Mtume (s.a.w.w.) Amesema

1. Kwa hakika kifo (shahada) cha Hussein kitaamsha mori, katika nyoyo za waumini, ambao hautapoa milele.

2. Amrisheni mema na kukataza maovu. La sivyo, waovu watatawala na mwito wenu, kuwa yule aliye bora (anapasa kutawala), hautatiwa maanani.

3. Yeyote anayekwenda kwa tajiri na kujifanya mnyonge mbele yake, kwa sababu ya mali aliyonayo, huwa ameshapoteza thuluthi mbili za dini yake.

4. Mfano wa watu wa nyumba yangu ni kama vile safina ya Nuhu. Yeyote aliyeipanda, aliokoka. Na aliyebaki nyuma (asiipande), alighariki.

5. Yeyote anayependa kumfurahisha mtawala wake, japo kwa kitu kidogo kitakachokuwa ni sababu ya kumuudhi Mola wake, huwa ameshaitoka dini ya Mwenyezi Mungu.