Jina lake lilikuwa Muhammad, 'Kunyat' (jina Ia utoto) ni Abu Ja'far, na majina yake ya heshima ni Taqi (Muadilifu) na Jawad (Mkarimu), hivyo aliitwa Imamu Muhammad Taqi. Kama vile Imamu Muhammad Baqir [a] alivyojulikana kabla yake kwa jina la Abu Ja'far, yeye naye anajulikana katika vitabu kwa jina la Abu Ja'far wa pili. Pia anajulikana kwa jina la "Hadhrat Jawad". Baha yake alikuwa Imamu Ali Ridha [a] na mama yake alikuwa Bibi Sakinah Khatun.
|