Amesema Bukhari na Muslim na wengineo kuwa: Imepokewa kutoka kwa Azzuhry naye amepokea kwa U'rwa bin Zubeir naye amepokea kwa Mwana Aisha (mkewe Mtume) kwamba: Malaika Jibril (a.s) alikuja kwa Mtume (s.a.w.) naye akiwa katika pango la Hiraa akamwambia: Soma, Mtume akajibu: Mimi sijui kusoma. Mtume anasema: Malaika akanikaba kwa nguvu mpaka nikazidiwa kisha akaniambia: Soma, Mtume akajibu: Mimi sijui kusoma. Kisha ndipo Malaika alipomsisitiza kwa nguvu akisema: "Soma kwa jina la Mola wako, ambaye ameumba. Amemuumba mwanadamu kutokana na damu iliyoganda. Soma na Mola wako ni Mtukufu kuliko wote". Qur'an, 96:1-3 Baada ya hapo, Mtume (s.a.w.) alirudi kwa mkewe mwana Khadija (a.s.) akiwa amejawa khofu kubwa. Alipoingia ndani alijitupa chini na huku akilalamika: "Nifunikeni, nifunikeni!!" Alipotulia akasema: "Ninaogopa sijui kitanipata nini?!" Khadija akamtuliza: "Sivyo! Wallahi Mwenyeezi Mungu hatakuangamiza abadani, wewe unaunga udugu, unavumilia matatizo, unasaidia wanyonge, unasaidia kuleta haki." Hapo Khadija akamchukua Mtume akampeleka kwa Ibnu ammi yake Waraqa bin Nawfal (alikuwa mnasara, mwandishi wa Injili kwa lugha ya kiibrania). Walipofika kwa Waraqa, Khadija akamwambia: "Ewe Ibnu ammi! Msikilize Muhammad aliyo nayo." Waraqa akamuuliza, "una nini?" Muhammad akamwelezea yote kama aliyoyaona, Waraqa akamwambia: "Huyu ni Malaika ambaye amepata kumteremkia vilevile Nabii Musa (a.s.) Ee!!!" Natamani kama nitakuwa hai wakati watakapokufukuza watu wako!!! Muhammad (s.a.w) akashituka: "Watanifukuza??" Waraqa akajibu: "Ndiyo, hakuna mtu yeyote anayeleta jambo kama hili uliloleta wewe isipokuwa atapigwa vita na watu wake". Taz: Sahihi Bukhari J.I uk, 5-6 Sahihi Muslim J. I uk, 97 Almuswannaf J. 5 uk, 322 Tarikhut Tabari J. 2 uk, 47 Madda hii (mwanzo wa Wahy) waandishi wameieleza kwa njia nyingi tofauti zenye kugongana. Hapa tutajaribu kuzitaja chache tu:
"Ninasikia ninaitwa nyuma yangu, ewe Muhammad ewe Muhammad, nikisikia hivyo mimi hukimbia ovyo." Waraqa akamkataza asiwe anakimbia bali akaze roho ili ayasikie anayoambiwa..." Muhammad alishika maelekezo hayo, mara aliposikia akiitwa: Ewe Muhammad! Sema, Bismillahir Rahmanir Rahim, Alhamdulillahi rabbil a'lamina.... mpaka mwisho wa suratul Fatiha. Akaambiwa: Sema: "Laa ilaha illallahu" Muhammad (s.a.w.) baada ya hapo alikwenda kwa Waraqa bin Nawfal, akamjulisha hali hiyo. Waraqa akambashiria habari njema yakuwa: "Hali kama hiyo alipewa pia Nabii Isa bin Maryam". Taz; Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 9 Assiratun Nabawiyya J. 1 uk 83 Assiratul Halabiyya J. 1 uk 250 Siiratu Mughlataya uk, 15 Taz: Albidayatu Wannihaya J.3 uk, 12 Siiratu Ibn Hisham J. 1 uk, 238 Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 239. Taz: Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 252. Taz: Tarikhul Yaa'quby J. 2 Uk. 23. Taz: Tarikhul Khamisi J. 1 Uk. 284 Assiratul Halabiyya J. 1 Uk. 243 Assiratun Nabawiyya J. 1. Uk. 83 Taz: Almuswannaf J. 5 Uk. 323
Taz: Albidayatu Wannihaya J. 3 Uk. 13.
|