Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
KULELEWA KWAKE

Ilimbidi Imamu Muhammad Taqi [a] ajitayarishe mapema kuzikabili shida. Alikuwa na umri wa miaka mitano tu baba yake alipoondoka Madina kwenda Khurasan (Iran); na hakumwona tena baba yake maishani mwake kwani alifariki miaka mitatu baada ya kumwacha mwanawe huko Madina. Labda ulimwengu ulifikiria kuwa huenda nafsi ya Imamu Ja'far Sadiq [a] ingebakia wazi kwa vile Imamu kijana alikuwa bado hajaelimishwa ipasavyo. Lakini ulimwengu ulishangazwa kumwona mtoto mdogo, mara baadaye, akijadiliana na wanavyuoni wakuu wa siku zile katika baraza Ia Mfalme Mamun na wakaukubali ubora wake.

Mshangao wao ulikuwa kitu cha kutegemewa maana hawakuamini kuweko kwa elimu ya Kimungu.