Sura Ya Hamsini Na Tatu: An-Najm
Imeshuka Makka. Ina Aya 62.
بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.
وَالنَّجْمِ إِذَا هَوَىٰ {1}
Naapa kwa nyota inapoanguka,
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمْ وَمَا غَوَىٰ {2}
Mwenzenu hakupotea, wala hakukosea.
وَمَا يَنْطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ {3}
Wala hatamki kwa matamanio.
إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ {4}
Hayakuwa haya ila ni wahyi uliotolewa;
عَلَّمَهُ شَدِيدُ الْقُوَىٰ {5}
Amemfundisha mwenye nguvu sana,
ذُو مِرَّةٍ فَاسْتَوَىٰ {6}
Mwenye umbo la sura, akatulia,
وَهُوَ بِالْأُفُقِ الْأَعْلَىٰ {7}
Naye yuko upeo wa juu kabisa.
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ {8}
Kisha akakaribia na akateremka.
فَكَانَ قَابَ قَوْسَيْنِ أَوْ أَدْنَىٰ {9}
Akawa umbali wa pinde mbili, au karibu zaidi.
فَأَوْحَىٰ إِلَىٰ عَبْدِهِ مَا أَوْحَىٰ {10}
Akampa wahyi mja wake alichompa wahyi.
مَا كَذَبَ الْفُؤَادُ مَا رَأَىٰ {11}
Moyo haukusema uwongo uliyoyaona.
أَفَتُمَارُونَهُ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ {12}
Je, mnabishana naye juu ya aliyoyaona?
وَلَقَدْ رَآهُ نَزْلَةً أُخْرَىٰ {13}
Na alimuona mara nyingine,
عِنْدَ سِدْرَةِ الْمُنْتَهَىٰ {14}
Penye Mkunazi wa mwisho.
عِنْدَهَا جَنَّةُ الْمَأْوَىٰ {15}
Karibu yake pana Bustani ya makazi.
إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ {16}
Kilipoufunika huo Mkunazi kilichoufunuika.
مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ {17}
Jicho halikuhangaika wala halikupetuka mpaka.
لَقَدْ رَأَىٰ مِنْ آيَاتِ رَبِّهِ الْكُبْرَىٰ {18}
Hakika aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake.