8. Kijalizo. Barua ya Wazi Kwa Wahubiri na Ma-Imamu wa Sunna

Twawauliza: kwa nini twaweka vikao vya mawaidha, khususan katika siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Muharram; na hatufanyi hivyo katika miezi mengine iliyobaki ya mwaka mzima?

Hakuna hadith (dalili) ambayo inatuambia tufanye hivyo, (kuzichukua siku kumi za Muharram na kuzifanya ni siku maalum za kufanyia ibadah fulani) na kuwa jambo hilo litatupa “thawabu” isipokuwa Bwana Mtume (s.a.w) ametuamrisha:-

Mtume (s.a.w) alifunga katika siku ya Ashura (tarehe kumi Muharram), na akawa amrisha (Waislamu) wafunge siku hiyo (Sahih al-Bukhari)

Zaidi ya hivi hakuna “Ibadah” nyengine ilioamrishwa khususan kwa siku hizi kumi.

Sasa yazidi tujiulize, kwa nini twazitukuza siku kumi hizi za Muharram na hatuzitukuzi siku kumi za kwa mfano, Dhul-Hijja au mwezi wowote ule mwengine? Hafsah (r.a) asema:-

Vitu vinne Mtume (s.a.w) alikuwa hakosi kuvifanya: kufunga siku ya Ashura; siku kumi za kwanza za Dhul-Hijjah na siku tatu za kila mwezi, na kuswali raka mbili kabla ya kupambazuka. (Mishkat al-Masabih)

Katika siku hizi hakuna kauli yoyote ya vikao vya mawaidha “waiz”, vilivyotajwa na Bwana Mtume (s.a.w). Swala letu mara ya pili ni kwa nini siku hizi kumi za Muharram? Yajulikana kwamba Mashia ndio walioanza mila hii ya kuomboleza Al-Hussein (maatam Hussein). Mwana-historia wa kishia Mr. Justice Amirali asema, “alievumbua na kuanzisha Maatam Hussein alikuwa Mazzal Dal Velmi Mshia katika mwaka wa 352 A.H. (miaka 300 baada ya tukio hilo).

Mtu huyu alizitenga siku hizi kumi za Muharram kuwa siku maalum za kulikumbuka tukio au msiba uliotokea huko Karbala. Mashia mpaka hivi leo wanazitukuza na kuzisherehekea siku kumi hizi za Muharram. Waandishi waki-Sabai wa Iraq walizua hadithi za urongo, za kikatili na za kutisha, kama vile kunyimwa maji ya kunywa (Hussein na watu wake) na kulazimishwa kupigana, kukatwa vichwa. Ambazo haziaminiki wala haziwezi kutegemewa na pia ziko mbali na ukweli.

Haya ni matamanio ya akili zao. Na urongo uliozuliwa ambao uko mbali na ukweli, haswa kuhusiana na tarehe na siku (aliofika Hussein Karbala) ambazo zaweza kukataliwa bila ya suala, kwani msafara wa Hussein ulikua umesafiri kwa muda mrefu na kwenye njia ngumu, na haiwezekani kuwa msafara huo uwe umefika (Karbala kutoka Mecca) kwa kutumia siku 20 au 22 peke yake.

Waliozuwa kuwa Hussein alifika Karbala tarehe 2 ya Muharram mwaka 61 A.H, walizua hivyo kwa makusudi ili waweze kuzua hadithi zao za urongo wanazoeleza matokeo ya siku hizo kumi, ambazo zimejaa vitendo vya ukatili, kunyimwa maji ya kunywa, mapigano na vita vya kulazimishwa.

Mwendo anaokwenda ngamia wa mizigo katika msafara ni maili mbili na nusu kwa saa. Kutoka Mecca mpaka Karbala ni takriban maili mia tisa na hamsini, na ukiwa unasafiri kwa masaa kumi na mbili kwa siku kwa mwendo huo wa maili mbili na nusu itakuchukua takriban siku 30 au 31 kufika. Na haiwezekani kufika kwa wakati mfupi kuliko huo.

Al-Hussein aliondoka Mecca tarehe kumi ya Dhul-Hijja 60 A.H. Wana historia wengi wakiwemo Ibn-Kathir wameandika kwamba: “Hussein akiwa na familia yake na watu sitini wakutoka Kufa waliondoka Mecca kwenda Kufa na tarehe walio ondokea ni kumi ya Dhul-Hijja.” Kwa kuetegemea kauli kama hiyo twaweza kusema haiwezekani kuwa Hussein alifika Karbala Tarehe 2 ya Muharram.

Lakini kwa mujibu wa wasimulizi wa kweli Hussein alifika Karbala tarehe kumi ya Muharram 61 A.H. na tarehe hii inakubalika. Na hii yatupa dalili kuwa makusudio ya kusimulia urongo kuhusiana na kufika kwa Hussein Karbala ni kuwawezesha warongo hawa waweze kutunga riwaya zao ambazo mpaka leo ndizo tunazodanganywa nazo.

Mambo yakiwa kama hivi tunavyoeleza basi kwa nini twaweka vikao vya mawaidha katika siku kumi hizi za Muharram, huku twajua kuwa yote yanayodaiwa yalitokea ni ya kutungwa na ni ya urongo mtupu.

Kwa ufupi riwaya ya kweli ni kwamba, watu wa Kufa walimshawishi Hussein amkatae Amiirul-mu’minin Yazid bin Muawiya, na wakamuahidi uwongozi ikiwa atakwenda nao Kufa. Lakini njiani Hussein akagundua kwamba watu hao wa Kufa wamemgeuka yeye kwa kumuua Muslim bin Aqyl, na Hussein akageuza msafara kuelekea Syria.

Alipofika Karbala alisimamishwa na jeshi la Amiirul-mu’minin na akakubali kumpa baia (kumtambua kama Amir) Yazid bin Muawiya. Watu 60 wa Kufa waliokuwa nae walijua watakuwa tabuni na Yazid kwa kumshawishi Hussein. Ndipo jeshi lilipokurubia kuzichukua silaha zao, wao (hao wakufi) wakaamua kuanzisha vita. Na katika mapigano hayo Hussein akauwawa (akapata Shahada).

Tokeo hili lilitokea wakati msafara wa Hussein ulipofika hapo Karbala tarehe kumi ya Muharram, na mapigano hayakuchukua zaidi ya hata saa moja. Na madai ya Mashia kwamba Hussein alikatwa kichwa chake ni urongo mtupu. Bali Hussein alizikwa kwa kila heshima na swala ya jeneza lake iliongozwa na mwanawe Ali bin Al-Hussein (Zeinul Abideen). Sasa ikiwa tokeo lenyewe halikuchukua hata saa moja kumalizika. Kwa nini sisi twasherehekea kwa kuweka mawaidha siku kumi nzima za mwezi wa Muharram?

Jee kufanya hivyo (kuweka vikao vya mawaidha katika siku kumi za Muharram) ni “ibadah” ambayo Allah (s.w.t.) au Mtume wake (s.a.w) ametuamrisha tufanye? Na ikiwa mwadai kwamba kwa kuweka mawaidha haya mwajaribu kuwaepusha wafuasi wa Sunni na kufuata ibada za Mashia basi twawaambia munayoyafanya ni makosa, na haya munayoyafanya ni uzushi na mwawapoteza wa Sunna kwa kuwaiga hao hao Mashia.

Kwa kuweka “Majlisi” hizi katika siku kumi za Muharram nyinyi mwatilia nguvu ibada ya Mashia wanaoifanya ya kuomboleza Al-Hussein ambayo haina mashiko yoyote yale katika Uislamu. Na ni mila ambayo haina msingi wakikweli na uliozuliwa na Mashia. Badili ya haya, mungeliwailimisha Waislamu uhakika wa mambo na ku’upinga urongo unaotapakazwa na Mashia kuhusu tokeo hili ambalo limetiwa katika akili za watu wa Sunna kwa muda wa karne kumi na mbili.

Ahlul-Tawheed