Hotuba zake zilikuwa zinapendeza sana. Wakati mmoja wa Hija huko Makka alitoa hotuba juu ya amri za Dini kwa namna nzuri mno kiasi ambacho wanachuoni wakuu waliokuwepo walishangaa na walikubali kuwa walikuwa hawajapata kusikia hotuba nzuri kama hiyo. Wakati wa Imamu Ali [a] ilizuka madhehebu mpya ambayo ilikomesheza Uimamu kwa Imamu Musa Kadhim [a] na hawakuamini Uimamu wa Imamu Ali Ridha [a]. Madhehebu haya yalijulikana kwa jina Ia "Wazifiyyah". lmamu Muhammad Taqi [a] alifaulu vizuri kuhubiria dhidi ya imani yao kiasi ambacho karibu kila mmoja wao alikubaliana naye na karibu wale wote walioifuata madhehebu hayo waliyotoka. Idadi kubwa ya wanavyuoni wakawa wanafunzi wake. Kama alivyoacha mhenga wake Hadhrat Ali [a], Imamu Taqi [a] nae ameacha idadi kubwa ya Hadithi za kuaminika na zinazojulikana sana. Pia ameacha hotuba fulani nzuri sana.
|