupa va Mitume kuwa kama inaonyeshwa kwenye jua, mawingu yatatanda. Kisha Imamu aliufunika ule mfupa na yeye mwenyewe aliomba mvua inyeshe na ikanyesha kwa wingi sana.
|