 |
MASAYYIDI WA UKOO WA RIDHAWI
Masayyidi (Masharifu) ambao wanajulikana kwa jina la Ridhawi wote wametokana na kizazi cha Imamu Muhammad Taqi [a] na wangekuwa wameitwa Taqawi kama pangekuwepo mfuatano wa ukoo wa Imamu Ridha [a] zaidi ya kupitia kwa Imamu Muhammad Taqi [a] ambao ungejulikana kwa jina Ia Ridhawi kwa kutofautishwa na wale wa ukoo waTaqawi. Lakini kizazi cha Imamu Ali Ridha [a] ni kile tu kilichotokana na lmamu Muhammad Taqi [a] na kwa kuwa Imamu Ali Ridha [a] alijulikana sana katika ulimwengu wa Kiislamu kwa sababu ya kuteuliwa kwake kuwa mrithi wa mfalme Mamun wa kiti cha ufalme, kizazi cha Imamu Muhammad Taqi [a] chote kiliitwa Ridhawi badala ya Taqawi.
|