Subject Index 
Search
Announcements
Feedback
UAMUZI WA HISTORIA

Wanahistoria waadilifu wa Kiislamu na Wakikristo wote kwa pamoja wanakubaliana kuwa ndoa alizosifunga Mtume wa Islamu [s] hazikusababishwa na tamaa ya kuitosheleza ashiki yake. Kama ingekuwa hivyo, basi hangemuona mwanamke aliyekuwa mjane mara mbili, aitwae Khadija, mwenye umri ya miaka 40 na yeye Mtume wa Islamu [s] akiwa kijana wa umri wa miaka 25 tu, umri ambao mtu huwa katika kiwango kamili cha ashiki.

Mtume Muhammad [s] aliishi na mke wake wa kwanza (ambaye wakati ule alikuwa mkewe peke yake), Bibi Khadija [a] kwa furaha, kwa mapenzi na uelewano mkubwa, kwa muda wa miaka 26 ingawaje wasichana wazuri wa Uarabuni waliweza kupatikana kwa urahisi na walikuwa tayari kuolewana na Mtume [s]. Munda wote huo (wa miaka 26) Mtume [s] hakuoa mke mwingine. Bila shaka Mtume [s] angelifikiria kuoa mke mwingine aliye na umri mdogo kuliko ule wa Bibi Khadija [a] wakati alipokuwa na Bibi Khadija [a], kama angelikuwa mwenye tamaa za kiashiki na mpenda wanawake; nasa wakati ule ambapo desturi za nchi yake zilikubaliana na ndoa za wanawake wengi.