Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
MAELEZO MACHACHE KUHUSU KABURI LA KADHIMAIN

Mtu yeyote anayeukaribia mji wa Baghdad kutokea upande wa Kaskazini au Magharibi atapendezwa kuona minara minne ya dhahabu katika mji wa Kadhimain, Kuba la Kadhim wawili ambao ni Maimamu Musa bin Ja'far [a] na Muhammad Taqi [a]. Kwenye lango kubwa lenye umbo la nusu mduara, kwenye ukuta unaolizunguka Kuba hilo pametundikwa mikufu mikubwa ambayo inaonyesha kwamba sehemu ile ni Takatifu.

Jengo la sasa lilijengwa mnamo mwanzoni mwa karne ya kumi na sita (ya zama za Ukristo), na limekuwa likitarizwa kwa nakshi nzuri nzuri.

Jengo hili linakumbusha kujengwa kwake na Shah Isma'ili wa kwanza (tangu mwaka 1502 hadi 1524 Masihiya), ingawaje sultani wa Kituruki, Suleiman Mkuu aliyeuteka mji wa Baghdad na akakaa humo kwa muda wa miezi minne katika mwaka wa 1534 Masihiya alikwenda sehemu takatifu za Mashia na inasemekana aliyatia nakshi zaidi yale Makuba ya Kadhimain. Hata hivyo, vigae vya zege, viliwekwa mnamo mwaka 1796 Masihiya na Shah Muhammad Khan aliyekuwa Mfalme wa kwanza wa ukoo wa Qachar. Mnamo mwaka 1870 Masihiya, mfalme Nasiruddin Shah Qachar aliviweka hivi vigae vya dhahabu katika Kuba moja na kwenye minara. Ni jambo la kufurahisha kuona kwamba tarehe zote za mabadiliko hayo zimeandikwa waziwazi. (Soma Kitabu cha maarifa yote kiitwacho "Encyclopaedia of Islam", chini ya kichwa cha habari "Kadhimain".

Hivyo ni wazi kwamba kuna miaka mia saba ya historia ya Kuba hili, kabla ya muda wa kutengenezwa kwa sasa kulikofanywa na Shah Ismail wa Kwanza. Maimamu wawili waliishi katika siku za awali za mji wa Baghdad ambapo kuta za Mji wa Mviringo wa mfalme Mansur katika upande wa Magharibi wa mto Tigris zilipokuwa bado zimesimama. Palikuwa na sehemu ya makaburi upande wa Kaskazini na Kaskazini ya magharibi zilizokuwa na majina kadhaa; likiwemo lile la Lango la Shamu, Ukoo wa Bani Abbas na lile la Lango la Majani Makavu, (Soma kitabu kiitwacho 'Tabaqat' cha Bwana Ibn Saad).

Maimamu hao wawili walizikwa karibu sana na kaburi la mwisho la upande wa Magharibi lakini wakati Bwana Ya'qubi, alipoandika kitabu chake cha Historia, sehemu yote ya Kaskazini ilikuwa imetengwa kwa ajili ya makaburi ya Maquraishi (Soma kitabu kiitwacho 'Tarikh') cha Bwana Yaqubi.