Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
KUFARIKI KWAKE

Kwa muda wa mwaka mmoja hivi baada ya kwenda Baghdad Imamu [a] hakusumbuliwa na Mu'tasim isipokuwa maisha ya Baghdad yalikuwa ya namna ya kifungo". Halafu silaha ile ile ya zamani (yaani ya kuuwa kwa sumu) ilitumika kwake na akapewa sumu akafa mnamo tarehe 22 Dhul-Qa'dah mwaka 220 Hijiriya. Alizikwa karibu na kaburi la Imamu Musa Kadhim [a]. Na mahali hapo pakajulikana kwa jina Ia Kadhimain (mji wa Kadhim wawili) na sasa kituo hicho kinaitwa Jawadain (mahali pa Jawad). Kimoja kati ya vyeo vya Imamu Muhammad Taqi [a] ni "Jawad".