Wakati Mfalme Mamun alipotangaza kuwa amemteua Imamu Ali Ridha [a] kuwa mrithi wake (wa kiti cha Ufalme) aliona ulazima wa kuwepo uhusiano bora na watu wa ukoo wa Bani Fatimah badala ya watu wa ukoo wa Bani Abbas; hivyo, kwa kujipendekeza kwa Mashia, alidhania kuwa itakuwa ni busara kuanzisha uhusiano mpya na watu wa ukoo wa Bani Fatimah, badala ya ule wa kiwahenga wa watu wa ukoo wa Bani Abbas na Bani Fatimah kuwa wote ni Bani Hashim. Kwa hiyo katika hadhara hiyo hiyo alipotangaza kuwa yeye anamteua Imamu Ali Ridha kuwa atakuwa mrithi wake (wa kiti cha Ufalme) alimuozesha dada yake kwa Imamu Ali Ridha [a] na akatangaza ndoa kati ya binti wake na Imamu Muhammad Taqi [a]. Labda alifikiria kuwa kwa kufanya hivyo angeweza kumshawishi Imamu Ali Ridha [a] kumuunga mkono. Lakini baada ya muda mfupi tu aliona kuwa Imamu [a] alithamini zaidi ujumbe wa Uislamu na kazi yake ya Uongozi wa Dini, na kuwa hakubali jambo jingine liingilie Sheria. Kwa hiyo aliyaona maisha yale mapya ya Imamu [a] akiwa jamaa ya mtawala huyo na wakati huo huo akichukua uzito wa kazi ya kuuhubiri Uislamu wa Kweli kuwa ni ya hatari kwa dola na utawala wake wa kijanja kuliko Madina. Kwa hiyo alimuuwa kwa kumpa sumu. Lakini sababu zilizomfanya amtangaze Imamu [a] kuwa ndiye mrithi wake wa baadaye bado zilikuwepo na bado anahitaji kuungwa mkono na Mashia na Mairani. Hivyo wakati alipojionyesha kuwa alikuwa na huzuni sana kwa kifo cha lmamu Ali Ridha [a] ili asijulikane kuwa alihusika na kifo hicho, ilimbidi pia aendelee na tangazo lake Ia kufunga ndoa kati ya binti wake na Imamu Muhammad Taqi [a]. Hivyo alimtaka Imamu Muhammad Taqi [a] kwenda Iraq kwa kuwa yeye pia alikwishahamia kwenye makao makuu ya zamani, Baghdad, akiwa na makusudio ya kuwaoza haraka.
|