Aya 27– 40: Wa Kuume
Maana
Na wa kuume; je, ni yapi ya wa kuume?
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutaja karama na neema aliyowaandalia waliotangulia, sasa anataja aliyowaandalia wale walio chini yao kuume. Amewaita wa kuume, kwa vile watapewa vitabu vyao kwa mikono yao ya kuume, kama ilivyotangulia kuelezwa. Hili lifutalo ndilo fungu lao katika Pepo.
Katika mikunazi isiyo na miba, na migomba iliyopangiliwa; yaani ndizi zilizopandana Na kivuli kilichotanda kisichokuwa na muda. Na maji yanayomiminika bila ya kukatika. Na matunda mengi kwa idadi na aina.
Hayakatiki wala hayakatazwi,
Miti ya duniani inazaa kwa msimu na mtunda yanakuwa ni ya mwenye mti tu, akimpa anayemtaka. Lakini miti ya Akhera matunda yake ni ya kudumu na yanatumiwa na kila mtu.
Na matandiko yaliyonyanyuliwa.
Yaani vitanda vya juu. Ajabu ni kauli ya mfasiri mmoja aliyesema urefu wa kitanda kwenda juu ni masafa ya miaka mia tano.
Hakika Sisi tumewaumba Mahurulaini upya, Na tutawafanya bikira wanaopenda waume zao, walio marika.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewaandalia watu wa kuume wanawake bikra, wanaowapenda waume zao na wote wakiwa na umri mmoja.
Mfasiri mmoja amekadiria umri wao kuwa miaka 33. na kimo cha dhiraa sitini kwa dhiraa saba; sawa na alivyokuwa Adam, kulingana na kauli yake mfasiri huyo.
Lengo la kuashiria haya ni kutanabahisha kuwa baadhi ya tafsiri haifai kuzitegemea, kwa sababu ni kusema bila ya ujuzi.
Kwa ajili ya watu wa kuume.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekariri kwa kiasi cha kusisitiza kwamba aliyoyataja ni ya watu wa kuume.
Fungu kubwa katika wa mwanzo na fungu kubwa katika wa mwisho.
Maneno yanaanza tena, kwamba watu wa kuumeni kuna waliokuwa katika zama zilizotangulia na wengine wa zama zitakazokuja; nao kwa kawaida watakuwa ni wachache kuliko watu wa kushoto:
وَقَلِيلٌ مِنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ {13}
وَأَصْحَابُ الشِّمَالِ مَا أَصْحَابُ الشِّمَالِ {41}
فِي سَمُومٍ وَحَمِيمٍ {42}
وَظِلٍّ مِنْ يَحْمُومٍ {43}
لَا بَارِدٍ وَلَا كَرِيمٍ {44}
إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُتْرَفِينَ {45}
وَكَانُوا يُصِرُّونَ عَلَى الْحِنْثِ الْعَظِيمِ {46}
وَكَانُوا يَقُولُونَ أَئِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ {47}
أَوَآبَاؤُنَا الْأَوَّلُونَ {48}
قُلْ إِنَّ الْأَوَّلِينَ وَالْآخِرِينَ {49}
لَمَجْمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَاتِ يَوْمٍ مَعْلُومٍ {50}
ثُمَّ إِنَّكُمْ أَيُّهَا الضَّالُّونَ الْمُكَذِّبُونَ {51}
لَآكِلُونَ مِنْ شَجَرٍ مِنْ زَقُّومٍ {52}
فَمَالِئُونَ مِنْهَا الْبُطُونَ {53}
فَشَارِبُونَ عَلَيْهِ مِنَ الْحَمِيمِ {54}
فَشَارِبُونَ شُرْبَ الْهِيمِ {55}
هَٰذَا نُزُلُهُمْ يَوْمَ الدِّينِ {56}