Kwa kweli tukitaka kuijadili mada hii kwa undani zaidi, itatulazimu tutumie muda mrefu katika kuchambua kifungu kimoja baada ya kingine. Na hilo litahitaji kuchukua nafasi ya kitabu kizima ili kujaribu kutatua utata huo. Lakini, kama wasemavyo wataalamu: "Maa Laa yudraku kulluhu laa yutraku kulluhu" yaani, "Yasiyowe za kupatikana yote, hayaachwi yote". Kwa hiyo nasi hatutaacha kutaja japo kidogo:
Imepokewa kutoka kwa Az Zuhry kutoka kwa U'rwa bin Zubeir kutoka kwa Mwana Aisha. Sasa: hapa tutaangalia mambo ya fuatayo:
Taz: Qamusir Rijal J. 6 Uk. 300 Algharat J. 2 Uk. 558-560 Na Mtume (s.a.w.) amesema juu ya Imam Ali (a.s.) kuwa: "Yeyote mwenye kumtukana Ali basi amenitukana mimi na mwenye kunitukana mimi amemtukana Mwenyezi Mungu". Taz: Mustadrakul Hakim J. 3 Uk. 121 Musnad Ahmad J. 5 Uk. 30 Alfusulul Muhimma Uk. 111 Tarikh Ibn Asakir J. 2 Uk. 184 Manaqibu Ali Uk. 394 Kwa hiyo, mtu mwenye kumtukana Mtume (s.a.w.) hawezi kuwa mwema hata kidogo, licha ya kupokea mafunzo ya dini kutoka kwake. Kitendo cha mke wa Mtume cha kutoka nyumbani mwake kwenda nje, ni jambo lililokatazwa na Mwenyeezi Mungu: "Na kaeni majumbani mwenu" 33:33 Mwana Aisha ameipuuza hukumu hii! Aidha, kitendo cha kumpiga Imam Ali (a.s.) ni jambo linalomuweka mtu mahala pabaya. Imepokewa kutoka kwa A'diyyi bin Thabiti kutoka kwa Zuhry amesema: "Amesema Imam Ali kuwa: "Ninaapa kwa ambaye ameumba mbegu na akaumba upepo, hiyo ni ahadi ya Mtume kwangu mimi kuwa: Hanipendi mimi isipokuwa mu'umin na hanibughudhi (hanichukii) mimi isipokuwa mnafiki". Taz: Sahihi-Muslim katika kitabul Iman Sahihit Tirmidhi J. 2 Uk. 301 Musnad Ahmad J. 1 Uk. 84 Tarikh Bughdad J. 2 Uk. 255 Hilyatul Awliyaa J. 4 Uk. 185 Kanzul Ummal J. 6 Uk. 394 Mustadrakul Hakim J. 3 uk 129 Al Istiab J. 2 Uk. 214 Addurrul ManthurAya ya 25 sura 47. Mwana Aisha ameipuuza hukumu hii! Nanikweli Mwana Aisha hampendi kabisa Imam Ali (a.s.). Hilo linathibitishwa na hali halisi, kwanza, amepigana na Imam Ali (a.s.) na kupiga hakuanzi kabla ya kuchukia. Na alipopata habari Mwana Aisha kuwa Imam Ali ameuliwa, alisujudu kumshukuru Mwenyeezi Mungu!!! Taz: Magatilut Talibina Uk. 27 Aljamal Uk. 83-84 Mwenyeezi Mungu anasema: "Haiwi kwa mwanamume aliyeamini, Mwenyeezi Mungu na Mtume wake wanapohukumu jambo wawe na hiari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyeezi Mungu na Mtume wake, hakika amepotea upotovu ulio wazi" 33:36.
Taz: Sahihi Bukhari J. 1 Uk. 152 Sahihi Muslim J. 7 Uk. 100. Musnad Ahmad J. 2 Uk. 315 Almuswannaf J. 11 Uk. 274 Sunannun Nasai J. 4 Uk. 118 Albidayatu Wannihaya J. 1 Uk. 317 Tarikhut Tabari J. 1 Uk. 305. Haiwezekani kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.) alikuwa mwoga hivyo, na Nabii Musa tu peke yake awe shujaa wa kuwang'oa macho malaika!!
"Waambie (Muhammad) roho takatifu ameiteremsha kutoka kwa Mola wako kwa haki, ili kuwaimarisha wale walio amini, na kuwa muongozo na habari njema kwa waliosilimu." 16:102 katika aya hizi timachunguza ibara isemayo: "ILU TUKUIMARISHE KWAYO MOYO WAKO". Kwa hiyo, moyo wa Muhammad uliimarishwa na Mwenyeezi Mungu sikiliza Mwenyeezi Mungu analifafanua hili: "Waambie (Muhammad) hakika mimi ninayo dalili ya wazi itokayo kwa Mola wangu" 6: 57 "Waambie (Muhammad) Hii ndiyo njia yangu, ninaita kwa ujuzi hasa, mimi na wanaonifuata." 12:108 Katika Aya hizi tunaangalia maneno: "MIMI NINAYO DALILI YA WAZI ITOKAYO KWA MOLA WANGU" "NINAITA KWA UJUZI HASA" kwahiyo, Mtume Muhammad (s.a.w.) anajua kuwa anayo dalili (ushahidi) ulio wazi, na kwa ajili hiyo, anawaita watu kwa ujuzi kamili. Hii si sawa na kusema: Muhammad (s.a.w.) uliimarishwa moyo wake na mnasara (Waraqa bin Nawfal).
|