Israa ni: Mwendo wa usiku, kama ilivyokuja katika Qur'an: "Utukufu ni wa yeye ambaye alimpeleka Mja wake usiku, kutoka Msikiti mtukufu (wa Makka) mpaka Msikiti wa mbali (Falastin) ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake, ili tumuonyeshe baadhi ya ishaara zetu" 17:1 Miiraji ni: Msafara ulioanzia katika Msikiti wa Falastin kwenda juu. Tukio la Israa limepokewa na waandishi wa Tarikh kwa njia tofauti, kuna wanaosema kuwa Israa ilitokea mwaka wa kumi na mbili baada ya kupewa Utume, Wengine wanasema ilikuwa mwaka wa kumi na moja, wengine mwaka wa kumi, wengine mwaka wa tano, wengine mwaka wa tatu na wengine mwaka wa pili. Taz: Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 108 Tarikhul Khamisi J. 1 Uk. 307 Assahihu Minsiiratin Nabi J. 1 Uk. 269 Kauli ya sawa katika mjadala huu ni: Israa imetokea katika mwaka wa tatu kwa sababu zifuatazo"
Taz: Tarikh Bughdad J. 5 Uk. 87 Mizanul'itidal J. 2 Uk. 297 Mustadrakul Hakim J. 3 Uk. 156 Majmauz Zawaid J. 9 Uk. 202 Kanzul Ummal J. 14 Uk. 97 Dhakhaairul U'qbaa Uk. 36 Katika hadithi hii tunajifunza kuwa: Mwana Fatima (a.s.) amezaliwa mwaka wa tano baada ya Biitha (kupewa Utume) kwa hiyo, Israa na Miiraji ilikuwa kabla ya kuzaliwa Mwana Fatima, kwa sababu Mwana Fatima ni Tunda la peponi alilokula Mtume siku aliyopelekwa Miiraji. Tunda lililobaki mgongoni kwake hata baada ya miaka miwili akazaliwa Fatima, Bibi bora kabisa katika mabibi wa Peponi - Hadithi. Taz: Assahihu Minsiiratin Nabii J. 1 Uk. 274 Usudul Ghaba J. 4 Uk. 18 Ikiwa Israa na Miiraji imetokea kabla ya kusilimu Abubakr, basi madai ya Laqabu isemwayo kuwa alipata Abubakri ya "SIDDIQ" yanatupwa: Kwa sababu ikiwa laqabu hiyo (kama inavyodaiwa) alupata baada ya kusadikisha msafara wa Mtume (s.a.w.) aliopelekwa katika Israa na Miiraji. Litawezekanaje hilo, ilihali wakati wa tukio la Israa na Miiraji Abubakri alikuwa kafiri! Hapo tasdiq itapatikana?!
|