Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
KUONEKANA KWA MWENYEEZI MUNGU

Suala la kuonekana Mwenyeezi Mungu, Waislaamu wamegawanyika makundi mawili, kuna wanaosema kuwa: Mwenyeezi Mungu anonekana hapa duniani na huko akhera. Na kuna wanaosema kuwa: Mwenyeezi Mungu haonekani hapa duniani wala huko akhera. Kila kundi lina hoja zake. Wasemao ataonekana wanategemea hoja mbili: Dalilul a'qly, Dalilun naqly.

  1. Dalilul a'qly - Kwa kupitia mantiq akili inaona kuwa: kwa kuwa chochote chenye kuwapo lazima uwiano wa kuonekana uwepo.
  2. Dalilun naqly: Mwenyeezi Mungu anasema:

  1. Na alipofika Musa kwenye miadi yetu, na akazungumza na Mola wake akasema: "Mola wangu! Nionyeshe ili nikuone." Akasema "Huwezi kuniona, lakini tazama jabali, kama litakaa mahala pake ndipo utaweza kuniona" 7:143
  2. "Nyuso siku hiyo zitang'aa zikitazama kwa Mola wao" 75: 22-23