Katika mwaka wa 218 Hijiriya mfalme Mamun alifariki na nduguye Mu'tamin alirithi kiti cha ufalme akitumia jina Ia Mu'tasim Billah. Mara moja barua za malalamiko ambazo Bibi Ummul Fazl alimuandikia baba yake sasa zilianza tena kummiminikia baba yake hakuzitia maanani barua hizo kwa kuwa mwenyewe alimuozesha kwa Imamu [a] ingawa watu wa ukoo wa Bani Abbas walipinga, sasa huyu baba mdogo alianza kuzisikiliza. Wakati wa ndugu yake Mamun, Mu'tamin aliwahi kukiwakilisha kikundi kilichopinga kuozwa kwa binti wa nduguye, Bibi Ummul Fazl kwa Imamu [a]. Zaidi ya hayo, alikuwa akiiogopa na kuihesabu sifa ya Imamu [a] ya uongozi wa dini kuwa si isiyokuwa na haki, chanzo cha hatari kwa utawala wake kama vile baba zake walivyofanya wakati wa enzi zao. Kwa hiyo mnamo mwaka wa pili wa utawala wake alimwagiza Imamu [a] aende kwake na alimwandikia barua Gavana wa Madina, aitwaye Abdul Malik kuhusu jambo hiIo. Hivyo Imamu [a] alimuacha mkewe, mama yake Imamu Ali Naqi [a] akae na Abdul Malik na yeye akaondoka kwenda Baghdad.
|