Ahmad ibn Mufaddal alitokana na watukufu wa Kishi'a na alikuwa ni mtu wa kusadikiwa na kuaminiwa. Dhahabi vile vile amemwelezea katika Mizan na kumpatia vifupisho vya jina lake. Abu Dawud na Nasa'i vile vile wamechukua riwaya kutokea kwake katika vitabu vyao vya Sahih kwa kupitia Al-Thawri naye ameripoti riwaya kutoka kwa Asbat ibn Nasr na Isra'il.
|