Taz: Kashful Ghumma J. 2 Uk. 63 Riwaya nyingine zinasema kuwa:
Taz: Suratul Aimmatil Ithna Ashar J. 1 Uk 452 Abdur Rahman bin Muljam alikutana na msichana mmoja katika khawariji aitwaye Qatwam, ambaye baba yake na kaka yake waliuliwa na Imam Ali katika vita vya Nahrwan. Msichana huyo alikuwa mzuri kupita kiasi, Abdur Rahman alipomtaka Qatwam, alimjibu: "Kama utaweza kunipoza moyo wangu utanipata" Akamuuliza: "Ni lipi litakalo kupoza moyo wako?" Akajibu: "Unipe dirham alfu tatu, mtumishi mmoja, mjakazi, mwimbaji, na umuue Ali bin Abi Talib. Abdur Rahman bin Muljam akasema: "Hayo mengine yote ni mepesi sana, lakini hili la kumuua Ali, ni dalili ya kuwa umenikataa. Kwa sababu haiwezekani kumuua Ali nami nikasalimika, tukaweza kuoana". Ilipofika siku hiyo, kwa kauli zilivyo khitilafiana, kama ulivyoona hapo juu, Abdur Rahman bin Muljam akatimiza lengo lake. Imam Ali amezikwa Kufa katika nchi ya Iraq. Taz: Kashful Ghumma J. 2 Uk. 62 Tabaqatul Kubra J. 6 Uk. 12 Tadhkiratul Khawas Uk. 179
Mu'awiya alipotaka kumtawalisha mwanawe Yazid, alitumia mbinu, akamjenga Juuda bint Al'ash'a'th bin Qays. Huyu alikuwa mke wa Imam Hasan (a.s.). Muawiya akampa sumu ili amtilie Imam Hasan. Na endapo atamuua, basi atamfanyia mambo mawili, la kwanza atampa dirham laki moja na la pili atamuoza mwanawe, Yazidi. Imam Hasan akapewa sumu hiyo na baada ya hapo alibaki siku arobainni akafariki dunia! Amekufa mfungo tano mwaka 50 Hijra. Taz: Kashful Ghumma J. 2 Uk. 207 Tadhkiratul Khawas Uk. 211 Wengine wanasema: Amekufa mfungo sita mwaka 49 Hijra. Taz: Tadhkiratul Khawas Uk. 211 Baada ya kufa Imam Hasan Juu'da alipeleka ujumbe kwa Yazidi wa kutaka kuolewa naye kama walivyoahidiana na baba yake Mu'awiya, Yazidi aliruka na kusema: "Hukuweza kumhurumia Hasan utanihurumia mimi!!? Kama umeweza kumuua yeye mimi utanimaliza mara moja, Yazid akakataa kumuoa. Taz: Dhakhairul Uq'baa Uk. 146. Imepokewa kwa mama Ummu Salama (mkewe Mtume) anasema: "Nilimuona Mtume (s.a.w.) akikipangusa kichwa cha Imam Husein na huku akilia. Nikamuuliza: "Unalilia nini!" Akasema: "Hivi sasa amenijulisha Malaika Jibril kuwa: Mtoto wangu huyu atauliwa katika ardhi litwayo "KARBALA" kisha akanipa gao la udongo na akaniambia: 'Huu udongo ndipo mahala atakapouliwa, utunze, siku yoyote utakapogeuka kuwa mwekundu basi jua yakwamba amekwisha uliwa". Taz: Dhakhairul' U'qbaa Uk. 147 Albidayatu J. 3 Uk. 174 Albidayatu Wannihaya J. 6 Uk. 230 Tarikhul Islam J. 3 Uk. 10 Almustadrak J. 3 Uk. 176 Kama ambavyo, siku aliyouliwa Imam Husein mbingu zilimlilia, na alama ya kuonyesha kuwa zinamlilia ni wekundu unao onekana kwenye mawingu. Kwa hiyo, Imam Husein (a.s.) analiliwa na mbingu mpaka leo hii. Taz: Tafsirul Qurtubi J. 16 Uk. 14
Taz: Siiratul' Aimmatil Ithna Ashar J. 2 Uk. 225 Taz: Tadhkiratul Khawas Uk. 350.
Kifo cha Imam Ali bin Musa kimetokana na maji ya matunda yenye sumu aliyopewa na Maamun. Baada ya kunywa Imam alibaki siku mbili kisha akafariki dunia, mwaka 203 wengine wanasema mwaka 202 na wengine wanasema mwaka 206. Taz: Siiratul' Aimmatil' Ithna Ashar J. 2 Uk. 341
Taz: Siiratul' Aimmatil' Ithna Ashar J.2 Uk. 448.
Hawa ni Maimam kumi na wawili katika AhIul Bayt (a.s.) walio pamoja na Qur'an. Amesema Mtume (s.a.w.) "Dini itaendelea kuwa imara mpaka isimame kiama, na mtasimamiwa na viongozi kumi na wawili, wote katika Maquraishi". Taz: Sahihi Muslim J. 6 Uk. 3-4 Sahihi Bukhari J. 4 Uk. 165 Sunan Abi Daud J. 3 Uk. 106 Musnad Ahmad J. 5 Uk. 86-90 Kanzul Ummal J. 13 Uk. 26-27 Hilyatul Awliyaa J. 4 Uk. 333 Na ameonya Mtume (s.a.w.) kwa yeyote ambaye hatawatambua Maimam hawa: "Yeyote atakaekufa na asimjue Imam wa zama zake, atakufa kifo cha kipagani". Taz: Sharhul Maqasid J. 2 Uk. 275 Al'mirqat J. 2 Uk. 509 Al'ghaadir J. 10 Uk. 260
|