Visa Vya Kweli

Sehemu Ya Kwanza
Author(s): 
Publisher(s): 

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Anecdotes. Sisi tumekiita, Visa vya Kweli. Kitabu hiki kime- andikwa na Sayyid Ali Akbar Sadaaqat. Kitabu cha Visa vya Kweli kimekusanya simulizi za visa vya kweli vilivyosimuliwa katika Qur’aniTukufu, hadithi na riwaya na vyanzo vingine sahihi. Kwa kweli, visa hivi hufundisha maadili mema kwa wanadamu, hivyo, kitabu hiki tunaweza kukiita kuwa ni cha maadili kwa kuwa visa vilivyoelezewa humu ni vya kimaadili.

Translator(s): 
Category: 
Topic Tags: 
Person Tags: 

Neno La Awali

Dhana ya maadili imekuepo toka alipoumbwa mwadamu. Siku za zamani, kulikuwa na tofauti ya wazi kati ya maadili “mema” na maadili “mabaya” ingawa si mara zote watu walikuwa wakifuata maadili mema. Katika zama za sasa, tofauti kati ya maadili mema na mabaya imefifia na kwa kiasi kikubwa maadili yametibuliwa. Na matokeo yake, kuna hatari kwamba ufisadi utakuwa wa nguvu kuliko maadili duniani kote.

Hakuna kisingizio kwa Mwislaamu kunasa katika hali hii mbaya na ya hatari. Kuna mwongozo uliowazi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kupitia Qur’ani tukufu na Mitume na Ma’sumin. Mtume Muhammad (s.a.w.w.) mwenyewe alisema, “Nimetumwa kama Mtume kwa lengo la kuyakamil- isha maadili.” Moja ya njia bora kabisa za kuyaelewa maadili ni kwa kusoma mifano halisi kutoka katika maisha ya Mitume na Ma’sumin, amani iwe juu yao wote.

Vitabu vichache vimeshaandikwa juu ya hadithi za maadili kutoka katika ulimwengu wa kiislamu, kimojawapo kikiwa “Pearls of Wisdom” (Lulu za Hikma), kilichochapishwa na Islamic Education Board of World Federation, machi mwaka 1993. Kwa kuzingatia umuhimu wa mada ya Akhlaq, Bodi ya elimu ya kiislamu ya World Federation inachapisha “Visa vya kweli kwa ajili ya kutafakari katika sehemu tano. Chanzo cha chapisho hili ni kitabu “Yaksad Mawzu wa 500 Dastani” cha Sayydi Ali Akber Sadaaqat. Tarjuma ya kutoka kifarsi kwenda Kiingereza ilifanywa na Sheikh Shahnawaz Mahdavi. Bodi ya Elimu ya Kiislamu World Federation ingependa kuwashukuru Sayyid Ali Akbar Sadaaqat na Sheikh Shahnawaz Mahdavi kwa jitihada zao na inawaombea kwa Mwenyezi Mungu awalipe vya kutosha.

(Tunaomba) Mwenyezi Mungu aikubali kazi hii kama jitihada nyingine ya Bodi ya elimu ya Kiislamu ya World Federation ya kueneza Uislamu.

Bodi ya Elimu ya Kiislamu
The World Federation of Muslimu Communities
Sha’aban 1424
Oktoba 2003.

Utangulizi

Kuna njia nyingi kwa ajili ya mwanadamu kupata mwongozo na kuibuka kutoka kwenye giza na kuelekea kwenye nuru. Kwa ajili ya ustawi wa mwanadamu na ukamilifu wa maadili yake, Mwenyezi Mungu ameumba uthibitisho, ushahidi na dalili1, katika idadi kubwa kiasi kwamba ziko nje ya uwezo wa kuhesabiwa na kukokotolewa. Kwa ajili ya mwongozo wa mwanadamu alituma mitume na dalili zilizo wazi,2 vitabu, miujiza na ishara ili pengine watu wanaweza kuitambua njia iliyonyooka na kupata ustawi na mafanikio.

Katika kipindi chote cha utume wake, Mtukufu Mtume (saw), katika suala la utakatifu wa kiroho na ukamilifu wa maadili, alikuwa ni kiigizo katika kauli na matendo, na hata alisema: “Nimetumwa (kama Mtume) kwa (kusudio la) kuyakamilisha maadili.3

Tatizo la mwanadamu lipo katika kutozingatia kwake amali njema, kuten- da kwake maovu, kupupia matamanio na utii kwa shetani. Baadhi ya watu wamejiachia (katika kufanya maovu) kiasi kwamba wanaendesha maisha yao kama wanyama. Kwa lengo la utakatifu na kuyaponya madili ya wanadamu, kupunguza kasi na kudhibiti hulka ya asili, Mtukufu Mtume alifanya kila aliloliweza na alitaja yote yaliyopaswa juu ya jambo hili.

Kupata fanaka katika ulimwengu huu na ulimwengu ujao (Akhera) kunawezekana tu chini ya uangalizi wa mwalimu na wakati huo huo si kila mtu anaweza kubainisha nukta mbili za mwisho (yaani maadili bora kabisa na duni kabisa) ili kuonyesha kwa vitendo njia ya kati na iliyo sawa. Yule mwenye Hikma isiyo na kikomo aliwaleta mitume wote na hususani Mtukufu Mtume (saw) kama “mwalimu na mkufunzi” wa maadili, ili kwa kufuata nyayo zake, watu wajitenge na maovu na wapate heshima ya duni- ani na Akhera.

Katika Qur’ani, kuna sura iitwayo Al-Qasas (masimulizi), ambayo yenyewe tu ni ushahidi kuwa mwanadamu anahitaji hadithi na masimulizi.

Katika sehemu nyingi ndani ya Qur’ani, hadithi za mitume wafalme wa mataifa zimetajwa. Kwa kuongezea Mwenyezi Mungu amezungumzia masuala yanayohusiana na vita, amani, familia, dini, jamii na mada nyinginezo, katika muundo wa hadithi na masimulizi. Kwa kuvisoma visa hivi, watu wanaweza kuelewa na kutofautisha kati ya njia ya maendeleo na ile ya kuporomoka kwa maendeleo, na kupanda na kushuka katika kila kipengele, hususani maadili.

Suratul Yusuf yote imetumika kusimulia kisa cha Yusuf, Yaqub, Zulekha na nduguze. Mwanzoni mwa sura Mwenyezi Mungu anasema:

“Tunakusimulia (Ewe Mtume) masimulizi bora kabisa kwa (kupitia) yale tuliyokufunulia katika Qur’ani hii. (Suratul Yusuf; 12:13)

Ambapo katika aya ya mwisho sura hii, anasema katika historia yao

“kwa hakika kuna mazingatio kwa watu wenye akili.” (Suratul Yusuf 12: 111).

Kwa hakika moja ya ustadi mkubwa kabisa wa Qur’ani ni hadithi hii ya Yusuf (as) iliyotajwa kuwa ni “simulizi bora kabisa” na mwisho (Qur’ani) inase- ma: “katika hadithi hizi kuna mazingatio kwa wale wanaotaka kuadilika na kufuata njia ya watu watimilifu.

Juu ya hili Amirul Muuminina (as) katika Nahjul Balaghah, anamuambia mwanawe Imam Hasan (as): “Ingawa sijafikia umri ule uliofikiwa na wa kabla yangu, nimezitazama tabia zao na nimetafakari matukio ya maisha yao.

Nilitembea katika maanguko yao mpaka nikawa miongoni mwao. Kwa kweli, kwa wema wa mambo yao niliyo (bahatika) kujua, ni kama nimeishi nao mwanzo hadi mwisho.

Hivyo nimeweza kubaini kilicho kichafu na kisafi na chenye manufa na chenye madhara.

Nimekuchagulia bora kabisa ya mambo hayo na nimekukusanyia nukta nzuri huku nikiyaacha yale yasiyo kuwa na manufaa.”

Miaka kadhaa huko nyuma, nilikuwa nimeandika kitabu juu ya maadili (kwa ajili ya kutibu maovu), kwa jina la Ihyaul Qubul. Tokea wakati huo, nilikuwa nikitafakari juu ya kuandika kitabu, juu ya hadithi za maadili. Hivyo ilitokea kwamba, kwa bahati ya Mungu, fursa ilinijia pamoja na hamasa ya kufanya kazi hii. Licha ya ukosefu wa vitabu muhimu, nili- tosheka na vile vilivyokuwepo na nikaanza kuandika kitabu hiki, nikiandi- ka hadithi nne mpaka tano kwa kila mada.

Kwa kweli sijakutana na kitabu chochote kilichoandikwa kwa mtindo huu. Vitabu kama Namunah-e-Maarif Islam na Pand-e-Taarikh vimekuwepo kwa takribani miaka 30 na nimevitumia pia (katika kuandaa mkusanyiko huu) lakini katika vitabu hivyo aya za Qur’ani, Hadithi, mashairi na ulin- ganishi, vyote vimekusanywa pamoja, ambapo mimi nimetosheka kwa kutaja hadithi tu huku nikiepuka kutoa maelezo yanayohusiana na aya za Qur’ani, hadithi, mashairi na ulinganishaji, (vitu ambavyo) visingeongeza tu ukubwa wa kitabu, bali pia vingeleta ugumu wa kueleweka kwa waso- maji wengi. Mkusanyiko huu ni kwa ajili ya umma kwa ujumla, watoto na wakubwa pia, ambao wana elimu ya msingi ya kusoma na kuandika. Kwa kadri nilivyoweza nimejitahidi kukwepa masuala ya kisayansi na vipen- gele vile vinavyohusiana na hadith ambavyo kueleweka kwake kungehita- ji uangalifu mkubwa na kulazimisha kwa jumla kwa ajili ya umma.

Ingawa baadhi ya visa vinawezekana visiwe na vipengele vyovyote vya uhalisi na uhakika, nilichokizingatia ni kunasihi na “kuchukua somo” la kipengele kilichomo humo, ambacho ninataraji wasomaji watukufu watafahamu na kuelewa.

Kadiri suala la kuhusisha kisa na mada mahususi linavyohusika, sisemi kwamba visa vinavyodokeza kwenye mada moja tu au ile mahususi ambayo imetajwa hapa; bali ni visa ambavyo vinaweza kuhusishwa na mada nyingine pia, kwa nyongeza kwenye mada ambayo chini yake imeta- jwa hapa.

Wakati kikisimulia maandishi au nikifanya tarjuma, sikujibana katika maana halisi, bali kwa utambuzi mzuri zaidi, nimeishia kwenye ufafanuzi wa maneno, kudokeza na maelezo yenye maana pia.

Ili kuepuka kuingiliana kwa mada na kurefusha mjadala, nimeepuka kule- ta mada zinazohusiana na zile ambazo tayari zimeshawasilishwa. Kwa mfano, Ithaar (tabia ya kufikiria wengine kuliko nafsi yako mwenyewe) imewasilishwa kama moja ya mada, lakini Infaaq (kutoa katika njia ya Allah) imeachwa.

Ili kuzuia msomaji asipatwe na uchovu na uchoshi, na kwa ajili ya sababu mbali mbali, nimeacha kuwasilisha visa vya kukinaisha, kama vile za wanafalsafa na washairi, lakini nimejitahidi kufanya mkusanyiko uwe tofauti tofauti. Kwa njia hii nataraji wasomaji watafurahia zaidi masimulizi haya.

Kwa kuzingatia ukweli kwamba uaminifu lazima uzingatiwe, nimetaja kila simulizi iliyowasilishwa hapa, kutoka kwenye kitabu, juzuu gani, na ukurasa gani imechukuliwa. Ni kwa ajili ya kupata mtiririko mzuri zaidi wa kazi kwamba nimejitahidi kusahihisha, kunakshi au kubadilisha baadhi ya maneno au sentensi za maandishi ya asili.

Inatarajiwa kutoka kwa wasomaji kwamba, baada ya kuvipitia visa na simulizi hizi, watatafakari na kuchukua mazingatio ili waweze kujijengea nguvu za kwenda katika ukamilifu wa madili, na Allah swt. akipenda wale waliojaaliwa maadili yenye kusifika wawasimulie wengine, kwa ajili ya kuzirekebisha roho dhaifu zaidi.

Na dua yetu ya mwisho (ni) Sifa zote njema zinamstahiki Allah swt, Mola wa walimwengu.

Said Ali Akbar Sadaaqat
Mordad, 1378 (July 1999)

 • 1. Qur’ani Tukufu, Sura Ibrahim – 14: 5
 • 2. Ibid, Suratul Hadiid 57:25
 • 3. Safinah al-Bihar, Juz 1,uk 411

Neno la Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Anecdotes. Sisi tumekiita, Visa vya Kweli. Kitabu hiki kime- andikwa na Sayyid Ali Akbar Sadaaqat.

Kitabu cha Visa vya Kweli kimekusanya simulizi za visa vya kweli vilivyosimuliwa katika Qur’aniTukufu, hadithi na riwaya na vyanzo vingine sahihi. Kwa kweli, visa hivi hufundisha maadili mema kwa wanadamu, hivyo, kitabu hiki tunaweza kukiita kuwa ni cha maadili kwa kuwa visa vilivyoelezewa humu ni vya kimaadili.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu ambapo kuna mmomonyoko mkubwa wa maadili. Kitabu hiki kitawafaa sana vijana walioko mashuleni na vyuoni, halikadhalika watu wa wazima.

Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kwa lugha ya Kiswahili kwa malengo yaleyale ya kuwahudumia wasomaji wetu wazungumzao Kiswahili ili wapate kuongeza elimu yao ya dini na ya kijamii kwa ujumla.

Tunawashukuru ndugu zetu, Dr. M. S. Kanju na Mwl. Aziz Njozi kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake.

Mchapishaji:
Al-Itrah Foundation
S. L. P. 1970
Dar-es-Salaam,
Tanzania.

1) Maadili

Allah Mwenye hikma Anasema:

“Na hakika wewe una tabia tukufu.” (Suratul Qalam: 4)

Mtukufu Mtume (saw) alisema: “Nimetumwa (kama mtume) ili kuja kukamilisha maadili.”

(Jaame Al Saadaat, Juz, 1. Uk. 23)

Maelezo mafupi:

Kwa mwanadamu, maadili huleta heri na fahari katika ulimwengu huu na wepesi huko Akhera. Kunyanyua hadhi ya mtu katika ukaribu wake na Mwenyezi Mungu na humsaidia katika ukamilifu wa dini yake, Mitume wote, mawalii na wateule wa Mwenyezi Mungu walikuwa na maadili ya kupigiwa mfano, na kila mu’umini anapaswa kujipamba kwa maadili hayo, ili mizani ya amali iwe nzito zaidi Siku ya Hukumu.

Mtukufu Mtume (saw) amesema: “Hatima ya muda wetu ni moja, kwa yule mwenye maadili mazuri. Maadili mabaya humfanya mtu ataabike kwa kubanwa mbavu kaburini na (adhabu ya) moto wa jahannam (huko akhera) na ukosefu wa marafiki katika ulimwengu huu.”

Mtu hapaswi kupimwa kwa mujibu wa maarifa yake, utajiri au cheo, bali kwa mujibu wa tabia zenye kusifika, zinazomfanya akubalike mbele ya macho ya Allah na kwa kuwa mtukufu na msifiwa mbele ya macho ya watu. (Taz: Tadhkirah al-Haqaaiq, uk. 57)

1. Mtukufu Mtume (Saw) Na Nua’imaan

Nua’imaan Ibn Amr Ansaari alikuwa ni mmoja wa masahaba wa mwanzo wa Mtukufu Mtume (saw) na alikuwa na maumbile ya uchangamfu na ukarimu.

Imesimuliwa kuwa siku moja Bedui mmoja aliwasili Madina na akampunzisha ngamia wake nyuma ya Msikiti (kisha) akaingia ndani ili awe kwenye hadhira ya Mtukufu Mtume (saw)

Baadhi ya masahaba wa Mtume walimshawishi Nua’imaan kwa kusema “Ikiwa utamuua ngamia huyu, tutagawana nyama yake miongoni mwetu, na Mtukufu Mtume (saw) atalipa bei yake kwa mmiliki.”

Kwa kufuata ushauri wao Nua’imaan alimuua mnyama yule. Mmiliki alipotoka nje ya msikiti na kukuta ngamia wake amekufa alikasirika sana na akaamua kulileta jambo hili mbele ya Mtukufu Mtume (saw). Nua’imaan wakati huo alikuwa amekwishakimbia.

Mtukufu Mtume (saw) alitoka nje ya msikiti, akamuona ngamia aliyekufa na kuuliza “Ni nani anayewajibika kwa kitendo hiki? Wale waliokuwepo walimtuhumu Nua’imaan, hivyo Mtukufu Mtume (saw) akamtuma mtu kwenda kumleta Nua’imaan mbele yake. Habari zilivuma kuwa Nua’imaan alikuwa amejificha katika nyumba ya Dhubaa’h Bint Zubeir1 ambayo ilikuwa karibu na msikiti. Alikuwa ameingia kwenye shimo kisha akajifunika na majani mabichi. Mtukufu Mtume (saw) alielezwa juu ya maficho ya Nua’imaan na yeye na masahaba zake wakaelekea kwenye nyumba ya Dhubaa’h walipofika hapo, mjumbe aliomuonyesha Mtume (saw) maficho ya Nua’imaan ambaye Mtume (saw) alimuamuru (mjumbe) alifungue shimo. Baada ya kufanyika hilo, Nua’imaan aliibuka huku mashavu na kipaji chake cha uso vikiwa vimefunikwa na majani mabichi.

Alipomuona, Mtukufu Mtume (saw) alimuuliza “Ewe Nua’imaan! Ni nini hiki ulichokifanya?

Aljibu, “Ewe Mtume wa Allah (Naapa) kwa Allah! hao watu waliokuleta kwenye maficho yangu, ndio hao hao walionishawishi nimuue ngamia!”

Mtukufu Mtume (saw) alitabasamu na kufuta majani kutoka kwenye mashavu na kipaji cha uso cha Nua’imaan kwa mikono yake mitakatifu. Kisha akalipa gharama ya ngamia kwa yule Bedui kwa niaba ya Nua’imaan.2

2. Khuzaima Na Mfalme Wa Urumi

Khuzaima Abrashi mfalme wa Arabuni, kamwe hakufanya kazi yoyote kubwa bila kwanza kutaka ushauri kutoka kwa mfalme wa Rumi ambaye alikuwa ni rafiki yake wa karibu. Wakati fulani, alikuwa na nia ya kupata maoni ya Mfalme (wa Urumi) juu ya heri ya wanawe, alimtumia barua kupitia mjumbe wake, katika barua aliandika:

“Nahisi ninapaswa kutenga utajiri mkubwa kwa kila mwanangu wa kiume na wa kike ili wasije wakataabika baada yangu. Ni nini maoni yako juu ya jambo hili?”

Mfalme wa Urumi Akajibu: “Utajiri ni kishawishi, hauna uaminifu na haudumu! Kitu bora kwa watoto wako itakuwa ni kuwapamba kwa maadili mema na tabia zenye kusifika, ambazo zitawapeleka kwenye uongozi wa kudumu katika ulimwengu huu na msamaha (wa dhambi) huko Akhera.3

3. Mwendo Wa Imam Sajjad (As)

Wakati fulani, ndugu wa Imam Sajjad (as) alimuendea Imam (as) na akaan- za kumkashifu na kumtukana. Imam (as) hakutamka neno lolote kumjibu lakini, baada ya yule mtu kuondoka kwenye mkusanyiko ule, aliwageukia watu waliokuwepo na kusema:

“Mmesikia aliyosema mtu huyu, sasa ninataka muambatane na mimi mkasikie kile nitakachosema kujibu kashfa na matusi yake”

Masahaba wakakubali, “kwa hakika tutaambatana nawe, kwa kusema kweli tulitaraji kuwa ungemjibu wakati ule ule”

Imam (as) aliondoka kuelekea kwenye nyumba ya mtu huyo na alisikika akisoma aya ya Qur’ani ifuatayo:

وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ {134}

“Na ambao wanazuia hasira (zao) na wanasamehe (makosa ya) watu; kwani Allah anawapenda wale wafanyao wema (kwa wengine) (Quran 3: 134)

Msimuliaji anasema: “Tuliposikia kisomo cha aya hii, tulijua kwamba Imam (as) alikusudia kuonyesha wema kwa mtu ambaye punde tu alikuwa amemtukana”

Alipofika kwenye nyumba ya mtu huyo, Imam (as) alimuita na akamjulisha kuwasili kwake. Alipomuona Imam, yule mtu akajua kuwa amekuja kujibu kashfa zake.

Lakini, mara tu Imam (as) alipomuona yule mtu, alisema, “Ewe ndugu (yangu)! Ulikuja kwangu na kusema vitu vya kutisha na visivyopendeza.

Ikiwa uliyoyasema juu yangu ni ya kweli, (basi) ninaomba msamaha kwa Allah, lakini ikwa sio, basi ninamuomba Allah ‘Azza wa Jallah akusame- he.” Yule mtu alishtushwa kusikia maneno haya na akatubu. Alimbusu Imam (as) baina ya macho na akaomba msamaha, akisema:

“Matusi yangu na kashfa hayakuwa na msingi na hayawezi yakahusishwa na tabia yako. Kwa kweli matusi yale yananistahili mimi zaidi kuliko wewe.”4

4. Ali (As) Na Mfanyabiashara Asiye Na Heshima

Imam Ali (as) wakati wa ukhalifa wake, mara nyingi alikuwa akitembelea masoko na kuwashauri na kuwaongoza wafanya biashara. Siku moja, alipokuwa akipita katika soko la tende, alimuona msichana mdogo akilia, Imam aliuliza sababu ya machozi yake ambapo (msichana) alieleza:

“Bwana wangu alinipa dirham moja (kwa ajili) kununulia tende. Nilizinunua (tende) kwa mfanya biashara huyu, lakini niliporudi nyum- bani, bwana wangu alizikataa. Sasa ninataka kuzirudisha lakini mfanya biashara anakataa kuzichua.”

Imam Ali (as) Ali alimgeukia mfanya biashara na kumuambia, “Mtoto huyu ni mtumwa na hana mamlaka yake mwenyewe. Chukua tende na umrudishie fedha yake.”

Mfanya biashara alisogea mbele na huku wafanya biashara na watazamaji wengine wakimtazama, alimpiga Imam kifuani katika jitihada za kum- sukuma atoke mbele ya duka lake. Watu waliokuwa wakishuhudia tukio hilo, walikimbia na kumuambia huyo mwanaume:

“Unafikiri unafanya nini? Huyu ni Ali Ibn Abi Talib (as)!”

Uso wa mfanya biashara ulipauka alipokuwa amesimama akaduwaa. Mara moja alichukua tende kutoka kwa msichana na akamkabidhi fedha. Kisha akamgeukia Imam (as) akaomba, “Ewe Amirul Muuminuun! Niwie radhi na nisamehe.”

Imam (as) alijibu,” Nitakuwa radhi na wewe tu pale utakapobadili tabia yako na kuwa njema na ukajali maadili na heshima.”5

5. Maliki Ashtar

Wakati fulani, Maalik Ashtar alikwa akipita katika soko la Kufah akionekana masikini sana. Alikuwa amevaa nguo nzito (iliyotengenezwa kwa kitambaa cha turbai) na alikuwa ameweka turbai kichwani kwake badala ya kilemba. Mmoja wa wafanya biashara alikuwa amekaa dukani mwake macho yake yalipoangukia kwa Maalik. Alimtizama kwa twezo na kwa dharau akamtupia kipande cha udongo.

Maalik alimpuuzia na aliendelea na safari yake. Hata hivyo mtu aliyem- tambua Maalik na aliyekuwa ameshuhudia tukio hilo, alimkanya mfanya biashara:

“Aibu juu yako! Unamjua uliyemdhalilisha punde tu?”

“Hapana.” Alijibu mfanya biashara

“Alikuwa ni Maalik Ashtaar, sahaba wa Ali (as).”

Baridi iliingia mwilini mwa mfanyabiashara alipowaza juu ya uovu alio- ufanya. Mara moja aliondoka na kumfuata Maalik ili akaombe msamaha.

Alibaini kwamba Maalik alikuwa ameingia msikitini ambako alikuwa akisali na akamua kumsubiri. Maalik alipomaliza kusali tu yule mfanya biashara alimuangukia miguuni na kuanza kuibusu, Maalik alimnyanyua na kumuuliza alichokuwa akifanya.

“Ninaomba msamaha kwa dhambi niliyofanaya,” alijibu mfanya biashara. Maalik akaeleza, “Hakuna dhambi juu yako. (Naapa) kwa Allah, nilikuja msikitini makhsusi kwa ajili ya kukuombea msamaha.”6

 • 1. Alikuwa ni binamu wa Mtukufu Mtume (saw) na mke wa Miqdad Ibn al-Aswad
 • 2. Lataaif al-Tawaaif, uk. 26
 • 3. Namunah-e-Ma’arif, Juz. 1, uk. 64, Jawaame al-Hikayaat, uk. 270
 • 4. Muntahal Aa’maal, Juz. 2, uk. 4
 • 5. Daastaan-ha Wa pand –ha, Juz. 1, uk. 46; Bihar al-Anwar, Juz. 9, uk. .519
 • 6. Muntahl Aa’maal, Juz. 1, uk. 212; Majumua’h Warraam - Ibn Abi Farraas

2) Ukarimu

Allah Mwenye Hikma, amesema:

“Kwa hakika Allah yupo pamoja na wanaojilinda na maovu na wanaofanya wema (kwa wengine).”1

Maelezao mafupi:

Allah humpenda mtu mwenye sifa ya ukarimu, kama ambavyo tu Allah ameonyesha upole kwetu, ni muhimu kwetu kuonyesha ukarimu zaidi kwa wengine. Hata kama mtu ametukosea, tunapaswa kujibu kwa upole na tusilipe uovu kwa uovu, kwani hili litaongeza mafuta kwenye moto na kuzidisha chuki na uadui.

Mwenendo wa wajumbe wa Allah (na Maimam) ulikuwa kwamba wak- isalimiwa, wanaitikia kwa salamu iliyo bora zaidi na kwa ukamilifu zaidi na wakifanyiwa wema, walikuwa wakiulipa, (tena) kwa kuzidisha (walivyofanyiwa wao).

Wale wanaofanya wema na kuonyesha ukarimu kwa wengine, huvuta mioyo ya watu, na wakati huohuo matendo yao yanamuumiza shetani.

Lazima ikumbukwe kwamba wale wanaofanya wema huwa hawamdhalilishi (wanayemfanyia wema) au kuharibu amali zao kwa kuweka aina yoyote ya masharti (kwa huyo waliyemfanyia wema).

Myahudi masikini alipata kukutana na muabudu moto tajiri wakiwa safari- ni. Muabudu moto aliyekuwa anamiliki ngamia na masurufu ya kutosha kwa ajili ya safari, alimuuliza, “Ni nini imani na Itikadi yako?”

Myahudi alijibu, “Ninaamini kwamba ulimwengu huu una aliyeuumba na ninamuabudu yeye na ninaomba hifadhi kwake. Ninaonyesha wema kwa yeyote anayeikiri imani yangu, lakini ninamwaga damu ya yeyote anayeto- fautiana na mimi. Ni nini itikadi yako?”

Muabudu moto alijibu, “Nina wapenda viumbe wote, simdhuru yeyote na ninaonyesha ukarimu na wema kwa marafiki na maadui pia. Mtu yeyote akinikosea, nina jibu kwa wema kwa sababu najua kuwa ulimwengu huu una muumba.”

Aliposikia hivi, Myahudi alisema, “Usidanganye sana. Mimi ni binadamu kama wewe, lakini wakati wewe unasafiri juu ya ngamia na una masurufu ya safari, hunipi chakula chako wala huniruhusu nikae kwenye ngamia wako.”

Muabudu moto aliteremka kutoka kwenye ngamia wake na akatandika kitambaa chini, akaweka chakula chake mbele ya mwenzake, myahudi alikula mkate na kisha akakaa kwenye ngamia ili kuondoa uchovu. Walikuwa wamesafari umbali fulani pamoja. Ghafla myahudi alipompiga ngamia kwa bakora alimlazimisha kukimbia. Yule Mwabudu moto alimwita:

“Ewe mtu! Nilionyesha upole kwako lakini sasa, unalipa ukarimu wangu kwa kuniacha peke yangu jangwani!”

Lakini haikujalisha chochote alichosema, nasaha zake hazikuwa na faida. “Nilikutajia kwamba nina muangamiza yeyote anaye tofautiana na mimi katika imani na itikadi,” Myahudi alimkemea huku akikimbia.

Muabudu moto alitizama juu mbinguni na kuomba: “Ewe Mola wangu! Nimemtendea mtu huyu vyema, lakini amenilipa uovu. Nitendee uadilifu.” Alipokuwa akisema haya, aliendelea na safari yake. Alikuwa amesafiri umbali mfupi tu, ghafla macho yake yalipoangukia kwenye ngamia wake, aliyekuwa amesimama peke yake baada ya kumbwaga myahudi chini. Myahudi, aliyekuwa ameumizwa vibaya, alikuwa akilalama kwa mau- mivu.

Alikuwa na furaha sana, muabudu moto alichukua ngamia wake, akapanda mgongoni mwake na alipokuwa anataka kuondoka Myahudi alilalamika: “Ewe mtu rahimu! Umevuna matunda ya wema wako na nimeshuhudia matokeo ya uovu wangu; sasa kwa kuzingatia imani zako, usiondoke katika njia ya wema; kuwa mpole kwangu na usinitelekeze katika jangwa hili.”

Muabudu moto alijiwa na huruma na akamruhusu kukaa kwenye ngamia na akampeleka mjini.2

1. Wema Wa Imam Husein (As) Kwa Mpanda Ngamia

Imam Sadiq (as) alisema: “Mwanaume mmoja alikuwa akimvuta mwanamke alipokuwa (mwanamke) amejishughulisha katika kutufu Kaaba. Mwanamke huyu alikuwa akinyanyua mikono yake mwanaume yule alipoweka mkono wake juu ya mkono wake (mwanamke) wakati huo Allah aligundisha mkono wake katika mkono wa mwanamke.

Watu walimiminika (kwenda) kushuhudia tukio hili la ajabu kwa wingi mkubwa kiasi kwamba utembeaji ulikwama. Mtu mmoja alitumwa kwa Amiri wa Makka kumjulisha juu ya tukio hili. Alikusanya wanazuoni wote na kwa ujumla wakajaribu kutafuta suluhisho la tatizo hili. Watu wengi pia wa kawaida walikusanyika wakitaka kujua hukumu itakayotolewa kwa uhalifu huu. Wote wakiwa wamesimama (huku) wametatizika, hatimaye Amiri alisema: “Je kuna mtu yeyote hapa kutoka katika familia ya Mtukufu Mtume (saw)?”

Wale waliokuwepo wakasema, “Ndio! Husein Ibn Ali (as) yupo hapa” Usiku ule Amiri aliamuru Imam (as) akaletwe mbele yake. Alitaka kujua hukumu ya tukio hili kutoka kwa Imam (as)

Kwanza, Imam (as) aligeukia Ka’aba na kunyoosha mikono yake alisima- ma katika hali hii kwa muda kisha akaomba dua.

Kisha alimfuata mwanaume yule akautenganisha mkono wake kutoka katika mkono wa yule mwanamke kwa nguvu ya Uimam wake. Yule Amiri alimuuliza Imam (as): “Ewe Husein (as) nimuadhibu?” “Hapana,” alijubu Imam (as).

Mtunzi anasema huu ulikuwa ni wema ambao Imam (as) aliuonyesha kwa mpanda ngamia lakini ni mtu huyu huyu aliyelipa kitendo hiki cha wema kwa kukata mikono ya Imam ili akwapue mkanda wake, katika giza la usiku wa 11 Muharram 61H.A.3

2. Abu Ayyub Ansaari

Abu Ayyub Ansaar alikuwa ni mmoja wa masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (saw). Mtukufu Mtume (saw) alipohama Makka kwenda Madina, makabila yote ya Madina yalimuomba akae lakini alisema:

“Sehemu nitakayokaa inategemea sehemu atakayokaa ngamia wangu.” Msafara ulipofika sehemu karibu na nyumba ya Maalik Ibn Najjar, ambayo baadaye ilikuja kuwa mlango wa msikiti wa Mtume, ngamia alikaa chini kupumzika. Lakini muda mfupi baadaye alisimama tena na akaanza kutembea, kisha akarudi sehemu ile ile aliyokuwa amekaa awali.

Watu wakaanza kumuendea Mtukufu Mtume (saw) na kumuomba akawe mgeni wao. Alipoona hivi, Abu Ayyub alinyanyua mfuko uwekwao kwenye siti ya ngamia wa Mtukufu Mtume (saw) kutoka kwenye mgongo wa ngamia na akaupeleka nyumbani kwake.

Mtukufu Mtume (saw) alipobaini kuwa mfuko wake haupo, aliuza “Nini kimetokea juu ya mfuko wangu?” Wale waliokuwepo walimjulisha kwam- ba Abu Ayyub alikuwa ameupeleka nyumbani kwake.

Mtukufu Mtume (saw) akasema: “Mara nyingi mtu anatakiwa aambatane na mzigo wake” kisha akaelekea kwenye nyumba ya Abu Ayyub na akakaa hapo hadi nyumba katika eneo la msikiti zilipokuwa zimejengwa.

Awali, Mtukufu Mtume (saw), alikuwa akiishi katika chumba cha chini wakati Abu Ayyub aliishi juu ghorofani lakini baadaye aliomba: “Ewe Mjumbe wa Allah! Sio sawa kwamba wewe ukae chini, wakati sisi tunaishi ghorofani juu: itafaa zaidi ikiwa utahamia juu.”

Mtukufu Mtume (saw) alikubali na akaomba vitu vyake vihamishiwe juu. Abu Ayyub alikuwa pamoja na Mtukufu Mtume (saw) na alishiriki katika vita kama Badr na Uhud, akipigana dhidi ya maadui wa Uislam akionye- sha ushujaa na ukakamavu wa kusifika.

Usiku akiwa anarudi nyumbani baada ya vita vya Khaibar, Abu Ayyub alikesha usiku kucha akilinda hema la Mtukufu Mtume (saw). Asubuhi ilipopambazuka, Mtukufu Mtume (saw) aliuliza: “Ni nani yupo nje huko?”

“Ni mimi, Abu Ayyub”, lilitoka jibu.

Mtukufu Mtume (saw) alisema mara mbili, “Allah akurehemu!”

Hivyo, Abu Ayyub kwa kupitia wema wake kwa Mtume, kwa fedha zake na roho yake, alinufaika na dua hii ya Mtukufu Mtume (saw).4

3. Malipo Ya Mashairi

Siku moja ya Nawruz, Mansur Dawaaniqi, Khalifa kutoka ukoo wa Bani Abbasi aliyechukua ukhalifa baada ya kaka yake Abu al-Abbas Saffaah, alimuamuru Imam Musa Kadhim (as) kuhudhuria katika Eid ya Nawruz, ilifanywa hivi ili watu waje na kumsalimia na kumpa zawadi ambazo ali- paswa kuzikubali.

Imam (as) alimuambia Mansur, “Nawruz ni Eid ya kimila ya Wairan haku- na kilichotajwa juu yake katika Uislam”

Juu ya hili Mansur alijibu “kitendo hiki kina hamasa za kisiasa na inakusudiwa kuwafurahisha askari wangu. Ninakuweka chini ya Mola mkuu kuwa ukubali ombi langu na uhudhurie katika mkusanyiko huo.” Imam (as) alikubali na akawasili katika hadhara ya Majenerari wa jeshi, Mamwinyi na watu wa kawaida walipita mbele yake wakamsalimia na kumpa zawadi zao.

Wakati huo huo Mansur alikuwa amemuamuru mmoja wa watumwa wake akae karibu na Imam akitunza kumbukumbu ya fedha na zawadi zina- zowasilishwa kwake.

Mtu wa mwisho kuja kumuona Imam (as) alikuwa ni mzee aliyemuambia: “Ewe mtoto wa Mjumbe wa Allah! Mimi ni mtu masikini na sina fedha za kukununulia zawadi, lakini zawadi yangu kwa leo ni aya tatu za shairi la maombolezo, ambazo babu yangu amezitunga kwa ajili ya babu yako, Husein Ibn Ali (as).” Baada ya kusema hayo akasoma aya hizo.

Imam (as) alishukuru kwa kusema; “Nimeikubali zawadi yako” kisha akamsomea dua mtu huyo. Kisha akamgeukua mtumwa na kumuagiza “Nenda kwa Mansur mjulishe juu ya zawadi hizi na muulize zifanyweje.” Mtumwa alifanya kama alivyoagizwa na aliporudi, alimuambia Imam (as): “Khalifa amesema: “Nimekupa wewe (Imam Musa Kadhim) kama zawadi, zitumie utakavyo.”

Imam (as) alimuambia yule mzee: “Chukua utajiri huu na zawadi hizi, kwani ninakupatia vyote hivi kama zawadi.”5

4. Yusuf (As) Na Nduguze

Miaka kadhaa baada ya tukio la nduguze Yusuf (as) kumchukuwa kwa udanganyifu nje ya mji. Kumpiga na kumtupa kisimani na hivyo kumlaz- imisha baba yao kulia mfulululizo na kusonononeka kwa hasara yake, wale ndugu walisikia kuwa Yusuf amekuwa Mfalme wa Misir. Wao na baba yao walienda kuonana naye.

Sentensi ya kwanza kabisa ambayo Yusuf aliitamka alipowaona, ilikuwa:

“Na kwa hakika alikuwa mwema kwangu aliponitoa gerezani…”6

Inavyooneka ni kwa sababu ya tabia njema kwamba Yusuf aliepuka kutaja matatizo aliyoyapata; kwanza kutupwa kisimani, kisha kufanywa kwake mtumwa na kisha matukio yasiyofurahisha, aliyokumbana nayo kutokana na matendo ya nduguze. Hakutaka kufufua kumbukumbu hizo chungu, ambazo zingewasababishia fedheha na mfadhaiko.

Kisha aliongeza, “Ni shetani aliyewashawishi ndugu zangu kunifanyia yale matendo yasiyofaa, kunitupa kisimani na kunitenganisha na baba yangu; hata hivyo Mwenyezi Mungu Mtukufu alinifanyia wema kwani aliyafanya matendo hayo kuwa ni njia ya kuipatia familia yetu utukufu na heshima!”

Kuyahusisha matendo ya kidhalimu na nduguze na shetani na kumuona yeye (shetani) kama mhusika mkuu wa uhalifu wa nduguze, ulikuwa ni mfano mwingine wa ukarimu na moyo wa kusamehe wa Yusuf. Hivyo ali- wakinga dhidi ya mfadhaiko na akawaacha na fursa ya kuomba msamaha kwa matendo yao.

Alisema:

لَا تَثْرِيبَ عَلَيْكُمُ الْيَوْمَ ۖ {92}

“Hakutakuwa lawama dhidi yenu (kuanzia) siku hii (Quran 12:92)

Kaeni kwa amani juu yangu, kwani nimewasamehe na nimeyasahau yote yaliyotokea, na kwa niaba ya Mwenyezi Mungu pia, ninaweza kuwapeni habari njema na tafuteni kutoka kwake ili Allah awasamehe na Yeye ni Mwenye rehema kuliko wenye rehema wote.7

إ


ِنَّهُ مَنْ يَتَّقِ وَيَصْبِرْ فَإِنَّ اللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ{90}

“Kwa hakika yule ajichungaye (dhidi ya maovu) na akawa na subira (hulipwa) kwani kwa hakika Allah huwa hapotezi ujira wa wafanyao wema.” (Qur’an 12:90)

Neno la mtunzi: Somo ambalo Hadhrat Yusuf (as) alimfundisha kila mmoja ni lile la kuonyesha wema na ukarimu kama majibu ya tabia mbaya, na tunataraji sisi pia tunaweza kufanya hivyo kwa ndugu zetu katika Iman, Inshaallah!

 • 1. Qur’ani Tukufu Suratu’l-Nahl 16:128
 • 2. Jawaame al–Hikayaat, uk. 24, Namunah- e ma’arif, Juz. 1, uk. 29
 • 3. Raahinama –e- Sa’adat, Juz. 1 uk, 36; Shajarah-e-Tuba, uk 422
 • 4. Payghambar Wa yaraan, Juz. 1, uk. 20-27; Bihaar al –Answaar, Juz. 6, uk. 554
 • 5. Muntahal Aamal, Juz, 2 uk.187
 • 6. Qur’ani Tukufu Suratul Yusuf 12:100
 • 7. Qur’ani Suratul Yusuf 12:92

3) Unyofu

Allah Mwenye hikma, amesema:

فَاعْبُدِ اللَّهَ مُخْلِصًا لَهُ الدِّينَ {2}

“Hivyo muabuduni Allah (peke yake) mkiwa waaminifu Kwake kati- ka dini.” (Quran 39:2)

Imam Ali (as) alisema: “Fanya matendo yako kwa unyofu, kwani (ukifanya hivyo) hata kidogo kitakutosha.1

Maelezo mafupi:

Unyofu ni ufunguo wa kukubaliwa amali zote. Mtu ambaye amali zake zimekubaliwa na Allah hata ziwe ndogo kiasi gani, ni mtu mnyofu na mtu ambaye amali zake zimekataliwa na Allah, licha ya wingi wake, sio miongoni mwa watu wanyofu.

Mtu mnyofu hujitahidi kuitakasa roho yake kutokana na maovu na hujibadilisha kufanya amali njema na kudumisha (unyofu wa) nia ili Allah azikubali amali zake.

Kiwango cha nia, maarifa na matendo yanahusiana na utakaso wa kiroho na usafi (wake), na kama mtu mnyofu angezingatia kikamilifu nafsi yake ya ndani, angeitambua dhana halisi ya upweke wa Allah. Kiwango cha chini kabisa cha unyofu ni wakati mtu anapofanya jitihadi kwa kadiri ya uwezo wake wote, akiwa hatarajii malipo kwa matendo yake wala hayapi umuhimu wowote.2

1. Watu Watatu Katika Pango

Mtukufu Mtume (saw) amesimulia:

“Watu watatu kutoka katika kabila la Bani Israil walikusanyika na wakaan- za safari, walipokuwa njiani, mawingu yalikusanyika na mvua kubwa ikaanza kunyesha na hivyo wakatafuta hifadhi katika pango lililokuwa karibu.

Ghafla jiwe kubwa lilibilingika na kuziba lango la pango, (na hivyo) kuwakwamisha watatu hao ndani na kuubadili mchana kuwa usiku kwa giza. Walikuwa hawana jingine la kufanya isipokuwa kumgeukia Allah kwa msaada.

“Tutumie matendo yetu ya unyofu kama njia ya kupata nusra kutokana na tatizo hili,” alishauri mmoja wao. Wengine wote walikubaliana na ushauri huo. Mmoja wao alisema “Ewe Mola! Unajua kuwa nina binamu yangu anayevutia sana kabisa na kwamba nilivutiwa naye na kumpenda sana, siku moja nilipomkuta akiwa peke yake, nilimchukua na nilitaka kukidhi matamanio yangu ya kimwili, aliposema: ‘Ewe binamu yangu! Muogope Allah na usiuharibu ubikra wangu.’

Niliposikia hivi nilivyunjilia mbali matamanio yangu ya kimwili na nikaamua kutofanya kitendo kiovu. Ewe Mola! Ikiwa kitendo changu hicho kilitokana na unyofu wa kweli na kwa nia ya kupata radhi Zako tu, tunusuru kutokana na huzuni na adhabu. Ghafla waliona kwamba lile jiwe limesogea kidogo, likiruhusu mwanga hafifu kuingia ndani ya pango.

Mtu wa pili alisema: “Ewe Mola! Unajua kwamba nilikuwa na baba na mama, walikuwa wazee sana kiasi kwamba miili yao ilikuwa imepinda kutokana na umri uliopindukia, na kwamba nilikuwa nikiwahudumia kila mara. Usiku mmoja nikiwa nimewaletea chakula, nilibaini kwamba wote walikuwa wamelala. Nilikesha usiku kucha karibu yao, na chakula mkononi, bila kuwaamsha nikihofia kuwasumbua. Ewe Mola! Ikiwa kiten- do changu hiki kilikuwa ni kwa ajili ya kupata radhi na furaha Yako, tufun- gulie njia na tupe wokovu.” Alipomaliza kauli yake, kundi lile lilibaini kuwa jiwe lile lilikuwa limesogea pembeni zaidi.

Mtu watatu aliomba: “Ewe Mjuzi wa yaliyofichikana na yaliyo dhahiri! Unajua mwenyewe kwamba nilikuwa na mfanyakazi aliyekuwa akinifanyia kazi. Mkataba wake ulipokuwa umefikia mwisho, nilimkabidhi ujira wake, lakini hakuridhika na alitaka zaidi na katika hali ya kutoridhi- ka na kutofurahi, aliondoka. Nilitumia ujira wake kununulia mbuzi, na nil- imhudumia tofauti, na punde nikawa na kundi la mbuzi. Baada ya kipindi fulani, yule mfanyakazi alinijia akitaka ujira wake na nikamuonyesha kundi la mbuzi.

Awali alifikiri ninamdhihaki, lakini baadae alipotambua umakini wangu alichukua kundi lote (la mbuzi) na kuondoka.3 Ewe Mola! Ikiwa kitendo hiki kilisukumwa na unyofu na kilikuwa kwa ajili ya kutaka radhi Zako, tuokoe katika mkwamo huu”

Kufikia hapo jiwe lote liliondoka katika lango la pango na wote watatu wakatoka, wakiwa na furaha na msisimko, na wakaendelea na safari yao.4

2. Ali (As) Katika Kifua Cha Amr

Amr Ibn Abd Wuud alikuwa ni mpiganaji ambaye, katika vita alikuwa ni sawa na askari 1000. Katika vita vya Ahzaab, aliwapa changamoto askari wa Kiislamu kupigana naye, lakini hakuna hata aliyekuwa na ujasiri wa kusimama mbele yake hadi Imam Ali (as) alipokwenda mbele ya Mtukufu Mtume (saw) na kuomba ruhusa ya kupigana naye.

Mtukufu Mtume alimuambia Ali (as): “Tambua kuwa huyu ni Amr Ibn Abd Wuud!” Imam Ali (as) kwa unyenyekevu alisema “(Na) mimi ni Ali Ibn Abi Talib,” na kisha akaenda katika uwanja wa vita na kusimama mbele ya Amr.

Baada ya mapambano makali, Imam (as) hatimaye alimuangusha chini na akakaa juu ya kifua chake. Walipoona hivi, jeshi zima la Waislamu lilimuomba Mtukufu Mtume (saw): “Ewe Mjumbe wa Allah, muamuru Ali (as) amuue Amr mara moja!”

“Muacheni kwani anayajua matendo yake vizuri zaidi kuliko mwingine yeyote,” alijibu Mtukufu Mtume (saw).

Ali (as) alipokuwa amekikata kichwa cha Amr, alikileta kwa Mtukufu Mtume (saw) ambaye alimuuliza “Ewe Ali! Ni nini kilichokufanya usite kabla ya kumuua Amr?

Akasema, “Ewe Mjumbe wa Allah! Nilipokuwa nimemwangusha chini, alinikashifu matokeo yake nikapatwa na hasira. Nilihofia kuwa kama ningemuua katika hali ile ya hasira, ingekuwa (nimemuua) kwa ajili ya kijifariji na kuiridhisha roho yangu. Hivyo niliondoka juu yake mpaka hasira yangu ilipokwisha na nikarudi kukitenganisha kichwa chake kutoka katika mwili kwa ajili ya furaha ya Allah na kwa ajili ya kumtii Yeye.”

Ilikuwa ni kwa sababu ya unyofu na pigo lenye thamani kwa upande wa Imam Ali (as) kwamba Mtukufu Mtume (saw) alisema: “Dhoruba la upan- ga wa Ali katika siku ya vita vya Khandaaq ni bora kuliko ibada ya wanadamu wote na majini.”5

3. Shetani Na Mchamungu

Katika kabila la Bani Israil, alipata kuishi mchamungu mmoja. Siku moja watu walimjulisha kuwa katika sehemu fulani, kulikuwa na mti uliokuwa ukiabudiwa na watu wa kabila hilo. Aliposikia hivi, aliruka kwa hasira, akachukuwa shoka yake na kuondoka kwenda kuukata mti ule.

Ibilisi, akatokea mbele yake kwa sura ya mtu mzee, alimuuliza, “Unakwenda wapi?” alijibu “Nina kusudia kukata mti ambao unaabudiwa ili badala yake watu wamuabudu Allah.”

“Jizuie mpaka utakaposikia nitakayoyasema.” Ibilisi alisema kumuambia yule Mchamungu. Yule Mchamungu akamuambia aendelee kusema. Ibilisi aliendelea: “Allah ana mitume, wake kama ingekuwa ni muhimu kuuan- gusha mti angekuwa amewatuma kuja kufanya kazi hiyo.” Lakini, Mchamungu hakukubaliana na Ibilisi na akaendelea na safari yake.

“Kwa vyovyote vile sitakuruhusu” ibilisi alisema kwa hasira na akaanza kupigana mieleka na mtu yule, katika mpambano huo mchamungu alimb- waga ibilisi chini. “Subiri nina kitu cha kukuambia” alisihi ibilisi “Sikiliza! Wewe ni mtu masikini kama ungekuwa na mali ambayo kwayo ungetoa zaka kwa waumini wengine ingekuwa bora zaidi kuliko kukata mti. Ukijizuia kukata mti, nitaweka dinari mbili chini ya mto wako kila siku.”

Mchamungu akasema huku akiwaza: “Ikiwa unasema ukweli, nitatoa dinari moja kama sadaka na nitaitumia dinari nyingine.

Hili ni bora kuliko kukata mti katika hali yoyote, sijatumwa kufanya kazi hii wala mimi sio Mtume mpaka nijitwishe mzigo wa huzuni na mashaka yasiyo ya lazima.” Hivyo alikubaliana na ombi la ibilisi na akamuacha.

Kwa siku mbili, alipokea dinari mbili na akazitumia, lakini katika siku ya tatu, hapakuwa na dalili ya fedha. Akiwa ameudhika na kusononeka, akachukua shoka yake akatoka kwenda kukata ule mti.

Njiani alikabiliana na shetani, aliyemuuliza: “Unaelekea wapi?

“Ninakwenda kukata ule mti.”

“Kwa vyovyote huwezi kwenda kufanya hivyo” alisema shetani.

Kwa mara nyingine tena walianza kupambana lakini mara hii ibilisi alimzi- di nguvu na akamwangusha chini, (kisha) akamuamuru, “rudi nyuma sivyo nitatenganisha kichwa na kiwiliwili chako.” Mchamungu alisema, “Niache na nitarudi, lakini niambie ilikuwaje nikaweza kushinda katika tukio la awali?”

Ibilisi alijibu: “Katika tukio lile umetoka kwa ajili ya Allah na ulikuwa na ikhlasi katika nia yako na matokeo yake Allah akanidhoofisha kwa ajili yako, lakini safari hii ulikasirika kwa ajili ya nafsi yako mwenyewe na dinari zako na hivyo nikaweza kukuzidi nguvu.”6

4. Siri Ya Mtumwa Muaminifu

Sa’eed Ibn Musayyab anasimulia: “Mwaka mmoja, kulikuwa na njaa kali na hivyo watu walikusanyika pamoja ili kuomba dua kwa ajili ya mvua. Nilitazama hivi na macho yangu yakamuangukia mtumwa mweusi aliyekuwa amejitenga na umati wa watu na akaibukia kwenye kilele cha kilima kidogo. Nilikwenda katika uelekeo alipokuwa na nilipomkaribia, nilibaini kwamba midomo yake ilikuwa ikijongea (akisoma) dua. Alipomaliza tu dua yake, wingu lilikusanyika angani. Alipoona wingu, mtumwa alimsifu Allah na akaondoka. Mara tu mvua ikatupiga sana mpaka tukafikiri kuwa tunaweza kuangamia. Nilimkimbilia mtumwa yule nikaona kwamba ameingia katika nyumba ya Imam Sajjad (as). Niliwasili mbele ya Imam (as) na nikasema:

“Ewe bwana wangu! Katika nyumba yako kuna mtumwa mweusi; tafad- hali niuzie” Akasema, “Ewe Sa’eed! Kwa nini badala yake nisikupe kama zawadi?” Na akamuamuru mkuu wa watumwa kuwaleta watumwa wote mbele yake. Walipokuwa wamekusanyika, nilibaini kuwa mtumwa mweusi hakuwa miongoni mwao. Nikasema, “Ninayemtaka hayupo hapa.” Imam (as) akasema hakuna mtumwa aliyebaki isipokuwa mmoja. Kisha akaamuru akaletwe, mtumwa huyo alipoletwa mbele yangu niliona kuwa ndiye mtu mwenyewe niliyekuwa nikimtafuta na hivyo nikasema: “Huyu ndiye ninayemhitaji!”

“Ewe mtumwa! Kuanzia sasa, Sa’eed ni bwana wako na nenda naye” aliagiza Imam (as). Mtumwa akanigeukia na kusema, “Ni nini kilichokusukuma unitenganishe na bwana wangu?” Nikajibu, “Niliposhuhudia dua yako ya mvua ikijibiwa nilitamani kukumiliki.” Aliposikia hivi, mtumwa alinyoosha mikono yake kwa ajili ya dua na akigeuzia uso wake angani akiom- ba: “Ewe Mola wangu! Hii ilikuwa ni siri baina yangu na wewe. Sasa kwa vile umeivujisha, nipatie kifo na unichukue kwako.”

Imam (as) na wote waliokuwepo walibubujikwa na machozi kutokana na hali ya mtumwa, huku nikitokwa na machozi nilitoka nje ya nyumba. Nilipofika nyumbani kwangu tu, mjumbe wa Imam (as) alifika na kusema, “Njoo kama unataka kushiriki katika mazishi ya sahibu yako.” Nilirudi nyumbani kwa Imam (as) pamoja na yule mjumbe na kukuta mtumwa ameshafariki.7

5. Ombi La Nabii Musa (As)

Nabii Musa alipata kumuomba Allah:

“Ewe Mola! Ni utashi wangu kumuona kiumbe wako aliyejitakasa kwa ajili ya ibada Yako na ambaye hajachafuliwa katika utii wake Kwako” Aliambiwa: “Ewe Musa! Nenda katika fukwe za bahari fulani ili nikuonyeshe unachotaka kukiona”

Nabii Musa alikwenda mpaka akafika karibu na bahari. Alipotazama pem- beni, aliona kuwa tawi la mti lililokuwa limeinamia juu ya maji, alikuwa amekaa ndege, akiwa amezama katika kumdhikiri Allah. Musa alipo- muuliza ndege (habari zake), ndege alisema: “Tangu Allah aliponiumba, nimekuwa katika tawi hili, nikimuabudu Yeye na dhikiri. Kwa kila dhikiri yangu moja hutokea dhikiri 1000 nyingine, na furaha ninayoipata kutokana na dhikiri ya Allah hunipatia virutubisho.”

“Je unatamani kitu chochote katika ulimwengu huu?”Aliuliza Musa (as). “Ndio. Ninatamani sana kuonja tone moja la maji kutoka kwenye bahari hii.” alijibu ndege Musa (as) akasema kwa mshangao “Lakini hakuna umbali mkubwa kati ya mdomo wako na maji! Kwa nini hutumbukizi mdomo wako ndani (ya maji) na kunywa?” Ndege akajibu, “kutokana na hofu kwamba isije ikawa raha inayotokana na maji ikanifanya nisahau raha ya kumdhukuru Mola wangu.” Aliposikia hivi, Nabii Musa (as) alishika kichwa chake kwa mshangao mkubwa.8

 • 1. Jaame’ al Saadaat Juz. 2, uk. 404
 • 2. Tadhkirah al Haqaaiq, uk 73
 • 3. Katika kitabu Mahaasim imetajwa kwamba ujira wake ulikuwa ni nusu dirham lakini alipokuja kuchukua, alipewa mara 18,000 zaidi!
 • 4. Naamunah-e-ma’arif , Juz.1, uk. 53; Farajun Ba’d al shiddah, uk 23; mahaasin e- Barqi, Juz. 2, uk 253
 • 5. Pand –e- Tarikh, Juz 5, uk. 199; Anwaar al- Nu’maaniyah; Ainal –Hayaah.
 • 6. Namunah-e-maarif, Juz. 1, uk. 54; Ihyaa al- uluum Juz. 4, uk.380; Riyadh al- Hikaaya, uk.140
 • 7. Muntahal Aamal, Juz. 2, uk. 38; Ithbaat al- Wasiyyah (cha Maasudi)
 • 8. Khazinah al- Jawaahir, uk. 318

4) Ustahamilivu

Allah mwenye Hikma Anasema:

فَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ وَمَنْ تَابَ مَعَكَ {112}

“Kisha simama imara (Ewe Mtume wetu Muhammad) katika njia iliy- onyooka kama ulivyoamrishwa (na Mola wako) pamoja na wale waliomgeukia Allah pamoja nawe. (Quran 11:112)

Imam Sadiq (as) anasema:

“Muumini yeyote anayepatwa na balaa na kisha akafanya subira, atalipwa thawabu sawa na mashahidi 1000.”1

Maelezo mafupi:

Kuvumilia na kustahamili kunaweza kupunguza ukali wa mabalaa na mis- iba. Mtu mwenye imani huwa haonyeshi ukosefu wa subira anapo patwa na mitihani, ili imani yake isiathirike. Imesemwa: “Muumini ni imara zaidi kuliko mlima. Hii ni kwa sababu (yeye) ni imara mbele ya maadui na kuonyesha ukakamavu wakati wa mabalaa kiasi kwamba huzuni huwa haipati nafasi katika moyo wa muumini mkamilifu.

Maisha, pamoja na matatizo yake mengi, hayataleta tatizo kwa wale wenye mioyo migumu. Ni wale tu ambao hawana unyofu katika ustahamilivu wao ndio huvunjika moyo wanapopatwa na msiba hata mdogo kabisa. Na iju- likane kama dini ya Allah imetufikia leo hii, ni kwa sababu ya ustahamilivu wa Mtukufu Mtume (saw) na subira ya Imam Ali (as).

1. Familia Ya Yasir

Katika kipindi cha kwanza cha Uislamu, familia ndogo ya watu wanne na iliyokuwa inakandamizwa ilisilimu. Kila mmoja wao alionyesha kiwango cha juu cha ustahamilivu katika kukabiliana na mateso ya kikatili ya washirikini. Watu hawa wanne walikuwa ni Yasir, mkewe Sumaiyah na waoto wao wawili Ammar na Abdullah.

Yasir alisimama imara katika dini yake akisumbuliwa na kashfa za maadui, hadi hatimaye alipokufa. Mkewe Sumaiyah licha ya umri mkubwa, kwa ukakamavu alistahamili mateso ya maadui hadi hatimaye Abu Jahl alipom- patia jeraha lake la mwisho.

Hivyo Sumaiyah alikufa shahidi kutokana na kipigo katika Tumbo Lake.

Abu Jahl, mbali na kumtesa Sumaiyah mwili wake, pia alikuwa akimtesa kisaikolojia wakati (Sumaiyah) alipokuwa mzee na dhaifu. Alikuwa akimuudhi kwa kusema: “Umefuata dini ya Muhammad sio kwa ajili ya Mungu bali kwa sababu umempenda Muhammad na umetekwa na sura yake nzuri.”

Mtoto wa Yasir, Abdullah pia alipewa mateso makubwa lakini yeye pia alibakia imara. Mtoto mwingine Ammar, alikuwa akipelekwa katika jang- wa linalounguza, akivuliwa nguo na kuvishwa koti la chuma la moto kati- ka mwili wake uliounguza nusu na kulazimishwa kulala katika mchanga wa moto, na chembe chembe zake zilikuwa kama vipande vya chuma kuto- ka katika tanuri la mhunzi. Mataokeo yake vyuma vya koti la chuma vilikuwa vikipenya kwenye mwili wa Ammar na walikuwa wakimuambia “mkane Muhammad (saw) na uwaabudu Lat na Uzza,” lakini Ammar kamwe hakusalimu amri kutokana na mateso yao.

Chuma kilichoungua kiliacha alama katika mwili wake kiasi kwamba Mtukufu Mtume (saw) alipomuona Ammar alikuwa anaonekana kufanana na mtu mwenye ukoma.

Alama kama za ugonjwa huo zilionekana usoni, mikononi na katika mwili wa Ammar (na) zilifanya aonekane kama mkoma.

Mtukufu Mtume (saw) alikuwa akisema hivi juu ya familia ya Yasir: “Enyi familia Yasir! Kuweni na subira na bakieni imara, kwani bila shaka peponi ndio makazi yenu”2

2. Wewe Sio Duni Kuliko Mchwa

Amir Taimur Gurgaan, alikuwa ni mtu imara na asiyeyumba katika kila tatizo, kiasi kwamba alikuwa haogopeshwi na tatizo lolote. Alipoulizwa sababu ya sifa hii, alisema: Wakati fulani nikiwa nimewakimbia maadui zangu na nikitafuta hifadhi katika gofu, nilikuwa nikitafakari juu ya hatma yangu ghafla macho yangu yalipomuangukia mchwa mdogo na dhaifu akiwa amebeba nafaka kubwa kuliko (hata) yeye mwenyewe, akijitahidi kupanda kwenye kilele cha ukuta.

“Nilipotizama kwa makini na kuhesabu kwa usahihi, nilibaini kwamba nafaka ilianguka kutoka kwenye kucha zake mara 67 kabla ya mchwa yule hatimaye kufanikiwa kufika na nafaka ile kwenye kilele cha ukuta. Kuona jitihada hizi za mchwa kulinitia nguvu kubwa ambayo kamwe sitaisahau.” Nilisema “Ewe Taimur! Kwa namna yoyote wewe sio dhaifu kuliko mchwa. Inuka na rudi kazini. Niliinuka nikakusanya nguvu zangu hadi hatimaye nikaja kupata ujasiri nilionao.”3

3. Hadhrat Nuh (As)

Hadhrata Nuh (as) aliishi maisha marefu na magumu ambayo yalitokana na kutumia muda mwingi miongoni mwa waabudu masanamu wagumu, akijaribu kuwaondolea imani zao za uongo. Hata hivyo licha ya hilo alistahamili na kuonyesha uimara bila kujali mateso na matatizo yao.

Wakati fulani watu walikuwa wakimpiga kiasi cha kupoteza fahamu kwa siku tatu nzima huku damu zikiendelea kutoka kwenye masikio yake. walikuwa wakimkamata na kumtupa ndani ya nyumba, lakini akirudiwa na fahamu alikuwa akiomba dua:

“Ewe Mola! Waongoze watu wangu kwani hawaelewi!”

Kwa takribani miaka 950 alikuwa akiwaita watu kwa Allah, lakini watu ndio kwanza walikuwa wanazidisha uasi wao na ukaidi. Walikuwa waki- waleta watoto wao kwa Nuh (as) wakiwaonyesha na kusema:

“Enyi watoto! Ikiwa mtatokea kuishi baada yetu, kuweni waangalifu kutomfuata mtu yeyote kichaa!” Kisha walikuwa wakimuambia, “Ewe Nuh! usipoacha hutuba zako, utapigwa mawe mpaka ufe. Hawa watu wanaokufuata, ni duni na dhalili, ambao wamesikia mazungumzo yako na kuukubali wito wako bila kutafakari na kuchunguza.”

Nuh (as) alipokuwa anaongea nao, walikuwa wakitia vidole vyao masikioni na kuvuta nguo zao kichwani ili wasisikie maneno yake wala kumuona uso wake. Mambo yalifikia hali isiyovumilika kiasi kwamba Nuh (as) alikosa cha kufanya isipokuwa kuomba msaada wa Allah na hivyo aliomba dua: “Ewe Allah! Nimezidiwa nguvu, nisaidie na niepushe nao.4

4. Sakkaki

Siraj al-Deen Sakkaki alikuwa ni mwanachuoni wa Kiislamu na mwenyeji wa Kharazm. Sakkaki alikuwa ni mhunzi kitaaluma. Wakati fulani, akiwa ametengeneza boksi dogo na laini la chuma kwa jitihada kubwa na matatizo, aliamua kulipeleka kwa mfalme wa wakati huo.

Mfalme na mawaziri waliipenda kazi ile lakini wakati amesimama akisubiri ujira wake, mwanachuoni aliingia katika jumba la kifalme, ambapo kila mmoja alimheshimu na kukaa mbele yake kwa kumtukuza na heshima. Sakkaki alivutiwa sana na akuliza ni nani alikuwa. Alijulshwa kuwa alikuwa ni mmoja wa wanachuoni wa zama hizo.

Sakkaki alisononeshwa na asili ya taaluma yake na (hivyo) akaamua kutafuta elimu. Alikuwa na umri wa miaka 30 alipokwenda shuleni na kuelezea haja yake ya kupata elimu. Mwalimu wa shule alimuambia: “Katika umri wako, ninatia shaka ikiwa unaweza kupata maendeleo yoyote, nenda zako na usipoteze wakati wako bila sababu.”

Lakini baada ya kusisitiza sana, Sakkaki alipata ruhusa na kutafuta elimu. Kumbukumbu yake ilikuwa dhaifu sana, wakati fulani, mwalimu wake alimuambia ahifadhi hukumu ifuatayo ya kidini: “ngozi ya mbwa hutaharika kwa kusindikwa;” lakini siku inayofuata alipotakiwa kuisoma mbele ya mwalimu wake, alisema: “Mbwa alisema: Ngozi ya mwalimu hutaharika kwa kusindikwa.” Waliposikia hivi wanafunzi na mwalimu waliangua kicheko na kumkejeli.

Miaka kumi ya jitihada haikutoa matokeo yoyote kwa Sakkaki, ambaye alihuzunika na kukata tamaa. Alikwenda milimani lakini alipokuwa kitem- bea huko, alifika sehemu ambapo matone ya maji yalikuwa yakidondokea kwenye jiwe kutokea juu. Udondokaji mfululizo wa maji ulikuwa umechimba shimo kwenye jiwe. Sakkaki alilichunguza jiwe kwa muda kisha akajisemea:

“Kwa hakika moyo wako sio mgumu kama mwamba huu. ukistahamili, hatimaye utafanikiwa. Alipokuwa ameazimia juu ya hili, alirudi shuleni kwake na kuanzia katika umri wa miaka 40, alianza kusoma kwa bidii kubwa zaidi, nguvu na subira.

Sakkaki hatimaye alifikia hatua ambayo katika fani ya sarufi ya Kiarabu na fasihi, wanazuoni wa zama zake walikuwa wakimtizama kwa heshima kubwa. Aliandika kitabu Miftaah al- U’luum, ambacho kina matawi kumi na mbili ya fasihi ya kiarabu na kinaonekana kuwa ni moja ya kazi kubwa na nzuri kabisa katika somo hili.5

 • 1. Jaamae’ al –Saadaat, Juz.3, uk. 404
 • 2. Hikaayaat -ha- e- Shanidan, Juz.5, uk. 25, Tafsir al-Manaar, Juz. 2, uk . 376
 • 3. Namunah –e- Maarif, Juz,1 uk. 174; Akhlaq –e- Ijtmaae uk, 41
 • 4. Taarikh –e- Anbiyaa, uk. 48-52
 • 5. Dastaan-ha-e-Maa, Juz.3, uk45

5) Kusuluhisha

Mwenyezi Mungu Mwenye hekma, amesema: “Na ikiwa pande mbili za waumini zitakuwa katika ugomvi, rejesheni amani baina ya pande mbili hizo.” (Suratul Hujurat; 49: 9)

Imam Sadiq (a.s) anasema:

“Kupatanisha baina ya watu wawili (wanaozozana) ni bora zaidi kwangu kuliko kutoa dinari mbili katika sadaka.”1

Maelezo Mafupi:

Moja ya matendo ya wajibu yanyotuwajibikia ni kuzikagua na kuzireke- bisha roho zetu. Mpaka mtu atakapojirekebisha yeye mwenyewe ndipo atakapoweza kuleta marekebisho kwa wengine. Kujaribu au kufanikiwa kuleta usuluhishi baina ya ndugu katika imani, ndugu, au majirani, ni jambo linalopendwa sana na Mwenyezi Mungu.

Kwa lengo la kuimarisha umoja na maelewano badala ya utengano na mifarakano ni muhimu kufanya kila jitihada kuleta suluhu. Kwa kweli katika baadhi ya kesi, huruhusiwa (hata) kutumia uongo mweupe. Wakati mwingine hufikia hata kuwa wajibu ili chuki ife na faraka iishe.

1. Utaratibu Wa Kusuluhisha

Wakati fulani, enzi za Imam Sadiq (a.s), Abu Hanifa, mtawala wa Hajjaaj, alikuwa na ugomvi na mkwe juu ya urithi. Mufadhal Ibn U’mar Kufi, mmoja wa masahaba wa karibu wa Imam Sadiq (a.s) alipita kwenye ugomvi huo. Aliposikia mabishano hayo alisimama na kusema kuwaambia hao wanaume wawili: “Twendeni nyumbani kwangu.” Walifanya kama alivyoomba. Walipofika nyumbani aliingia ndani na muda mfupi baadaye alitoka na mfuko wenye dirhamu mia nne alizowapatia (hao) watu wawili na akawasuluhisha. Kisha akaeleza: “Hizi sio fedha zangu bali ni za Imam Sadiq (a.s). Alinielekeza: “Wakati wowote utakapoona shia wetu wawili wakizozana juu ya fedha, wapatie fedha hizi na wasuluhishe.”

2. Uchukue Tahadhari Katika Usuluhishi

Abdat Malik amesema: Ulizuka mzozo baina ya Imam Baqir (a.s) na baad- hi ya watoto wa Imam Hasan (a.s). Nilimwendea Imam na nikamuomba niingilie katika jambo hilo ili niwasuluhishe, lakini Imam (a.s) alishauri: “Usiseme neno katika mzozo huu kwani tatizo letu ni kama lile la mzee kutoka katika Bani Israel, aliyekuwa na mabinti wawili. Mmoja wao ali- olewa na mkulima wakati mwingine aliolewa na mfanyakazi. Wakati fulani aliamua kuwatembelea. Kwanza alimtembelea binti yake aliyekuwa mke wa mkulima na alipofika katika nyumba yake, aliuliza juu ya afya yake, binti alisema: “Baba mpendwa, mume wangu amelima eneo kubwa la ardhi na kama mvua ingenyesha tungekuwa ni matajiri wakubwa katika Bani Israil yote.” Kisha alipokwenda kwenye nyumba ya binti mwingine, ambaye mume wake alikuwa ni mfanyakazi, aliuliza juu ya afya yake. Binti alisema “Baba mpendwa, mume wangu amefinyanga vyungu kwa kiasi kikubwa na kama Mwenyezi Mungu angezuia mvua mpaka vyungu vikauke, tungekuwa matajiri kuliko Bani Israil wote.” Alipoondoka kuto- ka kwenye nyumba ya binti yake wa pili, aliomba: “Ewe Mungu! Fanya kama unavyoona inafaa, kwani katika hali hii, siwezi kumuombea yeyote kati yao.”

Kisha Imam akamniambia, “Wewe pia huwezi kuingilia katika jambo hili. Kuwa mwanagalifu, usije ukaonyesha utovu wa nidhamu kati- ka upande mmojawapo. Jukumu lako kwetu, kwa ababu ya uhusiano wetu na Mtukufu Mtume, ni kututendea tofauti na kwa heshima.” 2

3. Malipo Ya Usuluhishi

Fudhail ibn A’yyadh amesema: Mtu mwenye sononeko la moyo alichukua kamba ambayo mke wake alikuwa ameisokota kwenda kuiuza sokoni ili kujinusuru yeye mwenyewe na familia yake kutokana na njaa. Baada ya kuiuza kwa dirhamu moja, alikusudia kununua mkate alipokutana na watu wawili wakigombana na kurushiana makonde kwa sababu ya dirhamu moja. Mtu (yule) alisogea mbele akawapa dirhamu moja na kusuluhisha baina yao. Kwa mara nyingine tena, akiwa hana kitu mkononi, alikwenda nyumbani na kusimulia tukio zima kwa mkewe. Mkewe alifurahi kwa mwenendo wake. Alitafuta ndani ya nyumba, akapata gauni kuukuu ambayo alimkabidhi mumewe, ili aiuze na kupata chakula.

Yule mtu alilipeleka gauni sokoni lakini hapakuwa na mtu aliyekuwa tayari kulinunua. Alipotazama pembeni alimuona mtu mwenye samaki mikononi mwake. Alimwendea yule mtu na kusema, “Tubadilishane bidhaa. Nipe samaki wako nitakupa gauni langu.” Muuza samaki alikubali na yule mtu alirudi nyumbani na samaki. Mke wake alikuwa akijishughulisha na usafishaji wa samaki, wakati ghafla kitu cha thamani kilipotoka tumboni mwa samaki. Alimkadhi mumewe kitu hicho ili akakiuze sokoni. Mumewe alikiuza kwa bei nzuri sana na alirudi nyumbani lakini kabla hajaingia ndani mtu fukara alikuja kwenye mlango na kusema, “Nipeni kutokana na hivyo alivyokupeni Mwenyezi Mungu.” Mara tu mtu yule aliposikia wito ule, alileta fedha zote na akamtaka maskini achukue fedha anazotaka. Muombaji alichukua fedha kiasi na akaanza kuondoka. Lakini alikuwa ametembea hatua chache tu wakati aliporudi na kusema: “Mimi sio masiki- ni. Nimetumwa na Mwenyezi Mungu na ninapaswa kukujulisha kuwa fedha ulizopata ni ujira wako kwa kuwasuluhisha watu wawili waliokuwa wakigombana.” 3

4. Mirza Jawad Agha Maliki

Juu ya mwanazuoni Mirza Jawad Adha Maliki (aliyekufa mwaka 1343A.H.), imerekodiwa kwamba katika hatua za awali za kutafuta utaka- so wa kiroho na baada ya kuwa amesoma chini ya mwalimu wake, mwanazuoni mkubwa Mulla Hasainquli Hamadani (aliyekufa mwaka 1311A.H.), kwa miaka miwili, alilalamika kwa mwalimu wake? “Katika kutafuta kwangu utakaso wa kiroho, bado sijaweza kupata kitu chochote”. “Jina lako ni nani?” aliuliza mwalimu. Akajibu “Wewe hunitambui mimi? Mimi ni Jawad Maliki Tabrizi.”

Hasainquli Hamadani aliuliza, “Je una uhusiano na familia fulani na fulani ya Maliki?” Mirza Jawad alikubali na kisha akaanza kuzungumza kwa kuwakosoa. “Wakati wowote utakapofika wa wewe kuwawekea viatu vyao mbele yao ili wavae, (ambacho unakiona ni kitendo duni na dhalili), mimi binafsi nitakuja kukuongoza,” alishauri Husainquli Hamadani.

Siku iliyofuata Mirza Jawad alipokwenda darasani alikaa nyuma ya wana- funzi wote na pole pole alianza kuzoea na kuwa na tabia ya kirafiki na wanafunzi wa familia ya Maliki wanaoishi Najaf. Iliendelea hivi mpaka ikafikia hatua ambapo alikuwa hata akiwawekea viatu mbele yao ili wavae. Ndugu wanaoishi Tibrizi walipolijua hili, chuki na faraka iliyokuwepo miongoni mwa wanafamilia hao, na amani ikaanzishwa miongoni mwao.

Baadaye Mirza Jawad alimwendea mwalimu wake, ambaye alimwambia, “Hakuna maelekezo mapya kwa ajili yako (Baada ya kuwasuluhisha wana ndugu wa familia ya Maliki). Endelea kufuata utaratibu huu wa sheria na nufaika kutokana nayo.

Neno la Mwandishi: Kwa bahati, kitabu Miftaah al-Falaah cha marhum Sheikh Bahaai ni kitabu bora kabisa cha kufuata.

Polepole Mirza aliendelea katika utafuaji wake. Alikuja katika Hauza ya Qum ambapo alianza kuwafundisha na kuwaongoza wanafunzi katika fani ya utakaso wa kiroho. Idadi kubwa ya watu, watu wa kawaida na wasomi walinufaika kutokana naye na mafundisho yake.

5. Ushauri Wa Waziri Wa Ma’mun

Wakati fulani, Ma’mun Khalifa wa ukoo wa Abbas alichukizwa na Ali Ibn Jahm Saami mshairi wa baraza, na akiwa katika shinikizo la hasira aliwaa- muru watumishi wake: “Muueni na mnyang’anyeni mali zake zote.”

Waziri wa Ma’mun, Ahmad Ibn Abi Dawood, katika njia ya kusuluhisha alimwendea na kuomba, “Ikiwa utamuua, mali zake tutamnyang’anya nani?” “Kutoka kwa warithi wake” alijibu Ma’mun. Ahmad akasema, “Katika hali hiyo, khalifa hatokuwa amemnyang’anya mali zake (Ali) bali zile za warithi wake, kwani baada ya kifo chake, atakoma kuwa mmiliki wa mali zake. Na kuchukua mali ya mtu kwa sababu ya kumwadhibu mwingine ni kitendo cha dhulma, ambacho hakifai kwa wadhifa wa khalifa.”

Ma’mun akasema, “Vizuri, kama mambo yako hivi, basi mfunge gerezani, pokonya mali zake na kisha muue.”

Ahmad aliondoka, akamuweka Ali Ibn Jahm gerezani na akamshikilia akiwa hai mpaka hasira ya Ma’mun ilipokwisha. Ma’mun alimsamehe Ali Ibn Jahm na akamsifu waziri kwa mwenendo wake na akampandisha cheo na hadhi. (Lataaif al-Tawaaif, uk. 98)

 • 1. Al-kafi, juz. 2, uk. 167
 • 2. Daastan-ha Wa Panda-ha. Juz. 1 uk. 134, Raudhah al-Kafi, uk. 85.
 • 3. Namunah-e-Ma’arif, Juz. 1, uk. 218, Farajun Ba’ad al-shiddah.

6) Matumaini

Mwenyezi Mungu Mwenye hikma, amesema: “Waache ili wale na kufurahi na ili matumaini yawadanganye, kwani punde watajua” (Qur’ani tukufu, Suratul Hijr (15): 3)

Imam Ali (a.s) anasema: “Kamwe matumaini huwa hayaishi.” (Ghurar al- Hikam, uk. 629)

Maelezo mafupi:

Watu ambao hawaridhiki na kile walichonacho katika ulimwengu huu na wanatamani vitu wasivyokuwa navyo wataendelea kuyafukuzia matarajio makubwa na ndoto kubwa. Mtu anayedhani kuwa mara zote ataendelea kuwa kijana, huwa hajali kifo na huwa na ndoto kubwa.

Wengi wa watakaoingia motoni watakuwa wamekwenda huko kama matokeo ya uahirishaji wao. Badala ya kuridhika na kile walichokuwa nacho, waliendelea kuahirisha kusafisha roho zao na kulipa madeni yao kwa ajili ya baadae na kuakhirisha matendo yao ya ibada mpaka watakapokuwa wazee.

Kwa hakika mtu anapaswa kupunguza matumaini, na ndoto zake, kufanya kila kitendo kwa wakati na muda wake, na kuepuka kuiamini “kesho,” jambo lisilojulikana na lisilokuwa na uhakika. 1

1. Isa (A.S) Na Mkulima

Imesimuliwa kwamba wakati fulani, Nabii Isa ibn Maryam (a.s) alikuwa amekaa akimtizama mkulima ambaye kwa kutumia koleo alikuwa aki- fanya kazi kwa bidii shambani mwake.

Hapo hapo Nabii Isa alimuomba Mwenyezi Mungu: “Ewe Mola! Muondolee matumaini na matarajio” Ghafla yule mtu alitupa koleo lake pembeni na akakaa chini kwenye kona.

“Ewe Mola! Mrejeshee matumaini na matarajio yake” Nabii Isa (a.s) alimuomba tena Mwenyezi Mungu. Yule mtu aliinuka kutoka kwenye sehehmu yake, akanyanyua kolea na akaanza kufanya kazi tena. Isa (a.s) alimfuata na akauliza, “Kwa nini ulifanya hivyo?” Mkulima alijibu, “Nilijisemea: ‘Wewe ni mzee ambaye maisha yake yamekaribia mwisho, ni kiasi gani unataka kufanya kazi na kujitaabisha?” Hivyo nikatupa koleo pembeni na nikakaa chini kwenye kona. Lakini baada ya muda, nilijise- mea: “Kwa nini hufanyi kazi? Bado uko hai na unahitaji riziki,” na hivyo nikachukua koleo nikarudi kwenye kazi yangu.” 2

2. Hajjaaj Na Muuza Maziwa

Siku moja Hajjaaj Ibn Yusuf Thaqafi, dikteta katili na waziri wa khalifa wa ukoo wa Abbas, Abd al-Malik ibn Marwaan alikuwa akitembea sokoni ali- poshuhudia muuza maziwa akiongea peke yake. Akiwa amesimama kwenye kona, Hajjaaj alimsikia akisema: “Nikiuza, maziwa haya, nitapa- ta kipato kizuri. Nitaweka akiba kutokana na mauzo haya na mauzo yajayo mpaka nitakapokuwa na fedha za kutosha kununulia mbuzi. Kisha nita- nunua kondoo jike na kutumia maziwa yake kuongeza mtaji wangu na ndani ya miaka michache, nitakuwa mtu tajiri ninayemiliki mbuzi wengi, ngo’mbe na aseti (nyinginezo).

Kisha nitamposa binti wa Hajjaaj, ambapo baada ya hapo nitakuwa mtu muhimu. Na ikiwa wakati wowote binti wa Hajjaaj ataonyesha uasi (kutotii) nitampiga teke vikubwa kiasi cha kuvunja mbavu zake.” Aliposema hivi alipiga teke kwa mguu wake ambao kwa bahati mbaya uligonga dumu la maziwa, na hivyo kumwaga vyote vilivyokuwemo. Hajjaaj alitokeza na akaamuru askari wake wawili kum- lazimisha muuza maziwa alale chini na kumcharaza fimbo mia moja.

Muuza maziwa alilalamika, “Lakini ni kwa kosa gani unaniadhibu?” Hajjaaj alijibu, “Je hukusema kwamba kama ungemuoa binti yangu ungempiga teke vikubwa kiasi cha kumvunja mbavu zake? Sasa, kama adhabu ya teke hilo, lazima uonje fimbo mia moja.”

3. Hamu Ya Kufa Shahidi

Amr bin Jamuh, mkazi wa Madinah na kutoka katika kabila la Khazraj, alikuwa ni mtu mkarimu na mwema. Kwa mara ya kwanza watu wa kabi- la la Khazraj walipofika kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) (Mtume) alitaka kujua mtu aliyekuwa kiongozi wa kabila lao. Walimjulisha kuwa alikuwa ni mtu aliyejulikana kwa jina la Jadd Ibn Qais, mtu aliyekuwa na asili ya ubahili.

Mtume (s.a.w.w) alisema: “Chifu wenu anapaswa kuwa A’mr Ibn Jamuh, mtu mweupe, mwenye nywele za mviringo.” Amr alikuwa mlemavu katika mguu wake mmoja na kwa mujibu wa sheria za Kiislamu alisamehewa kushiriki katika jihad. Alikuwa na watoto wanne wa kiume na muda wa vita vya Uhud ulipowadia, wote walijiandaa kupigana. “Lazima mimi pia nije na kupata (heshima ya) kufa shahidi, alisema Amr kwa tash- wishi.” Lakini watoto wake wa kiume walimkataza na walisema, “Baba tunakwenda vitani. Kaa nyumbani kwani sio wajibu kwako kupigana.”

Baba yule mzee alikataa kubadili mawazo na akasisitiza kushiriki katika vita. Watoto wake waliwakusanya jamaa zao kwa juhudi ya kumfanya abadilishe mawazo, lakini bila mafanikio. Amr (yule baba) alimuendea Mtukufu Mtume (saw) na akamlalamikia: “Ninatamani sana kupata shaha- da. Kwa nini watoto wangu wananizuia kwenda kupigana jihadi na kupata shahada katika njia ya Allah?”

Mtukufu Mtume (saw) akawaambia watoto wake: “Mtu huyu anatafuta kupata shahada. Na ingawa sio wajibu kwake kupigana, haikatazwi kwake kufanya hivyo.”

Akiwa mwenye furaha kubwa, Amr alichukuwa silaha na kuelekea kwenye mapambano.

Wakati wa mapambano, watoto wake walimuangalia wakati akiwa anapambana kwa ushujaa akijitosa kwenye moyo wa safu ya maadui, akipigana kishujaa, mpaka hatimaye akauliwa shahidi.

Kabla hajaondoka kwenda uwanja wa mapambano, aliomba: “Ee Allah! Nipe mimi shahada na usinirudishe nyumbani kwangu.” Mtukufu Mtume (saw) alisema kwamba maombi yake yalijibiwa. Hatimaye Amri alizikwa kwenye makaburi ya mashahidi wa Uhud. 3

4. Hali Ya Fedheha Na Aibu Ya Ju’dah

Imamu Hasan alikuwa mwenye sura ya kupendeza, mwenye uvumilivu mkubwa na mkarimu, na alikuwa mpole na mwenye moyo wa mapenzi kwa jamaa wa familia yake. Baada ya kuuawa shahidi kwa Imamu Ali (as), kwa muda wa miaka kumi Mua’wiyah, alianzisha mahubiri ya chuki, udanganyifu na uadui kuhusiana na Imamu Hasan (as). Alikusudia kumdhuru Imamu (as) katika nyakati mbalimbali, lakini hakufanikiwa kitu chochote. Kwa hiyo aliamua kumtumia mke wa Imamu Ju’dah, bint wa Asha’th Ibn Qais, ili ampe sumu.

Mua’wiyah alimshawishi kwa kumuahidi kwamba kama akimpa sumu Imamu Hasan Ibn Ali, atampa dirham elfu mia moja, na kwa nyongeza, atamuozesha kwa mtoto wake Yazid. Kwa matumaini ya kupata mali na msukumo wa wa kuwa mke wa Yazid, Ju’dah alikubali kutekeleza ombi lake. Mua’wiyah alimpa sumu ile ambayo aliipata kutoka kwa mfalme wa Urumi.

Siku ya joto kali sana, Imamu Hasan (as) alifunga (saumu). Wakati wa kufuturu, Imamu alikuwa na kiu kali mno, Ju’dah alimletea maziwa ambayo ameyachanganya na sumu.

Mara tu Imamu alipokunywa maziwa yale, alihisi athari ya sumu. Alitambua kilichotokea na akaguta kwa sauti: Inna lillahi wa inna ilaihi raajiu’n.

Baada ya kumshukuru Mungu kwamba sasa ataondoka na kutoka kwenye ulimwenu huu wa mpito kwenda kwenye ulimwengu wa milele, alimgeukia Ju’dah na akasema: “Ewe adui wa Mwenyezi Mungu! Umeniuwa, Mungu naakuuwe wewe! Kwa jina la Mungu, hutakuja pata hata kitu kidogo ambacho kwamba unakitagemea na kukitamani. Mtu yule amekudanganya. Mungu akufedheheshe wewe na yeye pia kwa njia za adhabu Zake.”

Uvumilivu wa Imamu Hasan (as) unaweza kupimwa kutokana na ukweli kwamba wakati Imamu Husein (as) alipotaka kujua jina la muuaji wake, Imamu Hasan (as) alikataa kufichua jina la Ju’dah.

Kwa mujibu wa hadithi moja, kwa siku mbili (na kwa mujibu wa nyingine, kwa siku arobaini), Imamu aliteseka kutokana na athari mbaya za sumu ile, mpaka hatimaye tarehe 28 Safar, 50 A.H., aliuaga ulimwengu huu yakini- fu akiwa na umri wa miaka 48.

Amma kwa Ju’dah alibeba matumaini yake na matamanio yake hadi kwenye kaburi lake kwani Mua’wiyah alihoji kwamba kama hakuweza kuwa muaminifu kwa Hasan Ibn Ali (as), vipi atategemewa kuwa kuwa muaminifu kwa Yazid; na hivyo alikataa kutekeleza chochote katika ahadi zake. Na kwa hali hiyo, alikufa katika hali ya fedheha na aibu. 4

5. Mughirah Awa Gavana Wa Kufa

Mughirah Ibn Shu’bah, ambaye alikuwa kwa asili ni mwenyeji wa Taaif na ameingia Uislamu katika mwaka wa 5 A.H. alikuwa mlaghai mkubwa, muovu na mwenye kupenda madaraka.

Wakati aliposikia kwamba Mua’wiyah ameandaa kwa ajili ya Ziyaad Ibn Abihi ili aishi Kufah ili baadae achukue ugavana wa Kufah kutoka kwake (Mughirah), upesi sana aliteuwa naibu katika Kufah na akaondoka kwenda Sham kukutana na Mua’wiyah.

Alionyesha matakwa yake ya kuhamish- wa Kufah, akimueleza Mua’wiyah:

“Kwa vile sasa nimekuwa mtu mzima, nakuomba utenge vijiji vichache vya Qirqisiya chini ya mamlaka yangu, ili mwenyewe niweze kujipumzisha.”

Mua’wiyah alitambua kwamba mmoja wa wapinzani wake, kwa jina la Qais, anaishi Qirqisiya na kama Mughirah angekwenda huko anaweza kuunda umoja naye dhidi ya Mua’wiyah.

“Tunakuhitaji na lazima ubakie Kufah,” alisema Mua’wiyah.

Mughiraha alikataa ofa hiyo, lakini msisitizo wa Mua’wiyah ulimshawishi na kusalimu amri. Ilikuwa ni usiku wa manane wakati Mughirah aliporudi Kufah. Mara moja aliamuru washirika wake kumtoa Ziyad Ibn Abihi na kumpeleka Sham.

Baada ya muda, Mua’wiyah alimteuwa Sa’id Ibn A’as kama gavana wa Kufa badala ya Mughirah, ambaye alimshawishi Yazid (mtoto wa Mua’wiyah) kwa kumuambia:

“Kwanini Mua’wiyah hafikirii kuhusu wewe? Ni muhimu kwamba aku- teuwa wewe kama mrithi wake na mfalme mteule!”

Yazid aliona rai hiyo kuwa yenye kuvutia kiasi kwamba aliiwasilisha kwa baba yake, Mua’wiyah, pamoja na kuungwa mkono na Mughirah, hati- maye Yazid alitangazwa mrithi wa Mua’wiyah.

Wakati huohuo Mua’wiyah alimteuwa Amr A’as kama gavana wa Misr, ambapo aliiweka Kufah chini ya mtoto wake Abdullah Ibn A’as.

Wakati Mughiraha alipolifahamu hili, alimuonya Mua’wiyah, “Kwa kiten- do hiki, je, hukujiweka wewe mwenyewe katikati ya midomo ya simba wawili?”

Akiwa amepata maelezo ya ujumbe huu, Mua’wiyah alimuondoa Abdullah kutoka Kufah na mara nyingine akamuweka Mughirah kwenye uongozi wa Kufah.

Hivyo, kwa njama mbili za ujanja (Yazid kuurithi ukhalifa, na hila ya ‘katikati ya midomo ya simba wawili’), Mughirah akawa gavana wa Kufah. Baada ya kutawala kwa muda wa miaka saba namiezi michache, alikufa kwa ugonjwa wa tauni akiwa na umri wa miaka arubaini na tisa.5

 • 1. Ilyas al-Quluub, uk. 167.
 • 2. Namunah-e-Ma’arif, Juz.1, uk. 298, Majmua’e Warran.
 • 3. Daastaan – ha-e-Ustaad, Jz. 1. uk. 48
 • 4. Muntahal Aa’maal, Jz. 1, uk. 231.
 • 5. Paighambar Wa Yaraan, Jz. 5, uk. 272-275.

7) Uaminifu

Allah Mwenye Hikma, amesema:

“Hakika Allah anawaamuruni mzirudishe amana kwa wenyewe…1

Imamu Baqir (as) alisema: “Kama muuaji wa Imamu Ali (as) ataweka amana katika miliki yangu, kwa hakika nitairudisha kwake.2

Maelezo mafupi:

Kama kitu chochote kinawekwa amana kwa mtu, kulinda usalama wa kitu hicho ni wajibu, na khiana kuhusiana nacho kumekatazwa, bila kujali kama mwenyewe ni mu’umin au kafiri.

Mtu muaminifu, kwa matokeo ya kulinda salama mali za watu, anakuwa mwenye kunufaika kwa rehema na neema ya Mungu.

Mtu ambaye si muaminifu kwa amana za watu anaweza kufananishwa na mwizi na Mungu humvisha mtu kama huyo kwa umasikini na ufukara.

Moja ya alama za imani kamili ni kuwa muaminifu kwenye amana za watu.

Amana inaweza kuwa katika muundo wa fedha, vitu au hata siri, Shetani humpotosha mtu muaminifu kwa kumsababisha yeye kuwa mwenye khi- ana kwenye amana alizowekewa na watu.

1. Uaminifu Wa Umm Salamah

Wakati Imamu Ali (as) alipoamua kuhamia Iraq na kuishi huko, alimk- abidhi barua zake na hati kwa Umm Salamah, ambaye baadae alizitoa na kumpa Imamu Hasan (as) wakati aliporudi Madina.

Katika hali kama hiyo, wakati Imamu Husein (as) alipoondoka kuelekea Iraq, yeye pia aliweka barua zake na hati katika hifadhi ya Umm Salamah pamoja na maelekezo kwamba aje kumpa mtoto wake mkubwa wakati atakapozihitaji kutoka kwake.

Baada ya kuuawa shahidi kwa Imamu Husein (as), Imamu Sajjad (as) alirudi Madina na Umm Salama akamk- abidhi hati zile.

Umar, mtoto wa Umm Salamah, anasimulia: Mama yangu alisema: ‘Siku moja Mtukufu Mtume (saw), akifuatana na Imamu Ali (as), walikuja nyumbani kwangu na akaniomba nimpatie ngozi ya kondoo. Baada ya kumpatia ngozi hiyo, aliandika vitu fulani katika ngozi hiyo na kuirudisha kwangu pamoja na maelekezo: ‘Yeyote yule atakayetaka amana hii kutoka kwako baada ya kutaja alama hizi, mkabidhi amana hii.’”

Kiasi muda ulivyopita, Mtukufu Mtume alifariki dunia. Muda ukapita na Imamu Ali (as) akawa Khalifa na bado hakuna aliyekuja kudai amana hii.

Umar anaendelea kusema:“Siku ambayo watu walikula kiapo cha utii kwa Ali (as), nilikuwa nimekaa miongoni mwao. Wakati anashuka kutoka kwenye mimbari, macho ya Imamu yakaangukia kwangu ambapo alisema: “Omba ruhusa kutoka kwa mama yako nataka kuonana naye.

“Niliharakisha kwenda kwa mama yangu na mara tu nilipomjulisha ombi la Imamu (as), alitamka kwamba alikuwa akiingoje siku hiyo.

“Imamu (as) aliingia na akamuomba Umm Salamah amkabidhi amana ambayo ina alama fulani. Mama alisimama na kutoa kijisanduku kidogo kutoka ndani ya sanduku kubwa na akamkabidhi. Kisha (mama) alinigeukia na kunishauri: ‘Usije ukamtupa Ali (as), kwani hakuna mwingine kama yeye aliye Imamu wa haki baada ya Mtukufu Mtume (saw).” 3

2. Khiana Ya Muuza Duka

Wakati wa utawala wa Azud al-Daulah Dailami, mgeni mmoja alikuja Baghdad akitaka kuuza kidani chenye thamani ya dinari elfu moja, lakini hakuweza kupata mnunuzi wa kukinunua. Kwa vile alikusudia kusafiri hadi Makka, alianza kutafuta mtu muaminifu ambaye angeweza kuhifadhi salama kidani chake.

Watu wakamuelekeza kwa muuza duka ambaye anajulikana kwa uchamungu wake. Yule mgeni akaweka kidani chake katika dhamana ya muuza duka na akaenda zake Makka.

Wakati aliporudi kutoka Makka, alimuendea muuza duka na akampa zawa- di ambazo amezileta. Kwa mshituko mkubwa wa yule mgeni, muuza duka akajifanya kama vile hamjui na akakataa kuwa na kitu chochote kinachomhusu yeye. Vurugu ikatokea kati yao, matokeo yake ambayo watu walikusanyika na kumtupa mtu yule (mgeni) nje ya duka la ‘mchamungu!’ Yule mtu akawa anamfuata muuza duka yule mara nyingi kudai kidani chake, lakini aliambulia matusi na kashifa.

Mtu mmoja alimshauri kumlalamikia kwa Mfalme Azud al-Daulah Dailami. Akiujali ushauri ule, mtu yule akaandika barua kwa Mfalme, ambaye alijibu:

“Kwa muda wa siku tatu, kaa ukingojea mlangoni kwa muuza duka. Siku ya nne, nitapita pale dukani, na wakati nitakapokusalimu itikia salamu zangu. Siku ifuatayo omba kidani chako kwa muuza duka na kisha nijulishe kitakachotokea.”

Mtu yule akafanya kama alivyoelekezwa. Siku ya nne, Mfalme kwa mbwembwe na hadhi kubwa, alipita dukani pale na punde tu macho yake yalipoangukia kwa mtu yule kutoka Baghdad, alimsalimu. Yule mtu akarudisha salamu. Mfalme, akionesha heshima kubwa na taadhima, alianza kulalamika: “Umekuja kutoka Baghdad lakini hukuona kuwa yafaa kunifanyia heshima ya fursa ya kunitembelea ili nikupatie malazi na kukukirimu.” Yule mgeni akaomba radhi kwa kutomjulisha mfalme kuwasili kwake. Wakati wote, muuza duka na watu waliomzunguka, waliangalia kwa mshangao, wakistaajabu mtu yule ni nani ambaye anaheshimiwa kiasi kile na mfalme. Yule muuza duka akaanza kuhofia maisha yake.

Mara msafara wa mfalme ulipopita, yule muuza duka akamgeukia yule mgeni na akasema: “Ndugu, ni lini hasa ulikuja kuweka kidani chako kwangu? Je, kina alama yoyote? Ngoja niangalie tena, huenda pengine sikuweza kukiona.” Yule mgeni akaelezea kilivyo kidani chake kwa muuza duka, baada ya kutafuta kwa muda mchache alikiona. Alimkabidhi yule mgeni na akasema: “Allah swt. anafahamu ukweli kwamba ilitoka tu akilini mwangu.”

Alipowasili mbele ya mfalme, yule mgeni alielezea kisa chote kwake. Mfalme aliamuru muuza duka akamatwe, alimvalisha kidani kile shingoni mwake, na akampeleka kwenye nyumba ya kunyongea watu. Kisha aka- muuru tangazo lifuatalo kutangazwa katika mji wote:

“Hiyo ni adhabu kwa yeyote anayechukua umiliki wa amana na kisha akakana kuwa nayo. Enyi watu! Chukueni tahadhari kutoka kwenye tukio hili!”

Kisha Mfalme akarudisha kidani kile kwa yule mgeni kutoka Baghdad na akampeleka mjini kwake.4

3. Kuwa Muaminifu Wakati Mtu Akikuamini

Abdullah Ibn Sinaan anasema: “Nilimuendea Imamu Sadiq (as) msikitini wakati ambapo alimaliza kusali sala yake ya Alasiri na alikuwa amekaa chini akielekea Qibla. Nikamuuliza:

‘Baadhi ya magavana na watawala watunaona sisi kuwa waaminifu na kuweka mali zao kwetu, lakini wakati huohuo hawalipi ‘khums’ yake. Je turudishe pesa zao au tuziweke kwa ajili ya matumizi yetu?”

Imamu (as) alijibu mara tatu: “Kwa jina la Mola wa Ka’bah! Hata kama Ibn Muljam, muuwaji wa baba yangu Ali (as) angeweka kitu katika amana kwangu, ningekirudisha kwake wakati wowote akikihitaji.” 5

4. Mchungaji Na Kondoo Wa Myahudi

Katika mwaka wa 7 A.H., Mtukufu Mtume (saw) na jeshi la askari elfu moja na mia sita, walitoka kwenda kuiteka ngome ya Khaibar, ambayo ilikuwa takriban maili 96 kutoka Madina. Askari wa Kiislamu walikuwa wameweka kambi katika jangwa linaloizunguka Khaibar kwa muda lakini utekeji wa ngome ukabakia kwa muda mfupi.

Wakati wa kipindi hiki, walijikuta wenyewe katika wakati mgumu kuhusiana na chakula na maji. Ukosefu wa chakula na njaa kali iliwalazimisha kula wanyama kama punda na farasi, ambao nyama yao hairuhusiwi kuliwa na Uislamu.

Katika mazingira haya, mchungaji mweusi, ambaye anachunga kondoo wa Mayahudi, aliwasili katika hadhara ya Mtukufu Mtume (saw). Alisilimu na kisha akamuambia Mtukufu Mtume: “Hawa kondoo ni za Myahudi kwa hiyo sasa nawakabidhi kwako.”

Mtukufu Mtume (saw) akajibu kwa uwazi: “Kondoo hawa wamewekwa kwenye umiliki wako kama amana, na katika dini yetu imekatazwa kuwa na khiyana kwenye amana ya mtu. Ni wajibu juu yako kuwapeleka kondoo hawa mpaka kwenye mlango wa ngome na kuwarejesha kwa wenyewe.”

Kwa kutekeleza amri hiyo, yule mchungaji aliwakabidhi kondoo wale kwa wenyewe kisha akarudi na kujiunga na jeshi la Waislamu.6

5. Mali Zilizowekwa Kwa Mtukufu Mtume (Saw)

Wakati Mtukufu Mtume (saw) alipohama kutoka Makka kwenda Madina, alimuacha Amirul-Mu’minin mjini Makka ili kwamba aweze kurudisha kwa wenyewe mali zilizowekwa amana kwa Mtume.

Handhalah Ibn Sufiyaan alimuelekeza Umair ibnWa’ail kwenda kwa Ali na akamuambie: “Nimeweka mithqal mia moja za dhahabu kwa Mtukufu Mtume (saw), kwa vile amekimbia kwenda Madina na wewe ni mwakilishi wake hapa, tafadhali nikabidhi mali yangu.” Handhalah aliongeza kwamba kama Ali akitaka ushahidi kuthibitisha madai haya, Makuraish wote watathibitisha ukweli wa madai ya Umair.

Mwanzoni, Umair alisita, lakini Handhalah alimshawishi kwa kumzawadia baadhi ya dhahabu na kidani cha Hind, mke wa Abu Sufiyaan. Umair alik- wenda kwa Ali (as) na akatoa madai hayo na kuongeza kwamba Abu Jahl, Ikramah, Uqbah, Abu Sufiyaan na Handhalah watashuhudia kwa ajili yake.

Imamu (as) akasema: “Ulaghai wao naujifunge kwao wenyewe.” Kisha akamuambia alete mashahidi wake karibu na Ka’bah. Wakati wote walipowasili, alianza kumsaili kila mmoja binafsi na mbalimbali, kuhusu mali iliyowekwa kwenye amana.

“Ilikuwa ni wakati gani ulipoweka mali yako kwa Muhammad (saw)?” Alimuuliza Umair kwanza.

“Ilikuwa ni asubuhi wakati nilipompa dhahabu hiyo na akamkabidhi mtumwa wake.” Alijibu Umair.

Imamu (as) akamuuliza Abu Jahl swali hilo hilo. Akajibu: “Mimi sijui.”

Wakati Abu Sufiyaan alipoulizwa, alisema: “Ilikuwa wakati wa machweo ya jua na aliiweka kwenye mikono yake ya nguo.” Wakati Handhalah alipoulizwa, alijibu: “Aliichukuwa amana hiyo wakati wa Adhuhr na kuiweka mbele yake.”

Wakati Uqbah alipoulizwa, alijbu: “Ilikuwa wakati wa Alasir Mtume alipochukuwa amana hiyo katika mikono yake mwenyewe na akaichukuwa nyumbani kwake.”

Na mwisho, wakati Imamu Ali (as) alipomuuliza Ikrimah, alijibu: “Ilikuwa kweupe na asubuhi mapema wakati Muhammad (saw) alipochukuwa amana hiyo na kuipeleka nyumbani kwa Fatimah (as).”

Kisha Imamu (as) aliwajulisha kupingana kwa maelezo yao na hivyo ulaghai wao ukawa dhahiri. Kisha akamgeukia Umair, alimuuliza: “Kwa nini wakati uliposema uwongo, ulionekena mwenye wasiwasi na uso wako ukapauka?” Umair akajibu: “Kwa jina la Mola wa Ka’bah! Sijaweka amana kitu chochote kwa Muhammad (saw). Ilikuwa ulaghai, Handhalah alinipa hongo, kidani hiki hapa, ni cha Hind, na jina lake limeandikwa juu yake, ni moja ya vitu vilivyowasilishwa kwangu kama hongo.” 7

 • 1. Qur’ani Tukufu 4:58
 • 2. Al-Kafi, Jz. 5, uk. 133
 • 3. Payghambar Wa Yaaraan, Jz. 1, uk. 275; Bihaar al-Anwaar Jz. 6, uk. 942.
 • 4. Pand-e-Taarikh, Jz. 1, uk. 202; Mustraf, Jz. 1, uk. 118.
 • 5. Namunah-e-Ma’arif, Jz. 1, uk. 354; Bihaar al-Anwaar, Jz. 15, uk. 149
 • 6. Daastan-ha Wa Pand-ha, Jz. 8, uk. 114; Sirah Ibn Hisham, Jz. 3, uk. 344.
 • 7. Rahnamaa-e-Sa’adat, Jz. 2, uk. 436; Naasikh al-Tawaarikh – Amirul- Mu’minin, uk. 676.

8) Mtihani

Allaha, Mwingi wa Hikma anasema:

الَّذِي خَلَقَ الْمَوْتَ وَالْحَيَاةَ لِيَبْلُوَكُمْ أَيُّكُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْغَفُورُ {2}

“Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha.”(Quran, 67:2)

Imamu Sajjad (as) amesema: “Allaha aliumba ulimwengi na wakazi wake ili kuwapa mtihani ndani yake.”1

Maelezo Mafupi:

Mtu anakabiliana na aina mbalimbali za mitihani katika ulimengu. Anajaribiwa kwa hofu, njaa, maradhi, kifo cha mpenzi wake wa karibu, hali mbaya ya kifedha, shutuma za uwongo, jirani muovu, na kadhalika na kadhalika.

Kwa vile ulimwengu ni sehemu ya matendo na mitihani, waliobarikiwa na wenye furaha ni wale ambao hawashindwi katika hatua yoyote ya maisha. Katika wakati mmoja, mtu anajaribiwa kwa njia ya utajiri na katika wakati mwingine kwa ufukara. Hupata mafanikio kwa kushukuru wakati wa ukwasi na uvumilivu wakati wa umasikini.

Kila mtu, bila tofauti yoyote, anapasika kwenye majaribio na mitihani ambayo huwa tofauti tu katika ‘aina’ na ‘uzito’ wake. Je, huoni jinsi baadhi ya watu ambao wamezoea kujigamba, hupoteza uvumilivu wao na kushindwa kwa unyonge katika mapambano ya mitihani?

1. Harun Makki

Sahl Khorasani alimuendea Imamu Sadiq (as) na akalalamika: “Kwa nini licha ya haki kuwa upande wako, husimami ukapigana? Hivi sasa kuna Mashia wako mia moja elfu, ambao ukiwaamrisha, mara moja wata- chomoa panga zao kwa ajili ya mapambano.” Imamu (as), kwa nia ya kumpa jibu la vitendo, aliangiza tanuru liwashwe. Kisha akamuamuru Sahl arukie ndani ya moto ule.

Sahl akasema: “Ewe Bwana wangu! Allah akun- yeshee Rehma na neema Zake! Usiniweke ndani ya moto. Nayafuta maneno yangu na vilevile nakuomba uondoe amri yako.”

Wakati uleule, mmoja wa wafuasi waaminifu wa Imamu (as), kwa jina la Harun Makki, aliwasili.

Alivyoingia tu Imamu (as) alimuambia kuvua viatu vyake na atembee ndani ya tanuru lile lenye moto. Mara tu Harun ali- posikia amri ya Imamu (as), aliingia kwenye lile tanuru na kukaa katikati ya moto unaowaka.

Kisha Imamu (as) alimgeukia Sahl na akaanza kumuelezea kwa mukhtasari kuhusu mazingira yaliopo katika Khorosan, kama vile alikuwa kule akishuhudia matukio yakitokea.

Baada ya muda, alimuambia Sahl: “Simama na tazama ndani ya tanuru.” Wakati Sahl alipochungulia, alimuona Harun amekaa akiwa amekunja miguu yake bila madhara ndani ya tanuru, akiwa amezungukwa na moto mkali. “Kuna watu wangapi kama hawa waliopo Khorasan?” Imamu (as) alimuuliza Sahl. “Kwa jina la Allah! Hakuna hata mtu mmoja kama Harun Makki katika eneo la Khorasan.” Alijibu Sahl.

Kisha Imamu (as) alieleza: “Sitasimama kupigana wakati sina hata wafuasi waaminifu watano. (Na kumbuka) tunaelewa sana ni wakati gani tutakaosi- mama na kupigana.”2

2. Bahlul Afanikiwa!

Harun Al-Rashid, Khalifa wa Bani Abbas, alitaka kuajiri jaji katika mji wa Baghdad. Baada ya kushauriana na wajumbe wake wa baraza, ilikubaliwa na wote pamoja kwamba hakuna mwingine ila Bahlul ndiye mwenye sifa za sawasawa kwa nafasi hiyo.

Bahlul aliitwa na nafasi ile akapewa yeye. Lakini Bahlul alikataa kukubali, akisema kwamba hafai kwa nafasi hiyo wala hana uwezo wa kubeba juku- mu hilo. Harun akasema: “Wakazi wote wa Baghdad wanaona kwamba hakuna mwingine isipokuwa wewe ndio unafaa kwa nafasi hii na wewe unakataa.”

Bahlul akaeleza: “Mimi mwenyewe najifahamu kuliko yeyote katika ninyi. Chochote nilichoeleza ima ni cha kweli au ni cha uwongo. Kama sababu niliyotoa ni ya kweli, basi itakuwa sio sahihi kwa mimi kuchukua wadhifa huu wa jaji wakati sina uwezo. Kwa upande mwingine, kama nimekudan- ganya, basi mwongo hastahili kuchukua wadhiufa huu.”

Lakini Harun akasisitiza kwamba Bahalul achukue jukumu hilo. Bahlul aliomba apewe muda wa usiku mmoja ili atafakari juu ya suala hilo. Asubuhi iliyofuatia, Bahlul alijifanya mwendawazimu na akaweka vitu katikati ya miguu yake akakimbia mitaani na katika masoko ya Baghdad, akipiga makele: “Wekeni nafasi kwa ajili ya punda wangu na kaeni kando asije akawapiga mateke.”

Mara tu watu walipoona mwendo wake huu wa kuchekesha, walisema kwamba Bahlul amekuwa mwendawazimu. Wakati Harun Al-Rashid alipojulishwa kuhusu hili, alisema: “Bahlul hakuwa mwenda wazimu; bali ameokoa dini yake na amekwepa makucha yetu.

Amelibuni hili ili kujizuia kutokana na kuingilia katika mambo na haki za watu.”3

3. Abu Hurairah Alishindwa!

Abu Hurairah alisilimu katika mwaka wa 8 A.H. Kwa hiyo alikuwa na Mtukufu Mtume (saw) kwa muda wa miaka miwili tu. Alikufa katika mwaka wa 59 A.H. akiwa na umri wa miaka 78. Abu Hurairah alichukuliwa kama mmoja wa sahaba wa Mtukufu Mtume (saw). Hata hivyo, alishindwa kunufaika kutokana na uswahiba huo mtukufu wa Mtume (saw) na kujikinga na kuboronga na makosa. Kinyume chake, aliitumia vibaya nafasi yake na akijiuza mwenyewe kwa ajili ya anasa za dunia hii.

Abu Hurairah alizoea kughushi hadithi na kuzihusisha na Mtukufu Mtume (saw) ili kupata utajiri. Wakati wa kwanza hili lilipotokea, Khalifa wa pili alimkataza kusimulia hadithi; katika tukio la pili, Khalifa alimuadhibu kwa kumpiga viboko, na katika tukio la tatu, alimfukuza kutoka mjini.

Wakati A’laa, gavana wa Bahrain alipofariki katika mwaka wa 21 A.H., Umar alimteua Abu Hurairah kama gavana kuchukuwa nafasi ya A’laa. Lakini kwa muda mfupi kiasi kikubwa cha pesa (dinari elfu mia nne) ziliingia mifukoni mwa Abu Hurairah. Matokeo yake Umar alimfukuza kutoka kwenye nafasi yake.

Mua’wiyah alikuwa akiwalazimisha baadhi ya masahaba na wafuasi (wa masahaba) kubuni hadith dhidi ya Amirul-Mu’minin, Ali (as) na mmoja wa watu muhimu katika kitendo hiki alikuwa ni Abu Hurairah. Wakati fulani Asbagh Ibn Nubata alimuambia Abu Hurairah: “Kinyume na mafundisho ya Mtukufu Mtume (saw) umewafanya maadui wa Ali (as) kuwa marafiki zako na kuwa na uadui kwake.” Aliposikia hili, Abu Hurairah alivuta punzi kwa ndani sana na akjisemea tu: “Inna lillahi wa inna ilahi raajiu’n.”

Uovu mwingine uliofanywa na Abu Hurairah ulikuwa kwamba, ili kupata utajiri kutoka kwa Mua’wiyah, alifuatana na Mua’wiyah mpaka kwenye msikiti wa Kufah na akapiga paji lake la uso mara nyingi mbele ya mku- sanyiko wa watu, kisha akasema: “Enye watu wa Iraq! Je, mnadhani mimi naweza kumhusisha na uwongo Mtukufu Mtume (saw) na hivyo nijiun- guze mwenyewe katika moto wa Jahannam? Kwa jina la Allah! Nimemsikia Mtukufu Mtume (saw) akisema: ‘Kwa kila Mtume kuna sehemu takatifu (aliyowekewa) na ya kwangu iko mjini Madina, kati ya milima ya E’er na Thaur. Yeyote atakayeanzisha uzushi (bid’a) katika sehemu yangu takatifu, laana ya Allah, malaika na watu wote iwe juu yake.’ Allah ni shahidi yangu kwamba Ali alianzisha uzushi ndani ya sehemu takatifu ya Mtukufu Mtume (saw).” (Allah aliepushilie mbali).

Mua’wiyah alifurahia sana kauli hii kiasi kwamba alimzawadia Abu Hurairah na akamfanya mtawala wa Madina.4

4. Ibrahim (As) Na Muhanga Wa Isma’il (As)

Allah swt. alimuamuru Nabii Ibrahi (as) kumtoa muhanga mwanawe Ismail (as). Alifanya hivyi ili kupima subira ya Ibrahim na utii wake kwa Allah. Kama Ibrahim (as) atafudhu mtihani huu, atakuwa ameonesha kustahiki kwake juu ya baraka na neema ya Allah.

Akiwa amepewa mtoto baada ya miaka mingi ya upweke bila mtoto, aliamriwa na Allah kumtoa muhanga kwa mikono yake mwenyewe kipenzi chake ambaye amekua na kufikia umri wa miaka 13.

Ibarahim (as) akamuambia Ismail (as): “Ewe mwanangu mpendwa! Nimeota nikiwa nakutoa muhanga; unasemaje kuhusu hili?”

“Mpendwa baba! Fanya kama ulivyoamrishwa, na insha-Allah, utanikuta mimi miongoni mwa walio imara.” Alijibu Ismail (as).

Kisha, akaimarisha azimio la baba yake kwa kumshauri: Baba, kifo kinau- ma sana na ninakiogopa sana kiasi kwamba kukifikiria tu hunifanya nisumbuke na kunihuzunisha, hivyobasi, ifunge mikono na miguu yangu kwa nguvu, nisije nikajipiga piga nayo wakati koo langu linakatwa na hivyo kupunguza malipo yaliyokadiriwa kwa ajili yangu. Na kwa nyongeza, kinoe kisu chako kiwe kikali ili kwamba kwa haraka niwekwe kwenye amani. Vilevile, niweke katika hali ambayo uso wangu uelekee chini ya ardhi na sio juu ya mashavu yangu, kwani naogopa kama macho yako yatatazama uso wangu, unaweza ukapatwa na huruma na kukuzuia wewe kutii amri ya Allah swt. Vua nguo zako ili zisipakwe kwa damu yangu na mama asiione damu yangu.

Kama ikiwezekana, mpelekee mama nguo zangu; huwenda zikamliwaza na kumpunguzia huzuni za kifo changu.”

Aliposikia khutba hii, Ibrahim (as) akajibu: “Ewe mwanangu! Kwa hakika wewe ni msaidizi bora kwangu katika kutekeleza Amri ya Allah.”

Ibrahim (as) alimchukuwa mtoto wake mpaka Mina (sehemu ya kutolea kafara), akanoa kisu chake na kisha akafunga mikono na miguu ya Isma’il (as), akamlaza kifudifudi uso wake ukielekea ardhini. Kisha Ibrahim akanyanyua kichwa chake kuelekea mbinguni na akaweka kisu juu ya koo la mwanawe. Lakini, wakati anafanya hivyo alitambua kwamba kisu hakikati. Alipokiangalia akaona kwamba kisu kile kikali kimekuwa butu. Tukio hili lilirudiwa mara nyingi, wakati ghafla sauti ya kimbinguni ilisikika ikisema:“Ewe Ibrahim! Hakika, umefanya kama ulivyoota na umetii amri uliyopewa.”

Jibril alileta kondoo kama mbadala kwa muhanga wa Ismail (as), ambaye hatimaye Ibrahim (as) alimtoa kafara. Kuanzia hapo, ikawa ni desturi kwamba wale ambao wanakwenda kufanya ibada ya Hija kila mwaka laz- ima watoe kafara kwa kuchinja mnyama pale Mina. 5

5. Sa’d Na Mtukufu Mtume (Saw)

Mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume (saw) kwa jina la Sa’d, alikuwa masikini sana na alichukuliwa kama mmoja wa watu wa Kishubaka (As’habu Suffa).6 Alikuwa akisali sala zake zote nyuma ya Mtukufu Mtume (saw), ambaye alikuwa akihuzunishwa vibaya na umasikini wa Sa’d. Siku moja, Mtukufu Mtume (saw) alimuahidi kwamba, kama akipa- ta pesa, atampa yeye Sa’d. Muda ulipita na hakuna pesa iliyokuja kwa Mtukufu Mtume (saw), ambaye alihuzunika zaidi kwa hali ya Sa’d. Ilkuwa wakati huo Jibril alishuka kutoka mbinguni na kuleta dirham mbili.

Akamuambia Mtukufu Mtume (saw): “Allah amesema: Tunafahamu huzu- ni yako kuhusiana na umasikini wa Sa’d. Kama unataka aondokane na hali hii, mpe hizi dirham mbili na muambie ajishughulishe na biashara.”

Mtukufu Mtume (saw) alichukuwa zile dirham mbili na akaondoka nyumbani kwenda kusali Sala ya Adhur alimuona Sa’d anamsubiri karibu ya moja ya vyumba vya msikiti. Wakati alipomgeukia, Mtukufu Mtume (saw) alimuuliza: “Je, unaweza kujishughulisha na biashara?” “Kwa jina la Allah! Sina mtaji wa kufanya biashara,” alijibu Sa’d. Mtukufu Mtume (saw) alimkabidhi zile dirham mbili na akamuambia aanze biashara na mtaji huu. Sa’d alichukuwa pesa ile na akasali Sala yake ya Dhuhr na Asr kisha akaondoka kwenda kuchuma riziki yake.

Allah alimbariki sana katika hali ambayo kila alichonunua kwa dirham moja, alikiuza mara mbili ya alivyonunua.Hatimaye, hali yake ya kifedha pole pole ikaimarika. Hili liliendelea mpaka mwishowe akanunua duka karibu na msikiti na akaanza kuendesha biashara yake pale.

Jinsi biashara yake ilivyopanda juu, alianza kuwa mzembe kuhusiana na utekelezaji wa ibada zake, hata ikafikia kiasi kwamba wakati Bilal anapoadhini hawi tayari kwa ajili ya Sala. Kabla ya hapo alikuwa tayari kwa ajili ya sala hata kabla ya dhana! Wakati Mtukufu Mtume (saw) alipoona kuchelewa kwa Sa’d katika Sala, alimuambia: “Sa’d ulimwengu huu umekufanya kuwa mwenye shughuli sana kiasi kwamba umekuachisha mbali na Sala zako!”

Sa’d akajibu: “Nifanye nini? Kama nikiacha mali yangu bila kuangaliwa, itapotea na nitaishia kwenye hasara. Kutoka kwa mtu mmoja, ni lazima nikakusanye pesa kwa bidhaa zilizouzwa, ambapo kwa mtu mwingine laz- ima nichukuwe umiliki wa bidhaa zilizonunuliwa.”

Mtukufu Mtume (saw) alikerwa sana na kujishughulisha mno kwa Sa’d na utajiri wake na upuuziaji wake kuhusiana na utekelezaji wake wa ibada. Wakati huo huo Jibril alishuka na kusema: “Allah anasema: Tunafahamu huzuni yako. Ni ipi katika hali hizi mbili unayopendelea kwa Sa’d?” Mtukufu Mtume akasema hali ya kwanza ni yenye manufaa kwa Sa’d. Jibril akakubali: “Ndio, mapenzi ya dunia humfanya mtu kuwa asiyejali Akhera. Zichukuwe zile dirham mbili ulizompa hapo mwanzo.”

Mtukufu Mtume (saw) alimuendea Sa’d na akamuambia ikiwezekana arudishe zile dirham mbili ambazo alimpa. Sa’d akamuambia: “Kama unataka, nitakupa hata dirham mia mbili.” Mtukufu Mtume (saw) akasema: “Hapana, nipe tu zile dirham mbili ulizochukuwa kutoka kwangu.”

Sa’d akakabidhi pesa zile kwa Mtukufu Mtume (saw) na kwa muda mfupi, hali yake ya kifedha ikarudia palepale pa mwanzo na kabla ya muda mrefu kupita alijikuta yuko kwenye hali yake ya mwanzo.7

 • 1. Al-Kafi, Jz. 8, uk. 75 (Toleo jipya)
 • 2. Hikaayat-ha-e-Shanidani, Jz. 4, uk. 65; Safinah al-Bihaar, Jz. 2, uk. 714.
 • 3. Panda-e-Taarikh, Jz. 1, uk.181; Raudhaat al-Jannaat, uk. 36; Gharaaib al- Akhbaar cha Sayyid Ne’matullah Jazaairi.
 • 4. Paighambar Wa Yaaraan, Jz. 1, uk. 154-166.
 • 5. Taarikh-e-Anbiya, Jz. 1, uk.164-169.
 • 6. Hawa ni watu ambao walikuwa hawana nyumba za kwao wenyewe, na hivyo wanaishi katika sebule au vyumba vya Msikiti wa Madina (Masjidu’n-Nabi).
 • 7. Daastaanha, Wa Pand-ha, Jz. 2, uk.78; Hayaat al-Qulub, Jz. 1, uk. 578.

9) Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu

Allah Mwenyer Busara, amesma:

“Nyinyi ni kundi bora mliotolewa kwa ajili ya watu, mnaamrisha mema na mnakataza maovu…”

Imamu Ali (as) alisema: “Mtu ambaye anajizuia kukataza maovu kwa moyo, mkono na ulimi ni kama mfu miongoni mwa walio hai.”

Maelezo Mafupi:

Mtu yeyote ambaye anataka kuamrisha mema na kukataza maovu, yeye mwenyewe lazima awe anajua kile ambacho ni halali na kile ambacho ni haramu, na asitende kinyume na kile anachohubiri. Lengo lake lazima liwe ni kuongoza watu.

Lazima azungumze kwa uzuri na awe anafahamu tofau- ti ya kiwango cha ufahamu wa watu. Kama akipingwa lazima aoneshe subira na kama akiungwa mkono na kupendelewa na watu, lazima amshukuru Mungu.

1. Bishr Haafi

Siku moja wakati Imamu Kadhim (as) alikuwa anapita karibu na nyumba ya Bishr Haafi, alisikia sauti ya muziki kutoka ndani nyumba hiyo. Wakati huo huo msichana kijakazi alitoka ndani na kutupa takataka. Imamu (as) akamuuliza: “Mwenye nyumba hii ni muungwana au ni mtumwa?” “Ni muungwana,” alijibu yule mjakazi. Aliposikia hivi, Imamu (as) akasema: “unasema kweli, kwani kama angekuwa mtumwa, angemuogopa bwana wake.”

Wakati msichana yule kijakazi aliporudi ndani ya nyumba, Bishr, ambaye alikuwa akinywa pombe, alimuuliza kilichomfanya akae muda mrefu huko nje. Mara tu msichana yule kijakazi aliposimulia kilichotokea, Bishr mara moja alisimama na kukimbia miguu mitupu kumkimbilia Imamu (as). Mara tu alipomfikia, alionesha aibu na toba juu ya vitendo vyake, aliomba msamaha na akarekebisha njia zake chafu.1

2. Mulla Hasan Yazid, Mkatazaji Maovu

Wakati wa utawala wa Fath Ali Shah Gajaar, kule katika mji wa Yazd, aliishi mwanachuoni mmoja, kwa jina akiitwa Mulla Hasan Yazdi,2ambaye aliheshimiwa sana na watu.

Gavana wa mji wa Yazd alikuwa akiwaonea watu na kuwatendea ukatili mkubwa kabisa. Mullah Hasan alimshauri kuacha kufanya viendo vyake viovu. Wakati alipokataa kurekebisha mwenendo wake huo, Mulla alilalamika kwa Fath Ali Shah, lakini hili nalo pia halikuzaa matunda.

Kwa vile Mulla alikuwa muangalifu hususan na heshima kwenye suala la kuamrisha mema na kukataza maovu, aliwakusanya watu wa Yazd, na kwa amri yake kwa pamoja walimtupa gavana yule nje ya mji ule. Wakati Fath Ali Shah alipofahamishwa tukio hili, alifadhaishwa mno na akaamuru Mulla Hasan Yazdi aletwe mbele yake mjini Tehran.

Mara tu Mulla alipofika, Fath Ali Shah alimuuliza kuhusu tukio hilo kati- ka mji wa Yazd. Mulla akajibu: “Gavana wako katika Yazd alikuwa dhalimu na nilitaka kuwaondolea watu uovu wake kwa kumtoa katika mji wa Yazd.”

Jibu hili lilimkasirisha sana Shah akaamrisha Mulla afungwe miguu yake. Amin-uddaulah akamuambia Shah: “Hana kosa. Ilikuwa bila ruhsa yake kwamba watu walimtupa gavana nje ya mji.”

Licha ya miguu yake kufungwa, Mulla Hasan alisema: “Kwa nini tudan- ganye? Nilitaka gavana atolewe nje ya mji wa Yazd kwa sababu ya uonevu wake.” Hatimaye, kwa ajili Amin-uddaulah kuingilia kati kamba zilifunguliwa kwenye miguu ya Mulla Hasan.

Usiku ule Shah alimuona Mtukufu Mtume (saw) kwenye ndoto huku vidole vyake viwili vya mguuni vikiwa vimefungwa. “Kwanini vidole vyako vimefungwa?” Alimuuliza Mtukufu Mtume (saw). Mtukufu Mtume (saw) akajibu: “Ni wewe uliyevifunga.”

Shah akasema kwamba kamwe hajawahi kufanya utovu wa adabu kama huo. Mtukufu Mtume (saw) akaeleza: “Lakini sio wewe uliyeamrisha Mullah Hasan Yazd miguu yake ifungwe?”

Shah akaamka usingizini akiwa na wasiwasi mkubwa. Aliamrisha Mulla Hasan apewe nguo za heshima na arudishwe kwenye mji wake kwa taad- hima na heshima kubwa. Mulla Hasan alikataa nguo zile na akarudi Yazd. Baadae, alikwenda Karbala na akabakia huko kwa maisha yake yote yaliyobakia.3

3. Amri Ya Mungu Kuuteketeza Mji

Mwenyezi Mungu aliwaamrisha malaika wawili kuuangamiza mji fulani. Walipofika kule, malaika wakaona mkazi mmoja wa mji ule akilalamika na kuomba kwa Mwenyezi Mungu. Mmoja wa malaika akamuambia mwenzake:

“Unamuona mtu yule anayeomba kwa Mwenyezi Mungu?”

“Ndio namuona, lakini amri ya Mwenyezi Mungu lazima itekelezwe.” Alijibu yule malaika mwingine. “Subiri. Ngoja nimuulize Mwenyezi Mungu ni kitu gain tufanye.” Malaika yule wa kwanza akamuomba Mwenyezi Mungu: “Katika mji huu kuna mtu mmoja anayekusihi na kukuomba. Je, tuendelee kutoa adhabu katika mji huu?”

Jibu likaja kutoka kwa Mwenyezi Mungu:

“Tekelezeni amri ambayo mmepewa, kwani mtu huyo hakusumbuliwa na na kuhuzunishwa kwa ajili Yangu, wala kuonesha kuchukizwa juu ya maovu yanayofanywa na watu wengine.”4

4. Yunus Ibn Abd al-Rahmaan

Wakati Imamu Kadhim (as) alipofariki dunia, wawakilishi wake walikuwa na utajiri mkubwa katika miliki zao. Kwa matokeo ya ubahili wao baadhi yao walianza kukataa kifo cha Imamu na kwa sbabu hiyo waliweka msin- gi wa madhehebu yanalojulikana kama Waaqifiyyah. Zayaad Qandi alikuwa na sarafu za dhahabu sabini elfu wakati ambapo Ali Ibn Abi Hamzah alikuwa na thelethini elfu.

Wakati huohuo, Yunus Ibn al-Rahmaan aliwalingania watu kuelekea kwa Uimamu wa Imamu Ridha (as) na kuyachukulia madhehebu ya Waaqifiyyah kama ya uwongo na ya kimakosa. Wakati Zayaad Qandi na Ali Ibn Abi Hamzah walipofahamu alichokuwa anafanya Yunus, walimtu- mia ujumbe wakimuuliza:

“Kwanini unawalingania watu kuelekea kwa Imamu Radha (as)? Kama lengo lako ni kupata utajiri, tutakufanya wewe kuwa tajiri.” Waliahidi kumpa sarafu elfu kumi za dhahabu kama atanyamaza na kuacha kuwalin- gania watu kuelekea kwa Imamu (as). Yunus Ibn Abi al-Rahmaan5 aliwa- jibu kwa kunukuu hadithi kutoka kwa Imamu Baqir (as) na Imamu Sadiq (as) ambayo inasema:

“Wakati uzushi (bid’a) unapojionesha wenyewe miongoni mwa watu, ni muhimu kwa wazee na viongozi kudhihirisha kile wana- chojua (ili watu wajizuie kutokana na maovu) na kama wakishind- wa kufanya hivyo, Mwenyezi Mungu ataondoa kutoka kwao mwanga wa imani.” Kamwe sitaacha jihadi katika njia ya dini na mambo ya Mwenyezi Mungu.

Baada ya kupokea jibu la kweli na wazi kutoka kwa Yunus, Ziyaad Qandi na Ali Ibn Hamzah wakawa maadui zake.

5. Khalifa Juu Ya Kipaa Cha Nyumba!

Usiku mmoja, Khalifa wa pili alikuwa anakagua mitaa ili kuhakikisha kwa ujumla hali ya mambo katika mji. Katika muda wa ukanguzi wake, alitokea kupita katika nyumba ambayo kwayo alisikia makelele yenye kutia wasi- wasi. Alipanda juu ya ukuta wa nyumba na akatazama ndani. Mwanaume na mwanamke walikuwa wamekaa pamoja, na jagi la pombe likiwa limewekwa mbele yao. Akiwakemea kwa ukali alisema: “Mnatenda dham- bi katika faragha mkiamini kwamba Mwenyezi Mungu hatadhihirisha siri yenu?”

Yule mwanaume akamgeukia Khalifa na akasema: “Usiwe na haraka kiasi hicho, kwani kama nimetenda dhambi moja, wewe umetenda tatu. Kwanza, Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani Tukufu; na usipeleleze.6 Hicho ndicho ulichofanya wewe sasa hivi. Pili, Amesema katika Qur’ani Tukufu; Na ingieni katika nyumba kwa kupitia milango yake,7 wewe umeingia juu ya ukuta. Tatu, Amesema katika Qur’ani Tukufu; Mtakapoingia katika nyumba, toleaneni salamu,8wewe hukufanya hivyo.”

Khalifa akauliza: “Kama nikikusamehe, utakuwa tayari kurekebisha tabia yako?” “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu! Kamwe sitarudia tena kitendo hiki,” alijibu yule mwanaume. Khalifa akasema: “Sasa unaweza kuwa kati- ka amani, kwani nimekusamehe.”

 • 1. Darsi Az Akhlaaq, uk. 128; Minhaaj al-Karaamah (cha Allamah Hilli)
 • 2. Mwandishi wa Muhij Al-Ahzaan.
 • 3. Hikaayat-ha-e-Shanidani, Jz. 3, uk. 146; Qisas al-Ulema, uk. 101.
 • 4. Jaame al-Sa’adat, Jz. 2, uk. 231
 • 5. Imam Ridha (as) alisema: Yunus Ibn Abd al-Rahmaan katika zama zake ni kama Salman Farsi alivyokuwa katika zama zake.
 • 6. Qur’ani Tukufu, 49:12
 • 7. Qur’ani Tukufu 2:189
 • 8. Qur’ani Tukufu 24:63

10) Haki

Allah, Mwenye Busara, amesema:

“…Kuwenu wasimamizi kwa ajili ya Allah mkitoa ushahidi kwa haki…”1

Imamu Ali (as) anasema: “Mtu ambaye huonesha utendaji wa haki kwa upande wake, Allah atamzidishia katika utukufu.”2

Maelezo mafupi:

Imani ya mtu haiwi kamili mpaka achunge haki kuhusiana na yeye mwenyewe na wengine. Allah atamzidishia heshima na utukufu wake.

Mwanadamu kwa asili, hupendelea nafsi yake mwenyewe na kupenda kila kitu ambacho kinahusiana na yeye. Vilevile anakuwa na tabia ya kutopenda kila kitu kibaya na kiovu. Hivyo, kama akimsaidia mwenye shida, atasifiwa na watu wote. Halikadhalika, (uadilifu huhitaji hilo) kama hapendelei chochote kibaya na kiovu kwa yeye mwenyewe, basi vilevile asikipendelee kitu hicho kwa watu wengine.

Hii pia huleta haki wakati wa kusuluhisha kati ya pande mbili zinazogom- bana; katu asipendelee upande mmoja dhidi ya mwingine, hata kama matokeo yake yatakuwa yenye hasara kwake mwenyewe.

1. Ushauri Kutoka Kwa Mtukufu Mtume (Saw)

Mwarabu alimuendea Mtukufu Mtume (saw) wakati alipokuwa anataka kuingia katika msafara wa vita.

Alichukuwa hatamu za ngamia wa Mtume, na akasema: “Ewe Mtume wa Allah! Nifahamishe mimi kitendo ambacho kitanipatia Pepo.”

“Kuwa na tabia nzuri wewe mwenyewe na kwa watu katika hali hiyo hiyo kama ambavyo ungetaka wao wawe hivyo kwako na kujizuia kutokana na kuwafanyia kile ambacho usingetaka wewe wakufanyie,” alishauri Mtume (saw) na akaongeza, “ziachilie hatamu (kwani nataka kwenda kwenye jiha- di).”3

2. Uadilifu Wa Ali (As)

Shu’bi anasimulia: “Kama walivyo vijana wengine, niliingia katika uwan- ja mkubwa wa Kufa, ambako nilishuhudia Amiru’l-Mu’minina (as) akiwa amesimama kando ya makonteina mawili ambayo yalikuwa yamejaa dha- habu na sarafu za fedha. Alikuwa na kiboko kidogo mkononi mwake. Kundi kubwa limekusanyika kandoni mwake na alikuwa akiwarudisha nyuma kwa kutumia kiboko chake kuwazuia ili wasivuruge ugawaji wa pesa hizo.

Imamu (as) alianza kugawanya pesa miongoni mwa watu mpaka zote zikaisha bila kubakisha chochote kwa ajili yake na akarudi nyumbani kwake mikono mitupu.

Nilirudi nyumbani na kumuambia baba: “Leo nimeona kitu cha ajabu sana lakini nilishindwa kutambua kama kitendo cha mtu huyu kilikuwa ni kizuri au kibaya kwa sababu hakubakisha kitu kwa ajili yake mwenyewe!” Baba yangu akaniuliza: “Mtu huyo alikuwa ni nani?” “Amiru’l-Mu’minina (as)” Nilijibu na kusimulia kile kilichotokea kule kiwanjani.

Baada ya kusikia uadilifu wa Ali katika kugawa pesa zile, baba yangu alianza kutoa machozi na akaniambia: “Mwanangu, umeshuhudia mtu bora zaidi kutoka miongo- ni mwa watu.”4

3. A’di Ibn Haatim

A’di mtoto wa mtu maarufu sana, Haatim Taai alikuwa mmoja wa wafuasi waaminifu wa Amiru’l-Mu’minina (as). Alisilimu tangu mwaka wa 10 A.H., siku zote A’di alikuwa katika kumhudumia Imamu (as), na amepigana vita vya Jamal, Siffin na Nahrawaan bega kwa bega pamoja naye. Katika vita vya Jamal alipata jeraha katika moja ya jicho lake na akawa chongo.

Wakati fulani alikuja kwa Mua’wiyah kwa madhumuni fulani. Mua’wiyah akamuuliza kwa nini hakuja na watoto wake. “Waliuawa wakati wanapigana sambamba na Amiru’l-Mu’minina (as),” alijibu. “Ali hakuwa mwadilifu kwako, kwa sababu aliwapeleka watoto wako kuuliwa ambapo yeye amewaweka watoto wake kuwa hai,” alisema Mua’wiyah. A’di akase- ma; “(Kinyume chake) mimi sikumfanyia uadilifu kwa vile yeye ameuawa, wakati mimi bado niko hai. Ewe Mua’wiyah hasira zetu kwako bado zinaunguza katika nyoyo zetu. Elewa kwamba (maumivu ya) kukatwa makoo yetu au uchungu wa kifo ni rahisi kwetu kuvumilia kuliko kusikia maneno kuhusu Ali (as).”5

4. Uadilifu Wa Abu Dharr

Akiwa njiani kuelekea kwenye vita vya Taabuk6, Abu Dharr aliachwa nyuma ya jeshi kwa sababu alikuwa amepanda mnyama anaekwenda pole-pole. Watu wengine walipogundua hili, walimjulisha Mtukufu Mtume (saw) ambaye alisema:

“Kama ana wema ndani yake, Allah atamfanya atufikie.”

Wakati huo huo, Abu Dharr, alikatishwa tamaa na mnyama yule akaamua kumuacha na akaendelea na safari yake kwa miguu. Mtukufu Mtume (saw) aliona sehemu nzuri aliamua kukita mahema pale, wakati mmoja wa Waislamu alipopiga kelele kwamba kuna mtu kwa mbali anawafuata.

Mtukufu Mtume (saw) akaomba: “Ee Allah! Na iwe ni Abu Dharr!”

Wengine wakamjulisha kwamba kweli alikuwa ni Abu Dharr. Mtume akaomba: “Allah amsamehe Abu Dharr! Amesafiri peke yake, atakufa peke yake na atafufuliwa peke yake.” kisha akawataka watu wampatie Abu Dharr maji, kwa vile anaonekana kuwa na kiu. Lakini wakati Abu Dharr alipowasili mbele yake, Mtume (saw) aliona kwamba alikuwa na chombo cha maji katika mizigo yake, na hivyo akamuuliza:

“Abu Dharr! Maji umekuwa nayo na bado umekaa na kiu wakati wote?” “Ndio! Ewe Mtume wa Allah! Wazazi wangu watolewe muhanga kwa ajili yako! Nikiwa njiani, nilishikwa na kiu kubwa. Nilifika sehemu ambako kulikuwa na maji. Nilipoyajaribu niliyaona kuwa baridi na matamu na hivyo nikajisemea mwenyewe: (Sio haki) kama nitayanywa maji haya kabla ya Mtukufu Mtume (saw).” Alijibu Abu Dharr.

Aliposikia hivi, Mtukufu Mtume (saw) akasema: “Ewe Abu Dharr! Allah swt. akusamehe makosa yako! Utaishi maisha ya upweke, kufa kama mgeni, mbali na nyumbani, na kuingia peponi peke yako.”7

 • 1. Qu’an Tukufu 5:8
 • 2. Jaame al-Sa’adaat, Jz. 1. uk. 368.
 • 3. Al-Kafi, Jz.2, sura ya Uadilifu, tr. 10.
 • 4. Al-Ghaaraat, Jz. 1, uk. 55; Dastaanhai Az Zindagi Ali, uk. 7.
 • 5. Ibid
 • 6. Taabuk ipo maili 300 kaskazini ya Madina.
 • 7. Paighambar Wa Yaaraan, Jz. 1, uk.49; Al-Isaabah, Jz. 4, uk. 65.

11) Ubinadamu

Allah Mwenye Busara anasema:

وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنْفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ {9}

“…Na wanawapendelea (Muhajirina) kuliko nafsi zao ingawa wao wenyewe ni wahitaji…” (Quran 59:9)

Mtukufu Mtume anasema: “Mtu ambaye atatamani kitu, (lakini) akaizima tamaa yake na akawapa wengine upendeleo kuliko yeye mwenyewe, dhambi zake zitasamehewa.”1

Maelezo Mafupi:

Daraja ya juu zaidi ya ukarimu ni ubinadamu. Mtu muungwana, licha ya kuwa na haja na mahitaji makubwa, hujitolea muhanga kwa kuwapa wengine upendeleo kuliko yeye mwenyewe.

Hata kitendo cha kutoa sadaka huwa na daraja ya chini kuliko ubinadamu. Kupata radhi ya Allah kunahitaji kutekeleza wajibu mkubwa ndani yake. Kama mtu, akiwa katika juhudi ya kuokoa maisha ya mtu anayezama majini, yeye mwenyewe akizama, sifa kutoka kwa Allah kwa kujitoa kwake muhanga, ni mara elfu zaidi kuliko sadaka ambazo huzitoa.

1. Mtumwa Muungwana

Abdullah Ibn Ja’far, mume wa Bibi Zainab (as) alikuwa ni mtu ambaye ukarimu wake hauna kifani. Siku moja, alitokea kupita kwenye shamba la mitende, alimuona mtumwa anafanya kazi pale. Wakati ule ule, chakula cha mtumwa yule kililetwa na akakabidhiwa. Alipokuwa anataka kula chakula chake, mbwa mwenye njaa alikuja mbele yake akitikisa mkia wake. Mtumwa yule aliweka sehemu ya chakula chake, mara moja mbwa yule akala chakula kile. Yule mtumwa akaweka tena chakula zaidi mbele za mbwa yule na mara moja akakila chakula kile. Hali hii ikaendelea mpaka akawa amekitoa chakula chake chote.

Abdullah, ambaye alikuwa anashuhudia tukio lile, akamuuliza yule mtumwa: “Mgao wako wa chakula ni kiasi gani kwa siku?”

“Ni kiasi ambacho umekiona hivi punde.” Akajibu yule mtumwa.

“Kama ni hivyo, kwa nini basi umempa mbwa upendeleo kuliko wewe mwenyewe?” aliuliza Abdullah.

“Mbwa huyu katoka mbali na alikuwa na njaa na sikuona kwamba ni vema kumfukuza katika hali hiyo ya njaa.” Alijbu yule mtumwa.

“Kitu gani kitakacho kutosheleza leo?”

“Nitaishinda njaa yangu kwa uvumulivu na uimara,” mtumwa yule akaeleza.

Abdullah alipoona ubinadamu ule wa mtumwa na kutokujali maslahi binafsi, alijiwa na mawazo yeye mwenyewe kwamba mtumwa yule yule alikuwa mkarimu sana kuliko yeye mwenyewe. Katika njia ya kumtukuza na kumfidia kwa ajili ya ubinadamu wake, Abdullah alimnunua mtumwa yule na shamba lile kutoka kwa mmiliki wake, akamuacha huru mtumwa yule na mwisho akalizawadia shamba lile lote kwake.2

2. Kadhia Ya Msikiti Wa Merv

Abu Muhammad Azdi anasimulia:

Wakati msikiti wa Merv uliposhika moto, Waislamu wakachukulia kwam- ba hiyo ilikuwa kazi ya Wakiristo na wakalipiza kwa kuzichoma moto nyumba zao.

Wakati mfalme alipojua kitendo hicho, aliamuru wale ambao wamehusika katika kitendo hicho wakamatwe na kuadhibiwa. Aliamrisha kwamba wahalifu lazima wapatiwe moja ya aina tatu ya adhabu – kifo, kukatwa mkono au viboko. Kila adhabu itaandikwa kwenye kipande kidogo cha karatasi ambacho kitawekwa ndani ya sanduku. Kila mhalifu alitakiwa kuokota kipande cha karatasi ndani ya sanduku na atapasika na adhabu iliyoandikwa humo.

Wakati mmoja wa watu hawa alipookota na kusoma karatasi yake, alian- gua kilio kwa sababu adhabu yake ilikuwa ni kifo. Kijana mmoja, ambaye alionekana kuwa na furaha kwa vile ataadhibiwa kwa kuchapwa viboko, alimuuliza yule mtu mwenye huzuni: “Kwa nini umehuzunishwa na kulia? Adhabu hizi hazitakuwa ni tatizo katika njia ya kutumikia dini.”

Yule mtu wa kwanza akajibu: “Tumetumikia dini yetu na kwa hiyo siogopi kifo, lakini ukweli ni kwmba ninaye mama mzee, na kwa vile ni mtoto wake pekee, anategemea kabisa juu yangu. Wakati akisikia kuhusu kifo changu, hataishi.”

Aliposikia hivi, yule kijana akatafakari kwa muda kidogo na kisha akase- ma: “Mama yangu hayuko hai wala sina mafungamano na yeyote. Tubadilishane hizi adhabu ili mimi niuawe badala yako wewe na wewe uchapwe viboko.”

Wawili wale wakabadilishana adhabu; yule akauawa, ambapo yule mtu mwingine baada ya kuchapwa viboko alirudi nyumbani kwa mama yake.

3. Vita Vya Yarmuk (Tabuk)

Katika vita vya Yarmuk, kikundi cha wanajeshi Waislamu walikuwa wakienda kwenye vita kila siku. Baada masaa machache ya mapambano, wale ambao hawakuumia na wale ambao wamepata majeraha kidogo hurudi, ambapo waliojeruhiwa au kufa huachwa kwenye uwanja wa mapambano.

Hudhaifah U’dwi, anaelezea: Siku moja, binamu yangu, pamoja na baadhi ya askari wengine, walitoka kwenda kwenye uwanja wa mapambano.

Kwa bahati mbaya, baada ya kukamilika kwa mapambano ya siku ile alishind- wa kurudi. Nilichukuwa chombo cha maji, nilikwenda kwenye uwanja wa mapambano, nikitumaini kumpa maji iwapo atakuwa hai.

Baada ya kutafuta kwa muda, nilimuona binamu yangu ambaye alikuwa hai kwa shida. Nilichuchumaa kando yake, na kumuuliza kama anahitaji maji. Alikubali kwa kichwa. Wakati huo huo, askari mwingine, ambaye amelala karibu yake, alinisikia alivuta pumzi kwa sauti kubwa kuonesha kwamba alikuwa na kiu kali sana.

Binamu yangu akaniashiria nimpe maji askari yule kwanza. Nilipokuwa nakwenda kumhudumia, niligundua kwamba alikuwa ni Hishaam Ibn A’as. Nilimuuliza kama alikuwa anahiji maji. Aliashiria kukubali. Wakati huo huo askari mwingine aliyejeruhiwa alitaka maji na Hishaam pia akakataa kunywa maji yale kabla ya askari yule mwingine hajanywa. Nilisogea kumuendea askari yule wa tatu, lakini nilipomfikia tu, alivuta pumzi yake ya mwisho. Nilirudi kwa Hishaam, niliona kwamba katika kipindi hiki kilichofuatia, naye pia amefariki. Niliharakisha kwa binamu yangu, nikamkuta akiwa amekwisha kufa pia!3

4. Ali (As) Katika Nafasi Ya Mtukufu Mtume (Saw)

Wakati viongozi wa Makureish walipotambua kwamba wakazi wa Madina wanatoa kiapo cha utii kwa Mtume, chuki yao kwake iliongezeka. Hatimaye, viongozi wao wakaamua kwamba mkesha wa kuamkia tarehe moja ya Rabi’ al-Awwal, shujaa mmoja kutoka kila ukoo wakusanyike pamoja, waizingire nyumba ya Mtume na kumuuwa akiwa amelala kitandani mwake.

Mwenyezi Mungu akaufichua mpango wao muovu kwa Mtume, ambaye alimuambia Amiru’l-Mu’muminin, Ali (as): “Kwa vile washirikina wanapanga kuniuwa leo usiku, Mwenyezi Mungu ameniamuru kuhama. Je, utalala kwenye kitanda changu ili wasijue kwamba nimeondoka?”

“Ewe Mtume wa Allah! Je, utakuwa hai na mzima wa afya kama nikifanya hivyo?” aliuliza Ali (as).

Mtukufu Mtume (saw) alimthibitishia kwamba itakuwa hivyo. Aliposikia hivi, uso wa Amiru’l-Mu’muminin (as) ukanawiri kwa furaha na akaporomoka chini katika sijda ya shukurani (kwa Allah Azza wa Jallah). Kisha akasema: “Uhai wangu na uwe muhanga kwa ajili yako! Nenda popote ambapo Allah amekuamuru wewe kwenda; kama unanihitaji mimi kufanya kazi yoyote kwa ajili yako, niamuru tu, na nitaifanya bila mashar- ti, na kutoka kwa Allah naomba rehema na mafanikio.”

Mtukufu Mtume (saw) alimchukua Ali kwenye mikono yake, huku machozi tele yakimtoka na akamuaminisha kwenye hifadhi ya Allah. Kisha, Jibril akamchukua Mtukufu Mtume (saw) kwa mkono wake na kumtoa ndani ya nyumba na kuelekea naye kwenye pango la Thaur.

Usiku ule, Amiru’l-Mu’muminin (as) alilala katika kitanda cha Mtukufu Mtume (saw) na akajifunika shuka lake.

Makafiri mwanzo walikusudia kushambulia nyumba ya Mtume katika usiku wa giza, lakini Abu Lahab, ambaye alikuwa pamoja nao, alishauri kinyume chake akisema kwamba ilikuwa ni usiku na wanawake na watoto walikuwa wamelala. Aliwaambia kusubiri mpaka asubuhi. Wakati asubuhi ilipoingia walikimbilia ndani ya nyumba na kumkuta Ali (as) katika kitan- da cha Mtume. Walimuuliza alipo Muhammad.

Kwani mlimuacha pamoja na mimi (hata sasa mniulize kuhusu aliko)? Mlitaka muondokane naye (na hivyo) kaondoka.” Alijibu kwa ukali.

Walimuacha Ali (as) na wakatoka kumtafuta Mtukufu Mtume (saw)4.

Hata hivyo, ilikuwa ni kwa ajili ya matokeo ya kitendo hiki (kilichopang- wa na Allah Azza wa Jallah) cha kujitoa muhanga kwa upande wa Ali (as), kwamba Mtukufu Mtume (saw) alibakia hai na bila madhara. Allah akateremsha Aya ifuatayo kwa tukio hili. Inafungamana na Ali (as):

أَلَمْ تَعْلَمْ أَنَّ اللَّهَ لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ {107}

“Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.” ( Quran 2:107)

5. Muhanga Binafsi Wa Haatim Taai

Wakati fulani kulikuwa na ukame katika sehemu ambayo Haatim Taai aliyokuwa akiishi. Chakula kikaisha kabisa mpaka ikawa hakuna kitu kili- chobaki na watu wakawa wanateseka vikali kwa njaa na dhiki.

Mke wa Haatim anasimulia: “Usiku mmoja kulikuwa hakuna hata tonge moja nyumbani mwetu. Haatim, watoto wangu wawili, A’di na Safaanah na mimi mwenyewe, tuliona kwamba hatuwezi kulala kwa sababu ya njaa tuliyokuwa nayo.

“Kwa shida kubwa, Haatim alimfanya A’di alale wakati mimi nilifanya hivyo hivyo kwa Safaanah. Kisha Haatim akaanza kusimulia kisa kimoja kwa nia ya kunifanya nilale, lakini ukali wa njaa ulinifanya kuwa macho. Pamoja na hivyo, nilijifanya niko kwenye usingizi mzito kiasi kwamba hata aliponiita mara nyingi, sikumjibu.

“Haatima alikuwa akichungulia kwenye jangwa kupitia kwenye tundu la hema, wakati alipoona kivuli kinasogelea upande wetu. Kilipofika karibu, Haatim alitambua kuwa alikuwa ni mwanamke na akaita: ‘Ni nani huyo?’ Yule mwanamke akaomboleza: ‘Haatim, watoto wangu wanapiga makelele kama mbwamwitu kwa ajili ya njaa kali waliyo nayo.’

“Haatim akamuambia yule mwanamke asiwe na wasiwasi, kwa vile atat- uliza njaa yao. Niliposikia hivi, niliamka kutoka kwenye sehemu yangu niliyolala na kumuuliza atalifanya vipi hilo. Akasema: ‘Nitamlisha kila mtu’

“Kisha alielekea kwenye punda wetu wa pekee tuliye naye na ambaye tunamtumia kwa kubebea mizigo yetu. Alimchinja na akatoa fungu mojawapo na akampa yule mwanamke akisema: ‘Ipike nyama hiyo na walishe watoto wako.’ Akanigeukia mimi na kusema: ‘Waamshe watoto ili na wao pia wapate kula.’

“Baada ya muda mfupi, aliongeza kusema: ‘Ni aibu kubwa kula ambapo wengine wanalala kando yako wakiwa na njaa.’ Alikwenda kuwaamsha yeye mwenyewe. Kila mtu alikula nyama ile isipokuwa Haatim ambaye alikaa na kupata furaha kutokana na kuwaangalia wakila.”

 • 1. Jaame al-Saadaat, Jz. 2, uk. 118.
 • 2. Hikaayat-ha-e-Shanidani, Jz.5, uk.114; al-Mahajjah al-Baidhaa, Jz. 6, uk. 80.
 • 3. Namunah-e-Ma’rif, Jz.2, uk. 435; Mustatraf, Jz. 1, uk.157.
 • 4. Daastan-ha Wa Pand-ha, j. 1, uk. 173; Mustatraf j. 1, uk.156

12) Bughudha

Allah Mwenye Busara anasema:

إِنَّ الَّذِينَ يُؤْذُونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ لَعَنَهُمُ اللَّهُ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ {57}

“Hakika wale ambao wanamuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera…(Quran 33:57)

Mtukufu Mtume (saw) anasema: “Hairuhusiwi kwa Mwislamu kumuan- galia ndugu yake Mwislamu katika hali ambayo humuumiza na kumuud- hi.”1

Maelezo mafupi:

Viumbe wote ni wa kaya ya (viumbe wa) Mungu na wenye sifa zaidi miongoni mwao ni waumini. Mtu yeyote ambaye hunufaika na uumbaji, anakuwa mpenzi wa Mungu, ambapo yule ambaye huwabughudi na kuwaudhi wengine, hususan waumini, katika hali yoyote, ni kama vile ametangaza vita na Mwenyezi Mungu.

Katika Siku ya Hukumu, Mwenyezi Mungu ataita: “Wako wapi wale ambao wamebughudhi na kuwatesa rafiki Zangu katika dunia.” Kundi la watu ambao miili yao itakuwa bila nyama, watajitokeza mbele ambako Mwenyezi Mungu ataamuru watupwe kwenye Jahannam.

Hivyo, ni muhimu kujizuia kutokana na kuwaumiza na kuwaudhi wengine wazazi, majirani, marafiki na kadhalika. Kama mtu ametenda kitendo hiki, msamaha unatakiwa utafutwe kwa wale wanaohusika.

1. Usumbufu Aliofanyiwa Imamu Sajjad (As)

Wakati wa Imamu Sajjad (as), aliishi mtu mjini Madina ambaye alizoea kuwafanya watu wacheke ili kujipatia riziki yake.

Baadhi ya watu walishauri wamkaribishe Imamu Sajjad (as) na kumuacha huyu mtu amfanye acheke kidogo katika juhudi ya kumsahaulisha Imamu kutokana na uzito wa maombelezo yake. Walikusanyika pamoja na walikuwa njiani kuelekea nyumbani kwake wakati walipomuana anakuja kuelekea waliko wao, akifuatana na watumwa wake wawili.

Wakati Imamu alipofika karibu, yule mchekeshaji alichukuwa joho la Imamu (as) kutoka mabegani mwake na kulivaa yeye mwenyewe. Watu waliokuwa wamemzungka wakaangua kicheko walipoona kichekesho hiki.

Imamu (as) akauliza: “Ni nani mtu huyu?” Wale watu waliomzunguka wakasema: “Ni mtu ambaye huwafanya watu wacheke na kupata pesa kutoka kwao kwa vichekesho vyake.”

“Mjulisheni kwamba wale ambao hutumia maisha yao katika njia isiyo na maana wakifanya matendo ya kipuuzi watakuwa ni wenye hasara katika Siku ya Hukumu,” alishauri Imamu (as).

Baada ya kusikia haya, mchekeshaji yule aliacha tabia yake ile ya maudhi na akarekebisha mwenendo wake.2

2. Qaroon Na Musa (As)

Nabii Musa (as), katika harakati za kutangaza dini yake, alikabiliana na uadui na ugumu kutoka kwa watu wanaofanana na Firaun. Bala’m, Bao’ora na hata binamu yake Qaroon. Qaroon alikuwa tajiri mkubwa mno na alikuwa na utajiri mkubwa kiasi kwamba vijana kadhaa wenye nguvu walihitajika kubeba funguo za hazina yake. Alikuwa mmoja wa mamwinyi wenye daraja kubwa na ushawishi, ambaye alikuwa akiwakandamiza wa chini yake.

Musa (as), kwa kutekeleza amri za Allah, alitaka Zaka kutoka kwake, lakini Qaroon alikuwa akisema: “Mimi vilevile ninao ujuzi wa Taurat na sio mdogo kwa Musa kwa hali yoyote ile; kwa nini nitoe Zakat kwake?” Hatimaye, kiburi chake kilimlazimisha kutumia mbinu chafu kujaribu kumdhalalisha Nabii Musa (as). Alimfuata mwanamke mmoja ambaye alikuwa na mwenendo mbaya lakini vilevile alikuwa mrembo sana na mwenye kuvutia. Akamuambia: “Nitakulipa dirham mia moja elfu mradi tu kesho wakati Musa (as) akiwahutubia Bani Israel, upige kelele mbele za watu kwamba Musa amezini na wewe.”

Mwanamke yule akakubali kulifanya hilo. Siku iliyofuatia Bani Israil walikusanyika, na Musa (as) akiwa na Taurati mkononi mwake alikuwa amejishughulisha katika kuwahubiria. Qaroon, kwa umaridadi wake wote, alikuwa mmojawapo wa walihudhuria pamoja na watumishi wake. Ghafla, yule mwanamke alisimama, lakini wakati anaangalia kwenye uso mtukufu wa Nabii Musa (as) aliona mabadiliko ya moyo na akapiga kelele:

“Ewe Musa! Elewa kwamba Qaroon ameniahidi kunipa dirham mia moja elfu kama nitakushutumu wewe mbele za Bani Israil kwamba umefanya zinaa na mimi; lakini (natamka kwamba) kamwe hujawahi kufanya kitendo hicho na Allah ameilinda haiba yako kutokana na uchafu kama huo.”

Wakati Musa (as) aliposikia haya, aliumia sana na kuvunjika moyo, na akamlaani Qaroon kwa kusema: “Ewe ardhi! Mkamate Qaroon na ummeze.” Kwa amri ya Mungu, ardhi chini yake ikapasuka upande na Qaroon akatumbukia ndani yake pamoja na utajiri wake wote.

Kwa mujibu wa taarifa nyingine, Musa alikuwa akiwahubiria watu kuhusu Sharia’h wakati akiwa katika harakati za kuhutubia alisema: “Mtu ambaye hana mke/mume na akajiingiza katika zinaa ataadhibiwa kwa kuchapwa viboko mia moja na kwa mtu ambaye ana mke/mume akitenda zinaa atapigwa mawe mpaka afe.” Wakati huo Qaroon akasimama na akasema: “(kama hili likiwa kweli) hata kama wewe umetenda kosa hilo?”

“Ndio” akajibu Musa.

Bani Israil wana imani kwamba wewe umetenda zinaa na mwanamke fulani.”

“Mlete huyo mwanamke hapa,” alidai Musa. “Kama akithibitisha dai hili, uko huru kutenda kwa mujibu wa sheria.”

Yule mwanamke akaletwa mbele ya Musa (as) ambaye alimlisha kiapo ili aseme kweli, akamuuliza:

“Je, mimi nimefanya zinaa na wewe?”Yule mwanamke ghafla alianza kuona mabadiliko katika mawazo yake na akatoa jibu ambalo lilikuwa kinyume na kile alichokusudia kusema. “Hapana! Wanadanganya,” alisema. “Qaroon alinilipa kiasi hiki na hiki ili nielekeze shutuma hizi kwako.”

Qaroon alidhalilika ambapo Musa (as) alianza kutoa machozi, alianguka chini katika sajda na akaomba: “Ee Allah! Adui yako ameniumiza na alitaka kuniabisha kwa njia za uzushi. Kama mimi ni Mtume Wako, nipe mam- laka juu yake.”

Kisha akamlaani Qaroon ambapo adhabu ya Mungu ilimpata na ardhi ikammeza.3

3. Imekatazwa Kumuumiza Mu’min

Husein Ibn Abi al-A’alaa anasimulia: “Niliondoka kwenda Makka nikifu- atana na watu wengine ishirini. Katika kila sehemu ya kupumzikia nilich- inja mbuzi, ili kuwapa watu chakula. Wakati nilipotokea katika hadhira ya Imamu Sadiq (as) aliniambia:

“Ewe Husein! Ole wako, unawaumiza na kuwasabibishia Waumini usumbufu.”

“Naomba kinga kutoka kwa Allah kutokana na kitendo kama hicho.” Nilisema.

Akaelezea: “Nilijulishwa kwamba katika kila sehemu ya kupumzikia unachinja mbuzi kwa ajili ya watu uliofuatana nao.”

“Ndio, lakini kwa jina la Allah, nimefanya hivyo kwa ajili ya ridhaa Yake.” Imamu (as) aliendelea kusema: “Hujui kwamba miongoni mwa watu hao kuna baadhi, ambao hutamani kupata utajiri ili nao pia wapate kufanya matendo mema kama wewe, lakini kwa kukosa njia, wamefadhaika.”

“Natubia kwa matendo yangu na kuazimia kwamba kamwe sitatenda kwa njia hiyo tena.” Nilisema.

Imamu (as) alishauri: “Mu’min katika macho ya Mungu, ni mwenye heshima zaidi kuliko malaika, milima, mbingu saba, ardhi saba na kila kitu kilichomo humo.”4

4. Kumuudhi Imamu Ali (as) ni sawa na kumuudhi Mtukufu Mtume (saw)

Amir Ibn Shaas Aslami, mmoja wa masahaba aliyekuwepo wakati wa suluhu ya Hudaibiyah, anasimulia: “Siku moja Ali (as) na mimi tulitoka wote tukasafiri kuekea Yemen. Wakati tukiwa safarini, ilitokea nikapatwa na hasira juu yake na moyo wangu ukajazwa husda juu yake.

Nilivyorudi tu kutoka safarini, nilikwenda moja kwa moja msikitini na kulalamika kwa watu kuhusu tabia yake. Kwa bahati mbaya, ilitokea kwamba maneno yangu hatimaye yalimfikia Mtukufu Mtume (saw).

Asubuhi moja nilipoingia msikitini, nilimuona Mtukufu Mtume (saw) akiwa pale pamoja na masahaba wachache, mara tu macho yake yalipoan- gukia kwangu, aliniangalia kwa hasira na aliendelea kufanya hivyo mpaka nilipokaa.

‘Ewe Amri! Kwa jina la Allah, kwa hakika umenibughudhi!’ alisema kwa mkato.

Niliguta: “Naomba kinga ya Allah kutokana na yeyote anaye kubughudhi au anyekuudhi wewe.”

Akaseama: ‘Ndio, umenisumbua kwani yeyote yule ambaye amemsumbua Ali (as) amenisumbua mimi pia.’”5

5. Uonevu Wa Mutawakkil

Mmoja wa makhalifa waovu wa Bani Abbas alikuwa ni Mutawakkil, ambaye hakuacha chochote katika nia yake ya kumuudhi na kumtesa Imam Hadi (as), kizazi cha Mtukufu Mtume (saw), Mashi’a na wanaofanya ziyara ya Imamu Husein (as).

Gavana wa Madina, Abdullah Ibn Muhammad, kwa maagizo ya Mutawakkil, Alimsumbua Imamu Hadi (as) mpaka kufikia hali ambayo Imamu (as) alilazimika kuandika barua ya malalamiko kwa Mutawakkil.

Baadae, Mutawakkili alimlazimisha Imamu (as) kuondoka Madina na kwenda Saamarra. Hapa, alianzisha wimbi jipya la mateso na unyanyasaji, ambao baadhi ya mifano yake inafuata:

Usiku mmoja, Mutawakkil alimuita Sa’id, bawabu wake, na kumuagiza apande juu ya nyumba ya Imamu (as) na achungulie ndani kwa kuangalia mali au silaha. Kama kitaonekana chochote katika hivyo, lazima vitaifishwe.

Katika tukio lingine, akitegemea juu ya shutuma za uwongo, aliamuru kikundi cha Waturuki kuvamia nyumba ya Imamu na kuchukuwa kila kitu ambacho kitaonekena na wamlete barazani. Wakati Imamu (as) alipoletwa barazani, Mutawakkili alikuwa anajishughulisha na unywaji wa pombe na (kwa dhihaka) alitoa pombe ile kumpa mtukufu Imamu (as) na akasema: “Soma mashairi kwa ajili yangu!”

Na bado katika tukio lingine, alitaka Imamu (as) alitwe mbele yake na akaamrisha watumwa wane wa Khazar Jilfi 6 kumshambulia Imamu (as) kwa panga, Lakini Imamu (as) akitumia nguvu za uimamu, kimiujiza alizuia shambulio hili.

Katika mwaka wa 237 A.H., aliamuru kaburi la Imamu Hsein (as) na nyumba katika eneo hilo zibomelewe na alitaka eneo hilo litumike kwa ajili ya kilimo. Aliamuru kwamba mkono au mguu wa yeyote ambaye atakuja kwa ajili ya kumzuru Imamu Husein (as) lazima ukatwe.

Umar Ibn Faraj, ambaye alifanywa gavana wa Makkah na Madina na Mutawakkili aliamrishwa kuzuia watu wasitoe msaada au kuonesha huruma kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (saw). Kutokana na woga watu wakajizuia kusaidia kizazi hiki cha Mtukufu Mtume (saw) ambao hali zao zikawa za huzuni na zisizofaa kiasi kwamba walikosa hata nguo nzurri za kuvaa. Unyanyasaji na mateso haya yalifikia hatua ambayo kwamba Muntasir, mtoto wa Mutawakkil, kwa mapenzi ya Amirul Mu’minin (as) hatimaye alishawishika kumuuwa baba yake mwenyewe.7

 • 1. Mtukufu Mtume (saw) alibakia kwenye pango la Thaur kwa muda wa siku tatu na katika siku ya nne alielekea kwenda Madina, na akifikia huko tarehe 12 Rabi’ al-Awwal katika mwaka wa 13 baada ya tangazo la utume, na katika uhamiaji huu kalenda ya Kiislamu ilianzishwa.
 • 2. Jaame’ al-Sa’adaat, Jz. 2, uk. 215.
 • 3. Darsi az Akhlaaq, uk. 120; Al-Amaali (Sheikh Mufid), uk. 128.
 • 4. Hikaayat-ha-e-Shanidani, Jz. 5, uk.122; Bihaar al-Anwaar, Jz. 13, uk. 253.
 • 5. Namunah-e-Ma’arif, Jz. 2, uk. 453; La-aali al-Akhbaar, uk. 135.
 • 6. Daastaan-hai AzZindagi-e-Ali, uk. 112; Mustadrak al-Sahihain, Jz. 3, uk. 122
 • 7. Hawa walikuwa watu wapumbavu, makatili na wenye macho madogo

13) Imani

Allaha Mwenye Busara, amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا آمِنُوا بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَالْكِتَابِ الَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِ {136}

“Enyi mlioamini! Mwaminini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Kitabu ambacho amemteremshia Mtume Wake.”(Quran 4:136).

Mtukufu Mtume (saw) amesema: “Imani ni (mchanganyiko wa) kusadik- isha katika moyo, kutamkwa na ulimi na kutendwa na viungo.”1

Maelezo mafupi:

Waumini wanawekwa katika daraja kwa kutegemea kiwango chao cha imani. Imani ina nguzo nne – tawakkul2,tafwidh3,ridha,4 na taslim5 - na mtu mwenye nguzo hizi, hupata utulivu na amani, na imani huleta ustawi na hali ya kudumu. Imani ya wale ambao ni dhaifu si imara wala ya kudumu.

Je, Imamu Sadiq (as) hakusema: “Allah swt. ameutoa ulimwengu kwa marafiki Zake na halikadhalika kwa maadui Zake, lakini imani, huiweka tu kwa wale walioteuliwa kutoka miongoni mwa viumbe Wake?”

Kwa hiyo, wale ambao wana imani ya kweli na kamili siku zote wamekuwa wachache; uvumilivu ukiwa ‘waziri’ wao na hikma, ‘kamanda’ wa jeshi lao.

1. Shahada Ya Haritha

Siku moja baada ya sala ya asubuhi katika jamaa, Mtukufu Mtume (saw) aliangalia msikitini na macho yake yakaangukia juu ya kijana mmoja, Haritha Ibn Maalik Ansaari, ambaye alikaa na kichwa chake kimeinamish- wa katika hali ya kusinzia. Uso wake ulikuwa umepauka, mwili wake ukiwa umekonda na dhaifu na macho yake yalionekena kunywea katika mifuko yake. Mtukufu Mtume (saw) akamuendea Haritha na akamuuliza: “Uko kwenye hali gani.”

“Najiona mwenyewe kama muumini wa kweli.” Alijibu yule kijana.

Mtukufu Mtume (saw) akauliza: “kila kitu kina ukweli; ni ukweli gani ulioko kwenye madai yako?”

“Ewe Mtume wa Allah! Nimepoteza imani na dunia.” Alijibu. “Ninakaa macho usiku (katika ibada), na kuvumilia kiu (kwa kufunga) wakati wa mchana. Ni kama vile nashuhudia Arish ya Allah na mswada wa filamu ya Kuhesabiwa, nikiona watu wa Peponi wakitembeleana wenyewe kwa wenyewe na kusikia makele ya watu wa motoni.”

Mtukufu Mtume (saw) akasema: Huyu ni mtu ambaye Allah ameunurisha moyo wake.” Kisha wakati akizungumza na Harith aliendelea: “Umepata utambuzi na umaizi, hivyo kuwa imara.” Harith akaomba: “Ewe Mtume wa Allah! Muombe Allah anipe shahada wakati napigana sambamba na wewe!”

Mtukufu Mtue (saw) akaomba kwa Allah ampe Harith kifo cha shahada. Baada ya siku kidogo, alitoa jeshi kwenda kupigana vita na Harith aliju- muishwa humo. Wakati wa mapambano Harith aliwauwa makafiri tisa kabala ya yeye mwenyewe kuuliwa, akiwa askari wa kumi kutoka kwenye jeshi la Waislamu kuonja kinwaji kitamu cha kifo cha shahada. 6

2. Kijana Ni Nani?

Imamu Sadiq (as) wakati fulani aliwauliza wanafunzi na masahaba ambao walikuwa wamemzunguka: “Kijana ni nani?” Mtu mmoja akajibu: “Ni mtu ambaye ni mdogo kwa umri.”

Imamu akasema: “Pamoja na umri mkubwa waliokuwa nao Watu wa Pango, kwa sababu ya imani waliyokuwa nayo, Mwenyezi Mungu amewaita ‘vijana’. Katika aya ya 10 ya sura ya al-Kahf, Anasema: ‘Wakati vijana walipotafuta hifadhi katika pango’” 7

Kisha akaendelea: “Yeyote yule mwenye kumuamini Allah na kutekeleza uchamungu ni kijana.”8

3. Viwango Vya Imani

Imamu Sadiq (as) wakati akiwa anamsemesha mshonaji wa matandiko ya ngamia na farasi, ambaye alikuwa akimhudumia, alisema:

“Baadhi ya Waislamu wana sehemu moja ya imani, ambapo kuna wengine, wana sehemu mbili au tatu au hata saba. Sio sahihi kumtwishwa mtu ambaye ana sehemu moja ya imani, mzigo wa matendo ambao sawa yake ni wa mtu mwenye sehemu mbili za imani. Halikadhalika, sio sahihi kumtwisha mtu ambaye ana sehemu mbili za imani mzigo wa matendo ambao sawa yake ni wa mtu mwenye sehemu tatu za imani.”

Imamu (as) akaendelea: “Ngoja nilete mfano mmoja: wakati fulani alikuwepo mtu ambaye kwamba jirani yake alikuwa ni Mkiristo.

Yule mtu akamlingania Uislamu na yule Mkiristo akakubali na akasilimu. Siku iliyofuatia wakati wa mapambazuko, yule Mwislamu alipiga hodi mlangoni kwa yule Mkirsto aliyesilimu. Alipoitikia, yule mtu akamuambia tawadha ili twende msikitini kusali.

Yule jirani (Mwislamu mpya) akakubali bila maswali na wote wakaelekea msikitini. Walisali sio tu Sala ya Asubuhi bali vilevile na sala nyingine nyingi mpaka jua likachomoza.

“Yule Mwislamu mpya akataka arudi nyumbani, wakati yule mtu aka- muambia: ‘Unakwenda wapi, siku ni fupi na punde hivi itakuwa ni wakati wa Sala za Adhuhuri. Tungoje mpaka tusali sala zetu za adhuhuri.’ “Hivyo walisubiri mpaka Adhuhuri, wakasali sala zao. Yule mtu aliye sil- imu alijiandaa kuondoka lakini yule mtu akamshawishi akae mpaka wakati wa Alasiri. Wakasali sala ya Alasiri ambayo baada ya kumaliza yule mtu aliyesilimu aliamua kuondoka. Yule mtu akamuambia karibuni sasa jua litazama na kwamba hawapaswi kuondoka kabla ya kusali sala ya Magharibi. Na kisha akamshawishi kusubiri mpaka vilevile wasali sala ya Isha. Mwishowe, wakarudi nyumbani.

“Siku iliyofuatia wakati wa mapambazuko, yule mtu tena akapiga hodi mlangoni kwa yue mtu aliyesilimu na kumtaka waende msikitini pamoja. Yule Mwislamu mpya akajibu kwa ukali: ‘Kwa dini yako hii bwana, tafu- ta mtu mwingine mwenye muda zaidi mikononi mwake kuliko mimi. Mimi ni mtu masikini na ninayo familia ya kukimu na kutunza!’”

Imamu (as) akahitimisha kwa kusema: “Mwislamu yule mjinga akamgeuza kwenye imani yake asili, Ukirsto.” 9

4. Imani Ya Sa’id Ibn Jubair

Sa’id Ibn Jubair alikuwa mmoja wa masahaba imara na waaminifu wa Imamu Sajjad (as). Hajjaaj alikuwa mtawala dhalimu mwenye kiu ya damu ambaye ametawala Kufa, Iraq na Iran kwa takriban miaka ishirini baada ya kuteuliwa na Bani Umayya na Bani Marwaan. Ameuwa takriban watu mia moja na ishirini elfu wakati wa kipindi chake cha utawala, na miongoni mwa marafiki na kizazi cha Ali (as) aliowauwa yeye, walikuwa ni watu kama Kumail Ibn Ziyaad Nakha’i, Qambar, mtumwa wa Ali (as) na Sa’id Ibn Jubair.

Hajjaaj alimuamuru Sa’id akamatwe wakati alipojua imani ya Sa’id na mwelekeeo wake kwa Imamu Ali (as). Mwanzo, Sa’id alikimbilia Isfahan, lakini Hajjaaj alipolijua hili, aliandika barua kwa gavana wa Isfahan akita- ka akamatwe. Gavana alikuwa anamuheshimu sana Sa’id na kwa hiyo, alimshauri aondoke Isfahan na kwenda sehemu iliyo salama.

Akitenda kwa mujibu wa ushauri huu, Sa’id aliondoka na kuelekea Qum na kisha akaendelea kuelekea Azerbaijan na kisha Iraq ambako alichagua kuingia katika jeshi la Abd al-Rahmaan Ibn Muhammad, ambaye alianzisha uasi dhidi ya Hajjaaj. Abd al-Rahman alishindwa na Sa’id alikimbilia Makka ambako aliishi mafichoni.

Wakati huo, Makka ilikuwa chini ya utawala wa Khaalid Ibn Abdullah Qasri, mtu moja katili sana, ambaye amewekwa pale na Khalifa Waliid Ibn Abd al-Malik, Waliid alimuandikia barua na akampa amri ya kuwakamata watu mashuhuri wa Iraq ambao walikuwa wanajificha mjini Makka, na kisha awapeleke kwa Hajjaaj. Hivyo, alimkamata Sa’id na kufanywa apelekwe Kufa. Wakati huo Hajjaaj alikuwa katika mji wa Waasit, mji ulioko karibu na Baghdad, ambako hatimaye Sa’id alipelekwa huko.

Hajjaaj alimuuliza kuhusu yeye mwenyewe, Mtukufu Mtume (saw), Ali (as), Abu Bakr, Umar Uthman na wengine wengi na kisha akamuuliza: “Je, nikuuwe vipi?”

“Kwa namna yoyote utakayochukua kuniuwa, unapasika na adhabu kwa mujibu wa sheria Siku ya Hukumu.” Alijibu Sa’id.

“Ningependa kukusamehe”

“Kama msamaha huo ni kutoka kwa Allah, basi nautaka, lakini kama ni kutoka kwako, basi siuhitaji.” Alijibu Sa’id.

Hajjaj akaamuru mwenye kuuwa kukata kichwa cha Sa’id mbele yake. Licha ya mikono yake kufungwa nyuma ya mgongo wake, Sa’id alisoma aya ya Qur’ani Tukufu ifuatayo:

إِنِّي وَجَّهْتُ وَجْهِيَ لِلَّذِي فَطَرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ حَنِيفًا ۖ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ {79}

“Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu kwa yule aliyeziumba mbingu na ardhi. Hali ya kuwa nimeacha dini za upotevu, tena mimi si katika washirikina.” (Quran 6:79)

Alivyosikia hivi, Hajjaaj aliamuru uso wake ugeuzwe mbali na Qibla, wakati ambako alisoma aya ifuatayo:

فَأَيْنَمَا تُوَلُّوا فَثَمَّ وَجْهُ اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ وَاسِعٌ عَلِيمٌ {115}

“Basi mahala popote mnakoelekea ndiko kwenye uelekeo wa Mwenye Mungu.”

(Quran 2:115)

Wakati Hajjaaj aliposikia hivi, aliamuru watu wake kuelekeza uso wa Sa’id aridhini. Wakati hili lilipofanywa, Sa’id alisoma aya ifuatayo:

مِنْهَا خَلَقْنَاكُمْ وَفِيهَا نُعِيدُكُمْ وَمِنْهَا نُخْرِجُكُمْ تَارَةً أُخْرَىٰ {55}

“Kutokana nayo tumewaumba na humo tumewarudisha na kutoka humo tutawatoa mara nyingine.” (Quran 20:55)

Hajjaj akapiga kelele: “Usipoteze wakati tena zaidi! Muuwe!”

Sa’id akashahadia Umoja wa Mungu na Utume wa Mtukufu Mtume (saw) na akaomba: “Ee Allah! Usimpe nafasi (ya kudumu) baada yangu ili asi- uwe mtu mwingine yule.” Wakati anatamka maneno haya, mwenye kuuwa akakata kichwa chake.

Baada ya shahada ya kifano hiki cha imani, Hajjaaj alipatwa na mvurugiko wa akili na hakuishi zaidi ya masiku kumi na tano. Kabla ya kifo chake, mara kwa mara alipoteza fahamu zake, lakini wakati anazindukana, huwa anarudia rudia kutamka:

“Kwa nini nilijiingiza katika suala la Sa’id Ibn Jubair?” 10

5. Cheo Cha Salman Farsi

Imani ina daraja kumi, na Salman Farsi alikuwa juu ya daraja yake ya kumi. Alikuwa na ilmu ya ghaib, uwezo wa kutafsiri ndoto na majanga, alikuwa mjuzi katika ilmu ya nasaba (genealogy) na hata alipata upendeleo wa kupata zawadi za Peponi hapa duniani. Mtukufu Mtume alisema: “Wakati wowote Jibril alipokuwa anashuka, alikuwa akisema kwa niaba ya Allah: Fikisha salam zangu kwa Salman!”

Hapa kuna mfano wa daraja ya juu ya imani ya Salman. Wakati fulani Abu Dharr alimtembelea Salman. Salman alikuwa ameweka chombo katika moto ili kupasha moto vilivyomo humo. Watu hawa wawili wakakaa pamoja kwa muda kidogo, wakiongea, ghafla kile chombo kikapinduka juu chini, lakini kwa mshangao wa Abu Dharr vitu vilivyokuwa mle ndani ya chombo havikumwagika. Salman akakichukuwa kile chombo na na kukirudisha tena jikoni. Baada ya muda kidogo kile chombo kikapinduka tena, lakini tena vitu vilivyokuwamo ndani ya chombo kile havikumwagika. Salman akakiokota tena na kukirudisha, akakiweka sawa sawa jikoni.

Akiwa ameshangaa, Abu Dharr alitoka upesi nyumbani kwa Salman na alikuwa amezama kwenye kutafakari. Kwa bahati ilitokea njiani akakutana na Amiru’l-Mu’minin (as) na akamsimulia kisa kile. Alipokwisha sikia simulizi ya Abu Dharr, Imamu (as) alisema:

“Kama Salman angekueleza yote yale aliyonayo katika ilmu, kwa hakika ungesema: Mola wangu kuwa na huruma juu ya muuwaji wa Salman. Ewe Abu Dharr! Salman ni ‘mlango’ wa Allah juu ya ardhi. Mtu anayetambua hadhi yake ni Mu’min ambapo ambaye anamkataa ni kafiri. Salman ni katika sisi Ahlul Bayt.”11

 • 1. Muntahal Aa’maal, Jz. 2, uk. 378-384.
 • 2. Bihaar al-Anwaar Jz. 69 uk. 69.
 • 3. Kutegemea juu ya Allah.
 • 4. Mtu kuaminisha mambo yake kwa Allah.
 • 5. Kutosheka na kuridhia juu ya alichokikadira Mwenyezi Mungu.
 • 6. Kujisalimisha kwa Allah
 • 7. Al-Kafi, Jz. 2, sura ya: Ukweli wa Imani, tr. 2 & 3.
 • 8. Qur’ani Tukufu 18:10
 • 9. Namunah-e-Ma’arif, Jz. 2, uk.479; Al-Kafi, sura ya ‘viwango vya imani’, tr. 2
 • 10. Daastaan-ha-e-Maa, Jz. 2. uk. 39-45.
 • 11. Muntahal Aa’maal, Jz. 1, uk. 114

14) Undugu

Allah, Mwenye Busara, anasema:

“Hakika waumini ni ndugu”1

Imamu Baqir (as) alisema:

“Ni wajibu juu yako kuwa na marafiki wa kweli kwa ajili yako mwenyewe, kwa vile ni rasilimali wakati furaha, na ni ngao wakati wa shida.” 2

Maelezo mafupi:

Katika umri wowote, undugu na urafiki ni muhimu kwa mtu ambaye ni mwenye kustahili kwao. Allah hakuweka juu ya watumishi Wake neema muhimu zaidi kuliko mafanikio katika kukaa na kushirikiana na marafiki wenye dini.

Lakini huoni kwamba neema ya kwanza ambayo Allah aliwapa Mitume wakati wa utume wao ilikuwa ni rafiki, ndugu na wali? Ni dhahiri kutokana na hili kwamba baada ya neema ya utambuzi wa Mungu na Mitume Wake, hakuna neema iliyo safi zaidi na yenye kuridhisha kama undugu katika njia ya Allah na rafiki mwema.

Mtu anapaswa kujizuia kutokana na kufanya urafiki na undugu na wale ambao wanatafuta urafiki huu kwa ajili ya hamu ya kupata kitu au ushawishi wa dunia.

Ndugu wachache (katika dini) ambao wana utambuzi mkubwa, ni bora kuliko kuwa na ndugu wengi ambao hawana sifa hii. 3

1. Mu’min Ni Ndugu Wa Mu’min Mwingine

Imamu Baqir (as) alisema: Wakati fulani, kikundi cha Waislamu kilitoka kwenda safari, lakini katika mwendo wa safari yao, walipoteza njia yao. Punde mahitaji yao yaliwaishia na wakapatwa na kiu kubwa.

(Wakati kukukiwa hakuna dalili za maji na kufikiria mwisho wao kuwa karibu) walivaa sanda zao na wakakaa chini, wakapumzika chini ya miti.

Ghafla, mzee mmoja aliyavaa mavazi meupe aliwaendea na akasema: “Amkeni hakuna cha kuhofia. Maji haya hapa kwa ajili yenu.”

Walinyanyuka kwa shida na kunywa maji yale mpaka wakazima kiu yao, baada ya hapo walimgeukia yule mzee, wakasema: Allah akubariki! Wewe ni nani?”

“Mimi natokana na jumuiya ya majini, ambayo ilikula kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (saw). Nilimsikia akisema: ‘Mu’min ni ndugu wa Mu’min mwingine. Ni macho yake na mwongozi wake pia.’ Sikuweza kukubali ninyi mfe kwa kiu wakati mimi niko hapa.” 4

2. Fungamano La Undugu

Muhammad Ibn A’jlaan anasimulia: “Nilikuwa nimefuatana na Imamu Sadiq (as) wakati mtu mmoja kutoka mji wa mbali aliwasili na kutusalimia.

‘Ndungu zako wana hali gani uliowaacha?’ Imamu (as) alimuuliza yule mtu. Aliwataja kwa wema na akawasifia sana. Imamu (as) kisha akamuuliza: “Je, matajiri wanawatembelea mafukara wanapokuwa wag- onjwa?”

Akasema wanafanya hivyo mara chache sana. Imamu (as) aliendelea: “Je, matajiri wanatafuta kujua hali za watu masikini?” “Mara chache tu,” alijibu yule mtu.

“Je, matajiri wanawasaidia masikini na mafukara?” aliuliza Imamu (as) Yule mtu akajibu: “unazungumzia sifa ambazo ni kidogo sana miongoni mwa watu wetu.” Imamu (as) akasema: “Vipi basi watu hawa wanajiona wenyewe kuwa ni Mashi’a (wetu wakati hakuna mafungamano ya udugu kati ya matajiri na masikini).” 5

3. Katika Mlango Wa Ndugu

Imamu Baqir (as) alisema: “Siku moja malaika alikuwa anapita katika nyumba, wakati alipomuona mtu amesimama mlangoni. Yule malaika aka- muuliza: ‘Kwa nini umesimama hapa?’ “Hii ni nyumba ya ndugu yangu na nataka kumsalimia.’ alijibu yule mtu. Yule malaika akauliza: “Ni ndugu na jamaa au ni kwa sababu una haja ya msaada wake ndio maana ukaja kumtembelea?” “Ukweli sio kama unavyoufanya uwe. Sisi ni ndugu kati- ka imani na nataka kumuona na kumsalimia tu kwa ajili ya Allah.”

“Mimi ni mjumbe wa Mungu,” yule malaika akasema. Ametuma salamu kwako na Amesema: ‘Ewe mja wangu! Umenitembelea na kutamani radhi Yangu na kadhalika hivyo, kama malipo kwako kwa ajili ya kushikilia haki na utukufu wa undugu wa kidini, Nimeifanya Pepo kuwa ya lazima kwako na nimekuweka mbali na moto na ghadhabu Yangu.” 6

4. Gavana Mkarimu

Mkazi mmoja wa mji wa Rey anasimulia: “Mwandishi mmoja wa Yahya Ibn Khaalid aliteuliwa kama gavana wa Rey. Nilikuwa na baadhi ya kodi za kulipa na niliogapoa kwamba gavana mpya angezitoa kutoka kwangu, kwani kwa njia hiyo, nitakabiliana na wakati mgumu. Baadhi ya rafiki zangu walinijulisha kwamba alikuwa ni mfuasi wa mtukufu Imamu (as), lakini niliogopa kwamba kama itakuwa sio hivyo, hatasita kuniweka gerezani.

Nikiwa na nia ya kufanya Hijja, nilijitokeza mwenyewe mbele ya Imamu Musa Kadhim (as) na kumjulisha mashaka yangu. Imamu (as) aliandika barua kwa gavana, yaliyomo katika barua ni kama ifuatavyo:

‘“Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema na Mwenye kurehemu. Elewa kwamba chini ya ‘Arsh (Kiti cha Enzi Kuu) ya Mungu, kuna kivuli cha rehema ambacho kwacho hakuna atakayeingia hapo isipokuwa yule ambaye anaoenesha wema na upole kwa ndugu zake katika imani, kumuondolea huzuni zake na kujitahidi kumfanya awe na furaha. Tazama! Mtu mwenye barua hii ni mmoja wa ndugu zako. Wassalaam.’

“Baada ya kurudi kutoka hijja, usiku mmoja nilielekea kwenye nyumba ya gavana na kumuambia askari wa zamu amuambie gavana kwamba kuna mtu ameleta ujumbe kutoka Imamu Kadhim (as). Mara tu alipojulishwa, gavana alikimbilia mlangoni katika hali ya furaha tupu. Alikuwa miguu mitupu na akanikumbatia na kurudia rudia kubusu paji langu la uso, kisha akauliza hali ya Imamu.

“Wakati akiwa amekwishaisoma barua ile ya Imamu (as), alinipa nusu ya mali ambayo alikuwa nayo na nguo alizokuwa nazo, na kwa vitu visivyo- gawanyika, alinipa pesa, inayolingana na nusu ya thamani yake, huku akiniuliza baada ya kila mgao: ‘Je, nimekufurahisha?’ Nami nilimjibu: Kwa jina la Allah! Umenifurahisha mno. Alitoa kitabu chake (cha orodha ya majina na madeni yao) akafuta madeni yote yaliyoandikwa kwenye jina langu, akanipa barua yenye amri ya kunipa msamaha wa kodi zote. “Niliomba ruhusa kwake ya kuondoka na kujisemea mwenyewe: Mtu huyu amekuwa mwenye huruma mno kwangu na hakuna njia ya kumlipa ukarimu wake. Ngoja niende Hijja tena na kule nimuombee na vilevile nimjulishe Imamu (as) kuhusu ukarimu na huruma zake (gavana huyo).

Mwaka ule nilikwenda Makka na kujitokza mbele za Imamu (as), nikamjulisha kile kilichodhihiri. Wakati nikiwa nasimulia tukio hili, niliona kwamba uso wake uliendelea kung’ara kwa furaha na hivyo nika- muuliza: Je, matendo yake haya yamekufurahisha?

Akasema: ‘Kwa jina la Allah! Matendo yake kwa kweli yamenifurahisha na vilevile yamemfurahisha Allah, Mtukufu Mtume na Amiru’l-Mu’minin (as)” 7

5. Ali (A.S), Ndugu Wa Mtukufu Mtume (Saw)

Moja ya hatua za maana zilizochukuliwa na Mtukufu Mtume (saw) miezi mitano au nane baada ya kuhamia Madina, ilikuwa ni kuanzisha mafunga- mano ya undugu kati ya Muhajirina (wahamiaji kutoka Makka) na Answar (Wasidizi - wenyeji wa Madina).

Abdullah Ibn Abbas anasema: Wakati aya: Hakika waumini ni ndugu8 ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume (saw) alitangaza undugu kuwa ni kanuni ya kawaida miongoni mwa Waislamu na akichukulia vyeo na daraja zao, alianzisha mafungamano kati ya kila watu wawili kwa kuwafanya ndugu wa kila mmoja; Abu Bakr na Umar, Uthman na Abd al-Rahman na kadhalika. Amiru’l-Mu’minin (as) alikuwa amejilaza mwenyewe ardhini, wakati Mtukufu Mtume alipomwendea na akasema: “Amka, Ewe Abu Turaab! Sikukufanya wewe ndugu wa yeyote kwani nimekubakisha wewe kwa ajili yangu mimi mwenyewe. 9

 • 1. Qur’ani Tukufu 49:10.
 • 2. Bihaar al-Anwaar, Jz. 78, uk. 251.
 • 3. Tadhikirah al-Haqaaiq, uk. 52.
 • 4. Al-Kafi, j. 2, sura ya Undugu wa Mu’min, tr. 10.
 • 5. Al-Kafi, j. 2, sura ya Haki ya Mu’min juu ya ndugu yake, tr. 10.
 • 6. Namunah-e-Ma’arif, Jz. 1, uk. 81; Jaame’ al-Akhbaar, uk.118.
 • 7. Pand-e-Taarikh, j. 2, uk.47; Bihaar al-Anwaar Jz. 11, Wasifu wa Imamu Kadhim (as).
 • 8. Qur’ani Tukufu; 49:10.
 • 9. Namunah-e-Ma’arif, Jz. 1, uk. 82; Kashf al-Ghummah; Tafsir al-Burhaan.

15) Kutosheka/Kujitegemea

Allah, Mwenye Busara, anasema:

“Usikodolee macho yako yale tuliyowastareheshea makundi mbalim- bali…” 1

Imamu Ja’far Sadiq (as) amesema: “Heshima ya Mu’min iko kwenye ibada ya usiku na hadhi yake iko katika kuwa kwake mwenye kujitegemea (yaani, mwenye kutosheka bila kutegemea mtu).” 2

Maelezo mafupi:

Kinyume cha sifa ya kulaumika ya ulafi, ni sifa ya kutosheka na kujitegemea. Katika matumizi ya kawaida, kama inasemwa kwamba mtu hana haja na kitu chochote, mara moja dhana inayokuja akilini ni kwamba mtu huyo ni tajiri. Hata hivyo, maana halisi ni kuwa mwenye kujitosheleza, kujitegemea, kinaifu na sio mwenye hamu kubwa ya kupata kile walichokuwa nacho watu wengine.

Watu ambao wako huru kuhusiana na kuwategemea viumbe wa Mungu, wanaheshimika sana na wana imani juu ya Mungu ambayo ni rasilimali kubwa mno.

Ukweli kwamba kuomba na kuhitaji kutoka kwa wengine kunalaumiwa, ni kwa sababu huondolea mbali heshima na hadhi ya mtu, humfanya kuwa mfungwa wa wengine na kupunguza mwelekeo wake kwa Mungu.

1. Somo Kutoka Kwa Mtukufu Mtume (S.A.W)

Mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume (saw) wakati fulani alijikuta akiwa katika umasikini mkubwa. Mke wake alimshauri kwenda kwa Mtukufu Mtume (saw) na kuomba msaada wake.

Yule mtu akamwendea Mtukufu Mtume (saw), lakini punde tu macho ya Mtume (saw) yalipoangukia kwa mtu yule, akasema:

“Kama atataka kitu kutoka kwangu, kwa hakika nitampatia kitu hicho, lakini kama atajionesha yeye mwenyewe kuwa ni mwenye kujitegemea na huru kutokana na kuhitaji, Allah atamfanya tajiri.” 3

Kusikia hivi, yule mtu akajisemea mwenyewe: “Mtukufu Mtume (saw) amenikusudia mimi kwa maneno hayo.” Bila kusema neno hata moja, alirudi nyumbani na kuelezea tukio lile kwa mke wake. Mke wake akasema: “Mtukufu Mtume (saw) naye vilevile ni mwanadamu; elezea mtanziko wako kwake na uone atasema nini.”

Yule mtu akarudi kwa Mtukufu Mtume (saw) kwa mara ya pili, lakini akasikia kauli ileile kutoka kwake na tena akarudi nyumbani bila kusema neno. Wakati hili linarudiwa kwa mara ya tatu, yule mtu akaazima shoka kutoka kwa mmoja wa marafiki zake na akaondoka kwenda kuelekea milimani. Siku nzima alifanya kazi ya kukusanya kuni, ambazo aliziuza kwa ajili ya kununulia unga na usiku ule yeye na mke wake walipata mkate kwa ajili ya chakula cha jioni.

Siku ya pili, alifanya kazi kwa bidii sana na akakusanya kuni zaidi na hii ikaendelea kwa siku kadhaa mpaka akawa na uwezo wa kununua shoka yake mwenyewe.

Baada ya kipindi Fulani, kwa matokeo ya kufanya kwake kazi kwa bidii, aliweza kununua ngamia wawili na mtumwa, na taratibu akawa mmoja wa matajiri.

Siku moja, alipohudhuria mbele ya Mtukufu Mtume (saw), alimsimulia yale matukio ya maisha yake na athari ya maneno yake, ambapo Mtukufu Mtume (saw) alijibu: “Nilisema (kabla): “Mtu anayetaka kuwa mwenye kujitegemea, Allah atamfanya kuwa ni mwenye kujitegemea.” 4

2. Alexander Na Deozhan

Wakati Alexander alipoteuliwa kuwa kamanda mkuu wa Ugiriki, watu kutoka sehemu zote walikwenda kumpongeza kutokana na kuteuliwa kwake. Hata hivyo, Deozhan filosofa mashuhuri, hakwenda kumuona na hivyo Alexander mwenyewe akaenda kumuona Deozhan. Deozhan alikuwa ni mtu ambaye hufuata sera ya kutosheka, kujitegemea na hatengemei juu ya watu.

Wakati akiwa amelala nje akiota jua, alihisi kwamba kundi la watu lilikuwa linamjia. Alijiamsha mwenyewe kidogo na macho yake yakaangukia kwa Alexander, ambaye alikuwa akija na ufahari na ukuu, lakini Deozhan alifanya kama vile tu anavyomfanyia mtu wa kawaida anayemtembelea. Alexander akamsalimia na akasema: “Kama unahitaji kitu chochote kuto- ka kwangu, niambie tu!”

“Nina ombi moja tu.” Akasema Deozhan. “Nilikuwa nafaidi joto la jua na kwa sasa unalizuia. Je, unaweza kusogea upande mmoja?” Wale waliofuatana na Alexander, waliyaona maneno yake kuwa ya kipum- bavu na kifedhuli na wakawa wanajisemea wenyewe, wakisema: “Mtu mjinga alioje huyu kupoteza fursa kama hiyo?” Lakini Alexander, ambaye alijiona mnyonge mbele yakutosheka kukubwa na kujitegemea kwa Deozhan, alitumbukia kwenye tafakari ya kina kwenye maneno haya.

Wakiwa njiani wakirudi, aliwageukia maswahiba wake ambao walimbeza Deozhan na akasema: “Hakika nisingekuwa Alexander, ningetamani kuwa Deozhan.” 5

3. Sio Chini Ya Ufadhili Wa Avicenna

Imesimuliwa kwamba wakati fulani, Avicenna, akiwa katika msafara wa kiwaziri wenye fahari kubwa na midundo ya ngoma na matarumbeta, alikuwa anapita karibu na mfagiaji ambaye alikuwa anasoma shairi hili lifuatalo kwa sauti kubwa huku akiwa anafanya kazi yake ya mikono:

“Ee nafsi! Nimekuheshimu kwa hali ya juu sana, hivyo kwamba wewe ni njia za usafi kwa ajili ya moyo.”

Aliposikia hivi Avicenna alitabasamu na akamuambia, “Hakika, umeiheshimu nafsi yako kwa hali ya juu sana kwa kujishughulisha katika kazi duni kama hiyo.”

Yule mfagiaji akasimama kufanya kazi, akamgeukia na akasema: “Ninaendesha maisha yangu kwa njia ya kazi hii ya hali ya chini ili kwamba nisilazimike kuwa chini ya ufadhilii wa Avicenna, kiburi na mwenye makuu.” 6

4. Usomaji Wa Sura Ya Al-Waaqia’h

Abdullah Ibn Masu’d alikuwa mmoja wa masahaba wa karibu sana na Mtukufu Mtume (saw) na aliondokea kuwa mtu mashuhuri na mwenye ari katika ulimwengu wa Kiislamu. Wakati wa ukhalifa wa Uthmani alibanwa na maradhi ya ghafla, ambayo hatimaye yalisababisha kifo chake. Wakati fulani Uthmani alikuja kumtembelea na akamkuta amehuzunika, akamuuliza: “Ni kitu gani kinakuhuzunisha hivyo?”

“Dhambi zangu,” akajibu.

“Niambie unataka nini ili nikutekelezee.”

“Nataka rehema ya Allah,” alijibu Ibn Masu’ud.

Khalifa akasema: “kama utaniruhusu, ninaweza kumuita mganga.”

“Mganga huyo ndiye aliyenifanya niumwe”

“Kama unataka, ninaweza kukupa zawadi kutoka kwenye hazina ya umma.” Ibn Masu’d akajibu kwa hasira: “Wakati nilipokuwa na shida, hukunipa kitu chochote na sasa kwa vile sina shida, unataka kunizawadia!”

Uthman akasisitiza: “Ngoja zawadi hizi ziwe kwa ajili ya mabinti zako.”

“Hawana haja na zawadi zako.” Ibn Masu’d akajibu kwa mkato:

“Nimewaelekeza kusoma Sura al-Waaqia’h kila usiku, kwani kwa hakika, nimemsikia Mtukufu Mtume (saw) akisema: ‘Mtu ambaye anasoma sura ya Al-Waaqia’h kila usiku, hatapatwa na umasikini.”7

 • 1. Qur'ani Tukufu 15:88
 • 2. Jaame al-Sa’adaat, Jz. 2, uk. 108
 • 3. Man sa’alana a’atwainahu wa man istaghinaa ghanaahu llahu. (Mwenye kutuomba tutampa na mwenye kutosheka Allah atamtajirisha)
 • 4. Pand-e-Taarihk, Jz. 3, uk. 129; Wafi, Jz. 2, uk. 139.
 • 5. Riwaayat-ha Wa Hikaayat-ha, uk. 30; Daastaan-ha-e-Paraakandeh, Jz. 2, uk.86.
 • 6. Namunah-e-Ma’arif, Jz. 1, uk. 162; Naamunah-e-Daanishwaraan.
 • 7. Daastaan-ha Wa Pand-ha, Jz. 7, uk. 112; Majma’ al-Bayaan, Jz. 9, uk. 211

16) Ubahili

Allah, Mwenye Busara, anasema:

الَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ النَّاسَ بِالْبُخْلِ وَيَكْتُمُونَ مَا آتَاهُمُ اللَّهُ مِنْ فَضْلِهِ ۗ وَأَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ عَذَابًا مُهِينًا {37}

“Ambao hufanya ubakhili na huwaamuru watu kufanya ubakhili, na wakayaficha aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila yake. Na tumewaandalia Makafiri adhabu yenye kudhalilisha.”(Quran 4:37)

Mtukufu Mtume amesema: “Mtu ambaye ni mjinga lakini mkarimu ni mwenye kupendwa zaidi na Allah kuliko mtu ambaye mchamungu lakini bahili.” 1

Maelezo mafupi:

Ubahili, au kujizuia kutoa vitu kwa watu wengine na kujikusanyia mali na utajiri kwa ajili yake mwenyewe mtu, ni moja ya alama ya mapenzi ya dunia. Humkwamisha mtu kutokana na kujipamba na nemsi mbalimbali zenye manufaa kama sadaka, ukarimu, kujitolea muhanga na kuwasaidia wengine. Ni kwa sababu hii kwamba Mtukufu Mtume (saw) amesema: “Hakuna bahili atakayeingia Peponi.”

Ubahili ni uovu wenye kuchukiza kiasi kwamba kama mtu akiathiriwa nao, huiweka familia yake katika umasikini, huchukia wageni kuja nyumbani kwake, hujizuia kuwatembelea watu wengine ili mtu yeyote asimtembelee, hujiepusha kushirikiana na watu wakarimu na hujisikia vibaya kuhusu ukarimu wa watu wengine. Mtukufu Mtume (saw) siku zote huomba kinga kwa Allah kutokana na uovu huu mbaya mno. 2

1. Dhambi Ya Mtu Bahili

Wakati fulani Mtukufu Mtume (saw) alikuwa amejishughulisha katika kutufu Ka’aba mara saba wakati alipomuona mtu ameshikilia pazia la Ka’aba na huku akiomba: “Ewe Allah! Kwa utukufu wa Nyumba hii, unisamehe!”

Huku akiwa amemkaribia, Mtukufu Mtume (saw) alimuuliza kuhusu dhambi zake. Yule mtu akajibu: “Dhambi zangu ni nyingi mno kwangu mimi kuzielezea kwake.”

“Ole wako! Dhambi zako ni kubwa au ardhi?” aliuliza Mtukufu Mtume (saw).

“Dhambi zangu.” Alijibu yule mtu.

“Dhambi zako ni kubwa au milima?” aliuliza Mtukufu Mtume (saw)

“Dhambi zangu.” Alijibu yule mtu.

“Dhambi zako ni kubwa au Arshi ya Allah.” Aliuliza Mtukufu Mtume (saw).

“Dhambi zangu.” Alijibu yule mtu.

Kisha Mtukufu Mtume (saw) akamuuliza: “Dhami zako ni kubwa au Mungu.

Kwa hili yule mtu akajibu: “Mungu ni Mkubwa Wa juu mno na Mtukufu mno.”

Mtukufu Mtume akaguna: “Ole wako! Nijulishe dhambi yako.” Yule mtu akaeleza: “Ewe Mtume wa Allah! Mimi ni mtu tajiri, lakini wakati masiki- ni anaponifuata na kuniomba msaada, nahisi kana kwamba komeo la moto limenifikia.”

Aliposikia hivi Mtukufu Mtume (saw) akaonya: “Kaa mbali na mimi na usinichome na moto wako! Kwa Yule, Ambaye amenipeleka mimi pamoja na mwongozo na heshima, kama ungesali kati ya al-Rukn na Al-Maqaam kwa muda wa miaka elfu mbili na kulia katika hali ya kipimo ambacho kwamba machozi yako yanatiririka kama mito na kuzima kiu ya miti, na baada ya yote haya, kama ungekufa ukiwa bado unayo dhambi hii ya ubahili, Allah atakutupa ndani ya Jahannam. Ole wako! Lakini hujui kwamba Allah amesema:

“Na ambaye ni bahili ni bahili dhidi ya nafsi yake mwenyewe 3 na vilevile amesema: “Na ambaye ameepushwa na ubahili wa nafsi yake, ni miongoni mwa waliofuzu.” 4

2. Mansur Dawaaniqi Na Ubahili Wake

Mansur Dawaaniqi, Khalifa wa pili wa Bani Abbas, alikuwa mashuhuri sana kwa ubahili wake. Kwa mfano, kwa matokeo ya ukaidi wake wa kukataa kutoa pesa zake. Huwapa onyo washairi ambao wanakuja mbele yake, kama ifuatavyo:

“Kama mtu mbali ya wewe, ikitokea vilevile na yeye analijua shairi amba- lo unataka kulisoma hivi punde au kama ikithibitishwa kwamba ni la mtu mwingine, usitegemee kupata malipo au zawadi.” Na kama mshairi aki- tokea kusoma shairi ambalo ni lake, Mansur humpa pesa kutengemeana na uzito wa karatasi aliyoandikia shairi lile!

Aidha, ana kumbukumbu kali na vilevile ana mtumwa na kijakazi, ambao ni wepesi isivyo kawaida katika kuhifadhi vitu kichwani.

Wakati mshairi anaposoma shairi lake, Mansur humuambia: “Shairi hili ulilonisomea sio jipya. Sio mimi tu ninayelifahamu bali hata huyu mtumwa na kijakazi wangu aliyeko nyuma ya pazia, wanalijua.

Kisha, kwa ruhusa yake, yule mtumwa atasoma shairi lile ambapo baada yake, yule kijakazi, akiwa amelisikia likisomwa mara tatu – mara moja na mshairi mwenyewe, mara moja na Mansur na mara moja na mtumwa – na yeye hulisoma pia. Kisha Mshairi yule aliyepigwa na mbumbuazi hutole- wa nje mikono mitupu bila zawadi yoyote!

Asmai’i, mshairi maarufu, alichukizwa na ubahili wa Mansur, na hivyo akaamua kutunga shairi kwa kutumia maneno magumu na kuliandika juu ya nguzo ya jiwe iliyovunjika. Wakati alipokwishafanya hivi, alivaa nguo kama bedui wa jangwani na akafunika uso wake wote isipokuwa macho yake.

Kisha aliwasli mbele ya Mansur huku akiongea lafidhi bandia, alimjulisha kwamba ametunga beti kadhaa za shairi na anaomba ruhusa yake ili azisome mbele yake.

Kwa kawaida, Mansur alimjulisha Asmai’i yale masharti ambayo aliyakubali. Kisha Asmai’i akaanza kusoma shahiri lake ambalo lina maneno magumu na yasiyo ya kawaida yenye kutatiza na sentenso changa- mani. 5 Mansur pamoja na upevu wake wa akili, na mtumwa na kijakazi pamoja na ukali wa akili zao, walishindwa kulihifadhi na kwa mara ya kwanza alionekana kutatizika na kushitushwa. Bila kuwa na njia nyingine ya kufanya, Mansur akamuambia: “Ewe ndugu! Inaonekena shairi hili ni kazi yako mwenyewe. Niletee karatasi yako ili nikuzawadie kwa uzito wake.”

Asmai’i akasema: “Sikuweza kupata karatasi ya kuandikia hivyo nime- andika shairi langu juu ya nguzo ya jiwe, ambayo kwa sasa iko kwenye mgongo wa ngamia yangu.” Aliileta nguzo ile ya jiwe na kuiweka mbele ya Mansur, ambaye alichanganyikiwa kabisa.

Alitambua kwamba hata kama angeweka hazina yake yote juu ya upande mmoja wa mizani, haitalingana na uzito wa nguzo ili ya jiwe. Alimgeukia yule mshairi na akauliza: Ewe Bedui! Wewe sio Asmai’i?”

Asmai’i aliondoa nguo aliyokuwa amejifunika usoni na kila mtu akaona kwamba mshairi yule alikuwa kweli ni Asmai’i.6

3. Waraabu Wanne Mabahili

Inasemekana kwamba walikuwepo Waraabu wane mabahili: Wa kwanza wao alikuwa ni Hatiah. Imesimuliwa kwamba siku moja Hatiah alikuwa amesimama mlangoni kwake na fimbo yake mkononi, wakati mtu mmoja aliyekuwa akipita hapo aliposema:

“Ewe Hatiah! Leo mimi ni mgeni wako.” Hatiah huku akionesha fimbo yake, hujibu kwa mkato: “Natumia fimbo hii kuwakaribisha na kuwakir- imu wageni wangu kwayo!”

Bahili wa pili alikwa ni Hamiid Arqat. Kuhusiana naye, imesimuliwa kwamba siku moja aliwakaribisha watu wachache kuwa wageni wake na akawapa tende ili wapate kula. Wale wageni wakati wakila tende zile, walikula na mbegu zake vilevile ambapo Hamiid alisababisha vurugu kwa kuwakemea kwa ajili ya kula tende na mbegu zake pia.

Bahili wa tatu alikuwa mtu mmoja kwa jina Abul Aswad Duali. Imesimuliwa kwamba siku moja alimpa ombaomba tende moja, ambaye alisema: “Mungu akupe tende moja katika Pepo.”

Aliposikia hivi, Abu Aswad Duali akasema: “Kama tukiwapa vitu watu mafakura tutakuwa mafukara kuliko wao!”

Bahili wa nne alikuwa ni Khaalid Ibn Safwaan, kuhusu yeye imesemwa kwamba wakati wowote dirham inapokuja kwenye mikono yake, ata- iambia: “Ewe pesa! Ni kiasi gani ulichohangaika na kusafiri kabla ya kufi- ka mikononi mwangu. Lakini (kwa vile umenifikia mimi) nitakuweka kwenye kasiki yangu, na ufungwa wako utakuwa wa muda mrefu na wa kuendelea.”

Wakati akisema hivi, huidondosha dirham ile kwenye kasiki yake na kuifunga.

Watu wakamuambia: “Kwa vile unamiliki mali nyingi mno na utajiri, kwa nini hutoi baadhi kama sadaka?” Akajibu: “Nina muda mrefu wa kuishi mbele yangu.” 7

4. Zakaat Kutoka Kwa Tha’laba Ansaari Haikukubaliwa.

Wakati fulani Tha’laba Ibn Haaib Ansaari alimuendea Mtukufu Mtume (saw) na kumuomba: “Ewe Mtume wa Mungu! Niombee kwa Mungu ili anipatie mali na utajiri.”

“Mali kidogo ambayo kwayo unaweza kutoa sadaka ni bora kuliko utajiri mkubwa ambao kwamba huwezi kutoa sadaka,” Mtukufu Mtume (saw) alimshauri. Tha’laba aliondoka lakini alimwendea Mtukufu Mtume kwa mara ya pili, na akarudia ombi lile tena. Mtukufu Mtume (saw) akasema: “Hutanitii. Kwa jina la Allah! Kama ningetaka kwamba milima igeuke dhahabu kwa ajili yangu, ingefanya hivyo.”

Mara ile tena akaondoka zake, lakini alirudi mara ya tatu tena na kutoa ombi lake tena kwa Mtukufu Mtume (saw) na kusihi: “Niombee tu. Naapa kwamba kama Mungu atanipa mali, yeyote mwenye haki kwayo, nitampatia.”

Mtukufu Mtume (saw) akamuombea na Mungu akajibu maombi yake. Tha’laba kwa kuanzia alinunua kondoo, ambao polepole waliongezeka idadi mpaka wakawa wengi.

Mwanzo, alikuwa akiswali Swala zake zote nyuma ya Mtukufu Mtume (saw), lakini baada ya mali na utajiri wake kuanza kuongezeka, aliweza tu kuhudhuria Swala ya Dhuhr na A’sir, na muda wote uliobaki aliutumia kuangalia kondoo wake.

Kadri muda ulivyokuwa ukipita, kazi zake ziliongezeka kufikia hali ambayo aliweza tu kuja Madina kwa ajili ya Swala ya Ijumaa na hatimaye hata hili likawa ni jambo lililopita. Alikuwa tu akija kwenye barabara iendayo Madina na kuuliza habari za mji huo kwa wapita njia.

Siku moja, Mtukufu Mtume (saw) alimuulizia, ambapo alijulishwa kwamba kondoo wa Tha’alaba wameongezeka marudufu na amefanya makazi yake nje ya Madina. Kusikia hivi, Mtukufu Mtume (saw) akatamka kwa sauti kubwa mara tatu: “Ole wake Tha’laba!”

Baada ya muda, aya inayohusu Zakaat iliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (saw). Mtukufu Mtume akateua watu wawili, mmoja kutoka Bani Sulaim na mwingine kutoka Bani Juhiyah, na akawapa mamlaka ya kimaandishi, kuwawezesha kukusanya Zakaat. Walipomwendea Tha’alaba, walimsomea amri ile kwa ajili ya kukusanya Zakaat. Baada ya kufikiri kidogo, Tha’alaba akasema: “Hii ni Jizyah (kodi ya kichwa) au kitu kinachofanana nayo. Nendeni mkakusanye kwa watu wengine na kisha mje kwangu.”

Walikwenda kwa mtu wa kabila la Bani Sulaim na wakamsomea amri za Mtukufu Mtume ambazo kwazo aliwakabidhi mmoja wa ngamia wake aliye bora kama Zakaat.

Wale wakusanyaji wakamueleza kwamba hawakumtaka atoe ngamia aliye bora katika ngamia zake, lakini akasisitza kwa kusema kwamba alikuwa anatoa ngamia huyo kwa hiari yake mwenyewe.

Wakusanyaji wakakusanya Zakaat kutoka kwa watu wengine na wakati wa kurudi, walimwendea tena Tha’alaba na wakataka Zakaat yake. Akasema: “Hebu leteni niione hiyo amri.” Baada ya kuisoma, alirudia tena kusema: “Hii inaonekana kuwa ni Jizyah au kitu kama hicho. Nendeni zenu na acheni mimi nifikirie juu yake hilo”

Wakusanyaji wakarudi kwa Mtukufu Mtume (saw), lakini kabla hawajase- ma aliguta: “Ole juu ya Tha’alaba!” na kuomba kwa ajili ya ukarimu kuto- ka kwa watu wa Bani Sulaim. Wale wakusanyaji walimsimulia kwa dhahiri jinsi walivyokabiliana na Tha’alaba ambapo aya ifuatayo iliteremshwa:

وَمِنْهُمْ مَنْ عَاهَدَ اللَّهَ لَئِنْ آتَانَا مِنْ فَضْلِهِ لَنَصَّدَّقَنَّ وَلَنَكُونَنَّ مِنَ الصَّالِحِينَ {75}

فَلَمَّا آتَاهُمْ مِنْ فَضْلِهِ بَخِلُوا بِهِ وَتَوَلَّوْا وَهُمْ مُعْرِضُونَ {76}

فَأَعْقَبَهُمْ نِفَاقًا فِي قُلُوبِهِمْ إِلَىٰ يَوْمِ يَلْقَوْنَهُ بِمَا أَخْلَفُوا اللَّهَ مَا وَعَدُوهُ وَبِمَا كَانُوا يَكْذِبُونَ {77}

“Na miongoni mwao wako waliomwahidi Mwenyezi Mwenyezi Mungu: Akitupa fadhila zake hakika tutatoa sadaka na hakika tutakuwa miongoni mwa watendao wema. Lakini alipowapa katika fadhila Zake, walizifanyia ubakhili wakageuka na huku wakipuuza. Kwa hiyo ukawalipa unafiki katika nyoyo zao mpaka siku ya kuku- tana nao. Kwa sababu ya kumhalifu Mwenyezi Mwenyezi Mungu yale waliyomwahidi na kwa sababu ya kusema kwao uwongo.”(Quran 9:75-77)

Moja wa jamaa wa Tha’alaba ambaye alikuwepo wakati wa aya hii ilipoteremshwa, alimjulisha Tha’alaba tukio hili. Baada ya kusikia hivi, aliharakia kwa Mtukufu Mtume (saw) na akamsihi akubali Zakaat yake, lakini alikataa akisema: “Mwenyezi Mungu ameniamuru nisipokee Zakaat yako.” Tha’lab alifadhaika aliposikia hivi.

“Haya ni matokeo ya matendo yako mwenyewe. Nimekuamrisha lakini umekataa kukubaliana na amri zangu,” alisema Mtukufu Mtume (saw).

Baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (saw) Tha’alab alimwendea Abu Bakr, ambaye naye alikataa kupokea Zakaat yake.

Wakati wa ukhalifa wa Umar, Tha’alaba alimwendea, lakini na yeye alikataa na Uthman naye aka- fuata mwendo huohuo, mpaka hatimaye kifo kikamchukua Tha’alaba.8

5. Sa’id Ibn Harun, Mbahili

Sa’id Ibn Harun, mwandishi kutoka Baghdad na wa zama moja na Ma’mun, Khalifa wa Bani Abbas, alikuwa akivuma vibaya kwa ubahili wake.

Abu Ali Dibil Khazaai, mshairi mashuhuri (amekufa 245 A.H.) anasema: “Nikiwa nimefuatana na baadhi ya washairi, nilikwenda nyumbani kwa Sa’id na tulikuwa pamoja naye kuanzia asubuhi mpaka mchana. Wakati adhuhuri ilipokuwa inakaribia, alianza kusikia njaa na matokeo yake akawa anahangaika.

Sa’id alikuwa na mtumwa mzee, ambaye alimuambia, “kama kuna kitu cha kula, hebu tuletee.” Yule mtumwa aliondoka na kurudi muda mfupi akiwa amechukuwa kitambaa kichafu cha chakula.

Alikitandika mbele yetu na akaweka juu yake kipande kimoja tu cha mkate mkavu. Kisha akaleta bakuli lililovunjika midomo yake lililojazwa maji ya moto, na ambalo lina jogoo mzee asiyepikwa na asiye na kichwa!

Wakati yule mtumwa anaweka lile bakuli kwenye kitambaa cha chakula, acho ya Sa’id yakaangukia juu yake na akaona yule jogoo asiye na kich- wa, alifikiria kwa muda kidogo na kisha akasema, “Ewe Mtumwa! Kikowapi kichwa cha jogoo huyu?” Yule mtumwa akajibu: “Nimekitupa.”

Alivyosikia hivi, Sa’id alipiga kelele: “Simruhusu yeyote mwenye kutupa miguu ya jogoo, achilia mbali kichwa chake. Kitendo hiki (chako) huwashiria ubaya (kwangu) kwani kichwa cha jogoo kina faida nyingi: Kwanza, kutokana na kichwa chake hutoka sauti ambayo huwajulisha waja wa Mwenyezi Mungu kuhusu muda wa Swala; kwa njia yake hii, waliolala huamka na wale wanaofanya ibada wakati wa usiku kujiweka tayari kwa sala za usiku.

“Pili, taji lake ambalo liko juu ya kichwa chake hufanana na taji la wafalme, na hivyo ana heshima ukilinganisha na ndege wengine. Tatu, hushuhudia malaika kwa njia ya macho mawili ambayo yamewekwa kwenye fuvu lake. Kwa nyongeza, washairi hufananisha rangi ya mvinyo na macho yake, kwa sababu wanapotaka kuelezea mvinyo mwekundu, wanasema: ‘Mvinyo huu ni kama macho mawili ya jogoo.’

“Nne, ubongo katika kichwa chake ni tiba ya matatizo ya mafigo. Aidha, hakuna mfupa ulio mtamu mno kama mfupa wa kichwa chake. Kama ulikitupa kwa mawazo kwamba sitakila, umekosea sana, na hata kama sikuki- la, familia yangu wangekila na kama hawatakila, hawa wageni wangu, ambao hawajakula chochote tangu asubuhi, wangekila.”

Aliendelea kwa hasira, “Nenda ukakilete na ukishindwa kufanya hivyo, nitakuadhibu.” Yule mtumwa akaomba kwa kusihi: “Wallahi! Mimi sijui ni wapi nilipokitupa.” Sa’id akasema kwa hasira: “Wallahi! Najua ni wapi umekitupa, umekitupa kwenye huo mtumbo wako mbaya!” “Wallahi! Mimi sikukila,” alilalama yule mtumwa, “wewe ndiye unaongopa.”

Huku akiwa amechukia, Sai’id alisimama na akamkamata yule mtumwa kwenye shingo kwa nia ya kumtupa chini kwenye sakafu, lakini katika harakati hizo mguu wake ukakanyaga lile bakuli likageuka na vyote vilivyokuwa ndani vikamwagika. Paka ambaye alikuwa amekaa karibu, alitumia fursa hiyo na kuokata yule jogoo asiye na kichwa na kuondoka naye. Sisi pia tukatoka ndani ya nyumba ile, tukamuacha Sa’id akizozana na mtumwa wake. 9

 • 1. Jaame’ al-Sa’adaat, Jz. 2, uk. 110.
 • 2. Thyan al-Qulub, uk. 96.
 • 3. Qur’ani Tukufu; 47:38.
 • 4. Qur’ani Tukufu; 59:9.
 • 5.
 • 6. Daastaan-ha-e-Maa, Jz. 2, uk.102; I’laam al-Naas, uk. 54.
 • 7. Namunah-e-Ma’arif, Jz. 2, uk. 463; Mustatraf, Jz. 1, uk. 171.
 • 8. Pand-e-Taarikh, Jz. 1, uk. 73; Asaad al-Ghaabbah, Jz. 1, uk. 237.
 • 9. Lataaif al-Tawaaif, uk. 341.

17) Uovu

Allah, Mwenye hikma anasema:

“Mnaweza mkakipenda kitu wakati ni kiovu kwenu”1

Imamu Sadiq (as) amesema: “Kwa hakika madhara ya uovu kwa mtendaji ni ya haraka sana kuliko yale ya kisu kwa nyama”2

Maelezo mafupi:

Mtu mbaya kuliko wote ni yule ambaye huuza Akhera yake kwa ajili ya maisha ya dunia hii, lakni mbaya zaidi ni yule ambaye huuza Akhera yake kwa ajili ya maisha ya dunia ya watu wengine.

Uovu hujidhihirisha katika sura mbalimbali, zote ambazo zinaweza kufupishwa kwa utovu wa utii wa Allah.

Kwa vile matendo yanategemea nia, fikra za kiovu huzaa matendo maovu. Mtu anapokuwa hana Allah katika upeo wake, hujiona kuwa na nguvu.

Hujiingiza katika aina mbalimbali za matendo maovu, bila moyo wake kuhisi hata chembe ndogo ya hofu ya moto wa Jahannam.

Kwa kila kiungo cha mwili kuna matendo maovu yanayohusiana nacho; masikio kwa utesi, macho kwa kuona vilivyokatazwa, ulimi kwa kusema uongo, na mikono kwa kuwadhuru mayatima. Hivyo ni lazima kuvihifadhi vyote dhidi ya uovu.

1. Mkosi Wa Jaludi

Baada ya shahada ya Imam Kadhim (as). Harun Al-Rashid, Khalifa kuto- ka ukoo wa Abbasi, alimtuma mmoja wa makamanda wake kwa jina la Jaludi kwenda Madina na alimuagiza: “Shambulia nyumba ya kizazi cha Abu Talib, waporeni wanawake na msiache chochote isipokuwa nguo moja kwa kila mmoja wao!”

Alipokuwa Madina Jaludi alianza kutekeleza amri ya Harun. Alipokaribia nyumba ya Imam Ridha (as), Imam (as) aliwakusanya wanawake wote wa nyumba ile katika chumba kimoja na yeye alisimama mlangoni, akimzuia Jaludi kuingia.

Jaludi alisisitiza kwamba lazima aingie ndani ya nyumba na kuwapora wanawake na kuchukua nguo zao. Imam (as) aliahidi kuwa yeye mwenyewe angekusanya nguo na mapambo yao na kuvikabidhi kwa Jaludi, kwa sharti kwamba ajiepushe kuingia ndani ya chumba.

Hatimaye Jaludi alikubaliana na ombi la Imam (as) ambapo (Imam) aliingia ndani ya chumba, akakusanya nguo na mapambo ya wanawake pamoja na vitu vingine vya ndani, kisha akamkabidhi Jaludi, ambaye mara moja alivipeleka kwa Harun.

Baada ya Harun, akawa mwanae Ma’mun, aliye chukua hatamu za ukhal- ifa. Ilitokea kwamba siku moja aliudhiwa na Jaludi na akataka kumpa adhabu ya kifo. Imam Ridha (as) alikuwepo katika baraza hilo na alimuomba Ma’mun amsamehe.

Jaludi kwa kukumbuka uovu wake wa nyuma aliomfanyia Imam, alifikiri kwamba Imam (as) angemlalamikia Ma’mun kuhusu uovu wake na hivyo, alimgeukia Ma’mun, (na) kusema: “Nakuweka chini ya kiapo cha Allah! Usikubali maneno yake kuhusiana na mimi.”

Maamun akasema: “(Naapa) kwa Allah! Sitakubali maneno yake” Alipo sema hivi, aliamuru Jaludi akatwe kichwa.3

2. Udanganyifu Wa Amr Ibn A’as

Baada ya tukio la upatanishi, ambapo Amr Ibn A’as, alimdanganya kwa hila Abu Musa Asha’ri na kumuondoa Ali (as) kutoka katika ukhalifa, Imam (as) alikuwa akiwalaani Amr Ibn A’as, Muawiya na Abu Musa baada ya sala za asubuhi na magharibi. Amr Ibn A’as pia alikuwa ni sehemu ya kundi lililohusika katika tukio la usiku Aqabah4 na hatimaye alilaaniwa na Mtukufu Mtume (saw).

Mzozo kati ya Imam Ali (as) na Muawiya ulipoongezeka, iliamuliwa kwamba shauri hili liamuliwe kwa upatanishi. Kwa bahati mbaya, watu wa Iraq walimchagua Abu Musa Ashari kumuwakilisha Imam (as) (Ingawa Imam mwenyewe hakufurahia uchaguzi huu), ambapo Muawiya alimch- agua Amr Ibn A’as kuwa muwakilishi wake.

Abu Musa, ambaye alikuwa katika moja ya vijiji vya Sham, aliombwa kuwasili Siffin na watu 400, miongoni mwao Shuraih Ibn Haani na Ibn Abas, waliambatana naye hadi Daumah al-Jundal, Amr Ibn A’as pia ali- wasili hapo na wenzake 400.

Ushauri na mapendekezo yote yaliyotolewa kwa Abu Musa (na watu wake) hayakufaa kitu kwani Amr ibn A’as kwa uovu wa nia na ufidhuli wa tabia aliokuwa nao, alikuwa na nguvu sana katika hila na udanganyifu kuliko yeye (Abu Musa).

Moja ya mbinu za Amr Ibn A’as ilikuwa ni kuonyesha heshima iliyotiwa chumvi juu ya Abu Musa. Alimuweka mbele ya mkusanyiko na alisistiza kwamba (Abu Musa) aongoze swala, huku Amr mwenyewe akiswali nyuma yake, na mara zote alipokuwa akiongea naye alimuita ‘Ewe sahaba wa Mtume wa Allah!’ Alikuwa akimuambia: “ulinitangulia katika usahaba wa Mtukufu Mtume (saw) na ni mkubwa kwangu, na hivyo sio sawa kwa mimi kusema juu ya lolote kabla wewe hujafanya hivyo.” Alionyesha heshima fulani ya uongo mpaka Abu Musa mwenye akili finyu akashawishika juu ya unyofu wake na akawa ana hakika kuwa nia yake pekee ilikuwa ni kuyaweka mambo vizuri. Kama sehemu ya mipango wake wa hila, awali Amr Ibn A’as alimchukua Abu Musa sehemu ya faragha na akaongea naye pembeni ili kuwazuia wengine wasimshawishi Abu Musa katika kufanya maamuzi.

Amr Ibn A’as alimuuliza, “Abu Musa, nini maoni yako juu ya Ali (as) na Muawiya?”

“Tuwaondoe Ali (as) na Muawiya katika ukhalifa na turuhusu suala la ukhalifa liendeshwe na Shuura,” alijibu Abu Musa.

Aliposiki hivi, Amr Ibn A’as alisema: “(Naapa) kwa Allah! Maoni yako ni sahihi kabisa na ni lazima tuyatekeleze” Baada ya kukubaliana hivi, wakaja mbele ya umma.

Abu Musa alisimama kwanza na akaanza kuzungumza wakati Ibn Abbas alipopiga kelele: “Kuwa makini kwani nina hofu Amri Ibn A’as amekute- ga. Mruhusu aongee kwanza kabla yako.”

Lakini Abu Musa alipuuza na kusema, “Eyi watu! Amr Ibn A’as na mimi tunawaondoa Ali na Muawiyya kutoka kwenye ukhalifa na tutamuidhin- isha tu Khalifa atakayechaguliwa kwa njia ya Shuura, hivyo ninamuondoa Ali (as) kutoka kwenye ukhalifa.”

Kisha Amr Ibn A’as muovu akasimama na kusema: “Mimi pia nina muon- doa Ali katika ukhalifa na ninamteuwa Muawiyya katika sehemu yake. Muawiyya anataka kulipiza kifo cha Uthman na hivyo anastahili zaidi wadhifa huu.”

“Wewe ni kama mbwa,” alipayuka Abu Musa “ambaye hushambulia mtu akimsogelea na hufanya vivyo hivyo pia mtu akimpa mgongo.

Amr Ibn A’as alilipiza, “Na wewe ni kama punda, ambaye hubeba mzigo wa vitabu lakini hafaidiki navyo hata kidogo”

Kwa kifupi, Amr Ibn A’as akisaidiwa na uovu wake aliibuka mshindi katika shauri la upatanishi! Baadaye Ibn Abbas alikuwa akisema: “Allah amfedheheshe Abu Musa! Nilikuwa nimemuonya juu ya nia ya kiovu ya Amr Ibn A’as na nilimshauri vyema, lakini alijifanya kiziwi na akakataa kuzingatia.”5

3. Ukatili Wa Hajjaji Ibn Yusuf Thaqafi

Sio matendo maovu tu yanayostahili adhabu bali nia za kiovu pia huwa na madhara. Kwa kweli ni kutokana na nia zao za kiovu kwamba makafiri na maadui wa Uislamu watakaa motoni milele.

Hajjaaj Ibn Yusuf Thaqafi alikuwa akionyesha ukatili mkubwa na uovu kwa kuwatilia sumu na kuwaua Masaadaat (kizazi cha Mtukufu Mtume). Wakati fulani, alipokuwa akitoka msikitini na kusikia vilio vya idadi kubwa ya watu, aliuliza “Ni akina nani hawa wanaolia?” Wale waliokuwe- po wakasema: “Hivyo ni vilio vya mateka, wanaoteswa kwa joto kali la jua.” Akasema: “Waambieni ‘ikhsanuu!’ (Ambaa au toka) ambalo ni neno la Kiarabu ambalo hutumika kumfukuzia mbwa.6

Gereza lake lilikuwa na wanaume 120, 000 na wanawake 20, 000 (4000 kati ya hawa wakiwa hawajaolewa ) na lilikuwa ni eneo moja kubwa lenye kuta lakini halikuezekwa (halina paa), kila wakati wafungwa walikuwa wakijaribu kujihifadhi kutokana na jua linalo unguza, ama kwa mikono yao au kwa njia nyingine, walinzi waliokuwa wakiwatizama walikuwa wakiwarushia mawe.

Chakula chao kilikuwa ni mikate iliyotengenezwa kwa shayiri na kuchanganywa na michanga, wakati kinywaji chao kilikuwa ni maji machungu. Wakati fulani, damu ya Masaadaat na watu waongofu ilikuwa ikitumika kuandalia mikate ya Hajjaj ambayo alikuwa akiila kwa furaha kubwa!

Mtu huyu muovu, mara zote alikuwa akisikitika kwa kutokuwepo Karbala na alikuwa akisema: “Oh! Ni jinsi gani natamani ningekuweko Karbala ili niwe mmoja katika walioshiriki kumuua Imam Husein (as) na masahaba zake!”7

4. Kuhalalisha Matendo Maovu

Imam Sadiq (as) alikuwa amesikia kwamba kuna mzee mmoja ambaye amekuwa maarufu kwa uchamungu wake. Siku moja alimuona akiwa amezungukwa na umati mkubwa wa watu.

Muda mfupi baadaye alitoka kwenye umati ule na akajitenga nao akaenda peke yake, ambapo Imam (as) alianza kumfuata. Baada ya muda mfupi Imam (as) aliona kwamba alikuwa amesimama karibu na duka la mikate ambapo kwa wizi alichukua mikate miwili. Baada ya umbali mfupi alisimama kwenye duka la matunda, akachukua makomamanga mawili kwa staili ileile na kwa mara nyingine tena akendelea na safari yake.

Alivyokuwa akitembea zaidi, mzee yule alimuendea mgonjwa akamkabid- hi mikate na matunda na alikuwa anataka kuondoka Imam Sadiq (as) alipomuendea na kusema, “Nimeshuhudia kitu kilichonishtua sana kutoka kwako,” na kisha akaendelea kumsimulia matukio aliyoyafanya. Yule mzee akasema, “Nafikiri wewe ni Imam Sadiq (as)” Imam (as) alijibu kwa kukubali. Yule mtu aliendelea, “Kwa hakika ni bahati mbaya kwamba licha ya kuwa ni kizazi cha Mtukufu Mtume (saw) hauonyeshi kujua chochote.”

Imam (as) akauliza, “Ni kitendo gani cha ujinga ulichokigundua kutoka kwangu?” Yule mtu akasema, “Lakini hujui kuwa Allah amesema katika Qur’ani:

مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا ۖ وَمَنْ جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا {160}

‘Yeyote afanyaye wema atalipwa mara kumi zaidi na yeyote afanyaye uovu, atalipwa mfano wake (mara moja)’ (Quran 6:160)

“Kwa msingi huu, nimeiba mikate miwili na matunda mawili nina mad- hambi manne katika hesabu yangu lakini katika upande mwingine, kwa kuwa nimetoa kwa njia ya Allah, nina thawabu arobaini. Ukipunguza nne katika arobaini, bado nina thawabu 36 katika hesabu yangu, nakuonea huruma, hauna maarifa ya mahesabu haya.”

Imam (as) akamueleza, “Lakini hujasikia aya hii ya Qur’ani inayosema:

إِنَّمَا يَتَقَبَّلُ اللَّهُ مِنَ الْمُتَّقِينَ {27}

‘Allah hukubali tu kutoka kwa wale wanaojilinda (na maovu).’ (Quran 5:27).

Umepata madhambi manne kwa kuiba na madhambi manne zaidi kwa umpa mwengine bila ruhusa ya wamiliki, hivyo umekusanya madhambi nane lakini hujapata thawabu hata moja.”

Baadaye Imam (as) aliwaambia masahaba zake, “kwa tafsiri hizo na uhalalishaji huo, sio tu kwamba wanajipotosha wao wenyewe, bali wanawapotosha na wengine pia.8

5. Matokeo Ya Uovu Huko Barzakh

Mwanazuoni mashuhuri, maarufu kwa uchamungu wake anasimulia: “Mmoja wa ndugu zangu alikuwa amenunua mali katika mwaka wa mwisho wa uhai wake, akitumia kipato kikubwa kilichotokana na mali hiyo kwa kukidhi mahitaji yake. Alipokufa, nilimshuhudia akiwa katika eneo la adhabu, katika hali ya upofu. Nilipomuuliza sababu yake alijibu:

“Nilikuwa nimenunua kipande cha ardhi, ambacho katikati yake kulikuwa kisima ambacho maji yake yalikuwa yakitumiwa na wakazi wa kijiji cha jirani, wao wenyewe na wanyama wao. Lakini njia yao katika ardhi yangu ilikuwa ikiharibu sehemu ya mazao yangu, hivyo, ili kulinda kipato changu na kuzuia wasiingie, nilikifukia kisima kwa mchanga na mawe na nikakifunika.

Matokeo yake wale wakazi wenye bahati mbaya walilazimika kusafiri umbali mrefu kwenda kupata maji yao, na huu upofu ni matokeo ya kitendo changu hicho.”

“Nilimuuliza, ‘Je kuna suluhisho lolote la tatizo lako hili?’ Alijibu, ‘Kama warithi wangu wangeonyesha huruma juu yangu na kukifungua kisima kile ili wengine wanufaike kutokana na maji yake tena, nitaondokana na tatizo langu hili.’

“Nilipowaendea warithi wake, niliwajulisha juu ya tukio hili walikubali kufanya msaada na haraka, kisima kilifunguliwa, na watu wakaanza kukitumia kama zamani.

“Baada ya muda nilimshuhudia marehemu tena, lakini mara hii niliona kuwa amerudishiwa kuona kwake na alinishukuru kwa kumsaidia kutoka katika taabu yake.’9

 • 1. suratul Baqara 2:216 .
 • 2. Taz. Jaame al- Saadat, Juz. 3, uk. 48.
 • 3. Raahnama –e- Sa’adat, Juz, 1, uk. 177; Aayaan al- Shi’ah, Juz. 1, uk. 60
 • 4. Baadhi ya watu walikusanyika pamoja wakala njama na kujificha karibu na njia ya mlima na kumshitua ngamia wa Mtukufu Mtume (saw) ili aangushwe chini na kuuawa. Na huu ni usiku ambao unaitwa “usiku wa Aqabah”
 • 5. Paighambar wa Yaaran, Juz. 1 uk. 136- 153; Biharul Anwar, Juz. 8, uk. 544
 • 6. Qur’ani Tukufu 23:108 - maneno waliyoambiwa watu wa motoni.
 • 7. Pand-e-Tarikh, Juz.3, uk. 163; Randhaat al-Jannaat, uk 133
 • 8. Namunah-e- Maarif, Juz. 4, uk. 275; Wasailul Shia, Juz. 2, uk 57
 • 9. Daastaan –ha-e Shigif, uk. 292

18) Misiba

Allah Mwenye hikma amesema:

فَأَمَّا الْإِنْسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ {15}

“Na kwa mwanaadamu, Mola Wake anapomjaribu, na kisha humtendea hisani ni kumfanya aishi maisha rahisi, husema: Mola wangu amenitukuza.”(Quran 89: 15)

Mtukufu Mtume (saw) amesema:

“Kwa hakika msiba kwa dhalimu huwa adhabu (yenye kurekebisha) na kwa muumini huwa ni mtihani”1

Maelezo mafupi:

Kwa mtu mwenye akili, misiba ni njia ya mapambo na heshima. Kuwa na uvumilivu mtu anapokabiliwa na msiba na kuwa imara wakati wa mitihani, huimarisha imani yake.

Mtu anayekabiliana na ugumu kwa subira, atapata rehema ya Allah, kama ilivyoelezwa na hikma ya kimungu, atapata uokovu na raha, ama hapa kati- ka ulimwengu huu au Akhera.

Kutoka katika moto wa majanga na misiba, huibuka mwanga wa pekee. Mtu ambaye huchukulia balaa na msiba kama mtihani, na hukabiliana nao vilivyo, atakuwa na busara zaidi kutokana na elimu ya ziada na uelewa aliopata. Sio mwenendo mzuri kulalamika kila mara juu ya misiba ya kidunia kama umasikini, maradhi, matatizo ya kifamilia nk.

1. Pamoja Na Malaika

Mmoja wa wagonjwa waislamu, ambaye alikuwa halalamiki juu ya misiba, alikuwa ni mtu aliyekuwa akiitwa Imran. Aliugua ugonjwa wa jongo na hakuna matibabu yaliyomsaidia. Kwa miaka 30 alilalia tumbo lake akiwa hawezi kuinuka, kukaa au kusimama, na hivyo shimo lilikuwa limechimbwa jirani na alipopumzika kwa ajili ya mkojo na kinyesi.

Siku moja ndugu yake A’laa, alimtembelea na alioona ile hali yake ya kuhuzunisha aliangua kilio, Imran alimuuliza, “Kwa nini unalia?” Ndugu yake alijibu, “Ni kwa sababu ninaona kwa miaka umekuwa ukitaabika katika hali hii ya kuhuzunisha”

Imran akasema, “usilie na usihuzunike kwa sababu hali hii, ambayo Allah amenipangia, inapendeza zaidi kwangu kuliko kitu kingine chochote, ninatamani nibakie katika hali hii ambayo Allah amenipangia, kwa muda wote nitakaoishi. Sasa nitakujulisha siri, ambayo haupaswi kuivujisha kwa yeyote katika muda wote nitakao kuwa hai; nipo pamoja na malaika, wananisalimia na mimi ninaitika salamu zao, na nipo karibu nao sana.2

2. Ali A’abid Gerezani

Ali A’abid (Ali Ibn Hassan Al-Muthallath) alikuwa ni mmoja wa watoto wa Imam Hasan (as) ambaye alikuwa amefungwa na Mansur Dawaaniqi na alikufa akiwa gerezeni. Ali A’abid alikuwa mstari wa mbele katika subira, ibada na kumkumbuka Allah.

Mansur alipowakamata watu wa kizazi cha Mtukufu Mtume (saw) na watoto wa Imam Hasan (as) aliwaweka katika gereza lililokuwa na giza sana kiasi kwamba mchana hauwezi kutofautishwa na usiku, isipokuwa kwa visomo na matendo ya ibada ya Ali A’abid. Matendo haya yalikuwa na mpangilio, yanayozingatiwa kwa nidhamu na ya kuendelea, na hivyo aliwafanya wengine wajue nyakati za sala.

Siku moja, kutokana na shida za kuwa mateka na uzito wa masaibu yake, Abdullah Ibn Hasan Al-Muthanna alipoteza subira na katika hali ya mashaka makubwa, alimuambia Ali A’abid: “Je hushuhudii mabalaa na hali ngumu? Hauombi kwa Allah ili atupe nafuu ya mateso yetu?”

Ali Aabid alibakia kimya kwa muda kisha akasema: “Ewe Ami! Kuna nafasi tukufu kwa ajili yetu Peponi, ambayo kamwe hatuwezi kuipata isipokuwa kwa kufanya subira katika hali hizi ngumu na hata ngumu zaidi ya hizi, na kwa ajili ya Mansur kuna nafasi mbaya kabisa ndani ya moto wa jahannam, ambayo hawezi kuifika isipokuwa kwa kututia katika mateso. Tukiwa na subira punde tu tutajikuta katika wepesi na raha, kwani kifo hakiko mbali na sisi. Lakini ukitaka nitaomba kwa ajili ya nusra yetu, lakini nikifanya hivyo, Mansur hatafikia hatua ile ya uovu, ambayo amepangiwa ndani ya jahannam.”

Aliposikia hivi, Abdullah mara moja alisema “Tutakuwa na subira”. Hazikipita siku tatu, Ali A’abid akafariki dunia huku akiwa katika sijida.

Abdullah alifikiri amelala na akasema “Amka mwanangu” Walivyojaribu kumnyanyua waliona hainuki na ndio wakajua kuwa amekufa.

3. Adui Aliyepangiwa Muumini

Nabii Huud (as) alikuwa akilima. Siku moja kundi la watu lilikuja katika nyumba yake kuja kuonana naye. Mke wake alikuja mlangoni na kuuliza: “Huyo ni nani?”

Walijibu, “Tumetoka katika mji kadha wa kadha, ambao umekumbwa na njaa na tuko katika hatari ya kuangamia. Tumekuja kwa Nabii Hud (as) ili kumuomba aombe dua kwa ajili ya mvua.”

Mke wa Hud (as) alisema: “Kama dua yake ingekuwa ni ya kujibiwa, angejiombea yeye mwenyewe, mazao yake mwenyewe yananyauka kutokana na ukosefu wa maji.”

Waling’ang’ania, “Yuko wapi hivi sasa?”

Aliwajulisha aliko ambapo kundi lile lilimwendea na kuwasilisha ombi lao kwake. Nabii Hud (as) alisali na kisha akaomba dua, baada ya hapo ali- wageukia na kusema, “Mnaweza kurudi kwani imenyesha katika mji wenu.”

Lakini walivyokuwa wanataka kuondoka, walimuuliza, “Tulipokwenda nyumbani kwako tulikutana na mwanamke, ambaye alisema: ‘Ikiwa dua za Hudi zingekuwa zinajibiwa, yeye mwenyewe siangekuwa amejiombea yeye mwenyewe?’”

Nabii Hud (as) akasema, “Mwanamke huyo ni mke wangu na ninamuom- ba Allah ampe maisha marefu.” “Kwa nini unaomba hivyo?” waliuliza wale watu.

Yeye akajibu, “Allah hakuumba muumini (yeyote), ila pia amempangia adui wa kumsumbua. Mwanamke huyu ni adui yangu na adui ambaye mimi niko juu yake, ni bora kuliko adui ambaye (yeye) anakuwa juu yangu.” 3

4. Muhammad Ibn Abi Umair Aliwatumikia Maimam Watatu (As)

Muhammad Ibn Abi Umair alipata fursa ya kuwatumikia Imam Kadhim, Imam Ridha, Imam Jawad (as), na wote Sunni na Shia wameshuhudia uaminifu na uongofu wake.

Alikuwa ni mfanya biashara wa nguo kitaaluma, na kifedha alikuwa tajiri. Aliandika vitabu 94 juu ya hadithi na fiqh. Kutokana na tabia yake njema na ujuzi wake wa majina ya Mashi’a, alikuwa akisumbuliwa sana wakati wa kipindi cha Harun Al-Rashid na Ma’mun, alikuwa akikashifiwa, akitiwa gerezani na mali yake ilipokonywa. Aliombwa awe jaji lakini alikataa ofa hiyo; kwa vile alikuwa anawafahamu Mashi’a wa Iraq, aliombwa kufichua majina yao, lakini alikataa kufichua majina yao, hivyo wakamtupa gerezani na mara nyingi alikuwa akicharazwa bakora nusu ya kufa. Wakati fulani, kwa amri ya Harun Rashid, Sindi Ibn Shaahak alimcharaza bakora 120 na alipaswa kununua uhuru wake kwa kulipa diriham 1000, kifedha alipata hasara ya diriham 100,000 na alibaki kuwa mfungwa kwa miaka minne.

Dada yake (Saidah au Minnah) alikusanya vitabu vyake vyote akavificha, lakini ilitokea siku moja, mvua ikanyesha na vitabu vyake vyote vika- haribiwa. Baadaye, hadithi alizokuwa akisimulia zilikuwa zinatokana na kumbukumbu kali aliyokuwa nayo au nakala ambazo wengine walikuwa wamezinakili kutoka kwenye vitabu vyake vya asili kabla ya kuharibuwa.4

5. Maisha Marefu Huambatana Na Mabalaa

Imesimuliwa kuwa wakati fulani Jibril (as) alimuendea Nabii Suleimani (as) akimletea bakuli lenye maji ya uhai na akamwambia: Mola wako amekupa chaguo ambalo ukilichagua, unaweza kunywa maji haya na kubaki hai hadi siku ya hukumu.

Suleimani (as) aliliweka suala hii mbele ya kundi la watu, majini na wanyama, akawataka ushauri na wote wakamshauri kuwa anywe yale maji na aweze kuwa wa milele.

Suleimani baada ya kutafakari, alibaini kuwa alikuwa hajapata maoni ya nungunungu na hivyo akamtuma farasi akamwite, lakini nungunungu hakuja. Kisha alimtuma mbwa na hapo akaja mara moja!

Suleiman (as) akamwambia, “Kabla sijataka ushauri wako juu ya shauri langu, ningetaka kujua kwa nini nilipomtuma farasi mnyama anaye hes- himiwa zaidi hukuja, lakini nilipomtuma mbwa, mnyama mbaya kuliko wote, uliwasili mara moja?” Nungunungu alijibu, “Farasi licha ya kuwa mnyama anayeheshimika, hana utii, ambapo mbwa licha ya kuwa mnyama mbaya kuliko wote, ana utii; akipokea mkate kutoka kwa mtu, hubakia kuwa mtiifu kwake katika maisha yake yote.”

Kisha Suleiman (as) akasema, “Bakuli lenye maji ya uhai limeletwa kwangu na nimepewa chaguo, ama niyakubali au niyakatae. Wengine wote wamenishauri niyanywe ili niwe wa milele.”

Nungunungu akasema, “Je maji haya ya uhai ni ya kwako tu au watoto wako, familia na marafiki wanaruhusiwa kuyanywa pia?” Akasema, “Hapana! Ni kwa ajili yangu tu.”

Kisha nungunungu akashauri, “Ni busara ukayakataa, kwani utakapopata maisha marefu, watoto wako wote, ndugu na marafiki wataondoka kabla yako, kila siku inayopita itakuwa ikikuletea msiba na huzuni na hivyo kufanya maisha yako kuwa machungu.” Suleiman (as) aliukubali ushauri huu na akauzingatia, (kwa) kuyarejesha maji ya uhai.5

 • 1. Jaamee’al-Akhbaar, uk. 113
 • 2. Dasaataan-ha- Wa panda, Juz, 7 uk. 148: La –aali al- Akhbaar, Juz.1 uk. 346
 • 3. Namunah-e- Ma’arif, Juz. 2 uk.612
 • 4. Mantahal Aamaal, Juz. 2, uk. 358
 • 5. Jawaame’ al-Hikayaat, uk. 95

19) Maradhi

Allah, Mwenye hikima, anasema:

“Na ninapougua hunirjeshea afya yangu.”1

Imam Ali (as) amesema: Kibaya zaidi ya umasikini ni maradhi ya mwili.”2

Maelezo mafupi:

Moja ya hazina za pepo, ambazo humfikia muumini katika ulimwengu huu ni maradhi. Ikiwa muumini wakati fulani na bila kukusudia atakosea na kufanya dhambi, Allah hataki (muumini) huyo arudi kwake akiwa amebeba mzigo wa dhambi, hivyo humpatia maradhi ili madhambi yake yasamehewe.

Mtu anayetaabika kwa maradhi humuomba Allah amrejeshee afya yake na Allah huipenda hali hii ya mgonjwa, kwani anataka mja wake aongee na kuwasiliana naye. Wakati mwingine Allah humpatia mtu maradhi ili kulinyanyua daraja lake la kiroho.

Mbora miongoni mwa wale wanaoumwa ni yule anayefanya subira katika mateso haya na kuficha maumivu yake na anajiepusha kulalamika juu ya ugonjwa wake kwa wengine mpaka anarejewa na afya yake na hupata malipo ya juu kabisa aliyopangiwa.

1. Daraja La Muumini Anayeteseka Kwa Mardhi

Siku moja Mtukufu Mtume (saw) alinyanyua kichwa chake mbinguni na kisha akacheka, mmoja wa masahaba zake alimuuliza sababu ya kucheka, ambapo Mtukufu Mtume (saw) alijibu kwa kusema:

“Kicheko changu kimetokana na mshangao. Malaika wawili walikuwa wameteremka kutoka mbinguni kuja kurekodi amali za muumini muongofu, mara zote walikuwa wakimkuta katika msala wa kusalia. Lakini safari hii waliona kwamba hayupo.

Alikuwa kitandani, akiwa amepatwa na maradhi. Walipanda mbinguni na kumuambia Allah: ‘Ewe Mola! Hatukumkuta mja wako katika sehemu yake ya ibada ya kawaida lakini badala yake tumemkuta amelala kitandani katika hali ya maradhi.

“Allah aliwaambia: ‘Hadi atakaporejewa na afya yake rekodini matendo yake yote ya ibada na amali njema alizokuwa akizifanya alipokuwa na afya. Ni wajibu kwetu kumlipa amali zote njema alizokuwa akizifanya alipokuwa na afya njema katika kipindi chote atakachokuwa anaumwa.’”3

2. Binti Yangu Hakupata Kuugua Kamwe!

Wakati fulani, Mtukufu Mtume (saw) alitoa pendekezo la kumuoa mwanamke mmoja. Baba yake alianza kumsifu (binti yake) na huku akieleza sifa zake, akisema: “Tangu alipozaliwa mpaka leo, kamwe hajapata kuugua.” Mtukufu Mtume (saw) aliposikia hivi aliondoka katika mkusanyiko huo.

Baadaye alisema, “Hakuna wema katika mwili ambao, kama punda milia, huwa hauugui. Magonjwa na misiba ni zawadi za Allah kwa waja wake ili wasije wakamsahau, maradhi na misiba husaidia kumfanya mtu amkum- buke (Allah).

3. Subira Katika Maradhi

Abu Muhammad Raqqi anasema: Wakati fulani niliwasili katika hadhara ya Imam Ridhaa (as) na nikamsalimia. Aliitika salamu yangu akauliza juu ya afya yangu na akaanza kuzungumza nami. Katika mazungumzo ghafla akasema: “Ewe Abu Muhammad, kila Mu’mini ambaye Allah humpatia misiba na ambaye hufanya subira, kwa hakika atakuja kupata daraja na malipo ya shahidi mbele ya macho ya Allah.”

Nilishangaa, Ni kwa uhusiano gani Imam (as) alisema hili? Hatukuwa tunazungumzia juu ya majanga na misiba, kwa Imam (as) ghafla kuibuka na aina hii ya kauli?

“Nilimuaga Imam (as) na nikaenda kwa rafiki zangu na wasafiri wenzangu ambapo ghafla nilisikia maumivu katika mguu wangu. Nilikesha na maumivu makali na asubuhi kulipopambazuka niliona kwamba mguu wangu umevimba.

Baada ya muda, uvimbe huu ukawa unauma sana. Nilikumbuka kauli ya Imam Ridha (as) ambapo alikuwa ameshauri subira katika mabalaa na jinsi nilivyokuwa nimewaza kuwa haukuwa umetolewa katika wakati muafaka.

“Katika hali hii nilifika Madina lakini huko, kidonda kikubwa kilikuwa katika mguu wangu, kikawa kinatoa usaha. Maumivu yalikuwa makali sana kiasi kwamba sikuwa na amani. Kisha nikaelewa kwamba Imam (as) alikuwa ameshajua hali hiyo pale alipozungumza nami na kunishauri kuwa mtulivu kwa njia ya subira. Kwa miezi kumi nilikuwa kitandani kutokana na ugonjwa huu.”

Msimuliaji anasema: Baada ya muda Abu Muhammad alirudiwa na afya yake kisha akaugua tena, hatimaye akafariki kwa ugonjwa huo.4

4. Imam Sajjad (As) Awasaidia Wakoma

Wakati fulani Imam Sajjad (as) alikutana na wakoma wakiwa wamekaa kandokando ya barabara na wakila chakula.

Aliwasalimia kisha akapita ghafla tena akasimama na kujisemea: “Allah hawapendi wenye kujivuna.”

Baada ya kusema hayo alirudi nyuma, akawendea wakoma na kusema, “Kwa sasa, nimefunga (na hivyo siwezi kukaa chini na kula nanyi chakula chenu. (Hata hivyo) ninawaalika na kuja nyumbani kwangu na kuwa wageni wangu.”

Waliukubali mwaliko huo na wakaenda nyumbani kwake ambako Imam aliwalisha na akawasaidi kwa kuwapa fedha.5

5. Deni La Mgonjwa Lalipwa

Usama Ibn Zaid alikuwa ni mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume (saw). Wakati fulani aliugua na hivyo Imam Husein (as) akamtembelea. Alipokaribia, Imam Husein (as) alimuona akiwa katika msukosuko mkubwa, akipiga mayowe mara kwa mara na kuonyesha maumivu makali.

Imam (as) akamuambia, “Ndugu (yangu)! Ni nini kinakufanya uwe na msukosuko huo na uwe na mashaka?”

“Nina mzigo wa deni la dinar 60,000” alijibu. Imam (as) alimfariji kwa kumuambia ninachukua jukumu la kulipa deni lako.

Usamah aling’ang’ania, “Nina hofu nitakufa kabla deni langu halijalipwa.” Imam (as) akasema, “Usiwe na wasiwasi! Nitalipa deni lako kabla ya kifo chako.” Aliposema hivi Imam Husein (as) aliamuru deni lake lilipwe mara moja.6

 • 1. Quran 26:80
 • 2. Nahju’l-Balaghah ya Faidh al-Islam, uk. 1270
 • 3. Daastaan-ha Wa Pand-ha, Juz. 6 uk.130, Tafsirul Nur al- Thaqalain, Juz. 5, uk. 68
 • 4. Hikaayat Shanidani, Juz.1, uk.166; Bihaar al- Anwaar, Juz. 45, uk 51
 • 5. Baa madrum, katika Guneh Barkhod Kuneem, uk 38
 • 6. Paighambar wa Yaara, Juz. 1, uk.193; Bihar aal- Anwaar, Juz. 10, uk.43

20) Wazazi

Allah, Mwenye hikma, amesema:

“Msiwaambie neno la dharau wala msiwafukuze.”1

Mtukufu Mtume (saw) amesema: “Wema kwa wazazi ni bora kuliko swala, swaumu, Hija, Umra na jihad katika njia ya Allah.”2

Maelezo mafupi:

Katika maeneo mbalimbali ndani ya Qur’ani, Allah amezungumzia suala muhimu sana na wema kwa wazazi; akiweka umuhimu mkubwa sana kiasi kwamba amefikia hata kusema:
“Msiwaambie Shh! wala msiwalaumu, na waambieni maneno mazuri.”

Ni dhahiri kwamba kutokana na aya hii si kwamba tu imekatazwa kuwaud- hi kwa njia yoyote, bali ni wajibu kuwafanyia wema na hisani. Watu wanaowaumiza (mioyo) wazazi wao, hata mara chache, lazima waombe msamaha wao na furaha yao kabla hawajaonja madhara yake, wanatakiwa wakumbuke kuwa watoto wao nao, baadae watakuja kuwatendea mabaya pia.

Juu ya matokeo yake huko Akhera, Mtukufu Mtume (saw) amesema: Ikiwa kwa kila tendo moja la kuwaumiza (mioyo) wengine mlango mmoja wa Jahannam hufunguka kwa ajili ya mtu huyo, basi milango miwili ya Jahannam itafunguka kwa yule anayewaudhi wazazi wake.3

1. Radhi Ya Mama

Mtukufu Mtume (saw) alimuendea kijana aliyekuwa anakufa na akamwambia: “Ewe kijana! Sema Laa Ilaaha illallah,” lakini ulimi wa kijana ulikuwa unashindwa kunyanyuka na ulikuwa unashindwa kutamka sentensi hiyo. Mtukufu Mtume (saw) aliuuliza umati uliokuwepo ikiwa mama wa kijana huyo alikuwepo. Mwanamke aliyekuwa amesimama karibu na kichwa cha yule mtu anayekufa, alisonga mbele na kusema yeye ndio mama yake.

Mtukufu Mtume (saw) alimuuliza ikwa alikuwa radhi na mwanawe ambapo alijibu “Hapana, sijaongea naye kwa muda wa miaka sita iliyopita.” Mtukufu Mtume (saw) akasema “Ewe mwanamke! Msamehe huyu na muwie radhi.” Yule mwanamke alikubali na akasema “Kwa sababu yako, ninamsamehe. Allah awe radhi naye!”

Mtukufu Mtume (saw) alimgeukia tena yule kijana na kumuomba atoe sha- hada na mara hii, baada ya kupata radhi ya mama, yule kijana aliweza kufanya hivyo.

Mtukufu Mtume (saw) alimuuliza, “Ewe kijana! Ni nini unacho kishuhudia wakati huu?” Akasema, “Ninamuona mtu mbaya kabisa wa sura ambaye anatokwa na harufu mbaya na ambaye anasubiri kuninyonga”

Mtukufu Mtume (saw) alimuelekeza yule kijana kusoma dua hii:

“Ewe ambaye unakubali amali njema chache na kusamehe madhambi mengi! Kubali kutoka kwangu amali njema chache na samehe madhambi yangu mengi, kwani wewe ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa rehema.”

Yule kijana aliposoma dua hii, Mtukufu Mtume (saw) akamuuliza tena anachoshuhudia. Akajibu: “Sasa ninamuona mtu mwenye nuru na mwenye sura ya kupendeza.

Amevaa nguo nzuri na ana harufu ya kuvutia. Anaonyesha wema na tabia njema kwangu.” (Baada ya kusema hivi yule kijana akafariki).4

2. Sahaba Wa Nabii Musa (As) Peponi

Wakati fulani Nabii Musa (as), alipokuwa anazungumza na Allah, aliom- ba: “Ewe Mola! Ninatamani kumuona mtu atakaye kuwa sahibu yangu peponi.” Jibril alishuka na kumuambia kuwa sahibu yake atakuwa ni muuza nyama aliyekuwa anaishi sehemu fulani. Nabii Musa alitoka na kwenda kumtafuta na akafika katika duka lake, ambapo alimuona kijana anayefanana na walinzi wa usiku akiwa katika hekaheka akiuza nyama.

Usiku ulipofika yule kijana alichukua nyama na akenda nyumbani kwake. Musa (as) alimfuata hadi walipo fika huko. Musa (as) alimfuata kijana huyo na kusema, “Je usingependa upate mgeni?” Yule kijana alikubali kwa moyo mkunjufu na akampeleka ndani.

Musa (as) alimtazama yule kijana akiandaa chakula. Alipomaliza alileta kikapu kikubwa kutoka ghorofa ya juu, humo akamtoa mwanamke mzee na kikongwe, alimuosha kisha akaendelea kumlisha kwa mikono yake mwenyewe. Wakati yule kijana alipotaka kukirudisha kikapu kwenye sehemu yake, Musa (as) aliona midomo ya yule bibi ikicheza alipokuwa akisema kitu fulani ambacho hakikueleweka. Kisha yule kijana akaleta chakula na wote wakakaa kula chakula cha usiku.

Musa (as) aliuliza “Ni uhusiano gani ulionao na huyu bibi kizee?”

Yule kijana alijibu “Ni mama yangu, na kwa vile hali yangu kifedha hainiruhusu kununua kijakazi kwa ajili yake, mimi mwenyewe nina jitahidi kumhudumia na kumtizama”

Musa (as) akauliza zaidi: “Ni maneno gani aliyoyasema mama yako kabla hujampeleka juu? Alijibu, “Kila ninapomuogesha na kumlisha huomba na kusema: Allah akusamehe na akuweke pamoja, na katika daraja la Nabii Musa (as) peponi.”

Alipo sikia hivi, Musa (as) akasema, “Ewe kijana! Ninakupa bishara njema: Allah amekubali dua ya mama yako na Jibril amenijulisha kuwa utakuwa sahibu yangu peponi!”5

3. Laana Ya Mama

Katika kabila la Bani Israil, alipata kuishi mchamungu mmoja kwa jina la Jareeh, ambaye alikuwa akijighulisha katika ibada ya Allah katika jumba lake la makasisi. Siku moja mama yake alimuendea alipokuwa anasali, na hivyo hakumuitikia. Akamwita kwa mara ya pili, lakini tena Jareeh hakumjibu. Hili lilipotokea kwa mara ya tatu, alikasirika na akamlaani kwa kusema, “Ninamuomba Allah asikusaidie!”

Siku inayofuata, malaya mmoja alikuja katika jumba la makasisi na kuzaa mtoto hapo na akatangaza: “Huyu ni mtoto wa Jareeh niliye mzalia”

Hili lilizua mtafaruku miongoni mwa watu ambao waliwaza, “Mtu huyu huyu ambaye hutufokea kwa uzinifu, yeye mwenyewe ameufanya.” Mfalme aliamuru apelekwe sehemu ya kunyongea watu. Mama yake Jareeh alipolijua hili, alianza kuupiga uso wake kwa sononeko ambapo (Jareeh) alimwambia, “Nyamaza, kwani ni kwa sababu ya laana yako ndio ninajikuta katika matatizo haya.”

Watu wakamuuliza: “Ewe Jareeh! Tutajuaje kama unasema kweli?” Aliwaambia wamlete mtoto kwake. Mtoto alipoletwa, alisali kisha akamhoji mtoto, “Baba yako ni nani?” mtoto kwa nguvu za kimungu na ruhusa akasema, “Baba yangu ni fulani na ni mchungaji (wa mifugo) na anatoka katika kabila fulani.”

Tukio hili liliyanusuru maisha ya Jareeh ambapo baada ya hapo aliapa kutotengana na mama yake na kumtumikia katika maisha yake yote.6

4. Kinyozi Mkweli

Mwanazuoni mkubwa, Sheikh Baqr Kadhim, aliyeishi karibu na Najaf-e- Ashraf, anasimulia kwamba kinyozi mkweli, alipata kusimulia hadithi hii:

“Nilikuwa na baba mzee, niliyemtumikia kwa bidii, nilifanya uangalifu mkubwa kamwe sikumpuuza, kiasi kwamba nilikuwa nikimuwekea maji chooni na ninabaki nikimsubiri nje hadi anapotoka. Katika wiki nzima nilikuwa nikimtizama isipokuwa siku za Jumatano jioni ambapo nilikuwa nikienda Masjidi Sahlah nikitarajia kukutana na Imam Mahdi (as).

“Jumatano moja nilikuwa na shughuli nyingi na sikupata wakati hadi jua lilipokuwa linakaribia kuzama. Hata hivyo nilitoka kwenda Masjidi Sahlah peke yangu gizani.

“Ulikuwa ni usiku wa mbalamwezi na nilikuwa nimesafiri theluthi moja ya safari yangu, ghafla nilipomuona mwarabu akiwa amekaa juu ya ngamia akinijia. Nilijisemea, “Mwarabu huyu kwa hakika atanipora” lakini alipokuja karibu, aliongea kwa lafudhi yetu na alitaka kujua nilikokuwa ninaelekea.

“Nilimwambia kwamba nilikuwa ninakusudia kwenda Masjidi Sahlah ambapo aliniuliza kama nilikuwa na kitu cha kula nilipomwambia sikuwa nacho, akasema: “Una chakula mfukoni mwako.” Nilipoingiza mkono mfukoni, nilikuta zabibu kavu nilizonunua kwa ajili ya mwanangu wa kiume lakini nilisahau kumpatia.

Kisha yule mwarabu akasema, “Ninakushauri uende ukamhudumie baba yako” alisema hivi mara tatu, kisha ghafla akatoweka. Ni baadaye nilipokuja kubaini kuwa alikuwa ni Imam Mahdi (as) mwenyewe niliyekuwa nimemuona na kwamba hakupendezwa kwamba nimeacha kumhudumia baba, hata kwa kusudio la kwenda Masjidi Sahlah siku za Jumatano jioni.7

5. Kumpiga Baba

Abu Quhaf, baba wa Abu Bakr, alikuwa ni mmoja wa maadui wa Mtukufu Mtume (saw). Wakati fulani alimkashifu Mtume (saw) na hivyo mwanae Abu Bakr alimchukua na kumpiga kwenye mlango.

Habari za tukio hili zilipomfikia Mtukufu Mtume (saw) alimwita Abu Bakr na kuuliza: “Je ulifanya jambo kama hilo kwa baba yako?” Abu Bakr alijibu kwa kukubali.

Mtukufu Mtume (saw) akasema, “Ondoka nenda zako, lakini kuanzia sasa na kuendelea, usimfanye tabia kama hii kwa baba yako.8

 • 1. Qur’ani Tukufu, Al-Israil 17:23
 • 2. Jaame’ al-sa’adat, Juz. 2, uk. 264
 • 3. Ihyaa al- Quluub, uk.129
 • 4. Darshai Az- Zindagi-e-payaambar, uk.116; Al-Amaali (Sheikh Tusi) Juz. 1, uk.63
 • 5. Pand-e- Taarikh, Juz.1, uk. 68; Tuhfa-e-Shaahi (Faadhil Kaashifi)
 • 6. Naamunah-e-Ma’arif, Juz. 2, uk. 548; Hayaat Al- Quluub, Juz. 1uk.482
 • 7. Muntahal Aamaal, Juz. 2, uk. 476; Najm al – Thaaqib
 • 8. Daastaan-ha Wa Pand-ha, Juz. 10, uk. 128; Wasa’ail al-Shi’ah, Juz.1, uk. 115 (Chapa ya zamani)

Orodha Ya Vitabu Viliyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation

1. Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na Nne
2. Uharamisho wa Riba
3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza
4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili
5. Hekaya za Bahlul
6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.)
7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.)
8. Hijab vazi Bora
9. Ukweli wa Shia Ithnaashari
10. Madhambi Makuu
11. Mbingu imenikirimu
12. Abdallah Ibn Saba
13. Khadijatul Kubra
14. Utumwa
15. Umakini katika Swala
16. Misingi ya Maarifa
17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia
18. Bilal wa Afrika
19. Abudharr
20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu
21. Salman Farsi
22. Ammar Yasir
23. Qur'an na Hadithi
24. Elimu ya Nafsi
25. Yajue Madhehebu ya Shia
26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu
27. Al-Wahda
28. Ponyo kutoka katika Qur'an.
29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii
30. Mashukio ya Akhera
31. Al Amali
32. Dua Indal Ahlul Bayt
33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna.
34. Haki za wanawake katika Uislamu
35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake
36. Amateka Na Aba'Khalifa
37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s)
38. Adhana.
39 Upendo katika Ukristo na Uislamu
40. Nyuma yaho naje kuyoboka
41. Amavu n’amavuko by’ubushiya
42. Kupaka juu ya khofu
43. Kukusanya swala mbili
44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara
45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya
46. Kusujudu juu ya udongo
47. Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s)
48. Tarawehe
49. Malumbano baina ya Sunni na Shia
50. Kupunguza Swala safarini
51. Kufungua safarini
52. Umaasumu wa Manabii
53. Qur’an inatoa changamoto
54. as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm
55. Uadilifu wa Masahaba

56. Dua e Kumayl
57. Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu
58. Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake
59. Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata
60. Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s)
61. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza
62. Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili
63. Kuzuru Makaburi
64. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza
65. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili
66. Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu
67. Tujifunze Misingi Ya Dini
68. Sala ni Nguzo ya Dini
69. Mikesha Ya Peshawar
70. Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu
71. Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka
72. Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje?
73. Liqaa-u-llaah
74. Muhammad (s) Mtume wa Allah
75. Amani na Jihadi Katika Uislamu
76. Uislamu Ulienea Vipi?
77. Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s)
78. Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)
79. Urejeo (al-Raja’a )
80. Shahidi kwa ajili ya Ubinadamu
81. Utokezo (al - Badau)
82. Kuanzia ndoa hadi kuwa wazazi
83. Myahudi wa Kimataifa
84. Uislamu na dhana
85. Mtoto mwema
86. Adabu za Sokoni
84. Johari za hekima kwa vijana
85. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza
86. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili
87. Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu
88. Tawasali
89. Imam Mahdi katika Usunni na Ushia
90. Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu
91. Hukumu ya kujenga juu ya makaburi
92. Swala ya maiti na kumlilia maiti
93. Shiya na Hadithi (kinyarwanda)
94. Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu
95. Hadithi ya Thaqalain
96. Fatima al-Zahra
97. Tabaruku
98. Sunan an-Nabii
99. Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)
100. Idil Ghadiri
101. Mahdi katika sunna
102. Kusalia Nabii (s.a.w)
103. Ujumbe -Sehemu ya Kwanza
104. Ujumbe - Sehemu ya Pili
105. Ujumbe - Sehemu ya Tatu
106. Ujumbe - Sehemu ya Nne
107. Shiya N’abasahaba
108. Iduwa ya Kumayili
109. Maarifa ya Kiislamu.
110. Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza
111. Ukweli uliopotea sehemu ya Pili
112. Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu
113. Ukweli uliopotea sehmu ya Nne
114. Ukweli uliopotea sehmu ya Tano
115. Johari zenye hekima kwa vijana
116. Safari ya kuifuata Nuru
117. Historia na sera ya vijana wema
118. Myahudi wa Kimataifa
119. Shahidi kwa ajili ya ubinadamu
120. Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

Back Cover

Katika Qur’ani, kuna sura iitwayo al-Qasas (Masimulizi), ambayo yenyewe tu ni ushahidi kuwa mwanadamu anahitaji hadithi na masimulizi.

Katika sehemu nyingi ndani ya Qur’ani, hadithi za Mitume na wafalme wa mataifa zimetajwa. Kwa kuongezea Mwenyezi Mungu amezungumzia masuala yanayohusiana na vita, amani, familia, dini, jamii na mada nyinginezo, katika muundo wa hadithi na masimulizi. Kwa kuvisoma visa hivi, watu wanaweza kuelewa na kutofautisha kati ya njia ya maendeleo na ile ya kuporomoka kwa maendeleo, na kupanda na kushuka katika kila kipengee, hususan maadili.

Kitabu hiki ambacho kiko katika sehemu tano, kimekusanya takriban visa vya kweli 500 juu ya maadili mema katika masuala ya uaminifu, imani, misiba, uchamungu, toba, ujinga, maombi, subira na mengine mengi.

Inatarajiwa kutoka kwa wasomaji kwamba, baada ya kuvipitia visa na simulizi hizi, watatafakari na kuchukua mazingatio ili waweze kujijengea nguvu za kwenda katika ukamilifu wa maadili, na Allah akipenda wale waliojaaliwa maadili yenye kusifika wawasimulie wengine ili kuzireke- bisha roho dhaifu.

Kimetolewa na kuchapishwa na:

Alitrah Foundation
S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2110640 / 2127555
Barua Pepe: alitrah@raha.com
Tovuti: www.ibn-tv.org