Imam Husayn (a.s) Amesema

1. Kufa katika utukufu ni bora kuliko kuwa na maisha ya udhalilifu.

2. Taifa linalonunua starehe za maisha kwa kubadilishana na hasira za Muumba, halipati kuongoka.

3. Iwapo hamna dini (mnayoiamini), basi kueni (angalau) watu walio huru.

4. Tahadhari na uepukane na ushirika wa mtu dhalimu, maana yeye hukuuza kwa kupata tonge moja (ya chakula) ama kiasi kidogo zaidi ya hicho.

5. Uhusiano, ushirikiano na tangamano na watu wanaotenda dhulma na ukatili, husababisha lawama na kutoaminiwa.