Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
TABIA YAKE ADHIMU

Imamu Muhammad Taqi [a] alikuwa ni mmoja wa watu wa ukoo wa Mtume [s] na aIikuwa na tabia nzuri kama za wale wengine wa ukoo huo. Kumfanyia kila mtu upole, kutosheleza mahitaji ya kila mhitaji, kuweka maisha rahisi na usawa kuwa ni mambo muhimu zaidi, kuwasaidia maskini kwa siri, kuwatendea mema hata maadui, ukarimu mkubwa na kila wakati kuwakarihisha wale wapendao kujifunza vilikuwa sifa kubwa ziIizomtofautisha lmamu Taqi [a].

Watawala wa koo za Bani Umayya na Bani Abbas hawakuwa na jambo Ia kufanya juu ya mtu wa ukoo wa Mtume [s] maana kwa sifa zao hizo walionyesha tofauti kubwa (iliopo kati yao na watu wengine) na kuonyesha ubaya wa watawala na majeshi yao.

Kwa hiyo kila mara walijaribu kuivuruga senta ya Kidini ya Madina na jaribio la Yazid kumfanya Imamu Husain [a] awe upande wake jambo ambalo baadaye lilisababisha masaibu ya Karbala au tukichukua mfano mwingine, Mamun kumteua Imamu Ridha [a] kuwa mrithi wake wa kiti cha Ufalme kulikuwa ni njia tofauti ya kudhihirishia msimamo wao ule ule wa siku zote. Wakati fulani nguvu za uovu zilijitokeza kuushambulia UkweIi na mara nyingine walijaribu kuvishinda 'vipingamizi' kwa kumwua lmamu Ridha kwa sumu.

Sasa Mamun aIifikiria kuwa wakati huo ulifaa kwa kumgeuza mawazo mtoto mdogo mwenye umri wa miaka minane au tisa ambaye ametengwa na baba yake miaka mitatu iliyopita na hivyo hatari iliyokuwepo kila mara kwa utawala wa Bani Abbas itaondolewa.

Mamun hakukuchukulia kushindwa kwake Imamu Ridha [a] kuwa iwe ndicho chanzo cha kukata tamaa kwake. Alifikiria kuwa haikuwa lazima kuwa ikiwa Imamu Ridha [a] hakuweza kushawishika (kwa sabahu alikwisha kuwa na tabia za kiutu uzima) mwanawe asingeliweza kufikiriwa kuwa si wa kumtumainia.

Lakini Mamun na watu wote wale ambao macho yao hayakuweza kuuona ukweli wa mambo, walistajaabu kuona kuwa mkwewe Mfalme wa ukoo wa Bani Abbas mwenye umri wa miaka tisa alikataa kukaa katika jumba la kifalme. Walimuona anashikilia kuendelea na tabia ya watu wa ukoo wake na walishangaa kuona kuwa alipokwenda Baghdad alikodisha nyumba ya kuishi badaIa ya kuishi katika majumba ya kifalme. Si hivyo tu, bali baada ya muda mfupi tu alikataa kuishi mjini Baghdad na kabla ya mwaka mmoja kwisha baada ya ndoa yake na binti wa mfalme, ilimbidi mfalme atengane na binti wake na kumruhusu aondoke na mumewe ambaye ilibidi matakwa yake yatiliwe na huyo mfalme mkuu na tena aliye baba mpenzi.

Huko Madina, Imamu [a] alirudia maisha yake ya zamani. Wakati wake mwingi aliutumia katika msikiti wa Mtukufu Mtume [s] ambamo wanafunzi wa Hadithi za Mtume [s] na Elimu ya dini walikwenda na kukuta kiti cha Imamu Ja'far al-Sadiq [a] kikiwa kimekaliwa tena na kiu yao ya kujifunza ikazimishwa.

Katika maisha yake ya faragha alikuwa na kawaida hiyo hiyo. Alimwekea mkewe Bibi UmmuI Fazl (bintiye Mamun) amri hizo hizo katika maisha yake kama alizowawekea wakeze wengine; baadaye kidogo alimwoa mwanamke mmoja tajiri wa ukoo wa Bwana Ammar bin Yasir (Mwenyezi Mungu na aiweke roho yake mahali pema Peponi) ambaye baadaye alikuwa mama wa lmamu Ali Naqi [a]. Ummul Fazl alimuandikia baba yake akimlalamikia juu ya jambo hilo. Hakika Mamun alikasirishwa sana kusikia hivyo lakini ilimbidi ajikaze. Kwa hiyo alimjibu akisema, 'sikukuoza kwa Abu Ja'far ili nimzuie asifanye yale aliyoyaamrisha Mwenyezi Mungu. Usinilalamikie juu ya mambo kama hayo tena.

Jibu hili lilikuwa la kusawazisha mambo hasa. La sivyo, pamekwishakutokea mifano ambayo kuwapo mwanamke bora (kufuatana na imani) kuliweza kuzuia kufanyika kwa ndoa ya pili. Mtume [s] hakuoa mke mwingine wakati wa uhai wa Bibi Khadija na wakati wa uhai wa Bibi Fatimah [a], Hadhrat Ali [a] pia hakuoa mke wa pili. Sasa Imamu Muhammad Taqi [a] aliona kuwa kwa vile Bibi Ummul Fazl akiwa binti wa Mfalme, alihitaji kutendewa tofauti na wake wengine. Imamu [a] alitaka kumuonyesha Bibi huyu kuwa mwenendo wa Uislamu haukutaka kuendekeza jambo hilo.