Sehemu ya Pili: Wajibu wa Mwanamune

Mlezi wa Familia

Mwanaume na mwanamke ni nguzo mbili za msingi wa familia, lakini kwa kuwa wanaume wamepewa sifa maalum kwa amri ya uumbaji, na kwa sababu ya uwezo wao wa mantiki ni imara zaidi ya ule wa wanawake, wao huchukuliwa kama walezi wa familia zao.

Mwenyezi Mungu Mweza wa yote amewaweka wanaume kuwa walezi wa familia zao na anasema kwenye Qur’ani:

الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ {34}

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi … (Quran 4:34)”

Kwa hiyo, wanaume wana jukumu kubwa na zito zaidi katika kuzisaidia familia zao.

Ni mwanaume ambaye kwa kutumia busara yake, anaweza kuisadia familia yake na kutayarisha mazingira kwa ajili ya furaha yao, na ni yeye ambaye anayeweza kuigeuza nyumba kuwa Pepo na mke wake kuwa kama Malaika.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alisema: “Mwanaume ni mlinzi wa familia yake na kila mlezi anao wajibu kwa hao waliopo kwenye ulinzi wake.”

Mwanaume ambaye anaisaidia familia yake, lazima atambue kwamba mwanamke pia ni binadamu kama mwanaume. pia mwanamke anayo matamanio na haki ya uhuru na maisha. Kumuoa mwanamke si kukodisha mtumishi, lakini ni chaguo la mwenza na rafiki ambaye atakuwa tayari kuishi pamoja katika maisha yote. Mwanaume lazima amtunze na amtimizie matakwa yake. Mwanaume si mmiliki wa mke wake, kwa kweli mwanamke anazo haki fulani kwa mume wake. Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qurani Tukufu:

وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ ۗ وَاللَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ {228}

“...Nao wanawake wanayo haki kwa sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanamume wana daraja zaidi kuliko wao…” (Quran 2:228)

Utunzaji Wa Mke Wako

Siri ya ustawi wa familia inategemea na jinsi mtu anavyomtunza mke wake, na hii ni kama ilivyowajibu wa mke kwa mume wake ambao unaeleweka kuwa katika kiwango sawa na Jihadi, pia unatambua kama tendo jema na lenye thamani sana. Lakini mwanaume ajifunze namna ya kumshughulisha mke wake, katika namna ambayo atageuka kuwa na tabia kama Malaika.

Kuhusu jambo hili, mwanaume lazima atafiti kuhusu tabia na matakwa ya mke wake. Lazima apange maisha yake kufuatana na matakwa ya mke wake na mahitaji sahihi. Mwanaume anaweza kwa tabia na msimamo wake kumshawishi mke wake katika njia ile ambayo inampendeza yeye (mke wake), kwake yeye mume na nyumba yake.

Hili ni somo ambalo linahitaji maelezo zaidi na mazungumzo ya kina yatawasilishwa baadaye kwenye kitabu hiki.

Mpende Mkeo

Mwanamke ni kituo cha wema na ni kiumbe chenye hisia kubwa sana. Kuwepo kwake hutegemea huruma na upendo. Huwa na shauku ya kupendwa na wengine na jinsi anavyopendwa zaidi ndivyo anavyofurahi zaidi. Hujitolea sana ili apendwe na wengi. Tabia hii ina nguvu sana ndani mwake hivyo kwamba akigundua kwamba hakuna mtu anaye mpenda, basi atajitambua kama ameshindwa. Atakasirika na atahisi kuvunjika moyo.

Kwa hiyo, kwa hakika mtu anaweza kudai kwamba siri ya mwanamume aliyefuzu katika maisha ya furaha ya ndoa ni jinsi anavyo onesha mapenzi kwa mke wake.

Bwana mpendwa! Mke wako kabla ya kuolewa na wewe, alikuwa anafaidi mapenzi ya wazazi wake na wema wa wazazi wake. Sasa ameingia kwenye mkataba wa ndoa na wewe na sasa amechagua kuishi na wewe katika maisha yake yote, anatarajia wewe umtimizie matakwa yake ya mapenzi na huba. Anatazamia wewe kuonyesha mapenzi zaidi kwake kuliko alivyopokea kutoka kwa wazazi wake na marafiki zake. Amekuamini wewe sana na ndio sababu amekupa udhamini wa maisha yake.

Siri ya ndoa yenye furaha hutegemea jinsi unavyodhihirisha mapenzi yako kwa mkeo.

Ukitaka kuuvutia moyo wake, ukitaka awe mtiifu kuhusu matakwa yako kama kuimarisha ndoa yenu, ukitaka mkeo akupende wewe, au adumishe uaminifu kuliko au… basi lazima kila mara uoneshe mapenzi na huba yako kwake.

Usipokuwa mwema kwa mke wako, basi anaweza kupoteza mvuto kwenye nyumba yake, halikadhalika na watoto pia. Na zaidi ya yote kwako wewe mwenyewe. Wakati wote nyumba yako itakuwa katika hali machafuko. Hatakuwa tayari kufanya juhudi kwa ajili ya mtu asiyempenda.

Nyumba ambayo ndani yake haina mapenzi, hufanana na jahanamu inayowaka moto, hata kama ni nadhifu sana na iliyojaa vitu vya anasa.

Mke wako anaweza kuugua au kupatwa na mfadhaiko. Anaweza kutafuta kupendwa na wengine kama hatoshelezwi na wewe. Anaweza asikuthamini wewe na nyumba yako pia, kiasi kwamba anaweza hata kuomba talaka!

Unawajibika kwa yote haya kwa sababu umeshindwa kumtosheleza mkeo. Kwa hakika ni kweli kwamba taratibu zingine za kutalikiana hutokea kwa sababu ya ukatili wa mume au kinyume chake.

Angalia takwimu zifuatazo. Mahitaji ya saikolojia ya mapenzi, uzembe wa waume kuhusu matakwa ya wake zao na kutokuzingatia umuhimu wa hadhi ya kiakili ya wanawake, ni vipengele ambavyo vimekuwa sababu ya kesi nyingi za kutalikiana.

Mnamo mwaka 1969 miongoni mwa kesi za kutengana 10372, katika kesi 1203 wanawake walionesha sababu ya kutaka kutalikiana kuwa ni kuvunjwa moyo kimaisha, kujihisi hathaminiwi na upungufu wa waume kutokujali matakwa na hisia kubwa za wake zao.” 146

Mwanamke alisema mahakamani; “Nipo tayari kuacha mahari yangu na hata kumlipa mume wangu fedha ili akubali kunipa talaka. Mume wangu anawapenda zaidi kasuku wake ndio sababu sitaki kuishi naye zaidi ya sasa.”

Mapenzi na urafiki wa familia ni thamani kubwa zaidi kuliko chochote na ndio sababu Mwenyezi Mungu ameiona hiyo kama mojawapo ya alama za uwezo na neema kubwa ambayo mwanadamu amepewa. Qurani Tukufu inasema:

وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ {21}

“Na katika ishara zake ni kuwa amekuumbieni wenza kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo ishara kwa watu wanaofikiri (Quran 30:21).”
Imamu Sadiq (a.s) alisema: Yeyote ambaye ni rafiki yetu huonesha wema zaidi kwa mke wake.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alisema: “Jinsi mtu anavyozidi kuwa mwaminifu ndivyo anavyozidi kuonesha wema kwa mke wake.”

Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Mmojawapo ya sifa bainifu ya Mitume wa Mwenyezi Mungu ni kwamba wote ni wema kwa wake zao.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alisema: “Maneno ya mwanaume anaye mwambia mke wake; ‘Ninakupenda kweli’ kamwe hayaondoki moyoni mwake.”

Kama mambo yalivyo, mapenzi na huba lazima yawe halisi na kuvutia kwenye moyo wa mwingine, lakini hata kupenda sana kwa mtu haitoshi, kwa kuwa ni muhimu kuonesha huba. Kwa kuonesha hisia zako kwa maneno na vitendo vyako, mapenzi unayoonesha, yatapata jibu zuri kutoka kwa mkeo na nyoyo zenu zitaimarisha muungano wa mapenzi.

Uwe wazi na udhihirishe mapenzi yako kwako bila kusita. Wakati yupo au hayupo, msifie. Mwandikie barua unapokuwa safarini na mtaarifu kwamba kutokuwa karibu naye unajihisi mpweke sana. Mara kwa mara mnunulie kitu kama zawadi. Mpigie simu unapokuwa ofisini au shughuli zako na umuulize hali yake.

Kitu kimoja cha muhimu sana kwenye akili ya mwanamke ni namna hizi za kuonesha mapenzi kwake.

Bibi fulani wakati analia kwa masikitiko alisema. “Niliolewa na mume wangu usiku mmoja wa majira ya kupukutika kwa majani. Tuliishi pamoja kwa amani kwa muda fulani. Nilihisi kuwa nilikuwa mwanamke mwenye bahati kubwa sana hapa duniani. Niliishi kwenye nyumba yake ndogo kwa miaka sita. Nilihisi ninayo furaha mara mia moja nilipogundua kwamba nilikuwa mja mzito.

Nilipomtaarifu mume wangu alidondokwa na chozi la furaha wakati amenikumbatia mikononi mwake. Alilia sana hivyo kwamba karibu angeshindwa kujizuia. Halafu akatoka nje na akaninunulia mkufu wa almasi kwa fedha yake ya akiba. Alinipa mkufu na akasema: ‘Ninatoa hii kwa mwanamke bora kuliko wote ambao ninewaona hapa duniani.’ Lakini baada ya muda mfupi alikufa kwenye ajali ya gari.”

Mheshimu Mke Wako

Mwanamke hujivunia utu wake kama ilivyo kwa mwanamume. Anapenda kuheshimiwa na watu wengine. Ataumia sana kimawazo kama akitukanwa au kudhalilishwa. Hufurahi anapo heshimiwa na huwachukia wale wanaojaribu kushusha hadhi yake.

Bwana mpendwa kwa hakika mke wako anatarajia kuheshimiwa na wewe zaidi kuliko watu wengine. Anayo haki kumtarajia mpenzi wake wa maisha na rafiki mzuri zaidi ya wote kumtunza yeye. Mke wako kufanya kazi kwa ajili ya faraja yako na watoto wenu na kwa hiyo anakutarajia wewe kumthamini yeye na juhudi zake.

Kumheshimu mkeo si jambo la kukushusha hadhi yako ila kwa kweli itakuwa ni uthibitisho wa mapenzi na huba yako kwake. Kwa hiyo, mheshimu mkeo zaidi ya wengine na sema naye kwa upole. Usiingilie kati au kumkemea anapozungumza.

Mwite kwa majina ya heshima na uadilifu. Onyesha heshima yako anapotaka kuketi chini.

Unapoingia nyumbani, akisahau kusema ‘Salaamu aleyk’ (yaani kukusalimia), basi anza wewe kumsalimia kwa kusema ‘salaamu aleyka.’

Sema ‘kwa heri’ unapoondoka nyumbani. Usiache kuwasiliana naye unaposafiri au unapokuwa haupo nyumbani. Mwandikie barua.

Dhihirisha heshima yako kwake unapokuwa kwenye mikusanyiko. Kwa dhati kabisa, epuka kumtusi kwa namna yoyote na kumfedhehesha. Usitumie lugha chafu au hata kumchokoza kwa kumtania. Usidhani ya kwamba kwa sababu upo karibu naye sana kwa hiyo hatojali ukimtania. Kinyume chake ni kwamba atachukia msimamo wa aina hiyo bila kukuonesha ishara yoyote. Mwanamke mwenye hadhi mwenye umri wa miaka 35, anasema kuhusu ombi lake la talaka; Ni miaka 12 tangu nimeolewa. Mume wangu ni mwanamume mwema na zipo tabia nyingi za mtu mwema na mpole ndani mwake.

Lakini kamwe hajataka kutambua kwamba mimi ni mke wake na mama wa watoto wake. Yeye ana dhani kwamba ni mtu anayeweza kuchanganyikana na kuzoeana na watu bila taabu, lakini maonesho yake hayo kuyafanya kwa kunitania na kunidhalilisha. Huwezi kuamini ni kiasi gani nimeumia katika hisia zangu. Neva zangu zimeathiriwa sana hivyo kwamba imenibidi niende kupata ushauri kutoka kwa bingwa wa maradhi ya akili ili nipate tiba. Nimezungumza na mume wangu kuhusu jambo hili mara nyingi. Nimemwomba asinifanyie hivyo.

Nimemkumbusha kuhusu nafasi yangu kama ‘mke wake’ na umri wangu na kwamba si stahili yake kunitania mimi mbele ya watu wengine hadi wanacheka au wanafurahia kitendo hicho. Nina hisi kuaibika mbele ya kila mtu na kwa sababu sijawahi hata wakati mmoja kuwa mcheshi, siwezi kushindana naye. Kwa kuwa matakwa yangu hayatekelezwi na mume wangu, ninataka kutengana naye. Ninajua sitakuwa na furaha nikibaki peke yangu, lakini siwezi kuishi na mwanaume ambaye hushusha hadhi yangu kila wakati ..”

Wanawake wote huwa na matamanio ya kuheshimiwa na waume zao na wote huchukia fedheha. Kama wanawake wengine kunyamaza wakati waume zao wanawadhalilisha huo si uthibitisho wa kuridhika kwao na tabia hiyo.

Ukimheshimu mke wako, na yeye atafanya hivyo kwako na uhusiano wenu utazidi kuimarika. Wewe pia utapata heshima zaidi kutoka kwa watu wengine. Kama ukimtendea vibaya mke wako na yeye alipe kisasi, hili tena si kosa lake ni kosa lako.

Bwana mpendwa! Kuoa si sawa na kupata mtumwa. Huwezi kumtendea mtu aliye huru kama mtumwa. Mke wako amekubali kuolewa na wewe ili aishi na wewe na kugawana maisha yake na mtu ambaye anampenda. Anatazamia mambo kama hayo kutoka kwako kama vile unavyotarajia kutoka kwake. Kwa hiyo, mtendee kwa namna ambayo wewe ungependa kutendewa.

Imamu Sadiq (a.s) akimnukuu baba yake, alisema: “Yeyote anayeoa, lazima amheshimu mke wake.”

Mtume (s.a.w) wa Mwenyezi Mungu alisema: “Mtu yeyote anaye mheshimu Mwislamu, Mwenyezi Mungu atampa heshima yake mwenyewe.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) pia alisema: “Hapana yeyote ambaye angewaheshimu wanawake isipokuwa watu wakarimu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) akaongeza kwa kusema: “Mtu yeyote anaye tukana familia yake, atapoteza furaha katika maisha yake.”

Uwe Na Tabia Njema

Dunia huchukua mkondo wake kufuatana na mpangilio linganifu. Matukio hutokea na kujidhihirisha moja baada ya lingine. Kuwepo kwetu katika ulimwengu huu mpana ni kama chembe ndogo ilioko kwenye mwendo na kuathiri chembe nyingine papo hapo.

Uendeshaji wa dunia huu haupo katika uwezo wetu na matukio ya dunia hii hayatokei kufuatana na utashi wetu. Tangu hapo ambapo mtu hutoka nyumbani kwake asubuhi hadi hapo anaporudi jioni, inawezekana hukabiliana na mamia ya mambo yasiyofurahisha.

Mtu hukutana na matatizo mengi sana katika uwanja wa maisha. Inawezekana mtu akakutukana, na mfanyakazi mwenzake asiye rafiki, utangojea basi kwa muda mrefu mno, umeshutumiwa kwa sababu ya kitu fulani ofisini, umepoteza fedha, au umekabiliwa na tukio lolote ambalo linaweza kumtokea mtu mwingine yeyote popote.

Inawezekana ukakasirishwa sana na matukio ya kawaida ya kila siku katika maisha yako hivyo kwamba unafanana na bomu lililotegwa na kulipuka wakati wowote.

Vema, inawezekana ukadhani kwamba huwezi kuwalaumu watu wengine au dunia kwa sababu ya bahati yako mbaya, hivyo kwamba unaporudi nyumbani, unajaribu kutoa nje hasira yako kwa mke wako na watoto wako.

Unaingia nyumbani kwako kama vile ‘Ziraili’ (malaika wa kifo) amewasili. Watoto hutawanyika kama panya wadogo mbele yako. Mungu na apishe mbali kwamba uone kitu fulani kilicho kosewa! Chakula, ama inawezekana kina chumvi nyingi au hakina chumvi, au kikombe chako cha chai hakijawa tayari, inaewezekana nyumba chafu, au watoto wanapiga kelele na kwa hiyo unapata kisingizio cha kulipuka kwa hasira ndani ya nyumba yako.

Halafu unamkasirikia na kumpigia kelele kila mtu, unawatukana unawapiga watoto na kadhalika. Wakati huo utakuwa umeigeuza nyumba ya huba na urafiki kuwa jahanamu iwakayo moto ambamo wewe na familia yako mtateseka.

Kama watoto wanaweza kukimbia kutoka nyumbani na kwenda mitaani, watafanya hivyo, na kama hawawezi kufanya hivyo, basi watahesabu sekunde hadi hapo utakapoondoka nyumbani.

Inaeleweka dhahiri ni mazingira ya kusikitisha na kutisha yalioje yanayotawala familia za aina hii. Kila mara upo ugomvi na mabishano. Nyumba yao kila mara imevurugika. Mke anachukia kuona uso wa mume wake.

Mwanamke anawezaje kuishi kwa furaha na mwanamume mkali na mwenye hasira?

Baya zaidi kuliko yote ni hatima ya watoto ambao watakulia kwenye mazingira hayo. Ugomvi wa wazazi wao kwa hakika utatia kovu kwenye roho na nyoyo zao zilizo nyepesi kuhisi. Watoto wanao wanaopata matatizo kama haya huendeleza tabia ya kuwa aina ya watu wenye hasira, wagomvi wenye huzuni na kuona kila jambo ni baya wakati watakapofika umri a utu uzima. Hukatishwa tamaa kwenye familia yao na hukengeuka. Inawezekana wakakutana na mitego ya watu waovu na kuanza kufanya uhalifu wa aina mbali mbali. Inawezekana wakawa na tabia ngumu sana kuelezeka na kuvurugikiwa akili hivyo kwamba wanaweza kuhatarisha maisha ya watu wengine kwa kuua au kujiua.

Msomaji anashauriwa kufanya utafiti wa historia ya maisha ya wahalifu. Takwimu na taarifa za kila siku za matukio ya uhalifu yote yanaonesha ukweli huu.

Yote haya yapo kwenye wajibu wa mlezi wa familia ambaye ameshindwa kudhibiti tabia yake na ameitendea vibaya familia yake. Mtu kama huyu kamwe hawezi kuwa na amani katika dunia hii na ataadhibiwa akhera.

Mpendwa bwana! Hatuna nafasi na hatuwezi kudhibiti mambo ya dunia hii. Mabalaa, shida, na matukio ya kusikitisha yote ni mambo yanayo ambatana na maisha haya. Kila mtu hupata matatizo wakati mbali mbali. Ni ukweli wa mambo kwamba, mtu hufika kwenye umri wa balekhe kwa kukabiliana na taabu. Mtu lazima apambane nayo kwa nguvu na lazima ajaribu kutafuta ufumbuzi wake. Binadamu wanao uwezo wa kukabiliana na mamia na matatizo madogo na makubwa na bila kukata tamaa chini ya mbinyo wa balaa.

Matukio ya dunia si ndio tu sababu ya kutibuliwa kwetu, isipokuwa hasa zaidi ni mpangilio wetu wa neva ambao huathirika na matukio kama haya na husababisha sisi tukose furaha. Kwa hiyo, kama mtu angeweza kudhibiti hali wakati anapokabiliwa na matukio ya maisha yasiyofurahisha, hangekasirika na kuchukia.

Tudhani ya kwamba umepatwa na tukio lisilofurahisha. Tukio hili ama ni matukio ya kila siku yalioambatana na hali ambayo hatuna uwezo wa kuingilia au hatuwezi kusaidia. Au inawezekana tukio hili ni lile ambalo sisi tunaweza kufanya uamuzi wetu.

Ni dhahiri kwamba katika mfano wa kwanza, hasira yetu hainge saidia kwa njia yoyote. Tutakuwa tunakosea kukasirika au kuhamaki. Lazima tukumbuke kwamba sisi hatukusababisha kutokea kwa tukio hilo na hata tujaribu kulikaribisha kwa uso wenye furaha.

Lakini kama tatizo letu ni la mfano wa pili, basi tunaweza kutafuta ufumbuzi unaofaa.

Kama hatutakata tamaa tunapokabiliwa na shida na kujaribu kujizuia, kwa kutumia busara, tunaweza kuyashinda matatizo yetu. Kwa njia hii hatuta kimbilia hasira ambayo inaweza kuwa tatizo juu ya tatizo.

Tunao uwezo wa kushinda matatizo yote kwa kutumia uvumilizu na hekima. Hivi si jambo la kusikitisha kwamba tunashindwa kudhibiti mambo yanayotokana na matukio yasioepukika maisha?

Zaidi ya haya kwa nini umlaumu mke na watoto wako kwa mabalaa yako? Mke wako anatekeleza mgawo wa wajibu wake. Anatakiwa kutunza nyumba na watoto. Anatakiwa kufua, kupika, kunyoosha pasi kufanya usafi na kadhalika. Unatakiwa kumtia moyo mke wako kama vile unavyomtendea.

Watoto wako pia wanafanya kazi yao. Wao pia wanamngojea baba yao wajifurahishe. Wafundishe mambo yaliyo sahihi na uwape hamasa wajifunze zaidi. Je, ni haki kwamba unakutana na familia yako ukiwa na uso wa kikatili na chuki?

Wanakutarajia wewe kuwatimizia matakwa ambayo ni haki yao. Wanatazamia wema kutoka kwako na wanataka uzungumze nao kwa upole na uoneshe furaha.

Watakuchukia sana kama ukidharau hisia zao na kama utaigeuza nyumba kuwa mahali pa giza ambamo hakuna furaha hata kidogo.

Unajua watateseka kiasi gani kutokana na tabia yako isiyopendeza na ya kikatili? Hata kama hutaichukulia familia yako kwa uzito uanostahili angalau ujihurumie wewe mwenyewe. Uwe na uhakika kwamba unaweza kuharibu afya yako kwa kuendeleza ukali.

Unawezaje kuendelea kufanya kazi na unawezaje kufuzu kupata mafanikio? Kwa nini uigeuze nyumba yako iwe jahannamu? Hivi si vizuri zaidi kwamba wewe uwe na furaha kila mara na uyakubali matatizo yako kwa busara na si hasira?

Hungetaka kuamini kwamba hasira haiwezekani kutatua matatizo yako, isipokuwa hasa zaidi matatizo yataongezeka? Hungekubali kwamba unapokuwa nyumbani unatakiwa kupumzika na kurudisha nguvu zako ili uweze kupata ufumbuzi unaofaa kwa matatizo yako akili yako ikiwa imetulia? Kutana na familia yako ukiwa na uso wenye tabasamu; taniana na watu wa familia yako kwa namna nzuri na jaribu kutengeneza mazingira ya furaha nyumbani kwako. Ule na kunywa pamoja nao na upumzike.

Kwa njia hii wewe na familia yako mtafurahia maisha na mtashinda matatizo yenu kwa urahisi. Ndio sababu dini tukufu ya Uislamu inaona tabia njema kuwa sehemu ya dini na ishara ya kiwango cha juu sana cha imani.

Mtume (s.a.w) alisema: “Mtu mwenye tabia njema amekamilika zaidi katika imani yake. Mtu mwema zaidi miongoni mwenu ni yule anayeitendea mema familia yake.”

Mtume (s.a.w) pia alisema: “Hakuna tendo jema zaidi kuliko tabia njema.”

Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Kuwatendea wema watu na kuwa na tabia inayostahili unapokuwa nao kufanya miji huwa na watu wengi zaidi na umri wa raia huongezeka.”

Imamu Sadiq (a.s) pia alisema: “mtu muovu hubakia kwenye mateso na uchungu.”

Luqman mwenye hekima alisema: “Mtu mwenye busara lazima afanye mambo kama mtoto mdogo wakati anapokuwa na familia yake, na kuendelea na tabia ya kiwanamume anapokuwa nje ya nyumba yake.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.w) alisema: “Hakuna furaha iliyo nzuri zaidi kuliko tabia njema.”

Mtume (s.a.w.w) pia alisema: “Tabia njema ni nusu ya dini ya Uislamu.”

Imesimuliwa kwamba alipokufa Sad bin Maadh mmojawapo wa sahaba mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w), Mtume (s.a.w) alishiriki kwenye maziko yake bila kuvaa viatu, kama vile alipoteza mmojawapo wa watu wa familia yake.

Mtume (s.a.w) aliweka maiti ya sahaba huyo karibuni kwa mikono yake iliyotakasika halafu akaufunika. Mama yake Sad ambaye alikuwa anaangalia heshima ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kwa mwanae alimwambia Sad: “Ewe Sad! furahia Pepo” Mtume (s.a.w.w) alimwambia:

“Ewe mama wa Sad, usiseme hivyo, kwa sababu Sad sasa hivi amepata mateso kwa njia ya kugandamizwa kaburini na kadhalika. Baadaye, Mtume (s.a.w.w) alipoulizwa kuhusu sababu ya mateso ya Sad, Mtume (s.a.w.w) alijibu; “Ilikuwa kwa sababu alikuwa anaitendea mabaya familia yake.”

Kulalamika Kusiko Na Lazima

Matatizo ya maisha ni mengi. Hakuna mtu ambaye anayo furaha kamili na hali yake. Lakini baadhi ya watu ni wavumilivu zaidi kwa matatizo yao kuliko wengine. Hujaribu kuyaweka katika kumbu kumbu ya akili zao na hawayataji isipokuwa kama ipo sababu ya kuyafichua.

Kwa upande mwingine, wapo watu ambao ni wadhaifu mno hivyo kwamba hawawezi kuishi na matatizo yao bila ya kuyafichua. Wanayo mazoea makubwa kulalamika hivyo kwamba kila wanapokutana na watu wengine, huanza kulalamika. Popote wendapo na wakati wowote wanapokuwa kwenye mkusanyiko, hulalamika kuhusu matukio ya kila siku ambayo yameathiri maisha yao. Inakuwa kama vile wametumwa kwenye misheni na shetani mwenyewe, kuharibu furaha ya wengine. Ndio maana marafiki wengi sana na ndugu hawapendi kutiwa wasi wasi na watu wenye tabia hii na hujaribu kuwakwepa kadiri iwezekanavyo.

Lakini lazima watu wawasikitikie wake zao, na watoto wao ambao wanatakiwa kuvumilia tabia yao. Kwa sababu hakuna mtu mwingine ambaye yupo tayari kusikiliza malalamiko yao, watu hawa hutoa matatizo yao mbele ya familia zao.

Wakati mwingine hulalamika kuhusu matumizi yao, kodi marafiki zao na wakati mwingine hulalamila kuhusu wafanya kazi wenzao biashara zao, maradhi, madakitari na kadhalika.

Watu hawa ni wenye kuona kila kitu kuwa kibaya hawaoni chochote kizuri katika dunia hii. Wanateseka wao na wengine, pia na hususan familia zao huteseka pia.

Mpendwa Bwana! Kuna maana gani kulalamika wakati wote? Unafanikiwa nini katika kulalamika?

Kwa nini familia yako iteseke kwa sababu wewe umekasirishwa na dereva wa teksi? Kwa nini umlaumu mke wako kwa sababu biashara yako haiendi haraka?”

Usisahau kwamba msimamo wako utaifukuza familia yako kutoka kwako. Watakukasirikia na kukata tamaa. Wanaweza hata wakakimbia kutoka kwako na inawezekana wakaangukia kwenye mtego wa uovu na ukhalifu

Jambo la mwisho ni kwamba tabia hii huweka kovu la kiakili kwa watu wako.

Je, huoni kwamba sio jambo jema zaidi kutokuharibu furaha ya familia yako? Unaporudi nyumbani, jaribu kusahau matatizo. Furahi na familia yako. Kula nao cheka nao na furahia kuwa pamoja nao.

Pia Uislamu unachukulia uvumilivu na kutokulalamika kuwa ni tabia njema na hata umetenga thawabu kwa sifa hii. Imamu Ali (a.s) alisema: “Matatizo yanapo mpata Mwislamu, si vizuri alalamike kuhusu Mwenyezi Mungu kwa watu wengine, isipokuwa anachotakiwa kufanya ni kumpelekea Mwenyezi Mungu matatizo yake ambaye ndiye mwenye ufunguo wa matatizo yote.”

Imamu Ali (a.s) pia alisema: “Imeandikwa kwenye Taurati; yeyote anaye lalamika kuhusu tatizo ambalo limempata kwa kweli atakuwa analalamika kuhusu Mwenyezi Mungu.”

Mtume (s.a.w.w) wa Uislamu alisema: “Yeyote anayepata matatizo ya afya yake na halalamiki kuhusu jambo hilo kwa watu, basi ni wajibu Mwenyezi Mungu kumsamehe dhambi zake zote.”

Kuanzisha Ugomvi

Baadhi ya wanaume wakati wote hutafuta visingizio vya kuona kosa katika kila kitu. Hulalamika kuhusu kila jambo dogo. Kwa nini meza hii chafu? Kwa nini chakula cha mchana hakipo tayari? Kwa nini jagi la maua lipo hapa? Hivi sijasema kabla kwamba visahani vya majivu visiwekwe chini? Na kadhalika.

Wanaume hushikilia msimamo huu hadi kufika kiasi cha kusababisha ugomvi na migongano ndani ya familia zao, na wakati mwingine familia huvunjika kwa sababu ya tabia yao.

Kama mambo yalivyo hatusemi kwamba wanaume hawana haki ya kuwaambia wake zao nini cha kufanya. Mwanzoni mwa kitabu hiki, wanawake walishauriwa kukubali haki hii. Tumesema kwamba wanawake hawatakiwi kuonesha kiburi kwa ushauri wa waume zao kuhusu mambo ya familia. Hata hivyo, wanaume wanatakiwa kutumia mantiki na busara zao. Wao ni walezi wa familia zao na kwa hali hiyo, wanatakiwa kuwa na mwenendo unaostahili.

Kama mwanaume anataka kushiriki kwenye mambo ya familia basi anatakiwa kuwa na mwenendo unaostahili.

Kama mwanaume anatakiwa kushiriki kwenye mambo ya familia basi anatakiwa kufanya hivyo kwa namna iliyo fanywa. Kwa kweli, kwa kuwa mwanaume hana muda wa kutosha kushiriki katika mambo yote yahusuyo nyumba yake na kwa sababu hana utaalamu muhimu kuhusu shughuli hizo, basi ni kwa manufaa yake kumwachia mke wake kazi za nyumbani. Mwanaume anatakiwa kumwacha mke wake afanye shughuli za nyumbani kwa uhuru.

Hata hivyo, wanaume kwa kisingizio cha kutoa ushauri, wanaweza kuwakumbusha wake zao kuhusu mambo fulani bila kuwalazimisha. Mara mwanamke mwenye busara anapoona matakwa ya mume wake kufuatana nayo. Kwa hiyo, mwanaume na mwanamke ambao hujaliana wao kwa wao na familia yao.

Kwa kuzungumza pamoja kwa jinsi ilivyo wanaweza kukubaliana mambo yote. Kwa njia hii, wanawake wengi wapo tayari kukubaliana na matakwa ya waume zao ya mara kwa mara.

Lakini kama kushiriki kwake ni kutafuta dosari na kulalamika mfululizo, basi huzoea na kwa hiyo, basi mke huzoea na kwa hiyo msimamo huu unakuwa jambo la kawaida na hakuna lolote la maana litakalo tokana na hali hiyo.

Mwanamke mwenye mume mlalamikaji, hatakuwa makini naye. Mke anaweza hata asijali mambo yake yanayofaa na muhimu. Atajishauri yeye mwenyewe: “Kwa nini nipoteze nguvu zangu, kama mume wangu hatosheki hata kidogo na kazi yangu?”

Si tu kwamba hatajali shutuma za mume wake, lakini anaweza hata akalipiza kisasi.

Hapa ndipo ambapo nyumba yao hugeuka kuwa uwanja wa vita. Kushutumiana mfululizo wao kwa wao kutatayarisha uwanja wa kutengana na hivyo familia huvunjika. Katika tukio hili mwanamke hatalaumiwa kwa sababu hata mke aliye na busara na mvumilivu atashindwa kuendelea kuvumilia kwa sababu ya msimamo wa mume wake wa kudhalilisha.

“Mwanaume alipiga simu kwenye kituo cha polisi na kudai kwamba mke wake aliondoka nyumbani kwake miezi miwili iliyopita na kwamba alikuwa anaishi na wazazi wake. Baada ya uchunguzi zaidi, mke wa huyu mwanaume alisema; ‘Mume wangu hapendi mtindo wangu wa kutunza nyumba.

Wakati wote hunilaumu kuhusu mapishi yangu na uendeshaji wa mambo ya nyumbani. Kwa hiyo nimemwacha ili nipate amani mahali pengine.’ ”

Wanaume lazima wakumbuke kwamba kazi za nyumbani ni eneo la wake zao kutekeleza wajibu wao. Ni makosa kuwanyang’anya haki yao au kuwageuza kuwa vibaraka. Ni busara zaidi kuwaacha waendeshe mambo ya nyumba jinsi watakavyo.

Matokeo yake, mke wako hufanya kazi kwa shauku kubwa, utafurahi na nyumba yako itakuwa makazi ya familia yenye furaha.

Mridhishe Na Mliwaze Mke Wako

Pia mwanamke, kama ilivyo kwa mwanamume, hupata mabadiliko ya hisia kubwa. Huhisi furaha, hasira, huzuni na kadhalika. Huchoka kutokana na kazi za nyumbani na inawezekana akaudhiwa na watoto.

Watu wengine wanaweza kumtibua kwa shutuma zao. Inawezekana akaingia kwenye mashindano na wengine. Kwa ufupi, mwanamke hukabiliana na matatizo mengi ambapo mengine miongoni mwa hayo humuathiri sana hivyo kwamba anaweza kukata tamaa kwa kiwango ambacho kitasababisha atoe majibu yasiyofaa hata kwa mambo madogo.

Hususan mfano huu ni kwa upande wa wanawake, kwa sababu wao ni wepesi sana na hutoa majibu kwa umakini zaidi kwa matukio yasiyo pendeza ikilinganishwa na wanume.

Wanawake ambao hupata matatizo huhitaji kutulizwa. Wanaume lazima wawafariji kwa sababu ni wenzi wao na wao ndio wanaoaminiwa na wake zao.

Mpendwa bwana! Unapomwona mke wako katika huzuni na hasira basi jaribu kuelewa hali yake. Kama ukiingia nyumbani kwako na hakusalimu, wewe mtolee ‘salaam’. Tendo hili halita kudhalilisha wewe. Ongea naye ukiwa katika tabasamu. Epuka ukali. Msaidie kazi za nyumbani. Uwe mwangalifu usimuudhi kwa namna yoyote. Usimtanie. Kama hajisikii kuzungumza, basi mwache. Usiseme: “Unasumbuliwa na nini?”

Kama anayo hali ya kutaka kuzungumza, msikilize na mliwaze. Jifanye unahusika zaidi na tatizo lake kuliko yeye. Mruhusu akwambie malalamiko yake kwako. Halafu, kama vile baba mwema au mume mwenye huruma jaribu kumsaidia apate ufumbuzi wa tatizo lake. Mpe moyo wa kuwa mvumilivu. Kwa busara na mantiki mfanye ayaone matatizo yake kama madogo. Imarisha tabia yake na msaidie kushinda sababu ya hasira yake, uwe mvumilivu na mtendee kufuatana na mantiki yako. Kwa hakika atauona, msaada wako kuwa unafaa na maisha yatarudi katika hali yake ya kawaida baada ya muda mfupi kwenu nyinyi wote.

Kinyume chake, ukimwendea isivyo sahihi, inawezekana ukasababisha mateso zaidi kwake. Pia wewe utateseka na inaweza kusababisha ugomvi mkubwa ambao utawapa usumbufu wote wawili.

Usitafute Makosa Yake

Hapana mtu yeyote hapa duniani ambaye anazo sifa zote na hana makosa. Watu wengine wanweza kuwa wanene sana au wembamba sana. Wenye midomo mikubwa pua kubwa au meno makubnwa. Wengine wanakuwa wachafu, hawana adabu, wenye haya, fidhuli, wenye kuvunjika moyo, hasira, wivu au wachoyo. Wanawake wengine si wapishi wazuri au mwanamke mwenye kipaji. Watu wengine wanaweza kuwa walaji sana au kutumia kwa fujo.

Kwa ufupi, hakuna mtu ambaye hana mapungufu, na hakuna mtu yeyote hapa duniani anayeweza kuchukuliwa kama kiumbe kilichokamilika.

Kwa kawaida, wanaume, kabla ya kuoa hudhani kwamba atakaye muoa awe hana dosari yoyote. Hawajali ukweli huu kwamba hakuna kiumbe kifananacho na malaika hapa ulimwenguni. Wanaume hawa, mara waoapo huwaona wake zao waliodhani wakamilifu, si wakamilifu na hivyo huanza kuonesha mapungufu yao. Hudiriki kuona kuwa ndoa zao hazikufuzu na wao wenyewe kuwa na ‘bahati mbaya.’

Wanaume hawa hulalamika kila mara na hawaachi kulalamika hata dosari ndogo za wake zao.

Wanaume wengine hukuza dosari sana hivyo kwamba kila mara huziona kubwa kama milima mirefu. Mara kwa mara huzitaja dosari hizo kwa wake zao na kuwadhalilisha. Pengine huzitaja hata mbele ya marafiki na ndugu.

Matokeo ni kwmaba, msingi wa maisha yao ya ndoa huanza kutetemeka. Mwanamke hufadhaika na hupoteza shauku kwa mume wake na familia yake. Atadhani hakuna mantiki yoyote kufanya kazi kwenye nyumba ya mtu ambaye humshutumu. Inawezekana akalipiza kisasi.

Mwanaume anasema kwa mke wake: “Tazama pua yako ilivyo kubwa, na mbaya ilioje!” Na mwanamke atajibu: “Si mbaya kama uso wako mbaya na kiwiliwili chake kilicho kwenda kombo!”

Halafu mwanaume atasema: “Meno yako yananuka harufu mbaya! Na mwanamke anajibu: “Funga domo lako kubwa.” Na kadhalika.

Kuendelea kwa mazungumzo haya hufungua mlango wa shutuma na kuigeuza nyumba kuwa uwanja wa vita ambamo wanandoa hutukanana na kushushiana hadhi.

Wakiendelea kuishi namna hii, hawatafurahia maisha yao tena hata kidogo, kwa sababu nyumba isiyokuwa na mapenzi ya familia na uaminifu, si mahali pa faraja.

Zaidi ya haya, mwanaume anayejihisi kwamba yeye hana bahati na ndoa yake imeshindikana, na mwanamke ambaye hudhalilishwa wakati wote, wote wawili wanaweza kupata maradhi ya kiakili na mengineyo.

Kama ukubwa wa ugomvi wao unazidi kuongezeka basi kila mara huwepo uwezekano wa hatari ya kutalikiana au kutengana. Kutalikiana ni hatua isiyosaidia sana kwa pande zote zinazohusika, haswa kama wapo watoto katika familia.

Jamii haingeheshimu mtalaka mwanaume au mwanamke. Zaidi ya hayo kutalikiana ni hatua inayosababisha hasara ya kiuchumi kwa mwanaume; ambayo si rahisi kurekebishwa hasa zaidi hii ni kweli hapo mtalaka anapotaka kuoa tena, kwani pia atahitaji kutumia fedha tena kwenye ndoa

yake ya pili. Zaidi ya hayo, hakuna uhakika wa mtalaka kupata mwanaume ambaye atamridhisha kufuatana na matumaini yake.

Kufunga ndoa mara ya pili haitakuwa rahisi kwa sababu ya historia yake. Hata kama mwanamume atapata mwanamke mwingine, bila shaka atakuwa na mapungufu fulani pia.

Anaweza hata akawa mbaya zaidi kuliko mke wake wa kwanza. Atakuwa hana budi kumvumilia. Hii ni kwa sababu wanaume wengine wanayo majivuno makubwa kukubali dosari zao.

Ni mara chache sana utamuona mwanaume ambaye ameridhika kabisa na ndoa yake ya pili. Imewahi kutokea kwamba baadhi ya wanaume hurudi kwa wake zao wa mwanzo.

Bwana mpendwa! Kwa nini umwangalie mke wako kwa lengo la kutaka kugundua dosari zake; na kwa nini utilie maanani sana kuhusu mapungufu madogo? Kwa nini uyakuze sana makosa yake hivyo kwamba husababisha mateso kwako wewe na familia yako?

Umepata kumuona mwanamke asiye na dosari kabisa? Wewe mwenywe ni mbora kiwango gani? Ni dosari zipi ndogo ndogo zinazostahili kuhatarisha kuvunjika kwa ndoa yenu?

Uwe na uhakika kwamba kama ukimuona mke wako kwa makusudio yenye mantiki na haki, itagundua mambo mengi mazuri kuhusu yeye. Wewe tazama na uone kwamba sifa zake zitazidi dosari zake.

Uislamu unauona msimamo huu kuwa na madhara na haupendezi na kwa hiyo unakataza watu wote kutafuta na kugundua makosa ya wengine.

Mtume (s.a.w) alisema: “Enyi mnao sema, kwa ndimi zenu tu kwamba nyinyi ni Waislamu lakini imani haijaingia nyoyo zenu! Usiwaseme vibaya Waislamu na usianze kutafuta makosa yao kwa sababu yeyote anaye tafuta na kugundua dosari za wenzake, atashutumiwa na Mwenyezi Mungu na hata kama mtu kama huyu yupo nyumbani kwake, atafedheheka.”

Puuza Mazungumzo Ya Uongo Ya Wakosoaji

Baadhi ya watu wanayo mazoea ya kuwazushia uongo watu wengine. Tabia hii isiyo pendeza hutengeneza uadui miongoni mwa marafiki, na ndugu na inaweza kuvunja familia. Imeweza hata kusababisha mauaji. Zipo sababu mbali mbali kuhusu tabia ya aina hii, kama wivu, hasira, kisasi na uadui.

Baadhi ya watu hukimbilia kutamka maneno ya kashifa ili waridhishe nafsi zao. wasikilizwe na watu wengine au kujifanya wanamuonea huruma mtu fulani. Lakini ni mara chache sana kwamba maneno ya kashifa huwa na makusudio mazuri.

Kwa hiyo, mtu mwenye hekima na mjanja anatakiwa kupuuza maneno kama hayo. Lazima afanye uchambuzi wa maneno ya msemaji kila mara ili aepuke kudanganya au kuvutiwa na uovu wake wa masingizio.

Jambo moja ambalo wanamume wanatakiwa kukumbuka ni kwamba kwa kawaida mama zao, dada zao, kaka zao, licha ya kuonesha urafiki, huwa hawafurahii uhusiano mzuri na wake zao.

Sababu ni kwamba, kabla ya kuoa mwanaume huishi na wazazi wake kwa miaka mingi ambapo huwa hana uhuru wa kutosha. Wazazi wake ambao wamefanya bidii kumlea wanayo matarajio ya kupata msaada kutoka kwake pindi wanapofika kwenye umri wa uzeeni.

Wazazi hata baada ya kumuoza mtoto wao wa kiume na kumpa uhuru bado wanayo matumaini kwamba atafuata ridhaa yao na matakwa yao. Hupenda mtoto wao wa kiume kuwatunza wao zaidi kuliko mkewe. Lakini ukweli ni kwamba, mwanaume anapoanza maisha ya ndoa, hujitahidi sana kwa ajili ya familia yake mpya, mke na kujitegemea.

Huelekeza mapenzi yake kwa mke wake na hufanya bidii kuhusu lengo hilo. Jinsi anavyozidi kuingia upande wa ndoa, ndivyo anavyozidi kuwa mbali na wazazi wake.

Hivyo mama yake na dada zake hususan hujihisi wamekosewa. Humuona bibi harusi kama tishio kwao kwani atakuwa amemchukua kijana wao kutoka kwao. Inawezekana wamlaumu bibi harusi kwa kumtenganisha kijana wao kutoka kwenye familia yake.

Wakati mwingine mama wa waume hudhani kwamba njia iliyo nzuri sana ya kukabiliana na hatari hii ni kutekeleza njia za kusababisha watoto wao (waume) wapunguze huba kwa wake zao.

Mama wa aina hii, ataanza kuonesha mapungufu ya mke wa mwanae, kutangaza uongo kuhusu bibi harusi, kusema maneno ya kashfa na kufanya njama dhidi ya muolewaji na kadhalika. Kama mwanaume anadanganyika kwa urahisi na mjinga, inawezekana akakubaliana na maneno ya kashifa ya mama yake. Hapo sasa mume atakuwa kitendea kazi kilichomo mikononi mwa familia yake ambapo matokeo yake baadaye atapoteza mvuto kwa mkewe. Akiwa kwenye ushawishi wa wazazi wake mwanaume ataanza kulalamika na kuonesha makosa ya mke wake. Atamlaumu mke wake wakati wowote itakapo wezekana.

Matokeo yake, nyumba ya familia itageuka kuwa baridi na isiyopendeza. Uchochezi wa wanaume kutoka kwa mama na dada zao huwaelekeza wanandoa kwenye ugomvi na hata kupigana. Katika hali hii, mke anaweza kukimbilia kuchukua hatua kali zaidi kama kujiua!

Mwanamke ambaye alikuwa katika siku zake za mwanzo wa ndoa, alimeza pini.

Baada ya kufanyiwa upasuaji kwa lengo la kuondoa pini kutoka tumboni mwake, alisema; Kama juma moja hivi lililopita, niliolewa. Siku nilipoingia nyumbani kwa mume wangu, nilihisi kuwa na bahati kama wanawake wengine walioolewa. Lakini baada ya siku chache tu, mume wangu na dada yake walianza kunilaumu. Msimamo wao ulifanya maisha yangu kuwa magumu sana. Hatimaye niliamua kujiua na nikameza pini chache.”

Mwanamke ambaye alikasirishwa na lawama za mume, shemeji yake, alijichoma moto na kufa kwa sababu ya majeraha makali.”

Mwanamke ambaye alikuwa katika siku zake za mwanzo za kuolewa aliudhiwa sana na msimamo mbaya wa mama mkwe wake hivyo kwamba alijichoma moto hadi kufa.”

Kwa hiyo, lawama, msimamo mbaya na maneno ya kashfa kutoka kwa mama, dada na kaka zao waume ni tabia ambazo zinaweza kuwa na madhara makubwa sana na hivyo mwanaume lazima atahadhari kuhusu usumbufu wao. Kama mambo yalivyo, haiwezekani kuwazuia watu wasiseme lakini inawezekana kutangua mazungumzo yao.

Mwanaume lazima atambue kwamba lawama zinazo elekezwa kwa mke wake na mama yake, dada zake na kadhalika hazina maana ya kuhurumiwa na kuwa na nia njema, isipokuwa sababu kubwa ni wivu, uadui uchoyo na kadhalika.

Mwanaume lazima akumbuke kwamba kwa sababu ya mke kwa kufanya uzingativu wa mume wake uelekee kwake, familia yake humuonea wivu na kumchukulia kama mporaji wa kijana wao. Kwa hiyo, hukimbilia kutumia njia za kuzuia mapenzi yao yasisitawi.

Mabwana wapendwa kwa ufupi, mama, dada na kaka zenu wa aina hii hawajali furaha yenu katika ndoa, lakini hususan wao wanaangalia matakwa yao. Kama wangekuwa wanahusika na furaha yako na mke wako wangefanya vinginevyo.

Ni jambo la kushangaza kwamba wazazi hutoa sifa nyingi sana kwa mwanamke anayetarajiwa kuolewa na mtoto wao wa kiume, lakini mara mtoto wao anapooa wazazi hao hugeuka na kuwa kinyume.

Mabwana wapendwa msidanganywe. mapungufu hayo ambayo familia yako huyapachika kwa mke wako hayana umuhimu wowote; na hata kama si madogo, kumbuka kwamba hakuna mtu aliye kamilika.

Kwa vyovyote vile, je, dada na mama yako au wengine wanao mlaumu mke wako, wao ni viumbe vilivyo kamilikia?

Kuzingatia maneno yao ya kashfa ni hali ambayo itaathiri maisha ya familia yako. Inawezekana ukaishia kuachana, na matokeo yake ni kwamba unaweza kuteseka kiakili na kiuchumi.

Kuoa mara nyingine haitakuwa rahisi. Hata kama utapata mwanamke mwingine wa kuoa, haileweki kabisa kwamba atakuwa mkamilifu kuliko yule wa kwanza. Utahakikishaje kwamba familia yako hawatamtendea vibaya kama walivyofanya kwa mkeo wa kwanza?

Kwa hiyo, ni vema umwambie mama yako, dada yako na wengine kuanzia sasa kwamba mke wako anakufaa na kwamba unampenda. Lazima uwatangazie kwamba lazima waache kumlaumu mke wako au vinginevyo mke wako au wewe mwenyewe utasitisha uhusiano nao.

Pindi watakapo hisi msimamo wako imara wataacha msimamo wao wa uchochezi na wewe na mke wako mtapata amani.

Lakini, bahati mbaya, baadhi ya mama na dada hawaachi tabia hiyo kwa urahisi na hukimbilia kwenye mashtaka yenye nia mbaya kama vile ugoni.

Tatizo linakuwa kubwa sana hivyo kwamba mwanaume anaweza akamtaliki au hata kumuua mke wake kwa sababu ya maneno ya mama yake.

Wanandoa vijana waliomba kutalikiana kwenye mahakama ya Tabriz. Mwanaume alisema mahakamani: “Mke wangu huandika barua za mapenzi kwa kaka yangu anayeishi Isfahan. Niliziona baadhi ya barua hizo chache jana usiku.” Mke wake alisema huku analia: “Mama mkwe wangu na wifi yangu hawanipendi na kunisumbua kila wakati. Lakini sasa kwa sababu matendo yao yenye fitina hayakumuathiri mume wangu, wameghushi barua kadhaa za mapenzi na wameziweka kwenye kabati langu la nguo ili wanichochee aniache.” Mahakama iliwasuluhisha wanandoa hao na kumshauri mume kumwambia mama na dada yake kuacha kufanyia vitendo viovu kwa bibi harusi wao.

Mwanamke mwenye umri wa miaka thelathini na nne alijimwagia mafuta ya taa na kujichoma moto. Majirani waliuzima moto haraka na walimpeleka hospitalini. Alipokuwa hospitalini mwanamke huyo alisema: “Mimi huishi na mume wangu na mama mkwe. Kila wakati huniona mimi nina makosa. Hutoa visingizio na kwa kawaida yeye ni mkali sana. Wakati wote haachi kusababisha ugomvi baina yangu na mume wangu. Jana nilikwenda madukani kununua vitu na ghafla nilikutana na rafiki yangu wa siku nyingi tulipokuwa tunasoma. Tulizungumza kwa muda mfupi halafu nilirudi nyumbani. Mama mkwe wangu alianza kuniuliza kwa nini nilichelewa? Nilimweleza lakini hakutosheka.

Aliniambia kwamba nilikuwa ninasema uongo na kwamba mwenye duka la nyama mtaani kwetu ni hawara yangu. Nilikasirika na kukata tamaa hivyo kwamba niliamua kujiua!”

Kwa hiyo, mwanaume kila mara anatakiwa kuwa na tahadhari na madai ya aina hiyo ambayo yanaweza kusababisha hatima ya hatari. Mume analazimika kufanya upelelezi kuhusu madai hayo kwa uvumilivu na asifanye uamuzi wa haraka.

Kama mambo yalivyo, wazazi wa mtu hufanya bidii na huteseka sana katika kumlea na kumkuza mtoto wao na hivyo huwafanya kuwa kituo cha matumaini yao yote. Wanamtegemea mtoto wao kuwa msaidizi wao watakapo kuwa wazee na mategemeo yao ni hayo tu. Kwa hiyo si haki mtu anapojitegemea asahau wajibu wake kwa wazazi wake. Lazima awatimizie matakwa ya hali zao hata baada ya kuoa.

Lazima adumise heshima yao na kuwa mnyenyekevu kwao. Anao wajibu wa kuwasaidia kwa kuwapa fedha endapo wanazihitaji. Si vema kusitisha uhusiano wake na wazazi wake na lazima awe anawaalika nyumbani kwake. Lazima amuamuru mke wake na watoto wake waoneshe heshima kwao. Lazima amwelekeze mke wake aelewe kwamba endapo atawaheshimu wazazi wake, hawataona, umuhimu wa kumuudhi na wanaweza hata kujivunia yeye na kumsaidia.

Mwisho, wanawake wanakumbushwa kwamba hawana haki ya kutarajia waume zao kuwaacha wazazi wao. Matarajio haya wala hayawezekani kuwa ya haki. Mwanamke mwenye busara anaweza kuwatembelea wazazi wa mume wake kwa namna ambavyo kwamba wanaweza kumchukulia yeye kama mwenzie muhimu katika familia yao. Hii inawezekana tu kama atawaheshimu, atataka ushauri kutoka kwao, akiwapa msaada na kadhalika.

Mazungumzo haya yameandikwa kwa kina kwenye sehemu ya kwanza ambapo unaweza kufanya rejea kwa taarifa zaidi.

Samehe Makosa Ya Mke Wako

mwanadamu aliyekamilika na sote sisi hufanya makosa mengi. Kama mambo yalivyo, hii ni kweli kwa wanamume na wanawake.

Kwa upande wa wanawake, anaweza kufanya makosa kwa kutokuwa na adabu kwa mume wake, kufanya kitu kinyume na matakwa yake kuwa mkali kwake, au kumwingiza kwenye hasara kiuchumi kwa sababu ya kuwa mzembe na kadhalika.

Kama mambo yalivyo, ni kweli kwamba wanandoa lazima waridhishane na waepuke kabisa kuudhiana wao kwa wao: Hata hivyo, hutokea mara chache kwamba mmoja wapo au wote watashindwa kukwepa kipengele hiki.

Baadhi ya wanaume hudhani kwamba wanatakiwa kuwa wakali kwa makosa ya wake zao kwa kuwa wanaamini hii kuwa ndio njia ya kuzuia kurudia kosa la aina hiyo.

Hata hivyo, uzoefu mara nyingi unaonesha matokeo kuwa kinyume chake kabisa. Mwanamke, ambaye mume wake ni mkali kwake, anaweza kuvumilia ukali wake kwa kipindi fulani, lakini hatimaye anaweza kuamua kujibu dhidi yake ikiwa kama matokeo ya kukatisha tamaa. Mke atazoea msimamo wake polepole hadi hapo atakapokuwa sugu.

Mume ambaye hatakuwa msamehevu kuhusu makosa ya mke wake, ni kwamba anamhamasisha mke wake kuwa jeuri na kukosa nidhamu. Anaweza kutaka kuendelea na msimamo huu ambapo kwa hakika atakabiliana na ugomvi mwingi wa mke wake. Wote wataishi katika hali ya uchungu kwa maisha yao yote.

Au anaweza akamwacha mke alivyo na asijihusishe naye kwa ukamilifu. Katika mfano huu mke wake, ambaye atahisi ameshinda, atakuwa hajali ridhaa na matakwa ya mume wake. Hali hii inaweza kufika kiasi kwamba hata hapo mke anapofanya makosa makubwa ya kudhamiria, atanyamaza. Hapo tena ndoa yao itakuwa imepoteza uchangamfu na wanaweza kukimbilia kutalikiana.

Kumbuka kwamba talaka husababisha madhara pande zote mbili kwa sababu kuanza maisha mapya si rahisi. Itakuwa hakuna uhakika wa kuwepo furaha baada ya kutalikiana.

Kwa hiyo, ukali haufai kutumika kila wakati na mara nyingi husababisha matukio yasiopendeza ambayo mtu anaweza kuyasoma kwenye magazeti. Njia nzuri kuliko zote ni kuwa mwenye kiasi na kutenda kimantiki. Samehe makosa yote madogo na yasio ya kukusudia yanayofanywa na mke wao. Hakuna haja ya kupiga kelele kwa ajili ya kosa la mke wako ambalo limefanyika bila kukusudia.

Kama mambo yalivyo, mara kwa mara mtu anaweza kuwashauri wenzake ili kuwasaidia wasirudie tena kosa la aina hiyo.

Watu hufanya makosa mengi kwa kutokujua, kwa hiyo ni vizuri zaidi kuwa shauri kwa uvumilivu kusahihisha matendo au maoni yao yaliyopotovu.

Kwa hiyo, mke wako hawezi kulazimishwa kurekebisha makosa yake; lakini badala yake unatakiwa kumpa maelezo kuhusu kosa, ili aweze kufanya uchaguzi, yeye mwenyewe asirudie tena kosa hilo.

Hivyo, si tu kwamba uelewano na kuheshimiana unabakia kama zamani, lakini pia kosa hilo litazuiwa na halitafanywa tena.

Ni busara kwa mwanamume kumzuia kimantiki mke wake asifanye makosa, lakini kama ataendelea kufanya makosa, basi kwa mara nyingine amsamehe na asijali makosa yake. Si rahisi kwa mume kuendelea kumpa adhabu mke wake au kujaribu kuonesha hatia yake ili amweke katika hali ya kuomba msamaha. Hii ni kwa sababu wanawake ni wajeuri kwa kawaida; na ukali usio stahili huwafanya watoe majibu zaidi kuliko ya hapo mwanzo. Hii inaweza kufatiwa na matukio yasiyopendeza na ya kuhofisha, kama vile kuachana au mauaji.

Uislamu umelielewa jambo hili nyeti, ambapo wanamume wamepewa wajibu kwa wanawake zao.

Imamu Ali (a.s) alisema: “Wavumilieni wanawake katika hali zote na semeni nao vizuri; na kwa kufanya hivyo wanaweza kurekebisha matendo yao”

Imamu Sajjad (a.s) alisema: “Ni haki ya mke wako kwamba unamtendea wema, kwa sababu yupo chini ya dhamana yako na unatakiwa kumlisha na kuvesha na unasamehe makosa yake ya kijinga.”

Imamu Sadiq (a.s) aliulizwa: “Mwanamke anazo haki gani kwa mume wake, ambazo kama akizitimiza ipasavyo, ataonekana kuwa mtu mwenye matendo mema?” Imamu alijibu: “Lazima ampe chakula na nguo na amsamehe makosa yake aliyoyafanya bila kukusudia.”

Imamu Sadiq (a.s) pia alisema; “Yeyote anaye waadhibu wale walioko chini yake, asitarajie kuheshimiwa au kupata cheo cha juu.”

Mojawapo ya sababu za ugomvi miongoni mwa wanamume na wanawake ni kwamba mama wakwe huingilia mambo ya familia zao.

Mama kabla ya kumuoza binti yake kwa mume, hudhani ya kwamba mkwilima wake kuwa mkamilifu na humthibitisha kwa binti yake kwamba ndiye atakaye mfanya awe na furaha. Atamheshimu na kumfanyia wema kwa matumaini ya kuwa na uwezo wa kurekebisha dosari zake ndogo ndogo baadaye.

Wakati mwingine mama mkwe humuona mkwilima wake hufuata matarajio yake na wakati mwingine hafuati. Katika mfano wa mwisho, anayo nia ya kumtengeneza mkwilima wake hadi hapo atakapo kubalika naye na katika utekelezaji wa hili hutumia kila njia zinazo wezekana kama vile za kwake mwenyewe na za uzoefu wa wengine na huanza kupanga namna ya kuwendea.

Wakati mwingine mama mkwe hujifanya mwenye huruma na wakati mwingine mkali. Anaweza akafanya mambo kama vile yeye ni mlezi na mfawidhi au anaweza akalalamika. Hata hivyo, chaguo zuri zaidi ni lile la kufanikisha lengo lake kwa kumvuta binti yake kwa kumfanya asifuate matakwa ya mume wake.

Huanza kumtumia binti yake na kwa hiyo humuamuru afanye tofauti nyakati mbali mbali. Kwa hiyo mwanaume humuona mke wake humlaumu leo na kesho kumuomba afanye kitu fulani.

Mwanamke mwenye uzoefu atafikiria kwamba mama angekuwa na huruma kuhusu ndoa yake na angefuata ushauri wake.

Hivyo kama mume wake hatafuata matakwa ya mama mkwe wake, ugomvi utaanza baina ya wanandoa na matokeo yake yanaweza kuwa kutalikiana au hata mauaji.

Hii ndio sababu wanamume wengi hawaelewani na mama wakwe zao. Huwalaumu kwa utovu wa adabu wa wake zao na huamini kwamba mama wakwe zao huwafundisha mabinti zao tabia mbaya.

Haitakuwa wazo mbaya kama mtu anajifunza kuhusu malalamiko ya wakwilima wachache.

Bwana M. Javda ameandika: “Mama mkwe wangu ni pepo mbaya, zimwi na joka la vichwa viwili. Mungu na amwepushe asiliwe na mbwa mwitu. Ameyafanya maisha yangu kuwa machungu sana hivyo kwamba ninapata wendawazimu na ninahisi kama vile nikimbie niende milimani na majangwani. Si mimi tu, ambaye nimechoshwa na hali hii. Huu ni mfano wa kawaida na ninadhani asilimia tisini na tano ya wanamume wana athiriwa na hawa mama wakwe na asilimia tano nyingine labda hawana mama wakwe.” Bwana F. Mohammed ameandika: “Mama mkwe wangu kila mara huingilia maisha yangu. Husababisha maudhi bila ya sababu ya maana. kila wakati husema maneno ya kashfa kuhusu familia yangu.

Wakati wowote ninaponunua kitu chochote kwa ajili ya mke wangu, mama mkwe wangu, huanza kuonesha dosari kuhusu kitu hicho. Hukosoa rangi yake au mtindo na hujaribu kuthibitisha kwamba kitu hakina thamani kwa mke wangu.” Bwana K. Parvis amendika: Mama mkwe wangu amenitendea kwa njia ambayo kwamba nimebakia kidogo nimtaliki mke wangu mara tatu. Huuma kama nge. Humfundisha mke wangu kuwa jeuri kwangu, kuacha kazi za nyumbani au kutarajia kisichowezekana kutoka kwangu. Wakati wowote anapokuja kututembelea, nyumba yetu hugeuka kuwa jahanamu. Kwa kweli sipendi hata kumuona.”

Wanaume wengi hujaribu kukabiliana na mvuto wa wakwe zao kwa wake zao kwa kuwekea mipaka uhusiano wao. Huwakataza wake zao wasiende kwa wazazi wao. Kwa ufupi, wanaume hawaelewani kabisa na mama wakwe zao na huonesha kutokupenda kwao kwa kila namna iwezekanayo.

Hata hivyo, mtazamo huu licha ya kwamba ni wa kawaida, si wenye mantiki na busara. Hii ni kwa sababu uhusiano wa mama na binti yake una nguvu sana na wa kimaumbile ambao hauwezi kuvunjwa kwa urahisi.

Inawezekanaje mwanaume kutarajia mke wake, kuwaacha wazazi wake ambao walitumia miaka mingi kumlea?

Matumanini haya hayatekelezeki na hata kama inatokea itakuwa kwa muda mfupi tu, kama ilivyo kwamba tendo lolote lisilo la kawaida halidumu muda wote.

Zaidi ya hayo kama mwanamke anahisi kwamba mume wake hawapendi wazazi wake, anaweza kuchukua msimamo kama huo kuhusu familia ya mume wake. Anaweza akawa hamtii, hamheshimu na kadhalika.

Juu ya hayo, msimamo huu wa mwanaume hutoa mwanya wa kisingizio kwa mama mkwe wake huingilia ndoa yake kwa ukali zaidi. Kwa ufupi, msimamo huu unaweza kusababisha matokeo mabaya na huenda yakawaelekeza wanandoa kutalikiana.

Kwa vyovyote vile kwa nini mwanaume ambaye anaweza kufaidika kutokana na kuelewana na wazazi wa mke wake, akimbilie hatua ya aina hiyo ambayo inaweza kumdhuru yeye na familia yake?

Mamlaka ya polisi wa India yalitoa taarifa kwamba mnamo mwaka 1971, sababu kubwa ya idadi ya matukio 146 ya watu kujiua wenyewe katika jiji la New Delhi ilikuwa uhusiano mbaya baina ya waume na mama wakwe zao.”

Mwanaume ambaye alikatishwa tamaa na mama mkwe wake kwa sababu ya kujiingiza kwake, alimtupa nje ya teksi.”

Mwanaume alivunja fuu la mama mkwe wake kwa nyundo. halafu kaka wa huyo mtu akakasirika na baada ya kumjeruhi kwa kisu akatoroka na kupotea.”

“Bwana…ambaye alikasirishwa na mama mkwe wake, alimwagia supu ya moto kichwani. Mama mkwe alipiga kelele na kupoteza fahamu. Alipelekwa hospitalini baada ya kupona akasema kwamba binti yake amemwambia mume wake kwamba anataka talaka na hakutaka kuishi naye zaidi ya hapo.”

Mwanaume ambaye alichoshwa na mama mkwe wake, alijiua mwenyewe.

Labda inafaa kutaja mambo mawili hapa: Ni dhahiri kwamba mama mkwe si tu ni adui kwa mkwilima wake, lakini ni kawaida yeye kumpenda mkwilima wake kama ilivyo jionesha mwanzoni mwa ndoa. Zaidi yake ni kwamba mama mkwe anajikuta yupo karibu na mkwilima wake kwa sababu ya kutaka kuona binti yake anafurahi. Kwa hiyo, mama mkwe anapoingilia maisha ya ndoa ya binti yake, haiwezekani kumaanisha kuwa kitu chochote isipokuwa kiwe na nia njema. Anamaanisha kuwa na huruma lakini wakati mwingine kwa sababu ya ujinga, huchukua hatua zisizo sahihi au hutoa ushawishi wenye madhara. Kwa hiyo, mtu asiwakosoe sana wake wa aina hii.

Uhusiano wa mama na mtoto ni wa asili ya maumbile ambao hauwezi kuvunjwa kwa urahisi, na yeyote anayefanya bidii ili kufanikisha hilo, kwa hakika atashindwa. Juhudi za aina hiyo ni kinyume cha kanuni za maumbile na haziwezi kuhalalishwa kwa vyovyote vile.

Kama vile mtu mwanaume anavyo wapenda wazazi wake, ndivyo ilivyo kwa mwanamke. Kwa hiyo, ni vizuri zaidi kuwa na uhusiano na wazazi wa wanandoa ambao unanufaisha pande zote mbili. Hii inawezekana tu kama mtu anaonesha heshima na wema. Mwanaume anaweza kwa kutumia busara, heshima, utiifu na kadhalika kuwa na uhusiano mzuri na wazazi wa mke wake. Lazima aoneshe mapenzi yake kwa mtoto wao. Asimlaumu mke wake mbele ya wazazi wake. Aombe ushauri na msaada wa kiroho kutoka kwao. Inapotokea wanatoa ushauri au kukosea kitu fulani, mkwilima anatakiwa kuonesha hilo kwa upole na kimantiki kwamba hapo wamekosea. Asiseme nao kwa ukali.

Mwanaume aliyeoa anatakiwa kuona uhusiano mzuri baina yake na wazazi wa mke wake kama wajibu wake na siri ya mafanikio ya ndoa yao. Matokeo yake ni kwamba matatizo mengi ya kifamilia yanazuiwa yasitokee na mengine mengi zaidi hupatiwa ufumbuzi. Kwa ufupi, si kila mara mama mkwe ndiye anayekuwa na hatia lakini wanamume wanatakiwa kuwa na busara ya kutosha na kuwa fanya kuwa na marafiki.

Wapo wanaume wengi ambao hufurahia uhusiano mzuri na mama wakwe zao.

Bwana Munuchehr ameandika: “mama mkwe wangu ni malaika au hata huzidi. Ninampenda zaidi ya ninavyompenda mama yangu mzazi, kwa sababu ni mwema na muelewa. Kila mara hutusaidia kutatua matatizo yetu. Kuwepo kwake ni dhamana na furaha ya familia yangu na ustawi wetu.”

Hata kama mtu anaye mama mkwe ambaye ni jeuri, mjinga na haiwezekani kuelewana naye, asimfanyie ukali. Wanawake wa aina hii wanaweza kufanya maisha ya mtu kuwa magumu, lakini ni vizuri kila mara kutoa majibu kwa upole dhidi ya tabia yao isiyofaa. Hii ni kwa sababu, kwa kuwa mwema kwao, mtu anaweza akapunguza hatari inayoweza kutokea kwenye ndoa yake.

Wakati huo huo, mwanaume anatakiwa kuwa karibu na mke wake na amfanye mke amwamini yeye. Lazima azungumze naye kuhusu matendo mabaya ya mama yake na kuthibitisha kimantiki kwake matokeo yasiyopendeza yanayoweza kusababishwa na tabia ya mama mkwe wake.

Ikiwa mtu anaweza kutengeneza maelewano ya kina na mke wake, basi matatizo mengi ikiwa ni pamoja na lile la mama mkwe wake litatatuliwa.

Kwa hiyo usidharau tabia njema, uwe na busara na uifanyie wema familia ya mke wako ili mpate kufuzu katika ndoa yenu.

Imamu Ali (a.s) alisema; “Kukuza urafiki ni nusu ya busara.”

Imamu Ali (a.s) pia alisema; Kujumuika na watu na kuwafanyia tabia njema humzuia mtu asifanye matendo mabaya na fitina.”

Imamu Ali (a.s) alisema; Jumuikeni na mfanye wema. Jiepusheni na kununa na kufarakana.”

Uwe Msikivu

Mwanamke ni kiumbe mwenye hisia kubwa ambazo hutawala mantiki yake. Mwanamke ni mjinga na mwepesi kuhisi kuliko mwanamume. Mwanamke anaweza kudanganywa kwa urahisi zaidi na hawezi kudhibiti matashi ya hisia zake. Hawezi kuamua kwa busara pindi anapotibuliwa. Anaweza kufurahishwa au kutibuliwa kwa urahisi sana.

Hivyo kama mwanaume ana usimamizi wa tabia na matendo ya mke wake, hatari za watu wengi zingeepukwa.

Ndio sababu dini tukufu ya Uislamu imemteua mwanamume kuwa kama mlezi wa familia yao na hufanya kuwa na wajibu kwa mambo ya familia.

Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qurani Tukufu:


الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنْفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّهُ ۚ{34}

“Wanamume ni wasimamizi wa wanawake kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanao jitihada hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde.”
(Quran 4:34).
Kwa hiyo mwanaume anayeonekana kama mlinzi wa familia yake, asifanye uzembe kuhusu matendo ya mke wake. Kila mara lazima afawidhi mambo ya mke wake na kufuatilia matendo yake. Lazima mume ahakikishe kwamba mke wake hapotoki au kujumuika na aina ya watu wabaya.

Mume lazima amweleze mke wake kimantiki kuhusu madhara ya rafiki mbaya. Asimruhusu kuondoka nyumbani akiwa amevaa nguo zisizofaa au zile zinazosababisha ashiki ya kijinsia. Asimruhusu mke wake ashiriki kwenye shughuli ovu au kuhudhuria mikutano isiyofaa.

Ni kweli kwamba kama mwanamke akiachwa peke yake katika matendo yake na kuchanganyikana na watu, inawezekana akanasa kwenye mtego wa watu wenye akili potovu na huishia kwenye upotovu.

Wanaume wanashauriwa kuangalia idadi ya wanawake ambao kwa sababu ya uzembe wa waume wao wamenasa kwenye mtego wa uovu. Wapo wanawake wengi ambao wamedanganywa kwenye karamu za usiku. Familia nyingi zimevunjika na watoto wengi wamepoteza familia zao. Kwa sababu ya mikusanyiko hiyo.

Mwanaume anaye mruhusu mke wake kuondoka nyumbani akiwa amevaa nguo zisizofaa, kuwa na marafiki wabaya na hamzuii kuhudhuria mikusanyiko yenye uharibifu, kwa kweli atakuwa anafanya kosa kubwa sana la uhaini kwake, kwa mke wake na kwa watoto wake.

Msimamo huu ungemwelekeza mke wake kwenye mamia ya sehemu za hatari ambamo hawezi kujinasua kwa urahisi. Petroli hushika moto kwa urahisi sana, kwa hiyo ni tendo la kipumbavu kuacha petroli karibu na moto na kudhani kwamba haitashika moto.

Ujinga ulioje wa watu ambao huwaruhusu wake zao au mabinti zao kujionesha mitaani huku wakiwa wanavaa nguo zisizofaa na wakati huo huo hawapendi nadhari au kutupiwa macho na wanaume kwa sababu ya mavazi yao!

Uhuru usio sahihi wa aina hii unayo matokeo mabaya sana. Kama mwanamke amefaulu kumshinda mume wake kuhusu matamanio yake yasiyo halali, ataongeza matakwa hayo hadi kwenye kiwango ambacho atafanya mambo yake kwa uhuru bila kumjali mume wake. Hii itasababisha matukio ya uovu kwenye familia.

Ndio maana Mtume (s.a.w.w) alisema: “Mwanaume ni mlezi wa familia yake na mlezi yeyote anao wajibu kwa wale walio chini kuwatimizia mahitaji yao.”

Mtume (s.a.w.w) pia alisema: “Waamrisheni wanawake kufanya mema kabla hawajakufanyieni ninyi uovu.”

Kwa nyongeza Mtume alisema: “yeyote anaye mtii mke wake, Mwenyezi Mungu atamtupa kwenye moto akitanguliza uso wake.”

Mtume aliulizwa: “Aina gani ya utiifu unaomaanishwa hapa?” Mtume

(s.a.w.w) alijibu: “Ni hapo ambapo mume humruhusu mwanamke ambaye humwomba mume wake ruhusa ya kwenda kwenye hamamu ya nje, watu kuhudhuria harusi, sherehe na mikusanyiko ya kutoa rambi rambi akiwa amevaa nguo za kumfedhehesha.”

Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Furaha kamili ya mwanaume ni kwamba awe mfawidhi na kiongozi wa familia yake.”

Mtume (s.a.w.w) wa Uislamu alisema: “Mtu yeyote anayemruhusu mke wake ambaye amejipamba, kuondoka nyumbani kwake ni mtu mwenye roho ya kikatili na yeyote atakaye mwita hivyo, atakuwa hakufanya dhambi.

Na mwanamke yeyote ambaye mume wake humruhusu kutoka nyumbani kwake akiwa amejipamba na kujipulizia manukato, kila hatua atakayo tembea, Mwenyezi Mungu atamjengea nyumba mume wake huyo katika Jahannamu.”

mwisho ninawakumbusha kuhusu mambo mawili: Ni sahihi kwamba mwanaume anatakiwa kuwa na hadhari kwa mke wake lakini zoezi hili linatakiwa kufanywa kwa uangalifu na busara. Mume hatakiwi kukimbilia kukasirika au matumizi ya nguvu. Asimwoneshe mke wake kwamba anaamuriwa au vinginevyo atatoa jibu kwa njia isiyopendeza. Njia iliyo nzuri kabisa, kwa mwanaume ni kuwa na huruma na uelewa. Lazima atekeleze zoezi hili kama mwenza mwenye upole na amwambie mke wake kuhusu madhara ya matendo maovu. Lazima atengenezewe mazingira ya kuchagua njia iliyo nyooka yeye mwenyewe kwa shauku na hamu.

Mwanaume anatakiwa kuwa na wastani, ni kwamba wala asiwe mkali sana na kiherehere ama asiwe mzembe.

Mwanamke, kama alivyo mwanaume, anahitaji uhuru na anatakiwa apewe uwezo wa kujiamulia la kufanya kwenye makundi yake kwa usawa unatakiwa.

Lazima mwanamke awe huru awe huru kuwasiliana na wazazi wake, kaka zake na dada zake, na lazima aruhusiwe kuwa na watu wa aina inayofaa.

Kwa ufupi, ipo mifano isiyo ya kawaida ambapo mwanamke ananyang’anywa utashi wake. Lakini hata kwenye mifano kama hiyo mtu hatakiwi kuvuka mpaka uliowekwa na kuwa mkali sana. Ukali wa kupita kiasi unayo madhara. Huharibu mazingira ya urafiki na husababisha maudhi. Mwanamke anaweza akajibu kwa ukali zaidi kutokana na ukali wa mume wake. Mke anaweza hata kuomba talaka.

Mwanamke kijana, mke wa… alimwambia mwandishi wa habari mahakamani: “Niliolewa na Bwana….Miaka mitano iliyopita. Tunao watoto wawili; mmoja wa kiume na mwingine wa kike. Wakati fulani mume wangu amekuwa anamchukulia kila mtu kwa namna ya ubeuzi. Haniruhusu mimi kushirikiana na mtu yeyote. Hata hufunga milango ya nyumba anapoondoka nyumbani. Sisi ni wafungwa ndani ya nyumba yake. Sasa, siwezi hata kwenda kwa wazazi wangu.

Watu wa familia yangu hawatutembelei, kwa sababu yake. Sijui nifanye nini! Kwa upande mmoja ni kwamba siwezi kuishi naye, na kwa upande mwingine, nina wasi wasi kuhusu hatima ya watoto. Kwa hiyo, niliamua kuleta shauri langu kwenye mahakama hii; labda wanaweza wakapitisha uamuzi fulani.”

Wanaume kama mume wa huyu mwanamke, kwa bahati mbaya ni wakali sana na si watu wa kawaida hivyo kwamba wake zao, licha ya kutaka kuishi pamoja na waume zao, huomba talaka. Wake zao huudhika sana, licha ya kuwa na watoto, wapo tayari kutengana nao.

Kwa nini mwanaume amkatae mke wake asishirikiane na ndugu zake wa karibu? Kwani haelewi kwamba ukali ukizidi kiasi, hutayarisha uwanja kwa baadhi ya wanawake kukengeuka? Kwani hajasikia au hajaona familia zilizosambaratika kutokana na tabia ya aina hii?

Hata kama mke wa mtu atavumilia ukali wa mtu, patakuwepo upungufu wa huba inayo changamsha mazingira ya familia ndani ya nyumba. Inawezekanaje mtu kutarajia mke aliyeko kifungoni kuwa mwema kwa mume wake na watoto au kufuatilia kazi za nyumbani kwa hamu?

Haki Za Kinidhamu Za Mume

Ingawaje mume na mke ambao hutengeneza maisha ya pamoja ya familia, hugawana na kushirikiana katika kuendesha mambo ya nyumba yao, wanaweza kuwa na maoni tofauti kuhusu mambo fulani. Mwanaume anaweza kuhisi kwamba ni yeye ndiye anayetakiwa kuwa na uamuzi wa mwisho kuhusu mambo ya familia, bila kupata upinzani kutoka kwa mke wake.

Wakati huo huo mke wake anaweza akakataa kazi yake kama upande uliomtiifu. Ubishi na ugomvi unaweza ukaanza kwa sababu kila upande unajaribu kuanzisha mamlaka juu ya upande mwingine. Suluhu nzuri zaidi ya tatizo kama hili ni kwamba pande zote zinatakiwa kuacha kujionesha kama unao mamlaka makubwa zaidi kuzidi upande mwingine, na kujaribu kupata ufumbuzi wa matatizo yao kwa njia ya mazungumzo na uelewano wa kina. Hii inawezekana tu kufanikiwa kama pande zote zinaacha ukaidi.

Baadhi ya wanamume huwaamuru wake zao kufanya mambo mengi na kama wakikabiliwa na upinzani, wanadhani ni sahihi kuwashika, kuwaadhibu au hata kuwapiga wake zao. Msimamo huu si sahihi kabisa. Mwanaume wa kipindi cha ujahiliya ambaye alipungukiwa ubinadamu, alifanya mazoea ya kuwapiga na kuwaumiza wake zao.

Mtukufu Mtume (s.a.w) alipiga marufuku kuwapiga wanawake, isipokuwa katika hali isiyozuilika ambapo adhabu huwa wajibu.”

Mtume (s.a.w) pia alisema Nina shangazwa na mwanaume anaye mpiga mke wake, ambapo ni yeye mwenyewe, zaidi ya mke wake ambaye anastahili kupigwa. Enyi watu, msiwapige wanawake zenu kwa kutumia fimbo kwa sababu tendo la namna hiyo lina ulipizaji kisasi.”

Kumuonea mwanamke ambaye kwa utashi wake amekubali kuolewa na mwanamume, ambaye anataka kupata faraja na utulivu na yeye, na ambaye anamtarajia mume wake kushirikiana wote katika matatizo, si sahihi. Kwa kweli Mwenyezi Mungu anamdhamini mwanamke kwa mume wake kwa njia ya ndoa na maonevi ya mwanaume kwa mke wake ni kutokuwa mwaminifu kwa dhamana ya Mwenyezi Mungu.

Imam Ali (a.s) alisema; Wanawake wamedhaminiwa kwa wanamume na kwa hiyo, wao si wamiliki wa bahati zao au mabalaa yao. Wao wapo na nyinyi kama dhamana ya Mwenyezi Mungu, kwa hiyo msiwaumize na msifanye maisha yao kuwa magumu.”

Mwanaume ambaye humpiga mke wake, hulazimisha uharibifu kwenye roho hivyo kwamba anaweza akapata mateso yasiyo elezeka na upendo wa familia na uchangamfu unaweza ukatoweka kabisa. Mwanamume mwenye ghadhabu anaweza kudunisha uhusiano mzuri wa ndoa na mke wake na kushushiwa hadhi? Hii kwa kweli ni aibu.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alisema: “Enyi wanaume! Inawezekanaje yeyote miongoni mwenu ampige mke wake na baadaye amkumbatie?”

Mwanaume, isipokuwa awe na haki ya pekee kwa mke wake, inayofanana na zile ambazo zitatajwa kwenye sura hii haruhusiwi kisheria kumlazimisha mke wake kufanya jambo lolote au kukimbilia matumizi ya kipigo kuhusu utovu wa utiifu. Mathalani mwanamke kisheria hawajibiki kufanya kazi za nyumbani kama kufagia, kupika, kufua, kutunza watoto, kushona na kadhalika. Licha ya kuwa wanawake walio wengi hufanya kazi hizi za mama wa nyumbani kwa kutaka wao wala si za lazima.

Wanaume wanatakiwa kuwashukuru wake zao kwa kazi zao za ndani ya nyumba. Kwa hiyo, hapana mwanamume mwenye haki ya kuhoji au kumwadhibu mke wake anapokabiliwa na kukataa kwake kutekeleza kazi za nyumbani.

Uislamu unapendekeza adhabu ya kipigo kwenye mifano miwili tu ambapo hali zake hukiukwa:

Mfano wa kwanza; Mwanaume ameruhusiwa kisheria katika Uislamu kupata na kutoshelezwa na tendo la Ndoa na kupata starehe ya kila aina kutokana na uhusiano huu na mke wake. Mke anawajibika kisheria kukubali matamanio ya ngono kutoka kwa mume wake. Kama mwanamke anakataa kumtosheleza mume wake, mume katika hatua ya kwanza anatakiwa amshawishi katika njia na mpangilio unaostahili. Hata hivyo, kama mwanaume anahisi kwamba mke wake anataka kuleta hali hiyo, basi kwa kuchunguza hatua zilizo bainishwa anaweza kumwadhibu.

Mwenyezi Mungu anasema:


الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنْفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ اللَّهُ ۚ{34}

“Wanaume ni wasimamizi wa wanawake kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanao jitihada hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde.”
(Quran 4:34).

Kwa hiyo, Qura’ni inamruhusu mume kumpiga mke wake kama hatua ya mwisho ya kutoa adhabu, kama inatokea mke anaonesha tabia mbaya kwa mume wake kuhusu matakwa yake ya ngono.

Hatua ya kwanza ni kutoa ushauri. hatua ya pili; Mwanaume aache kulala kitanda kimoja na mkewe au amgeuzie mgongo na kwa njia hii anatakiwa kuonesha hasira yake. Kama hakuna jibu linalotarajiwa hadi mwishoni mwa hatua ya pili na bado mwanamke anaendelea kukataa, mume anaruhusiwa kumpiga mke wake kidogo.

Mume, hata hivyo, haruhusiwi kuvuka mpaka uliowekwa na kukimbilia kumuonea. Wanaume wanakumbushwa kuhusu yafuatayo: Lengo la adhabu ya kipigo kwa mke wa mtu linatakiwa kuwa njia ya kumuelimisha na si kulipiza kisasi.

Kipigo kinatakiwa kufanywa kwa kutumia mkono au mti mwembamba na mwepezi.

Kipigo kikali cha kuweza kubadilisha rangi ya ngozi kuwa buluu au nyekundu hakiruhusiwi na mhusika lazima apigwe faini (dia).

Kupiga sehemu nyororo na nyeti za mwili kama vile macho, kichwa tumbo na kadhalika, hakiruhusiwi.

Adhabu ya kipigo haitakiwi kuwa kubwa mno hivyo kwamba haitasaidia kuanzisha hasira na fikra mbaya miongoni mwa wanandoa kumwelekeza mke kwenda kwenye kiasi cha kutotii zaidi.

Mwanaume (anaye nuia kumwadhibu mke wake kwa kutumia njia hii) anatakiwa kukumbuka kwamba ataendelea kuishi na mke wake na kwamba upendo wa familia usiharibiwe.

Mwanaume haruhusiwi kumpiga mke wake kama zipo sababu halali zilizomfanya asikubali matakwa yake.

Mathalani kama mke yupo kwenye siku zake za hedhi, saumu ya mwezi wa Ramadhani, awe amevaa vazi la Hija (Ihram) au mgonjwa. Sababu hizi zinakubalika na mwanamume hawezi kumwadhibu mke wake kwa kukataa matamanio yake kwa sababu hizo zilizotajwa.

Mfano wa pili; Mwanamke anaweza kutoka nje hapo tu ambapo ameruhusiwa na mume wake. Akitoka nje bila ruhusa hairuhusiwi kisheria na kufanya hivyo ni dhambi.

Hadith imesimuliwa kwamba Mtume (s.a.w.w) hakumruhusu mwanamke yeyote kutoka nje ya nyumba yake bila ruhusa ya mume wake. Alisema; Mwanamke yeyote ambaye hutoka nje ya nyumba yake bila ruhusa ya mume wake, atapata laana kutoka kwa malaika wote walioko mbinguni na wote wale wanao muona, wawe majini au wanadamu, hadi anaporudi nyumbani kwake.”

Hii ni hali ya mume yeyote ambayo lazima iangaliwe na wake zao.

Lakini wanaume hawatakiwi kuwa wakali sana kwa wake zao. Ni bora zaidi wao kuwaruhusu wake zao kutoka nje kila inapowezekana.

Hali hii ya wanaume haimaanishi kuonesha nguvu au kujaribu kuwashinikiza wake zao, lakini ni njia ya kuwazuia wanawake wasiende kwenye sehemu zisizo pendeza na zisizofaa.

Kuwa mkali sana si tu kwamba ni jinsi isiyofaa, lakini inaweza kuathiri uhusiano wa familia au hata kumsukuma mwanamke kuelekea kwenye utovu wa nidhamu na uovu.

Mwanaume lazima amzuie mke wake asiende kwenye sehemu za mikusanyiko zenye uovu na zisizofaa. Huu ni wajibu wa kidini kwa wanawake kuwatii waume zao. Mwanamke asiye mtiifu anaweza kuadhibiwa na mume wake. Hapa tena adhabu inatakiwa kutekelezwa hatua kwa hatua.

Hata hivyo, mwanamke anaweza kutoka nje ya nyumba yake kwa sababu maalum bila ya ruhusa ya mume wake na wanamume hawaruhusiwi kuwaumiza wake zao katika mifano kama hiyo: Kutoka nje kwa ajili ya kujifunza amri muhimu za dini.

Kutoka nje kwa ajili ya Hija pale ambapo anao uwezo muhimu wa kifedha na kutekeleza Hija.

Kutoka nje ya nyumba kwa ajili ya kulipa deni almuradi deni hilo haliwezi kulipwa bila kutoka nje.

Wanamume Wa Kutuhumu

Ni haki ya wanaume kuchunguza wake zao lakini si kwenye kiwango cha tuhuma na kutokuaminiana. Wanaume wengine hutuhumu na kutilia shaka uaminifu wa wake zao. Hii ni hatari na kufanya maisha kuwa magumu kwa familia yote.

Mwanaume anayesumbuliwa na tabia hii, wakati wote hutafuta dosari na kukusoa. Humfuatilia mke wake kwa karibu sana kwa humfuata kila aendako. Hupata ushahidi wa kusaidia sababu yake ya kutuhumu kutoka kwenye kila kitu. Kama akimuona au akiona picha ya mwanaume kwenye vitu vyake au akiona barua aliyoandikiwa na mwanaume au akimwona mwanaume anamtazama, atapata uhakika kuhusu kutokuaminika kwa mke wake. Kama mke wake akificha barua kutoka kwake, atadhani ni barua ya mapenzi. Asipoonesha mapenzi yake kama ilivyokuwa zamani atatilia shaka uaminifu wake.

Anaweza hata kufikiria kwamba kwa kuwa binti yake hafa nani na yeye, mke wake lazima alizini.

Mifano yote ya aina hii inaweza kuonekana kama uthibitisho imara wa udanganyifu wa mwanamke wa mume anayemtuhumu mke wake. hali huwa mbaya sana kama ndugu au rafiki akikubaliana na tuhuma yake.

Familia nyingi ambazo zimeathiriwa na maradhi haya, huteseka sana. Mwanaume anaweza kujishughulisha kama mpelelezi ndani ya nyumba. Na mke wake anaweza kuhisi kama vile alikuwa amefungiwa jela. Wote wawili wanaweza kupata maradhi ya kiakili na ndoa yake kuwa hatarini. Wanaweza hata kukimbilia kutalikiana au mauaji.

Ipo mifano mingi ya kuua na kujiua ambayo imetokea kutokana na tuhuma. Katika hali hii mwanaume na mke wake lazima watahadhari kuhusu uwezekano wa matokeo mabaya sana na kwa kutumia busara na utambuzi, huondoa hatari yoyote, ambayo ingetisghia ndoa yao au hata uhai wao. Wanatakiwa tu kuwa na tahadhari ya uwezekano wa hatari na kuweza kufikiri bila wasi wasi ili waweze kushinda matatizo yao.

Mwanaume anatakiwa kuacha ushabiki wake na wivu wa kupindukia. Lazima atumie mantiki. Lazima atambue kwamba kumtia hatiani mke wake kwamba ni mgoni si jambo dogo na kwamba madai ya aina hii huhitaji uthibitisho uliokamili.

Mwenyezi Mungu amesema kwenye Qurani Tukufu:


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اجْتَنِبُوا كَثِيرًا مِنَ الظَّنِّ إِنَّ بَعْضَ الظَّنِّ إِثْمٌ


ۖ


{12}

“Enyi mlioamini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi . . .”
(Quran 49:12).

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) alisema: “Yeyote awaye, ambaye atamshitaki kwa kumsingizia mke wake kwa kuzini atapoteza thawabu zake zote za matendo mema kama vile ambavyo nyoka huvua ngozi yake ya zamani. Na kwa kila unywele kwenye mwili wake, dhambi elfu moja zitaandikwa kwenye rekodi yake (kwa ajili ya siku ya hukumu).”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w) pia alisema:

“Mtu yeyote ambaye atamshitaki mwanaume au mwanamke muumini kwa kumsingizia, Mwenyezi Mungu atamning’iniza kwenye lundo la moto ili apate adhabu ya dhambi yake siku ya Hukumu.” 201.

Alimuradi kutokuaminika kwa mwanamke hakujathibitishwa kwa ushahidi ulio thabiti, mwanaume hana haki yoyote ya kumshitaki, vinginevyo atakuwa anafanya dhambi ambayo, kufuatana na Uislamu ataadhibiwa kwa kuchapwa viboko themanini.

Ushahidi utokanao na dhana hauoneshi lolote. Barua za zamani, picha na kadhalika hazithibitishi lolote.

Kutunza vitu kama hivyo si sahihi, lakini hili ni kosa ambalo hufanywa na vijana wengi na si jambo la kujihusisha nalo kabisa.

Kama mwanamke anaonekana anazungumza na mwanaume mgeni, licha ya kwamba si sahihi yeye kufanya hivyo, jambo hili haliwezi kuaminika kuwa uthibitisho wa kutokuaminika kwake.

Hii ni kwa sababu inawezekana alifikiria ingekuwa ni jeuri kutokuzungumza na mwanaume huyo, au inawezekana mwanamume huyo hakuwa mgeni lakini alikuwa rafiki yake baba yake au kaka.

Kama mwanamke anampongeza mwanaume, ingawa asingefanya hivyo, inawezekana kuwa hiyo ilikuwa kurahisisha na kwa hiyo haiwezekani liwe tendo la kuonesha kutokuaminika kwake.

Kama mwanamke anasema uongo kuhusu uhusiano fulani au akificha barua zake, inawezekana iwe kwamba ipo sababu nzuri ya kufanya hivyo au anaweza kuogopa mashtaka ya mume wake yasio na maana.

Kama mwanamke amekuwa hamchangamkii mume wake, inawezekana ametibuliwa naye, inawezekana ni mgonjwa au anaweza kuwa na matatizo mengine.

Kwa ufupi, katika mazingira yote ambayo yanaweza kuonesha dalili za kutokuwa mwamnifu anaweza kupata sababu nyingi na nzuri zinazotengeneza uwezekano wa makosa yeyote kuwa bure.

Bwana mpendwa! Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu acha tabia ya kutuhumu. Jione wewe mwenyewe kuwa mwamuzi wa haki na ulione tatizo kimantiki. Pima kiwango cha uwezekano wa mkeo kutokuwa mwaminifu na uelewe kama ndivyo, ni tuhuma tu au hata la kuaminika?

Sisemi kwamba wewe usijali na uwe mzembe lakini unatakiwa kuchukua hatua kufuatana na ushahidi ulio nao na si zaidi ya hapo. Kwa nini ukuze tatizo kwa kufuata tuhuma isiyo na msingi na uyafanye maisha kuwa magumu kwako na familia yako. Wewe ungejisikiaje kama mtu yeyote angekushitaki kwa jinsi isiyo ya haki? Kwa nini ujifedheheshe mwenyewe na mke wako? Kwa nini usimhurumie mke wako? Imepata kukujia fikira kwamba hatimaye mke wako anaweza akukengeuka kwa sababu ya wewe kutokumwamini na mashitaka ya kumsingizia?

Imamu Ali (a.s) alimsimulia mwanae Imamu Hasan (a.s): “Uwe mwangalifu usifanye mambo kama mtawala ambapo haupo hivyo kwa sababu hii inawezekana kuwaelekeza watu wanaofaa kwenye dhambi”

Kama unamtuhumu mke wako, usimwambie mtu yeyote unayemuona, kwa sababu wanaweza kuthibitisha tuhuma yako kwa vile ni maadui zako, wepesi kuamini au uzembe. Wanaweza hata kuimarisha hutuma yako na kukusababishia ukosefu wa furaha katika dunia hii na akhera. Hususan, usimwambie mama yako au dada yako kwa sababu ni kawaida watakubaliana na wewe na kwa hiyo kuongezea tuhuma yako.

Lazima utafute ushauri kutoka kwa watu wenye busara na marafiki na ndugu wenye uzoefu.

Msimamo mzuri zaidi, hata hivyo, ni wewe mume kuzungumza na mke wako na mwambie akueleze. Lakini usitake kuthibitisha uhalifu wake. Sikiliza yale ambayo wanakuambia na uamue kama mwamuzi mwenye haki ambaye hana upendeleo.

Angalau ujaribu kumuamini na uchukulie kana kwamba shemeji yako wa kiume anakuletea ushahidi juu ya dada yako wewe kutokuwa muaminifu. Kwa nini ulishughulikie jambo hili bila huruma na kumuona mhusika kuwa mhalifu aliye thibitishwa?

Uwe na busara na uvumilivu, vinginevyo utamwacha bila sababu ya maana. Kama unavumili mateso ya kuwa mtalaka lakini unao uhakika gani kuhusu mke wa ndoa ijayo?

Bado utaendelea kuwa unatuhumu. Kosa lao ni nini kama ni wewe ambaye unasumbuliwa na maradhi haya? Uwe na busara na jaribu kuelewa tatizo lako mwenyewe.

Uwe na tahadhari usije ukajiua au kumua mke wako. Kwa sababu, utaharibu maisha yako hapa duniani na Mwenyezi Mungu Mweza atakuwadhibu huko Akhera.

Lazima uelewe kwamba kumwaga damu siku moja kitendo hicho kitajulikana halafu ama utanyongwa au utafungwa kifungo cha maisha.

Kama hutakubaliana na jambo hili basi tazama takwimu za waliotiwa hatiani.

Wake za wanaume wenye ugonjwa wa kutuhumu pia wanao wajibu mkubwa kuhusu familia zao. Wanawake hawa lazima wajitolee muhanga na kuthibitisha uwezo wao katika hali ngumu kama hiyo.

Mama mpendwa kwanza kabisa mume wako ameambukizwa ugonjwa wa hatari ambapo yeye, kwa kutaka yeye mwenyewe, huchukua hatua zisizo sahihi ambazo zingehatarisha familia yenu.

Lazima uoneshe mapenzi yako kwake kadiri uwezavyo. Lazima awe na uhakika kwamba ni yeye tu katika maisha yako. Uwe mvumilivu kuhusu tabia yake, usimpigie kelele, usikatae kusema naye na usiwe kaidi kwake.

Ukihisi kwamba anafuatilia barua zako au anadhibiti kurudi na kutoka kwako nyumbani, usifanye upinzani. Mwambie kila kitu, mwambie ukweli. Epuka kusema uwongo au kukanusha matukio ambayo yametokea.

Kama akigundua kwamba umemdanganya kuhusu suala lolote, ataona hilo kama uthabitisho kuhusu udanganyifu wako, ambapo haitakuwa rahisi kurekebisha uharibifu wake.

Kama mume wako mwenye maradhi ya kituhuma akikuzuia ushirikiane na mtu fulani au anataka ufanye kazi fulani, basi kubali neno lake vinginevyo sababu ya wasi wasi wake kwako itaimarika. Kwa ufupi epuka matendo yote ambayo yanaweza kumfanya akutuhumu.

Imamu Ali (a.s) alisema: “Yeyote anayejiweka wazi kwa shutuma, asiwalaumu wale wanao mtuhumu.”

Kama mume wako anaonesha chuki kwa mtu yeyote, lazima uache mawasiliano na mtu huyo kabisa.

Bibi mpendwa! Ni bora zaidi wewe kuiweka familia yako pamoja kwa lengo la kudumisha urafiki na watu wengine. Usidhani kwamba wewe ni mtumwa kwenye minyororo ya mume wako, lakini tambua kwamba bado wewe ni mke wa mwanaume.

Kumbuka ulipofanya mapatano ya ndoa na mume wako, ulikubali mgawo wote wa nyakati za furaha na huzuni katika maisha. Hivi itakuwa haki wewe kumtendea mabaya mume wako ambaye anaumwa maradhi ya kutuhumu? Weka pembeni mawazo yasiyo pevuka na uwe na busara. Kwa jina la Mwenyezi Mungu kujitolea kwako kwa kiwango chochote kwa ajili ya familia yako ni kitendo cha manufaa. Mwanamke mzuri ni yule anaye weza kuvumilia hali ngumu.

Imamu Ali (a.s) alisema: “Jihadi ya mwanamke ipo kwenye kuvumilia matendo ya kashifa na hamasa ya mume wake.”

Usifanye jambo lolote ambalo lingemfanya mume wako akutuhumu. Usiwatazame wanaume wengine.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alisema: Mwenyezi Mungu atamkasirikia sana mwanamke aliyeolewa anayependa kuwatazama wageni.”

Usishirikiane na wanaume wageni. Usiondoke nyumbani bila ruhusa ya mume wako. Usipande magari ya wageni. Usafi wako tu peke yake hautoshi, lakini ungeepuka kitu chochote ambacho kingeamsha tuhuma ya mume wako. Inawezekana akutuhumu kwa mambo madogo sana kutokana na tabia yako.

Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 alisema mahakamani; Ilikuwa wakati wa baridi ya mwaka 1963, ambapo ilikuwa siku ya barafu niliingia kwenye gari la mjomba wa rafiki yangu. Aliniambia kwamba mjomba wake angenipeleka hadi nyumbani kwangu kwa gari lake. Nilikubali nikaingia kwenye gari lake. Tulipofika nyumbani mume wangu alikuwa amesimama karibu na mlango wa nyumba na kwa vile sikutaka mume wangu kuniona ndani ya gari la mtu mwingine nilimwomba mjomba wa rafiki yangu aendelee na safari na alifanya hivyo. Baadaye mume wangu ambaye alikwisha niona ndani ya gari hilo, aliniuliza kuhusu suala hili, lakini nilikanusha kila kitu. Akawa ananituhumu zaidi na ilifika kiwango ambapo hakuamini hata ushahidi wa rafiki yangu. Sasa ni miaka minane wala haishi na mimi ama kunipa talaka. Sijui hata la kufanya.”

Unadhani ni nani wa kulaumiwa katika hadith hii? Ningesema kwamba mwanamke ana hatia zaidi kuliko mume wake. Ni mwanamke ambaye kwa uzembe wake na wepesi wa fikira, alijiweka yeye na mume wake katika hali hii.

Kwanza, kabisa mwanamke hangekubali msaada wa lifti ya gari la mgeni kwani hilo si jambo sahihi kufanywa na mwanamke yeyote. Haistahili na ingeweza kuwa hatari.

Pili, hangefanya alivyofanya baada ya kumuoana mume wake. Angesimamisha gari na kumpa mume wake maelezo ya kina.

Tatu, mojawapo ya makosa ya mwanamke ilikuwa kumwambia dereva kuendelea na safari.

Nne, hangekataa baada ya kuulizwa. Angeeleza kila kitu katika hatua hii ya kuchelewa na ingesaidia kupata ufumbuzi wa tatizo.

Kama mambo yalivyo, pia mwanaume alikosea. Si lazima aone tukio hili kama ndio ushahidi wa kutoa uamuzi kuhusu hatia ya mke wake. Lazima afikirie uwezekano kwamba mke wake inawezekana alipanda gari la mgeni kwa uzembe na halafu labda kwa sababu ya woga alimwambia dereva asisimamishe gari na kama ilivyo kawaida akakanusha jambo lote.

Lazima apeleleze jambo hili mara atakapo hakikisha kwamba hana hatia, lazima awe msamehevu.

Mwanamke Asiye Mwaminifu

Mara tu mwanamke akionekana ana hatia ya kuzini, kwa kutumia uthibitisho madhubuti, mume wake atakuwa katika hali ngumu sana. Kwa upande moja heshima yake inakuwa hatarini na kwa upande mwingine kuvumilia fedheha ya aina hii si rahisi.

Anahisi amenasa kwenye mtego wa kutokuafikiana ambamo si rahisi kujinasua.

Mwanamume aliyeko kwenye hali hii anaweza kuchagua kufanya mojawapo ya haya yafuatayo:

(a) Anaweza kunyamaza kimya kuhusu jambo lenyewe ili aokoe heshima yake na kwa ajili ya familia yake.

Lakini lazima ataishi akikumbuka jambo hili katika maisha yake yote. Kama mambo yalivyo chaguo hili halikubaliki kwa mtu yeyote mwenye kuheshimika, kwani haitakuwa rahisi kuvumilia kuishi na mke wake mzinzi na uwezekano wa kupata mtoto wa haramu. Mapenzi makali ni sifa inayopendeza sana kwa mwanamume hivyo kwamba mwanamume ambaye hana sifa hiyo hawezi kufurahia neema ya Mwenyezi Mungu Mweza. Ni maisha ya fedheha na aibu ilioje watu hao walio nayo ambao hawajali kutokuaminika kwa wake zao. “Mtume (s.a.w.w) alisema: ‘Harufu nzuri ya Peponi yaweza kunuswa katika umbali wa safari ya miaka mia tano, lakini makundi mawili ya watu yatanyimwa; nayo ni wale watu ambao wamelaaniwa na wazazi wao na mume wa mke aliye zini.’ Swali liliulizwa; ‘Ewe Mtume (s.a.w.w) wa Mwenyezi Mungu; nani huyu mume wa mke aliyezini? Mtume alijibu: ‘Mwanaume ambaye anamjua mke wake kuwa ni mzinzi, na hunyamaza kimya kuhusu suala hili.’ ”

(b) Angeweza kumuua mwanaume aliyezini na mke wake au wote wawili mke wake na mwanaume mzinifu. Anaweza kulipa kisasi na kupata amani. lakini tendo hili ni la hatari kwani halingekuwa na mwisho mzuri, kwa sababu mauaji hayangefichwa daima milele. Muuaji lazima angejulikana na kuadhibiwa. Hangeweza kuthibitisha kutokuaminika kwa mke wake ndani ya mahakama; na kwa hiyo uwezekano wake kuachiliwa kutoka jela ungekuwa mdogo sana. Ingewezekana hata kupewa adhabu ya kifo. Hivyo angepoteza maisha yake na watoto wake wangekengeuka. Kwa hiyo, si busara kwa mwanaume kuhatarisha maisha yake kwa sababu ya kulipa kisasi. Mwanaume anatakiwa kuwa na busara na mtaratibu na kuweza kudhibiti hasira yake hadi apate ufumbuzi unaofaa kwa tatizo lake.

Angejiua ili asiendelee kuona kutokuaminika kwa mke wake na aishi maisha ya fedheha. Tendo la kujiua wala si lenye busara kwa sababu upande moja amejiua, ambayo yenyewe ni dhambi kubwa katika Uislamu na muuaji lazima aadhibiwe na Mwenyezi Mungu mnamo Siku ya Hukumu. Kwa upande mwingine amejinyima maisha. Hii ni mantiki ya aina gani ambayo ingeshawishi kujiua kama kisasi cha uhalifu wa mtu mwingine.

Angeteseka katika maisha yajayo na pia kumpa uhuru mkubwa zaidi mke wake kuendelea kuzini zaidi.

Angemtaliki mke wake. Hiki ni kitu cha busara zaidi kufanya. Ni sahihi kwamba talaka ingeharibu maisha ya familia yake na ingeleta madhara zaidi kwake na watoto wake, lakini hakuna njia nyingine yeyote. Ni bora zaidi yeye kumtaliki mke wake na achukue watoto wake, kwa sababu si sawa kuwaacha waishi na mama yao mwovu.

Kama mambo yalivyo, kulea watoto si kazi rahisi kwa mwanaume, lakini lazima ahakikishe kwamba Mwenyezi Mungu angemsaidia. Angemsaidia yeye kuendesha tabia ya kuheshimika.

Usitamani Wanawake Wengine

Mwanaume lazima ajitahidi sana kuchagua mwanamke ambaye atamfaa.

Yupo kwenye fursa ambapo anaweza kuwa mwangalifu na kuchukua tahadhari katika kumpata mwenza ambaye ataishi naye katika maisha yake yote. Hata hivyo, baada ya kuoana, si sahihi yeye kuanza kutamaani wanawake wengine. Ni sharti asifikirie wanawake wengine isipokuwa mkewe.

Lazima atambue kwamba msichana ameacha familia yake ili aishi naye na si sahihi kwa mume kuendekeza matamanio ya kitoto. Lazima afanye jitihada kuiweka familia yake mpya pamoja na lazima ajaribu kutengeneza mazingira ya kirafiki nyumbani.

Mwanaume ambaye anataka kuwa na furaha yake mwenyewe, baada ya kuoa lazima aache mawazo ya kijinga na lazima abadilike ili aendane na maisha mapya.

Haina maana kwa mwanaume aliyeoa kutaniana na wanawake wengine au kuonesha mapenzi kwao. Mwanaume pia hangetaka mke wake ataniane na wanaume wengine. Mwanamke naye hangetaka msimamo wa aina hii kuendekezwa na mume wake kwa wanawake wengine.

Mwanamke anayemuona mume wake anakuwa karibu na kuwazoea wanawake wengine, ataona wivu na kukata tamaa. Hataipenda nyumba na familia yake. Huenda akalipa kisasi kwa kufanya kitendo cha aina ile ile au ataomba kutalikiwa.

Mwanamke alilalamika mahakamani kuhusu mume wake. Alikuwa ameolewa kwa miaka thelathini na tatu akasema kwamba mume wake kila mara anayo mazoea ya kutaniana na wanawake wengine.”

Mwanamke alilalamika mahakamani kwamba kila mara mume wake alikuwa anaonekana kuvutiwa na marafiki zangu. Akasema kwamba aliacha kuwaalika marafiki zake nyumbani kwake kwa sababu walifikiri mume wake alikuwa anavutiwa nao na kwamba yeye-mke alikuwa anaona aibu kwa sababu yake.”

Haistahili kwa mwanaume aliyeoa kutupa jicho la mapenzi kwa wanawake wengine. Kuwatazama wanawake wengine kwa matamanio husababisha shauku, mfadhaiko na kutokujali familia.

Mwenyezi Mungu anasema katika Qurani Tukufu:


قُلْ لِلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ۚ{30}

“Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. . (Quran 24:30).
Imamu Sadiq (a.s) alisema: ‘Mtazamo wenye matamanio ni mshale wenye sumu uliotupwa na shetani. Upo uwezekano mkubwa kwamba mtazamo kama huo ungekuwa sababu ya huzuni na masikitiko kwa muda fulani.’

Kuonesha mapenzi, mabingwa wa maradhi ya akili wanasema ni ugonjwa. Jicho ambalo limezoea tabia hii, haliwezi kutosheka. Kutazama kwa njia hii huwa sababu ya uharibifu mwingi, ambapo vijana wanaweza kukengeuka na kuacha njia iliyonyooka. Kile ambacho macho hayakioni moyo hauwezi kutamani.

Mtu anaweza kujizuia katika hatua za mwanzo kuhusu matokeo mabaya ya mitazamo iliyozuiwa, lakini hatimaye atashindwa na kuvutiwa na kile anachokiona.

Imamu Sadiq (a.s) alisema; ‘Mitazamo iliyokatazwa ya mara kwa mara huamsha matamanio katika moyo wa mtu na hiyo inatosha kumpotosha mtazamaji.’

Uislamu, kwa kutambua madhara ya mitazamo ya kizinifu kama hiyo, umeharamisha moja kwa moja.

Mwanaume ambaye ghafla anapomuona mwanamke huko barabarani au mahala pengine, anatakiwa kuelekeza macho yake mahali pengine au afumbe macho yake. Asiwaangalie wanawake kwa muda mrefu. Hii inaweza kuwa ngumu mwanzoni, lakini akifanya zoezi kidogo anaweza kumudu.

Watu wenye busara wanatambua kwamba kujizuia kwenye mitazamo iliyokatazwa ni zoezi ambalo lingewatokeza kama vile mauaji, uhalifu, kujiua, kuchanganyikiwa kiakili, mfadhaiko, kudekeza tamaa ya moyo, kuondoa hatari nyingi ambazo zingejitokeza wazi, ugomvi wa famili na kadhalika.

Ninatambua matatizo ambayo yana wakabili vijana katika kipindi hiki, na ninajua kwamba kufumba macho ya mtu ili yasione uchafu wa mitaani na penginepo si jambo rahisi, lakini hakuna njia nyingine yoyote zaidi ya kudharau hayo.Mwanaume anayeweza kufumba macho yake ili asione wanawake wengine, atakuwa amepata ulinzi dhidi ya maovu mengi. Badala yake atafurahia familia yake na kupata utulivu wa akili.

Bwana mpendwa! Kama unataka kupata furaha, mara tu ukioa usiwatilie maanani wanawake wengine. Usiwape pongezi wanawake wengine mbele ya mkeo. Usiseme: “Natamaani labda ningemuoa fulani… nilikosa fursa nyingi nzuri.” Maneno ya aina hiyo yanaweza kumkera mke wako na anaweza asikuchangamkie wewe na maisha kwa ujumla. Anaweza hata kufanya kama ulivyo fanya na kusema kwa mtindo huo huo.

Matokeo yake ni kwamba maisha yako yanapungukiwa furaha. Ni wa kusikitikiwa wanaume waovu na kuwaacha wake zao, kama vile hawajapata kujua mapenzi na uaminifu wa familia. Wanaume wa aina hii ni kama wanyama ambao huelekeza juhudi zao zote kwenye kula, kulala na kuondoa hamu ya ngono. Huonekana kama vile ni wageni wa ubinadamu na mapenzi.

Uwe Mwenye Kushukuru

Kazi ya utunzaji wa nyumba inaweza kuonekana kama kazi rahisi kwa wanaume wengine, lakini itakuwa ni jambo la kuridhisha kukubali kwamba kazi hii ni ngumu na inachosha.

Mama wa nyumbani! Hata kama atafanya mchana kutwa na usiku kucha hataweza kumaliza kazi yake yote.

Kupika kufanya usafi, kufua nguo na kunyosha pasi kuosha vyombo na kuvipanga, kutandika vitanda na kupanga fenicha na zaidi ya yote kuwatunza watoto, si siku moja, lakini, ni kila siku ni ngumu sana.

Mwanaume anaweza kufikiri kwamba mke wake anapika tu mara tatu kwa siku na kusahau kazi zake zingine nyingi sana.

Ni mwanaume huyo tu ambaye atakuwa tayari kukaa nyumbani kwa kipindi cha mwezi moja na afanye kazi ya nyumbani ndiye atajua shinikizo lililopo, na hapo ndipo atakapo pendezwa na juhudi za mke wake.

Mke wa nyumbani hufanya kazi hii yote kwa furaha lakini hutarajia mume wake kupendezwa naye na kuonesha shukrani zake.

Bwana mpendwa! Kuna ubaya gani ukimpa ahsante mke wako kwa kazi ya kutunza nyumba? Kwa nini usioneshe upendo kwa chakula anachopika? Kuna ubaya gani ukimshukuru mke wako kuhusu juhudi zake za kutunza watoto? Hutambui kwamba kupendezwa kwako kwa jitihada zake ni kitendo cha kumtia moyo na kumchangamsha?

Kama hutajali jitihada zake, au hutaki kumshukuru atapoteza mvuto wa kazi ya kutunza nyumba na halafu wewe utalalamika. Lazima utambue kwamba wewe unaweza kuwa chanzo cha uvivu wa mkeo.

Kama mgeni anakupa upendeleo mdogo, ungemshukuru mara nyingi sana, lakini mke wako anayekupendelea mara nyingi, humshukuru hata mara moja! Wewe haupo tayari kumfurahia kwa kuonesha kupendezwa kwako kwa jitihada zake zote.

Mama wa nyumbani mwenye umri wa miaka ishirini na tisa aliandika kutoka Tehran. “Nimeolewa na mwanaume asiye na shukrani na asiye pendezwa ambaye hajali kabisa kazi yangu ya kutunza nyumba. Ninafua, ninafanya usafi, ninapika, ninapamba nyumba, ninafuma sweta kwa ajili ya familia, hupiga rangi viatu vyake, hupiga pasi nguo zake na kadhalika na hajawahi kunishukuru hata mara moja. Wakati wowote ninapomwambia kuhusu kazi za nyumbani huingilia kati na kusema kwamba nisisifie kazi hiyo mbele yake. Anadharau juhudi zangu, ambapo kufaulu kwake kunategemea sana bidii yangu.”

Baadhi ya wanaume hufikiri ni kitendo cha ujasiri wa kiume kutojali kazi za nyumbani za wake zao. Wanadhani kama wakitoa pongezi kwa kazi hiyo ya wake zao, wanawake wataharibika. Wanaweza hata kuamini kwamba mume na mke hawahitaji kupeana ahsante wao kwa wao.

Imani hii si sahihi, kwa sababu yeyote anaye tenda wema kutoka katika mtizamo wa kisaikolojia anahitaji kupewa shukrani na kuthaminiwa.

Kufurahia jambo la mtu humpa hamasa ya kufanya vizuri na hii ni kweli hususan kwa mama wa nyumbani ambaye hufanya kazi ya kuchosha kila siku tena na tena.

Hivyo Uislamu unaona kitendo cha kutoa shukrani ni sifa njema katika tabia ya mtu. Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Yeyote anayemsifu Mwislamu, Mwenyezi Mungu humwandikia sifa nyingi hadi Siku ya Hukumu.”

Mtume (s.a.w.w) wa Uislamu alisema:

“Yeyote anayemheshimu Mwislamu, na kusema naye kwa uchangamfu, na humwondoshea huzuni, wakati wote atakuwa kwenye neema za Mwenyezi Mungu.”

Pia Uwe Msafi Nyumbani

Kufuata kanuni za usafi kwa kila mtu na kila mahali ni muhimu. Mtu lazima aweke mwili wake na nguo zake katika hali ya usafi, wakati wote. Lazima aoge angalau mara moja kwa wiki na lazima aoshe uso wake na mikono yake kwa sabuni, achane nywele zake, anyoe nywele, aoshe miguu yake, avae soksi safi kila siku na lazima pia avae nguo zenye tohara. Dini tukufu ya Uislamu inasisitiza sana kuhusu usafi na kuvaa vizuri.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alisema: “Usafi ni sehemu ya imani (ya Uislamu).”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alimuona mtu aliyekuwa mchafu, nywele zake hazikuchanwa na yeye hakuwa katika hali ya kuvutia. Mtume (s.a.w.w) alisema: “Kutumia neema za Mwenyezi Mungu ni sehemu ya imani ya Uislamu.”

Mtume (s.a.w) wa uislamu pia alisema: “Mtu mchafu atakuwa mfanya ibada mchafu wa Mwenyezi Mungu.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliongeza kwa kusema: “Jibril alisisitiza sana kupiga mswaki meno hivyo kwamba nikawa nayahofia.”

Imamu Ali (a.s) alisema: “Mwenyezi Mungu ni mzuri na hupenda uzuri. Na pia hupenda kuona athari za neema Zake zinapotumiwa na waja wake.”

Usafi na uzuri si kwa ajili ya wanawake tu, lakini wanaume lazima pia wanatakiwa kuwa safi na wavae vizuri. Baadhi ya wanaume hawajali usafi wao na huoga mara moja kwa kipindi fulani. Hawajali nguo zao zipo katika hali gani na hawajali hata kunyoa ndevu zao. Wananuka harufu mbaya sana hivyo kwamba huwafanya wengine kuwa mbali nao.

Wanaume ambao ni waangalifu kuhusu usafi na huweka umuhimu kuhusu nguo zao, mara nyingi hufanya hivyo nje ya nyumba zao. Ni kwamba wanaonekana safi na kuvaa vizuri nje ya nyumba kwa ajili ya watu, si ndani ya nyumba zao kwa ajili ya familia zao. Huonekana nadhifu sana mitaani, kwenye mikusanyiko na kadhalika lakini mara tu wanaporudi nyumbani; huvaa nguo zilizochakaa. Mara chache sana kuangalia hali ya nywele zao na nyuso zao wanapokuwa nyumbani kwa ajili ya familia zao.

Wanaweza hata wasijali kunawa uso kabla ya kunywa chai ya asubuhi. Wanaume wa aina hii huzifanya familia zao zisiwajali.

Bwana mpendwa! Kama huwezi kumvumilia mke aliye mchafu na aliye vaa nguo zilizo chakaa na unatarajia aonekane safi na mzuri akiwa nyumbani, basi uwe na uhakika kwamba anatarajia hivyo hivyo kutoka upande wako. Mkeo pia, huchukia mume mchafu, anaye nuka na asiye nadhifu. Mke wako anataka kukuona wewe katika hali safi na nadhifu.

Kama utashindwa kutosheleza matarajio yake kuhusu unadhifu, anaweza akawaona wanaume wengine ambao wanaonekana safi na nadhifu na anaweza hata kudhani kwamba wametokea dunia nyingine. Atakulinganisha na wao na yawezekana akapoteza mvuto kwako. Kwa nini unaonekana safi kwa ajili ya wageni huko mitaani lakini unaonekana mchafu mbele ya mke wako na watoto wako.

Kwa hiyo, dini tukufu ya Uislamu inawaamuru wanamume wajipambe mbele ya wake zao.

Mtume (s.a.w.w) wa Uislamu alisema: “Ni wajibu kwa mwanaume kumpa mke wake chakula na nguo na asionekane mbele yake akiwa mchafu na hapendezi. Kama angetimiza yaliyotajwa hapo juu, haitamwia vigumu kutekeleza haki za mke wake.”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) pia alisema: “Enyi wanamume lazima mjiweke katika hali ya usafi na kuweni tayari kwa wake zenu kama ambavyo nyingi mnavyotaka wake zenu kuwa tayari kwa ajili yenu.”

Hasan bin Jiham anasema: “Nilimuona Hadhrat Abu al-Hasan (a.s) ambaye alipaka rangi nywele zake. Niliuliza kama kweli alipaka rangi nywele zake” Alisema: ‘Ndio, mapambo ya mwanamume kwa ajili ya mke wake kusaidia kumweka mke katika uaminifu. Wanawake wanaoacha njia safi na kuanza kufanya uovu ni kwa sababu ya uzembe na makosa ya waume zao.’ Hadhrat Abu al-Hasan alisema: ‘Unapenda kumuona mke wako katika hali ya uchafu?’ Nilijibu: ‘Hapana’ Halafu akaongezea: ‘Hufikiria kama unavyo fikiria wewe.’ ” Imamu Rida (a.s) alisema: “Wanawake wa Bani Israel waliacha njia iliyosafi kwa sababu waume zao hawakujali usafi wao na unadhifu wao.” Halafu Imamu akaongeza: “Vile unavyo mtarajia mke wako, ndivyo anavyotarajia kwako.”

Mtunze Mke Wako

Mume na mke kila mara huhitaji ushirikiano wa kila mmoja wao na kuonesha mapenzi kwa kila mmoja. Hata hivyo, haja hili huwa kubwa zaidi wakati wa ugonjwa na matukio mengine yanayo fanana na hilo. Mtu mgonjwa, kama vile anavyohitaji daktari na dawa, huhitaji matunzo na uangalizi wenye mapenzi. Muuguzi mzuri humsaidia mgonjwa kupona vizuri na haraka.

Mwanamke pia hutegemea mume wake kumtunza yeye wakati anaugua na kulala kitandani. Mke anatarajia mume kumtunza yeye zaidi ya wazazi wake.

Mwanamke anaye fanya kazi nyumbani kama mtumishi wa nyumbani anastahili uangalizi ulio na mapenzi kutoka kwa mume wake. Anatarajia kwamba ni haki yake mume wake amuuguze.

Malipo ya tiba na dawa ni mojawapo ya matumizi ya kawaida ya maisha na mwanaume anao wajibu wa kumpa fedha hizo muhimu. Mwanamke anayefanya kazi nyumbani bila mshahara wowote, hakika anayo haki ya kumtarajia mume wake kulipa gharama ya tiba yake.

Wapo wanaume ambao hawana aibu kufanya isivyo haki. Huwatumia wake zao wakati wana afya njema na wenye uwezo, lakini hukataa kulipa fedha wanapo ugua. Fedha yoyote ndogo wanayotumia kwa ajili ya tiba ya wake zao huilalamikia sana. Baadhi ya wanaume, wakiona gharama ya tiba ni kubwa wanaweza hata kuwaacha wake zao. Tabia hii ni sawa kweli? Mwanamke mmoja alikuwa analalamika kuhusu mume wake. Alisema: “Nilikuwa nafanya kazi kwa bidii nyumbani na nilipita kwenye nyakati nyingi za furaha na shida na mume wangu. Hata hivyo, sasa nimeugua, mume wangu anataka kuniacha!”

Bwana mpendwa! Kama unapenda kuwa na furaha na maendeleo ya familia yako, lazima umpeleke mkeo kwa daktari anapougua. Lazima ulipe gharama ya matibabu yake. Zaidi ya hapo, lazima umuuguze kwa wema. Sasa amewaacha wazazi wake ili aishi na wewe, anatarajia wewe kuwa na mapenzi zaidi kwake kuliko wazazi wake. Yeye ni mwenzako na mama wa watoto wako! Mhurumie na mpe matumaini ya kupona haraka. Mpikie chakula. Tayarisha chakula kinachofaa na nunua vifaa vilivyoelekezwa. Mlishe chakula. Yote haya yatamfanya mke wako afurahi.

Wanyamazishe watoto. Uwe mwangalifu wakati wa usiku. Wakati wowote akiamka muulize hali yake anavyojisikia. Kama hawezi kulala kwa sababu ya maumivu, basi na wewe uwe macho. Unaweza hata kuwaambia watoto wenu wakusaidie kumwangalia mama yao. Usimwache hata kidogo mke wako bila huduma, hasa zaidi anapokuwa anaumwa. Wakati kama huo, mke wako ataona mapenzi yako na yeye atakupenda zaidi. Atajivuna kwa sababu hiyo na atakuwa tayari kukuhudumia wewe na watoto zaidi, mara atakapo pona.

Mtume (s.a.w.w) alisema: “Mtu mzuri zaidi miongoni mwenu ni yule ambaye ni mwema zaidi kwa familia yake, na mimi ni mwema kuliko wote kwa familia yangu.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) wa Uislamu pia alisema: “Yeyote anayefanya jitihada kutambua haja ya mgonjwa, dhambi zake zitasamehewa, na atakuwa kama siku aliyozaliwa.” Mmoja wa maansari (wenyeji wa Madina) aliuliza: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wazazi wangu na watolewe muhanga kwa ajili yako, ni vipi endapo mgonjwa anatoka miongoni mwa familia yako- Ahlul –bait? Hakuna thawabu nyingi zaidi katika mfano huu?”

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alijibu: “Ndio.”

Uchumi Wa Familia

Kufanya mpango wa sadaka ya mke ni wajibu wa mume. Ni kwamba mwanaume anawajibika kulipa gharama za mke wake kama chakula, nguo, nyumba, daktari na dawa. Atakuwa anakosea kama hata mgharimia mke wake na anaweza kushitakiwa kisheria.

Mtu hawezi kutarajia familia iishi bila matumizi yeyote ya fedha. Watu wa familia wote wanahitaji chakula, nguo, dawa na mahali pa kuishi. Hata hivyo, wanaweza wakaomba vitu visivyo muhimu ambavyo mwanaume anaweza kukataa kuvinunua na asikubaliane na matakwa yao mbali mbali.

Mtu mwenye busara atatumia fedha kufuatana na uwezo wa kipato chake. Lazima abainishe bidhaa muhimu na avinunue katika mpango wa kipaumbele wakati wowote anapoweza. Lazima pia aweke akiba ya fedha kwa matumizi ya siku za shida. Kiasi fulani cha fedha lazima kitengwe kwa ajili ya kodi ya nyumba au kununua mahali pengine. Lazima mume asisahahu umeme, maji, nishati na simu. Kodi na ada za shule lazima zikumbukwe. Lazima kabisa aepukane na kutumia zaidi ya bajeti na kulipa vitu visivyo muhimu. Mpango mzuri wa matumizi ya fedha utamwepusha mtu asifilisike au kuwa na madeni.

Mwenyezi Mungu huona matumizi yaliyopangwa vizuri ni ishara ya imani na anasema ndani ya Qurani:


وَالَّذِينَ إِذَا أَنْفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا


{67}

“Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili bali wanakuwa katikati baina ya hayo”. ( Quran 25:67).
Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Yapo makundi manne ya watu ambao sala zao hazitafika kiwango cha kukubaliwa; Kundi moja ni la watu ambao hutumia vibaya utajiri halafu humwomba Mwenyezi Mungu Mweza, ‘Ee Mwenyezi Mungu naomba riziki. Halafu Mwenyezi Mungu hujibu, si nilikuagiza uwe mwangalifu katika matumizi yako. ’ ”

Abdullah bin Aban anasema: “Nilimuuliza Musa bin Jafar (a.s) kuhusu utunzaji wa familia ya mtu na akasema: ‘Ubadhilifu na uchoyo vyote ni sifa mbaya. Mtu lazima awe na kiasi.”

Mtu mwenye busara ataepuka kukopa fedha na hawezi kuchukua mkopo kwa matumizi mabaya. Uchumi unaotegemea mikopo (na riba), inayopokewa kutoka kwenye mabenki na taasisi zingine si sahihi kiislamu na kimantiki haufai.

Kununua vitu kwa mkopo, ingawa hufanya nyumba yako ionekane nzuri, lakini faraja na utulivu wa akili hutoweka.

Kwa nini mtu ananunua vitu visivyo muhimu kwa bei ya juu zaidi na kujaza mifuko ya wenye mabenki kwa malipo kidogo? Ni maisha ya aina gani hayo ambapo kila kitu hupatikana kwa bei ya mkopo? Kwani si vema zaidi kwa mtu kungoja na kuweka akiba ili anunue bidhaa kwa bei nafuu?

Ni kweli kwamba kupata fedha ni vigumu na huathiri sana maisha ya mtu. Hata hivyo, la muhimu zaidi ni jinsi mtu anavyotumia fedha yake. Zipo familia zenye vipato vizuri ambazo kila mara ni wadeni wa wengine. Zipo pia familia nyingi zenye vipato vya chini ambao huishi kwa raha. Tofauti baina ya makundi haya mawili ni jinsi ya fedha inavyo tumiwa. Kwa hiyo, inafaa zaidi ama mwanaume aendeshe udhibiti wa matumizi au awe msimamizi wa mtu ambaye anawajibika nayo.

Mwisho, inakumbushwa kwamba ubakhili ni mbaya kama ufujaji, kama mwanaume anacho kipato zaidi lazima aifurahishe familia yake zaidi na kuwapa mahitaji yao muhimu kadiri iwezekanavyo.

Utajiri na fedha vyote ni vya kutumia na kuwezesha upatikanaji wa vitu muhimu vya maisha, na si vya kulundika na kuviacha hapa duniani.

Ishara za utajiri lazima zionekane wazi kwenye familia ya mtu na nyumba. Kuna manufaa gani kufanya kazi kwa bidii halafu kinachopatikana kisitumike?

Mtu mzima atumie utajiri kuhusu familia yake na starehe yake mwenyewe. Inachukiza kuona mtu ambaye anao uwezo wa kifedha lakini watoto wake wanatamaani chakula kizuri na nguo nzuri. Watoto wa mtu bakhili kungoja kifo chake ili wagawane utajiri wake. Kama Mwenyezi Mungu Mweza wa yote anampa mtu neema zake, neema hizi lazima zidhihiri katika maisha ya mtu huyo.

Mtume (s.a.w.w) wa Uislamu alisema: “Si mwenzetu (si mfuasi wa Mtume s.a.w.w) ambaye anazo fedha lakini huiweka familia yake mbali na utajiri wake.”

Musa bin Jafar (a.s) alisema: Jamaa ya mtu ni watu wanaomtegemea. Hivyo, yeyote anayepewa neema za Mwenyezi Mungu, lazima azisambaze kwa wale wanao mtegemea ili wafarijike, au vinginevyo neema hizo zitaondoshwa kwake.”

Imamu Rida (a.s) alisema: “Ni jambo la manufaa kwa mtu kuwapa watu wa familia yake starehe itokanayo na matumizi yake, ili wasingoje hadi hapo atakapofikwa na mauti.”

Imamu Ali (a.s) alisema: “Tayarisha matunda kwa ajili ya watu wanaokutegemea kila siku ya Ijumaa ili kwamba watafurahia kuja kwa Ijumaa.”

Saidia Kufanya Kazi Za Nyumbani

Licha ya kwamba utunzaji wa nyumba ni wajibu wa wanawake, lazima ieleweke kwamba kuendesha mambo ya nyumbani si kazi rahisi.

Mke ambaye ni mama wa nyumbani hata akitumia muda kiasi chochote kile kwa utunzaji wa nyumba, hatoweza kumaliza kazi hiyo yote kwa wakati moja. Hii ni kweli hasa zaidi pale ambapo anatakiwa kuwakirimu wageni au anapougua na kadhalika. Kazi ya kutunza nyumba humchosha mke wa nyumbani na hivyo wanaume wanatarajiwa kuwasaidia wake zao katika suala hili.

Si haki kwamba mwanamume awe amekaa nyumbani bila ya shughuli yoyote ambapo mke wake anashughulika na kazi nyingi mbali mbali. Inafaa tu mume kumsaidia mke wake kadiri iwezekanavyo na wakati wowote awezapo. Msaada huu ni ishara ya huba ambayo humvutia mke kwa mume wake na familia yake.

Si ujasiri wa kiume hata kidogo kwamba mwanaume hapaswi kugusa kitu chochote ndani ya nyumba, bali kutoa amri tu kumpa mkewe. Nyumba ya familia si makao makuu ya kutoa amri, isipokuwa hapo ni mahali pa upendo, wema na ushirikiano.

Bwana mpendwa! Usidhani kwamba wewe ukifanya kazi za nyumbani ni kushusha hadhi yako. Kinyume chake ni kwamba, mke wako atapendezwa sana na kitendo chake cha kumsaidia.

Mtume (s.a.w.w) wa Uislamu ambaye ni mtu anaye heshimiwa sana katika historia, alikuwa na desturi ya kusaidia kazi za nyumbani.

Ayisha, mke wa Mtume (s.a.w.w) alisema: “Wakati wowote Mtume

(s.a.w.w) anapokuwa hana kazi, alikuwa na desturi ya kushona nguo zake, kutengeneza viatu vyake na alikuwa anafanya kazi nyumbani kama wanaume wengine.”

Rudi Nyumbani Mapema

Mwanaume asiye na mke anao uhuru wa kutumia muda wake, lakini pindi anapooa, lazima abadilishe mpango wake. Hawezi kukaa nje kwa muda wowote anaotaka. Anatakiwa kumtaarifu mke wake mahali alipo na kadhalika. Lazima asisahau kwamba mke wake huwepo nyumbani siku nzima, husafisha nyumba, huosha vyombo na hupika. Humngoja arudi nyumbani mara tu anapomaliza kazi zake, ili amuone, azungumze naye na kufurahia kuwa naye.

Watoto pia huwa na matumaini ya kumuona baba yao. Si haki kwamba mwanaume aache familia yake nyumbani na yeye afuate starehe zake mahali pengine.

Ndoa si tu kulisha chakula na kuimvisha nguo familia yako. Mwanamke ni mwenza wa mume wake na si mtumishi. Mke hayupo pale kwa ajili ya kufanya kazi mchana kutwa na kulishwa chakula lakini hasa zaidi anayo matarajio ya kuwa na rafiki wa kudumu na mwenza.

Baadhi ya wanaume kwa kweli hawafanyi sawa, hawana haki na wapumbavu. Huwaacha wake zao na watoto wao nyumbani na kutumia muda wa usiku kucha mahali pengine. Fedha ambayo wangetumia na familia nyumbani, anaipoteza mahali pengine.

Wanaume wa aina hii bado hawajaelewa maana ya mapenzi na huba na huona starehe zao zisizo na thamani na chafu kama ndio njia ya maisha mazuri. Hawatilii manani ukweli kwamba vitendo kama hivyo huwadhalilisha. Wengine hutambua vitendo kama hivyo kuwa vya kipumbavu na kijeuri.

Wanaume wa aina hii ni sababu ya huzuni kwa wenyewe na familia zao. Matendo yao huwashawishi wake zao kudai talaka kutoka kwao.

Mwanaume ambaye alimtaliki mke wake, alisema mahakamani: “Mwanzoni mwa ndoa yangu, nilikuwa na marafiki fulani ambao nilikuwa nikitoka nao kwa matambezi, ambapo humwacha mke wangu nyumbani… na nilikuwa na desturi ya kurudi nyumbani kesho yake alfajiri. Mke wangu ambaye alichoshwa na hali hii, alipewa talaka.

Tulikuwa na watoto kumi, ambao nilitaka kukutana nao mara mbili kwa mwezi. Kipindi fulani kilipita tukitekeleza mpango huu. Lakini sasa ni muda mrefu tangu watoto wangu wajifiche na ninayo shauku kubwa kuwaona watoto wangu.”

Mwanamke alisema; “Nimekata tamaa kwa upweke. Mume wangu hajali kabisa kuhusu mimi. Kwa ajili ya starehe zake huwa nje hadi asubuhi sana.”

Bwana mpendwa! Sasa umeoa. Usiendekeze tabia ya kikapera. Wewe unawajibika kwa mke wako na watoto wako, acha kushirikiana na marafiki wasiofaa rudi nyumbani mara unapomaliza kazi yako. Furahia maisha ya familia na mke wako na watoto wako. Hata kama starehe zako za kila siku usiku si zenye uovu, hata hivyo, zinaweza kusababisha madhara kwako na maisha yako ya ndoa.

Uwe Mwaminifu

Baada ya mapatano ya ndoa maisha binafsi ya watu wawili yanalingana na kuwa maisha ya ushirika moja wa kijamii. Kiapo kitukufu cha ndoa kinamaanisha kwamba mwanaume na mwanamkie wanapeana ahadi kila moja kuwa pamoja katika maisha yao yote, kusaidiana wao kwa wao, kuwa mwema na mwelewa wakati wote, wakati wa neema na wakati wa shida, wakati wa ugonjwa na afya njema na huzuni na kadhalika.

Utu unadai kwamba mwanandoa anatakiwa kuwa mwaminifu kwa ahadi yake. Wanandoa hawatakiwi kusahau mkataba wao hata kwenye hali ngumu. Msichana mdogo ambaye huchagua mwanamume mmoja kuishi naye katika maisha yake yote hatarajii kuwa amekuwa mwanamke wa makamo ya utu uzima. Si haki kwamba mwanaume atafute starehe na mwingine na kumwacha mke wake.

Mwanamke ambaye hutoa mchango mkubwa katika kujenga familia madhubuti katika mazingira mazuri ya maendeleo ya uchumi, hatarajii mume wake kumpenda mwanamke mwingine.

Mwanamke anayefanya bidii nyumbani kwa kawaida anayo matumaini kwamba mume wake hatamnyima mapenzi na huba yake wakati wa ugonjwa na kutokuwa na uwezo wa kufanya kazi. Jambo la mwisho kabisa hatarajii mume wake kutafuta starehe ya kwake peke yake.

Baadhi ya wanaume kwa kweli hawashituki. Wakati wake zao ni vijana na maumbo ya kuvutia wanafurahia kuwa nao, lakini huwaacha wanapo zeeka.

Mwanaume alimtaliki mke wake kwa sababu ya kuwa na kisirani, kwani tangu walipooana baba yake alikufa na mjomba wake akafilisika.

Mwanaume aliye muoa mwanamke kijana kwa kumpenda, alimtaliki baadaye kwa sababu hakumpenda tena.

Mwanamke… alilalamika mahakamani: “Nimeishi na mume wangu kwa miaka mingi, lakini sasa nimepata maradhi anasema kwamba hataki mke mgonjwa!”

Bwana mpendwa! Wewe si hayawani ambaye maisha yake yote ni kula na kukidhi matamanio ya kimwili. Wewe ni binadamu mwenye mchomo wa moyo, dhamira na tabia ya kujitolea. Hivi ni haki kweli kwamba wewe unafuatilia starehe zako nje ya nyumba yako?

Kama ndio, basi wewe ni muonevu na kwa hali hiyo wewe utaadhibiwa hapa hapa duniani. Ukitumia muda wako na mwanamke mwingine, basi, kwa ajili ya starehe utulivu wa akili yako na utapata maradhi ya kuharibikiwa akili. Watoto wako hawatakubali na watajibu kwa kukukashifu.

Kama mke wako anaugua, chukua hatua muhimu za kumtibu, na kama anayo maradhi yasiotibika, basi endelea kuishi naye, jitolee kumsaidia na usioe mke mwingine akingali hai.

Usimuudhi wakati huo mgumu. Ungetarajia nini endapo wewe ungekuwa katika hali hiyo? Ni haki kabisa kwamba yeye angetegemea hivyo hivyo kutoka kwako.

Ni sahihi kwamba wewe unapo ugua mke wako atataka umtaliki? Je hujafedheheka mbele ya marafiki na ndugu? Kwa hiyo kama unakubali kwamba uaminifu na unyofu ni sifa nzuri, basi jaribu kuwa mwaminifu.

Elimu Na Mafundisho

Mwanamke kijana ambaye ndio kwanza kaolewa anao wajibu wa kuendesha mambo ya mume wake na katika hali hiyo atahitaji ujuzi wa kupika, usafi, kunyosha nguo, kushona, kupanga fenicha, kukaribisha wageni wake, kushirikiana na watu wengine, kumtunza mtoto wake na kadhalika.

Mume wake atatarajia mke wake kujua yote haya. Hata hivyo, mategemeo yake yanaweza yasifanikiwe takriban muda wote kwa sababu ujuzi wa mke wake kijana kuhusu utunzaji wa nyumba ama haupo kabisa au upo kidogo sana.

Mtu afanyeje? Hili ni tatizo katika jamii zetu. Wazazi hawajali, wala mfumo wa elimu hauna mipango ya kutosha kukidhi haja hii. Hata hivyo, mtu anatakiwa kupata ufumbuzi wa tatizo hili.

Kwa vile mwanaume anakusudia kuishi na mke wake kwa maisha yake yote lazima amsaidie kumuelimisha, kwa sababu kwa kawaida wanaume huwa na umri mkubwa kuzidi wa wake zao na hivyo wanao uzoefu zaidi.

Mwanaume kwa uvumilivu anaweza kumuelemisha mke wake na kumfundisha vitu ambavyo anavijua. Anweza hata kumuuliza mama yake, dada au shangazi zake kuhusu mambo ambayo hayajui, au anaweza hata kununua vitabu vinavyohusu masomo kama ya kupika, ushonsji, utunzaji wa nyumba na kadhalika.

Mwanaume vile vile lazima amhimize mke wake kusoma vitabu ambavyo vitaonesha kimaadili kuwa ni vyenye manufaa. Lazima asahihishe upungfu wake wa maadili kwa adabu nzuri na sio kwa upinzani, au vinginevyo atageuka dhidi yake.

Mwanaume, kwa kutumia uvumilivu wake, anaweza kumwelimisha mke wake kwa mujibu wa njia yake ya maisha katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo wa ndoa yao. Inawezekana asifaulu asili mia kwa mia lakini bila shaka atakaribia kutosheleza mahitaji.

Elimu ya aina hii inahitaji uvumilivu, muda na busara, lakini mwanaume lazima ajaribu kuipata. Hii ni kwa sababu mwenza mzuri ni mama mzuri kwa watoto wake ni neema kwa mwanaume.

Mojawapo ya mambo muhimu ambayo mwanaume Mwislam aliyeoa anatakiwa kukumbuka ni ukweli kwamba mke wake pia ni Mwislam, na inawezekana awe hatambui utaratibu wa maisha ya Kiislamu na sheria zake. Inawezekana asijue hata kuhusu wudhu, kusali na kadhalika.

Kwa kweli ni wajibu wa wazazi kuwafundisha watoto wao mambo yote muhimu ya Kislamu na maadili. Kwa bahati mbaya, hata hivyo, wazazi hawajui kabisa kuhusu ukweli huu, na bila kuwafundisha mabinti wao kitu chochote kuhusu Uislamu, wanawaozesha. Hivyo wajibu wao huangukia kwenye mabega ya waume wanaowaoa.

Bwana mpendwa! Ni wajibu wako kumzoeza mke wako maadili ya Kiislamu na kumfundisha mambo yaliyohalalishwa na yale yaliyo haramishwa katika dini. Mfanye ajifunze kuhusu tabia za Kiislam. Kama huwezi kufanya hivi, basi tafuta msaada kutoka kwa wengine au fanya mpango wa vitabu na makala zenye elimu ya Uislamu na mwambie asome na kufanya kwa vitendo. Unaweza hata kufanya mpango wa elimu na maelekezo yake kupitia kwa mtu mwaminifu na aliyeelimika.

Kwa ufupi, ni wajibu wa mwanaume kumtia moyo mke wake kumuamrisha kufanya mema na kumkataza kufanya mabaya. Kama mwanamume atafuata wajibu wake huu, basi atafurahia kuwa na mwenza mwenye tabia njema, mwema, muaduilifu na mke mwenye busara.

Hata hivyo, kama mwanamume anaamua kutojali wajibu wake atateseka kwa kuwa na mke mjinga ambaye imani yake ni dhaifu na ambaye hana kinga dhidi ya uovu. Pia mume ataulizwa na Mwenyezi Mungu huko akhera kuhusu uzembe wake huu.

Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qurani Tukufu:


يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا قُوا أَنْفُسَكُمْ وَأَهْلِيكُمْ نَارًا وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ


{6}

“Enyi mlioamini jiokoeni nafsi zenu na watu wenu (wa nyumbani – wake zenu watoto wenu nk.,) kutokana na moto ambao kuni zake ni watu na mawe…” (Quran 66:6)
Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Aya hiyo hapo juu ilipoteremshwa mmoja wapo wa Waislamu alikuwa analia na kusema; ‘Mimi siwezi kujinusuru hata mimi mwenyewe kutoka kwenye moto wa Jahanamu na ninatakiwa kuwajibika kuinusuru pia familia yangu kutoka kwenye Jahanamu!’ Mtume (s.a.w.) alimwambia mtu huyu: “Ingetosha kama tu ungewaagiza kufanya mambo hayo ambayo wewe unayafanya na uwakataze wasifanye yale ambayo wewe mwenyewe unajizuia kuyafanya.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema: “Wanaume wameumbwa kuwa viongozi na kuwajibika kwa familia zao, na kwa namna hiyo wanawajibu kwa watu wanaowategemea.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.) pia amewakumbusha wanawake: “Waambieni waume zenu wafanye matendo mema kabla hawajawashawishi nyinyi kufanya mabaya.”

Kupata Mtoto

Moja ya mambo ambayo huweza kuwa ni nukta zenye kuumiza kwa wanandoa ni kuhusu kupata mtoto.

Ni kwamba mwanamke atataka kupata mtoto lakini mume wake anakataa au kinyume chake. Tatizo hili wakati mwingine huwa kubwa sana na matokeo yake wanandoa wanaweza kuishia katika kutalikiana.

Bibi…alilalamika mahakamani na kusema: “Niliolewa nikiwa na umri wa miaka ishirini na saba ambapo mume wangu alikuwa amemaliza masomo ya Chuo Kikuu. Alikuwa mkufunzi kwenye mojawapo ya chuo kikuu na nilihisi kuwa nilikuwa mwanamke mwenye bahati. Hata hivyo mume wangu hataki kuzaa mtoto. Simwelewi kwa sababu sote afya zetu ni nzuri na tunazo fedha za kutosha kuwa na angalau watoto wawili. Si kwamba hawataki watoto, kwani anawatunza vizuri wapwa zake.

Nina umri wa miaka thelathini na kama ilivyo kawaida ningependa kuwa mama. Mume wangu anaelewa hisia zangu lakini husema kwamba mtoto atakuwa sababu ya usumbufu katika maisha yetu na kuendelea.” Mwanamke huyu, wakati anajizuia asilie, anakabiliwa na tatizo ambalo ni zito sana hivyo kwamba wanandoa hawa waliamua kutalikiana, ili yeye aweze kuolewa tena na mwanamume mwingine na yeye apate muda wa kutosha kufanya utafiti wake wa kisayansi.”

Kupenda watoto na kuzaa ni matamanio ya kawaida ya binadamu na hata ya hayawani. Watoto ni matunda ya maisha na urithi mzuri kuliko wote wa mwanadamu.

Maisha ya mtu mwenye watoto hayatasitishwa na kifo chake lakini, hakika yataendeshwa kama vile maisha yalivyo panuka. Mtu asiye na mtoto au watoto atahisi mpweke na aliye tupwa na atajihisi vibaya zaidi atakapo kuwa mzee.

Nyumba isiyo na watoto ni mahali panapo chosha na haitakuwa changamfu na upendo. Ndoa isiyo na watoto, wakati wowote ipo katika hatari ya kuvunjika. Hivyo watoto ni chanzo cha uchangamfu na kudumu kwa familia.

Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Furaha ya mtu imo katika kupata watoto.”

Mtume (s.a.w.) wa Uislamu alisema: “Zaeni watoto wengi kwa sababu mnamo Siku ya Hukumu nitajivunia idadi yenu juu ya umma nyingine.”

Kumpenda mtoto ni matamanio ya kawaida, lakini baadhi ya watu hupotoshwa kutoka kwenye kawaida yao na wanaathirika na maradhi ambayo huwafanya kutafuta visingizio kama vile upungufu wa fedha, kuwa ndio sababu ya kuwafanya wasipende kuzaa. Hata hivyo, Mwenyeyzi Mungu amehakikisha kwamba atawaruzuku viumbe Vyake vyote.

Bakr bin Saleh alisema: “Niliandika barua kwa Hadrat Abu al-Hasan (a.s) nikisema kwamba nilikuwa nachukua hatua za kuzuia nisipate mtoto kwa muda wa miaka mitano; kwa sababu mke wangu alikuwa anasita kupata mtoto, na kwamba alikuwa anasema kwamba ukosefu wa fedha ungefanya kazi ya kulea mtoto kuwa ngumu.’ Nilimuuliza Hadrat Abu al-Hasan maoni yake kuhusu jambo hili.” Akajibu: “Usizuie kupata mtoto, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mweza atampa riziki.”

Mwenyezi Mungu Anaweza hata kuongeza riziki ya familia kwa sababu ya neema za watoto. Wapo watu wengi ambao walikuwa na shida kabla ya kupata watoto, lakini walipata maisha ya raha baadaye.

Baadhi ya watu huona watoto kama usumbufu. Hii si kweli na kwa kweli watoto ni chanzo kizuri sana cha furaha na kiburudisho kwa wazazi.

Kama ilivyo, kutunza watoto si kazi rahisi na yenye matatizo, lakini maadam inaafikiana na kanuni ya asili, mtu anaweza kuvumilia matatizo na kwa hali hiyo inafaa kukubali usumbufu uliomo humo.

Ufinyu ulioje wa akili wa wanaume na wanawake ambao kwa sababu ya kutokupata watoto wanakimbilia kuachana! Je si kweli kwamba inashangaza mwanaume mwenye elimu, anakataa kukubali sheria za utaratibu wa jambo la asili kwa kung’ang’ania kiasi cha hata kuwa tayari kumpa talaka mke wake?

Wanandoa wengine hukubaliana kupata mtoto lakini hubishana kuhusu wakati wa kupatikana mtoto. Mwanamke au mwanaume wa aina hii angesema; ‘Mtu lazima awe huru wakati wa umri mdogo kwani mtoto atamnyima uhuru wa kustarehe.

Ni vema kungoja hadi baadaye kupata mtoto mmoja au wawili.’ Kama wote mume na mke wanatofautiana kwa maoni, basi mabishano yataanza ambayo yanaweza kuishia kwenye kutalikiana.

Na tukumbuke kwamba kama mtu anataka watoto, basi lengo hili lingetekelezwa katika kipindi cha mwanzo kabisa cha ndoa. Hii ni kwa sababu watoto wanaozaliwa na wazazi vijana kwa kiasi fulani huwa bora kuliko wale wanaozaliwa na wazazi wenye umri mkubwa zaidi. Kwanza, watoto hawa afya zao huwa njema zaidi na wanaonekana kuwa na nguvu nyingi zaidi. Pili, kwa kuwa wanatokana na wazazi vijana, wanaweza kuishi kwa muda mrefu zaidi na wazazi wao. Wanaweza kusomeshwa zaidi na kulelelewa vizuri zaidi. Lakini watoto walio zaliwa na wazazi wenye umri mkubwa hunyang’anywa uongozi na mafundisho ya wazazi wao kwa sababu ya kifo au kukosa uwezo. Tatu watoto wa wazazi wenye umri mdogo wangeweza kufika kwenye umri wa kuwa na familia zao na kuanza kufanya kazi, ambapo wazazi wao wakingali hai. Hivyo wanaweza kuwa msaada mkubwa sana kwa wazazi wao watakapo kuwa wazee.

Kwa ufupi, kuzaa watoto wakati wa ujana ni vema zaidi kuliko umri mkubwa. Lakini hiki si kipengele cha muhimu sana hivyo kwamba kisababishe ugomvi na kutalikiana. Ni vema kwa mwanaume au mke kukubaliana kwa maelewano wasiruhusu suala hili kutengeneza mwanya katika ndoa yao.

Baadhi ya wanandoa hushindwa kuelewana kuhusu idadi ya watoto ambao wangetaka kuzaa.

Mwanamke akiwa amemshikia mtoto mikononi mwake alisema: “Miaka minne baada ya kuoana, nilizaa watoto wa kike wawili na mume wangu, lakini kwa kuwa alitaka mtoto mwanaume, nilipata ujauzito kwa mara nyingine na tena nilijifungua mtoto mwanamke. Sasa ninao watoto watatu wanawake. Mume wangu anafanya kazi benki na mshahara wake hautoshi familia yetu. Hivi karibuni amekuwa akisisitiza kwamba nibebe mimba mara nyingi hadi nizae mtoto wa kiume. Lakini mimi sipo tayari kwa mpango huu kwa sababu kipato chake hakitoshi kuwasomesha watoto wetu kwa namna tunavyotaka. Nimemwambia mara nyingi kwamba watoto wanaume na wanawake wote ni wazuri. Nina hofia kwamba kama nikibeba ujauzito tena nitazaa mtoto mwanamke tena.

Nina uhakika kwamba atataka kusisitiza tupate mtoto mwingine. Hatutakubaliana katika jambo hili na hivyo tumeleta shauri letu mahakamani.”

Ni sahihi kwamba kusomesha na kuelekeza watoto wengi ni vigumu na hii hususan ni kweli wako ambao hawana kipato cha kutosha.

Kwa hiyo, ni vema wanandoa kuamua kuhusu idadi ya watoto kwa mujibu wa kimaadili na uwezo wa kifedha. Lazima waelewane na waweze kupata ufumbuzi wa matatizo yao kwa kutumia busara na wema. Si sahihi kwa yeyote miongoni mwao kusisitiza kitu kisicho na mantiki.

Zipo familia nyingi ambazo ama wanao watoto wengi au zinatosheka na mtoto mmoja au wawili.

Baadhi ya wanandoa hutofautisha kuhusu jinsia ya mtoto (watoto) wanaotaka kuzaa. Wanandoa wengine, wanaume na wanawake hupenda kuzaa mtoto mwanaume na hawapendi kuzaa watoto wanawake. Kuzaliwa kwa mtoto mwanamke ni tukio ambalo lingemfanya mzazi mwanamke ajihisi ana hatia na kwa hiyo angenyamaza kwa sababu ni yeye ndiye amezaa. Lakini mwanamume huenda akaonesha kutokuridhika kwake. Wanaume wapo tofauti. Baadhi yao hawaoneshi kutokuridhika kwao wazi wazi na huishia kuonesha tu uso wa kuogofya. hawatilii maanani kuwahudumia wake zao baada ya kujifungua. Huonekana na huzuni.

Baadhi ya wanamume, hata hivyo huwa wakali sana wanapopata taarifa ya kuzaliwa mtoto wa kike. Huwakasirikia wake zao na huanzisha shutuma za makosa yao. Hupinga na kuanzisha ugomvi. Wanaume wengine huamua hata kuwapiga wake zao au kuwataliki.

Mwanamke alisema mahakamani; “Niliolewa miezi kumi na tano iliyopita na nikapata ujauzito miezi sita baadaye. Hivi karibuni, muda wa kujifungua ulipokaribia, mume wangu aliniambia kwamba nizae mtoto mwanaume. Lakini nilihisi kwamba ningezaa mapacha au hata watatu. Siku chache zilizopita nilijifungua mapacha wa kike. Nilifurahi sana kuhusu jambo hili, alitibuka na akaondoka hapo chumbani. Baadaye nilimuomba awapeleke watoto nyumbani, alinikaripia na kunilaumu kwa kuzaa mapacha wanawake. Akaniambia niondoke kwake, kwa hiyo nilikwenda kwa wazazi wangu na sasa ninaomba anipe talaka.”

Bibi… alimwambia mwandishi wa habari mahakamani: “Baada ya miaka ishirini na moja ya ndoa na kuzaa watoto watano, ninalazimika kuyaacha maisha ambayo nimeyapatia mchango mkubwa sana, kwa kumpisha mwanamke mwingine ambaye ameweza kuzaa mtoto mwanaume.

“Ninao watoto wanawake watano wazuri ambao ni wenye vipaji na ambao si tatizo kabisa kwa baba yao. Ni ipi hatia yangu kama siwezi kuzaa mtoto wa kiume. Mume wangu ananilaumu kwa kutokuzaa mtoto wa kiume na anataka mimi nimruhusu kuoa mwanamke mwingine.”

Kwa bahati mbaya, sifa hii imeendelezwa na watu wengine tangu enzi za Ujahiliya (kipindi cha ujinga) kwamba hutilia shaka maumbile ya binadamu ya jinsia ya kike. Huoni aibu kuzaa watoto wa kike na huhisi wamedhalilishwa.

Katika zama zaa ujinga, watu walikuwa na desturi ya kuzika watoto wa kike wakingali hai! Qurani Tukufu imesema kuhusu matendo yao ifuatavyo:


وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُمْ بِالْأُنْثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ


{58}

“Na mmoja wao akibashiriwa kwa msichana, uso wake unasawijika, naye kajaa chuki.” (Quran 16:58),

يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِنْ سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ


{59}


“Anajificha asionekane na watu kwa ubaya wa aliyo bashiriwa! Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama uovu wa wanavyohukumu!” (Quran 16:59).
Lakini Uislamu unapinga fikira hii isiyo sahihi na kuwaona wanawake na wanamume kuwa wapo sawa.

Mtume (s.a.w.) wa Uislamu alisema: “Miongoni mwa watoto wenu walio bora zaidi ni mabinti zenu.”

Mtume (s.a.w.w) wa Uislam pia alisema: “Ishara ya mwanamke mwenye bahati ni yule ambaye mwanaye wa kwanza ni mwanamke.”

Kwa nyongeza, Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alisema: “Yeyote ambaye anawalea watoto wanawake watatu au dada watatu, Pepo itakuwa ya kwake.”

Kama mtoto mwanamke angekuwa duni, Mwenyezi Mungu hangefanya ukoo wa Mtume (s.a.w.) uendelee kupitia kwa Hadhrat Fatima Zahra (a.s).

Bwana mpendwa! Unadai kwamba wewe ni mstaarabu na binadamu wa kisasa, kwa hiyo acha fikira za aina hiyo. Kuna tofauti gani wewe ukiwa na mtoto mwanamke au mwanamume. Wote hawa ni watoto wako na wote waweza kuelekea kwenye ubora. Mtoto mwanamke pia anaweza kuwa mtu mashuhuri kwa malezi yako sahihi ya elimu. Mtoto mwanamke ni bora zaidi ya mtoto mwanamume kwa kiasi fulani:

Kwanza, mtoto mwanamke ana huruma zaidi kwa wazazi wake anapokua na kujitegemea. Watoto wanawake, kama wazazi hawawapi upendeleo wowote zaidi ya watoto wao wanamume, wangekuwa na mapenzi zaidi kwao.

Pili, mtoto mwanamke mahitaji yake hayana gharama kubwa kama ya mtoto wa kiume, kwa sababu kwa kawaida hadumu muda mrefu nyumbani kwa wazazi wake, kwani huolewa mapema katika umri wake na huwaacha wazazi wake akiwa na vitu vichache tu vya kuanzia maisha yake mapya. lakini, wavulana huwa wa makamo ya vijana ambao huweza kuishi na wazazi wao kwa muda mrefu. Wazazi watalipa gharama ya elimu yake, wtamtafutia kazi, watalipa gharama zake wakati wa miaka miwili ya kutumikia jeshi, kama upo umuhimu, na halafu kumuoza mke, baada ya hapo angehitaji kupewa nyumba, mabusati, samani, na kadhalika. Angehitaji hata msaada wa fedha kutoka kwa wazazi wake baada ya kuoa.

Tatu, kama wazazi hawatafanya ubaguzi baina ya mtoto wao mwanaume na mwanamke, na kama watamtendea wema mkwilima wao, mkwilima wao mara nyingi huenda akawasaidia wao wakati wa matatizo na kwa kawaida huwa mwaminifu zaidi kwao kulinganisha na mtoto wao wa kiume.

Kwa vyovyote vile, hivi huwa ni kosa la mwanamke inapotokea anazaa mtoto mwanamke?

Mume na mke wote wanahusika katika tendo la kuzaa na mwanaume hana haki ya kumlaumu mke wake kwa jambo hili. Vinginevyo ni sawa kabisa mwanamke naye kumlaumu mume wake kuhusu jambo hili. Hata hivyo, hapana yeyote kati yao anaye laumiwa kwa jambo hilo kwani ni utashi wa Allah pekee wenye kuamua jinsia ya mtoto.

Wapo baadhi ya wataalamu ambao wanaamini kwamba jinsia ya mtoto inaweza kuamuliwa kutokana na jinsi mama anavyopata lishe yake wakati wa ujauzito wake. kwa hiyo, kama wapo watu wanaopendelea mtoto wao awe na jinsia wanayotaka wao, wanaona wataalamu na kwa hiyo watazuia hali ya kuwalaumu wake zao.

Mtu mwenye akili si lazima afadhaike kwa kupata mtoto mwanamke, lakini lazima afurahi sana. Anatakiwa kuonesha furaha yake, huba yake kwa mke wake na anatakiwa hata kumpa mke wake zawadi.

Angeweza kusherehekea kupatikana kiumbe kipya na hata kuchukua hatua za kimantiki katika kumridhisha mke wake kwamba mtoto mwanamke ni bora kama alivyo mtoto mwanaume, iwapo mke wake atakuwa amefadhaika kwa sababu ya kupata mtoto mwanamke.

Baba mwenye busara hawezi kubagua baina ya mtoto wake mwanaume na mwanamke, hangemlaani yeyote kwa kupata mtoto mwanamke na kwa hiyo angepambana na fikira za kipindi cha ujahiliya.

Mwanaume alisikia habari ya kuzaliwa mtoto wa kike wakati alipokuwa na Mtukufu Mtume wa Uislamu (s.a.w.w). taarifa hiyo ilimvuruga. Mtume

(s.a.w.w) alisema: “Kwa nini umefadhaika?” Alisema: ‘nilipokuwa ninatoka nje ya nyumba yangu, mke wangu alikuwa katika uchungu wa kujifungua, na sasa nimeletewa taarifa kwamba nimepata mtoto mwanamke.’ Mtume (s.a.w.w) alisema; “Ardhi inayo nafasi ya kumtosha yeye, na mbingu inampa hifadhi na Mwenyezi Mungu atampa riziki. Yeye ni ua lenye kutoa harufu nzuri ambamo kutoka humo utapata furaha kubwa.”

Ujauzito Na Kuzaliwa Mtoto

Muda wa kudumu ujauzito ni kipindi nyeti chenye matukio ya majaliwa kwa maisha ya mtoto. Tabia ya lishe ya mama pamoja na harakati za kimwili na za kisaikolojia ni mambo ya muhimu kwake na maisha ya kimbe kilichomo kwenye tumbo lake la uzazi.

Afya au maradhi ya mtoto, nguvu au udhaifu, ubaya wa sura au uzuri wa sura na tabia yake nzuri au mbaya na sehemu ya akili na busara, huanzishwa kwenye tumbo la uzazi la mama. Mmoja wapo wa wataalamu ameandika: “Wazazi wa watoto ama wanaweza kukua kwenye ngome ya afya au kwenye uharibifu wa maradhi. Ni wazi kwamba uharibifu wa maradhi si sehemu inayofaa kuishi roho ya milele au mwanadamu. Hii ni sababu ambayo kwamba wazazi wanaaminika kubeba wajibu mkubwa sana ikilinganishwa na uumbaji wote.”

Kwa hiyo, kipindi cha mimba hakiwezi kufikiriwa au kufanywa kama cha kawaida. Mara tu mimba inapoanza, wazazi hupewa wajibu mkubwa.

Wazazi wanaweza bila kufahamu kusababisha matatizo ya aina nyingi, yaliyo mengi baina yao yanaweza kuwa magumu sana kurekebishwa, kwa sababu ya uzembe mdogo wakati wanapofanya kazi zao.

Yafuatayo ni mambo ambayoyanayofaa kuangaliwa: Chakula: Kilengwa kilichomo kwenye tumbo la uzazi la mama yake, hula chakula na kukua kwa lishe ya damu yake. Kwa hiyo, chakula cha mama kinatakiwa kuwa na virutubishi vya kutosha ili viweze kumpa mtoto vitu vya asili anavyo vihitaji, pia kwa ajili ya ustawi wa mama. Kwa hiyo, upungufu wowote wa vitamini, protini, mafuta, sukari au wanga katika ulaji wa mama inaweza kusababisha madhara katika afya ya mtoto. Imam Sadiq (a.s) alisema: “Chakula cha kilengwa kinapatikana kwenye lishe anayopata mama.” 256.

Tatizo kubwa ambalo linawapata wanawake wengi sana wajawazito ama katika kipindi fulani cha ujauzito au kipindi kikubwa cha ujauzito, hupungukiwa na ladha ya lishe bora, kwani hupatwa tabia ya tamaa ya vyakula fulani huku akisikia kinyaa kwa vyakula vingine.

Kwa sababu kawaida hula chakula kidogo wakati wa kipindi hiki, lazima wahakikishe kwamba chakula chao si kizito na wakati huo huo kiwe na virutubisho vya kutosha ili kiweze kumpa mtoto vitu vya msingi.

Ufuatiliaji wa mpangilio ya chakula katika kipindi hiki cha ujauzito ni mgumu sana, hususan kwa watu wasio na uwezo wa kifedha na wale ambao hawana ujuzi wa ubora wa vyakula mbali mbali. Wajibu mkubwa anao baba ambaye anatakiwa kufanya jitihada kubwa kutoa vyakula vya msingi kwa mke wake. Kutokujali kwa upande wa baba kungeweza kusababisha madhara kwa mtoto anayekua, ambapo yeye ndiye atakaye wajibishwa hapa duniani na akhera.

Hali ya kiakili: Mama, wakati wa ujauzito anahitaji utulivu na anatakiwa apate hisia ya uzoefu wa kupenda maisha. Hii ina faida kwa mama na mtoto wake. Baba akiwa ni mwenye wajibu wa kumpa mke wake mazingira ya amani na uchangamfu, lazima ajaribu kwa bidii zaidi wakati wa kipindi cha ujauzito wake. Mume kwa wema na upendo, anatakiwa kuwa na mwenendo kwa namna ambayo mke wake anaweza kujivuna na kufurahi kuhusu yeye kuwa na ujauzito, lazima aone fahari kwamba maisha ya kiumbe kingine yanategemea kwake na kwamba anawajibu wa ustawi wake.

Mjamzito aache miondoko ya kushtua. Mwanamke mwenye mimba anatakiwa kuepuka shughuli nzito na anatakiwa kupumzika sana. Kunyanyua kitu kizito au miondoko ya haraka ya mwili inaweza kusababisha madhara yasiyo rekebika kwake, mtoto au wote. Wanawake wajawazito wanatakiwa kuepuka kazi ngumu na waume zao wanatakiwa kujitolea kufanya kazi kama hizo.

Woga wa uchungu wa Kujifungua. Kujifungua mtoto mara nyingi huwa si kazi nyepesi. Maumivu ya uchungu wa kujifungua wakati mwingine huwa makali sana.

Wanawake wajawazito mara nyingi huwa na wasi wasi kuhusu maumivu yaliyomo na uwezekani wa hatari yanayohusishwa na kujifungua mtoto, inayofuatiwa na kipindi cha kupata ahueni baada ya kujifungua. Ingawa wanawake wanatakiwa kustahamili ujauzito, uchungu wa kujifungua na kulisha watoto wao, wanamume pia wanatakiwa kugawana wajibu wa kulea watoto wao.

Ingawa kiinitete kinatungwa kwenye tumbo la uzazi la mwanamke pia yupo baba wa mtoto ambaye amefanya kazi muhimu katika kutungwa mimba. Kwa hiyo, wanamume wanatakiwa kuhakikisha kwamba wake zao wanapata maliwazo wakati wa kujifungua na kuwa tayari kusaidia endapo chochote kitahitajika haraka.

Ni kazi ya kibinadamu na kiislamu kwa wanaume kufanya kila wawezalo kwa wake zao wajawazito kwa kuwapa matunzo ya kitabibu na mahitaji ya kurahisisha kujifungua. Mwanaume anatakiwa kuwa na mke wake baada ya kuzaliwa kwa mtoto, lakini kama hawezi kufanya hivyo anatakiwa ampigie simu au amtumie ndugu zake wakae naye. Anatakiwa kujaribu kumrudisha nyumbani yeye mwenyewe na amsaidie kufanya kazi za nyumbani ili mke wake apate mapumziko ya kutosha na kurudisha tena nguvu iliyopotea. mwanaume anaye mfanyia mke wake wema, atazawadiwa na Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.w) alisema: “Mwanaume aliye mbora sana miongoni mwenu ni yule anayemfanyia mke wake wema.

Na mimi miongoni mwenu ni mwanaume mbora sana kuhusu kuwafanyia wema wake zangu.”

Imamu Sadiq (a.s) alisema: “Mwenyezi Mungu na amrehemu mwanaume ambaye kufanya uhusiano mzuri na mke wake, kwa sababu Mwenyezi Mungu anamteua mwanaume kuwa mlezi wa mke wake.”

Mwanaume anaye mtendea mke wake wema, atafanya mazingira ya familia yake kuwa machangamfu na ataimarisha misingi yake. Mke wake, kwa upande wake, kamwe hatasahau mapenzi ya mume wake na huba yake. Matokeo yake mshikamano wa ndoa unakuwa imara zaidi.

Msaada wa kuwalea watoto

Mtoto ni tunda la ndoa. Wote wawili wanamume na wanawake wametoa mchango katika kupatikana kwa mtoto na lazima wagawane matatizo na starehe zinazohusishwa kuwapo kwake. Kumlea mtoto ni kazi ya wazazi wote na si mama peke yake. Ingawa mara nyingi zaidi ni mama ndio wanaolea watoto wao na kuwalisha kuwaweka katika hali ya usafi na kadhalika, baba wasidharau juhudi hizo. Sio sahihi kwa mwanaume kudhani kwamba kazi ya kutunza watoto ni ya wanawake tu na kwamba wanaume hawana wajibu katika jambo hili. Si haki kwamba baba aondoke na kumwacha mke wake na mtoto ambaye analia na aende kupumzika kwenye chumba kingine.

Mpendwa ndugu! Mtoto wako ni wajibu wako pia. Unadhani ni haki kumwacha mkeo na mtoto anayelia ambapo wewe unapumzika kwenye chumba kingine? Hii ni njia inayofaa kufanya mambo nyumbani mwako? Kama vile unavyofanya bidii nje ya nyumba, mkeo hufanya bidii ndani ya nyumba; na anahitaji usingizi kama vile unavyohitaji usingizi. Yeye pia hafurahii kilio cha mtoto, lakini huvumilia.

Ndugu yangu! Ubinadamu halikadhalika na Uislamu unakutaka wewe umsaidie mkeo katika kumlea mtoto wenu. Ama mnatakiwa msaidiane kwa pamoja au mpeane zamu. Kama mkeo anakosa usingizi kwa usiku wote na analala baada ya sala ya alfajiri, halafu usitegemee kwamba atakutayarishia staftahi kama siku zingine. Kwa kweli unatakiwa wewe mwenyewe utayarishe staftahi yako na ya mkeo ili pindi akiamka akute kila kitu tayari mezani. Mke wako hawajibiki kumlea mtoto wenu wakati wote unapokuwa haupo nyumbani au upo safarini. Kwa ufupi unatakiwa umsaidiea mkeo na mgawane wajibu wa kulea mtoto. Kwa njia hii, maisha ya familia yenu yataimarishwa.

Mwisho wanawake lazima pia wakumbuke kwamba waume zao hufanya bidii kupata riziki ya familia na wasitegemee kwamba wanaweza kuwadai zaidi ya uwezo wao. Wanawake wasitegemee waume zao ambao wamechoka kuanza kuwasaidia kulea watoto mara wanaporudi kutoka kazini.

Kikwazo Kikubwa Katika Kusuluhisha Tofauti

Kikwazo kikubwa sana katika kusuluhisha ugomvi wa kifamilia ni ubinafsi na kiburi. Kwa bahati mbaya, watu wengi huathiriwa na tabia hizi. Watu kama hawa hupungukiwa na sehemu fulani ya akili ambapo hukubali tabia zao tu na kukataa za wengine na hawataki kukubali makosa yao. Hususan ni hatari sana ambapo ghasia ya tabia inafanikishwa na mtu mwingine yaani, kuwakosoa wengine kwa makosa yao. Wakati mwingine mume na mke wote husumbuliwa na tatizo hili kwa maana hiyo, watagombana kila siku. Kila mmoja atamlaumu mwenzake na wakati huo huo kila mmoja wao atakataa kuhusika kabisa na makosa yote.

Wakati mwingine kama upande moja tu utaumia kutokana na dosari hii ya kukoseana, kila mmoja atamwona mwenzake analo kosa na kwa kufanya hivyo watakuwa wanajikomboa kabisa kutokana na kulaumiana.

Pale ambapo mume na mke wote wanakumbwa na usumbufu wa vurugu hii, ni vigumu sana kuwasuluhisha, kwa sababu hawatakuwa tayari kuzingatia ushauri wa mtu yeyote. Wakati ambapo kila mmojawao anasikiliza redio au anaangalia vipindi vya runinga vinavyohusu mambo ya familia, wataona dosari fulani ya tabia ambayo inaendekezwa na mwenza wake na kwa hiyo ataanzisha lawama zake hapo hapo. Lakini dosari yoyote ikizungumziwa inayogusa udhaifu wao watajifanya hawasikii na wataelekeza fikira zao kwenye mambo mengine. Wanaweza kununua kitabu kinachohusu maadili ya familia na kumpa mwenza wake, bila wao kuwa na hisia zozote za kuwa na hamu ya kusoma yaliyomo humo.

Ubinafsi unaweza kuwa mkali sana hivyo kwamba muathirika hataweza hata kutambua tatizo hilo. Katika hali kama hiyo, uhusiano baina ya wanandoa unaharibika na hata usiwezekane kuendelea. Matokeo yake ni, ama maisha yataendelea katika hali ya ugomvi, huzuni, kutokuwa na furaha au hata kutalikiana.

Kwa hiyo, inashauriwa kwamba wanandoa wote waache tabia ya ubinafsi na kiburi. Wanandoa ambao wanatatizwa na hali hii, wanatakiwa wapate muda wakae pamoja, na wawe kama majaji wawili waaminifu wazungumzie matatizo yao. Kila mmoja amsikilize mwenzake kwa umakini na bila upendeleo wowote. Kila mmoja wao anatakiwa kufahamu dosari zake bila kusahau hata iliyo ndogo sana pamoja na nia ya kuzirekebisha. Halafu wote wawili wanatakiwa waamue kujisahihisha wao wenyewe; lakini ni hapo tu ambapo wanahisi umuhimu wa uelewano wa kina na ambapo wote wanatamaani kufufua mapenzi yao na utulivu ambao ulikuwapo baina yao.

Hata hivyo, inapokuwa hakuna uwezekano wa kupatikana suluhu, wanandoa wanatakiwa kuwasilisha matatizo yao kwa mtu mwenye uzoefu, mwaminifu, mtambuzi wa kutegemewa na mwema. Kama mtu kama huyo ni rafiki au ndugu, hiyo itakuwa nafuu yao kwa sababu wanaweza kumwambia kila kitu na kungoja hukumu yao. Lazima wamsikilize na kuupokea ushauri wake na kutia nia ya kuutekeleza kwa vitendo.

Kama ilivyo, kuamini ushauri wa jaji si rahisi, lakini mtu ambaye anajali familia yake na uimara wake, amani kudumu kwake anatakiwa kuvumilia na baadaye afurahie matokeo yake yenye manufaa.

Wazazi wa wanandoa wa aina hiyo, kama wanatambua matatizo ya kifamilia ya watoto wao, wanatakiwa kuwashauri wamuone Kadhi mwenye uzoefu, mwaminifu na nia njema. Wazazi hawatakiwi kuonesha upendeleo kwa mume au mke., Kwa njia hii, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, matatizo yao yanaweza kutatuliwa.

Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qurani Tukufu:


وَإِنْ خِفْتُمْ شِقَاقَ بَيْنِهِمَا فَابْعَثُوا حَكَمًا مِنْ أَهْلِهِ وَحَكَمًا مِنْ أَهْلِهَا إِنْ يُرِيدَا إِصْلَاحًا يُوَفِّقِ اللَّهُ بَيْنَهُمَا ۗ إِنَّ اللَّهَ كَانَعَلِيمًا خَبِيرًا


{35}

“Na mkichelea kutakuwepo mfarakano baina ya mume na mke basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke, wakitaka mapatano mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye Khabari.”(Quran 4:35)

Talaka

Licha ya kwamba talaka ni kitendo halali, ni kitendo kinacho chukiza na ni kibaya kuzidi vitendo vyote.

Imam Sadiq (a.s) alisema: “Oeni lakini msitalikiane, kwa sababu talaka inaweza kutetemesha Arsh ya Mwenyezi Mungu.”

Imam Sadiq (a.s) pia alisema: “Mwenyezi Mungu huipenda nyumba ambayo inakaliwa na wanandoa na huchukia nyumba ambayo wanandoa wametalikiana. Hakuna kitendo kinacho mchukiza Mwenyezi Mungu kuliko kutalikiana.”

Ndoa si kama kununua jozi ya viatu au soksi ambapo vitu hivi vikichujuka kwenye matamanio ya mmiliki wake, huvitupa na kununua jozi nyingine ya viatu. Ndoa ni makubaliano ya kiroho ambayo hufanywa na watu wawili kwa lengo la kuishi pamoja kama marafiki wa kuliwazana, na wapenzi hadi kifo chao. Makubaliano haya yameegemezwa kwenye matumaini haya hivyo kwamba msichana huwaacha wazazi wake na kuungana na mume wake.

Mwanaume hufanya jitihada na kufanya bidii kwa msingi wa makubaliano hayo ya kimungu. Hulipa gharama za harusi yake na hununua vitu muhimu kwa ajili ya maisha yake mapya na hufanya kazi kwa ajili ya faraja ya familia yake.

Ndoa si jambo la kukata kiu cha tamaa ya kimwili na wanandoa hawawezi kuiharibu kwa visingizio vidogo. Licha ya kwamba kutalikiana ni tendo halali, linachukiza sana na watu wanashauriwa kuepukana nalo kadiri iwezekanavyo.

Bahati mbaya, tendo hili ambalo linachukiza sana, limekuwa jambo la kawaida sana kwenye nchi za kiislamu na misingi ya familia imetikisika sana, hivyo kwamba kwa ujumla watu hawana imani tena kuhusu ndoa.

Kuvunja ndoa inaruhusiwa hapo tu ambapo hali si ya kawaida na inalazimu iwe hivyo.

Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alisema: “Malaika Jibril aliniusia kuhusu wanawake sana hivyo kwamba nilifikiri kwamba wanamume wasiwataliki isipokuwa kama wanazini.”

Kesi nyingi za kutalikiana hazina sababu za msingi, isipokuwa visingizio visivyo komaa. Yaani, sababu za kesi nyingi zaidi za talaka ni hafifu na hazifai kuwaathiri na kuwatenganisha wanandoa. Mume au mke, kwa sababu ya ubinafsi, anaweza kukuza jambo dogo na kuamua kwamba maisha yao ya ndoa lazima yakome.

“Bibi fulani mwenye umri wa miaka ishirini na nne, alimwambia mumewe awaalike wazazi wake kwenye chakula cha jioni chenye gharama kubwa. Kwa kuwa hakutekelezewa ombi hilo, alidai talaka.”

“Mwanaume alimtaliki mke wake kwa sababu alikuwa anazaa watoto wanawake tu. Wanandoa hawa walikuwa na watoto wanawake watano.”

“Mwanamke aliomba talaka kwa sababu mume wake aliamini mafundisho ya kumfikiri Mungu kwa njia ya tafakuri na hakuonesha kupenda maisha.”

“Mwanamume alidai talaka kwa sababu alitaka kumuoa mwanamke tajiri.”

“Mwanamke aliomba talaka kwa sababu mume wake alikuwa na tabia ya kuficha fedha zake kwenye mikono ya shati.”

“Mwanaume alimtaliki mke wake kwa madai kwamba ana balaa tangu walipooana baba wa mume alifariki na ami yake alifilisika.”

Wanandoa ambao hawana heshima na busara, wanaweza wakanasa kwenye mtego wa mambo madogo kama hayo na kudai talaka.

Wanandoa wanaotaka kutengana, wasifanye haraka kutelekeza jambo hilo. Wanashauriwa wafikiri kwa uangalifu kuhusu athari na maisha yao ya baadaye kwa makini na halafu waamuwe. Hususan lazima watafakari kuhusu mambo mawili:

Jambo la kwanza: wanandoa wanaotaka kutalikiana kwa kawaida hutaka kuoa au kuolewa tena. Lakini lazima wakumbuke kwamba baada ya kutalikiana, watu wanaojulikana kama watalaka hawatakuwa na sifa nzuri kuhusu ndoa. Watu huwafikiria kuwa wenye ubinafsi na si waaminifu.

Baada ya kupata taarifa ya maisha ya ndoa ya siku za nyuma ya mwanamume na kutaliki, mwanamke anaweza kuwa na shaka kuhusu uaminifu wa mwanaume au tabia yake.

Mwanamke mtalaka ni nadra sana kupata fursa ya kuolewa tena. Kwa sababu wanaume kwa kawaida hawaoneshi kuvutiwa sana kuoa mwanamke mtalaka na hutilia shaka kuhusu uaminifu wake.

Kwa hiyo, mtalaka anawezekana akaishi peke yake kwa muda wote wa maisha yake na atateswa na upweke pia.

Kuwa mpweke ni hali ngumu sana na watu wengine wapweke hupendelea zaidi kifo kuliko maisha ya aina hiyo yasiyovumilika.

Mwanamke wa miaka ishirini na mbili ambaye aliachika, alijaribu kujiua mnamo usiku wa siku ya harusi ya dada yake. Alikuwa na mtoto mmoja.

Hata kama mwanaume anafaulu kuoa tena, haitajulikana kabisa kwamba maisha yake mapya yatakuwa mazuri zaidi kuliko ya mke wake wa mwanzo. Mke wake wa pili anaweza kuwa mbaya zaidi. Mwanaume wa aina hii hupendelea kumtaliki mke wa ndoa ya pili na kurudi kumuoa mke wa kwanza. Lakini kwa kawaida huwa wamechelewa sana.

Mwanaume wa miaka themanini alisema mahakamani; “Nilikuwa na maisha mazuri nilipomuoa mke wangu wa ndoa ya kwanza, takriban miaka sitini iliyopita. Lakini baada ya muda alianza kunifanyia ubaya kwa hiyo nikamtaliki. Nilioa wanawake wachache baada ya hapo lakini nilihisi kwamba mke wangu wa kwanza alikuwa mwaminifu zaidi miongoni mwao. Nilimuona na nikampa rai ya kurudiana naye. Yeye, ambaye pia alichoka maisha ya upweke alikubali na sasa tunataka kuoana tena.”

Mwanaume alimtaliki mke wake wa pili kwa sababu hakutaka kuwalea watoto wawili aliozaa kwenye ndoa yake ya kwanza. Halafu akaamua kumuoa tena mke wake wa kwanza ambaye alimtaliki miaka mitano ya nyuma.’ Jambo la pili: Wanandoa ambao wanataka kutengana lazima wafikirie pia suala la watoto wao. Faraja ya watoto imo kwenye familia yenye wazazi wote wanao ishi pamoja na wanawalea kwa pamoja.

Baada ya kuvunjika kwa maisha ya familia, watoto hufadhaika sana. Kama ni baba yao tu anaye watunza, hawatakuwa na maisha na mama yao wa kambo. Mama wa kambo si tu kwamba wanashindwa kutekeleza kama mama halisi, lakini wanaweza kufikiri watoto wa kambo ni mzigo. Mama wa kambo wengine huwanyanyasa watoto wa kambo na kuwafadhaisha kwa kukusudia na baba zao hunyamaza kimya.

Bibi harusi wa miaka kumi na nne ambaye alitaka kujiua alisema akiwa hospitalini. Wazazi wangu walitengana nilipokuwa na mwaka mmoja.

Baba yangu alioa tena baada ya mwaka mmoja na nusu na sasa tunaishi wote. Mama yangu wa kambo alikuwa na desturi ya kunipiga na hata alinichoma moto kwa chuma mara kadhaa. Baba yangu licha ya kuwa na uwezo wa kifedha alinikataza nisisome. Takriban mwezi mmoja uliopita baba yangu alinioza kwa mtu mwenye umri wa miaka arobaini na tano.

Msichana wa miaka kumi na tatu alijinyonga. Msichana huyu aliishi na kaka zake wawili. Mmojawapo wa hao kaka zake alisema; “Wazazi wetu walitengana miaka takriban mitatu iliyopita. Mama yangu aliolewa tena na mwanamume mwingine na baba alikufa miezi miwili iliyopita. Ilikuwa saa 12:30 jana jioni nilikuja nyumbani nikamkuta dada yangu amejinyonga.”

Pia, kama mama anachukua wajibu wa watoto wake, basi watakosa baba halisi ambaye angewatunza. baba wa kambo mara nyingi ndiye sababu ya kukosekana furaha kwa watoto wake wa kambo.

Mwanamke alimsaidia mume wake wa ndoa ya pili kumfunga mtoto wa kambo mwenye umri wa miaka nane kwenye kitanda. Halafu wakafunga mlango na wakaondoka kwenda matembezini. Waliporudi nyumbani,walikuta mtoto wao ameungua moto hadi kufa kwa sababu ya moto uliounguza nyumba.

Talaka huharibu familia na huwaacha watoto wanatangatanga hawana hifadhi. Watoto mara nyingi huteseka kwa sababu ya ubinafsi wa wazazi wao.

Watoto wanne wenye umri wa miaka kumi na mbili, tisa, sita na minne walikwenda kwenye kituo cha polisi. Mtoto mwanamme mwenye umri mkubwa zaidi alisema: “Wazazi wetu walitengana muda fulani uliopita. Wakati wote walikuwa wanabishana na walikuwa na tabia ya kugombana kila siku mchana na usiku. Sasa wametalikina, hapana mmojawao ambaye yupo tayari kutulea sisi.”

Watoto ambao hawana mlezi anayefaa na mazingira ya familia, mara nyingi hukengeuka. Kutokupata elimu ya kutosha na mtu mwenye huruma katika maisha yao, huwafanya wasumbuliwe na hisia za udhalili. Wanaweza hata kufanya uhalifu wa viwango mbali mbali, wakati wa utoto au utu uzima.

Mtu anaweza kutambua jambo hili na kusoma matukio kwenye magazeti kila siku.

Kwenye utafiti uliofanywa kwenye kituo cha kurekebisha vijana, ni wazi kwamba katika vijana wahalifu mia moja kumi na sita wa kituo hiki, watu themanini walithibitisha kwamba mama zao wa kambo waliwanyanyasa ndio sababu wakafanya uhalifu.”

Mpendwa bibi na bwana! Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya watoto wako wasio na kosa, kuweni wasamehevu nyinyi kwa nyinyi wanandoa. Msikuze matatizo madogo na msipende kung’ang’ania ubishi. Msitafutane makosa nyinyi kwa nyinyi. Fikirieni mambo yenu ya siku zijazo na watoto wenu.

Kumbukeni watoto wenu wanawategemeeni nyinyi na wanatumaini kupata furaha yao kutoka kwenu. Wahurumieni na msiharibu maisha yao.

Kama mkidharau matamanio yao ya ndani na kama mkivunja nyoyo zao ndogo, hamtaweza kuepuka athari ya masikitiko yao. Kwa hiyo, hamtaweza kuwa na maisha yenye faraja pamoja.