Sura Hamsini Na Nne: Al-Qamar
Imeshuka Makka. Ina Aya 55.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi Mwenye kurehemu.
اقْتَرَبَتِ السَّاعَةُ وَانْشَقَّ الْقَمَرُ {1}
Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!
وَإِنْ يَرَوْا آيَةً يُعْرِضُوا وَيَقُولُوا سِحْرٌ مُسْتَمِرٌّ {2}
Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Uchawi unaoendelea.
وَكَذَّبُوا وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ ۚ وَكُلُّ أَمْرٍ مُسْتَقِرٌّ {3}
Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo lina wakati maalum.
وَلَقَدْ جَاءَهُمْ مِنَ الْأَنْبَاءِ مَا فِيهِ مُزْدَجَرٌ {4}
Na bila ya shaka zimewajia habari zenye makaripio.
حِكْمَةٌ بَالِغَةٌ ۖ فَمَا تُغْنِ النُّذُرُ {5}
Hikima kamili, lakini maonyo hayafai.
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ ۘ يَوْمَ يَدْعُ الدَّاعِ إِلَىٰ شَيْءٍ نُكُرٍ {6}
Basi jiepushe nao. Siku atakapoita mwitaji kuliendea jambo linalochusha.
خُشَّعًا أَبْصَارُهُمْ يَخْرُجُونَ مِنَ الْأَجْدَاثِ كَأَنَّهُمْ جَرَادٌ مُنْتَشِرٌ {7}
Macho yao yatainama; watatoka makaburini, kama kwamba wao ni nzige waliotawanyika.
مُهْطِعِينَ إِلَى الدَّاعِ ۖ يَقُولُ الْكَافِرُونَ هَٰذَا يَوْمٌ عَسِرٌ {8}
Wanamkimbilia mwitaji; makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu