read

Athari Mbaya za Hasira na Tabia Mbaya.

1003. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 302:

“Hasira inaiharibu imani kama vile siki (huwa chachu) inavyoharibu asali.”

1004. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 303:

“Ghadhabu ni ufunguo wa kila aina ya shari.”

1005. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amenakili kutoka kwa mzazi wake a.s. ambaye amenakili kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ambaye Amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 27:

“Mtu mmoja alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ili afundishwe tendo ambalo litaondoa kizuizi baina yake na Jannah.

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia:
Usiwe mkali;
usiwaombe watu vitu,
watakie watu kile ujitakiacho wewe mwenyewe.”

1006. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2, Uk. 303:

“Yeyote yule anayezuia ghadhabu zake, basi Allah swt atazificha siri zake.”

1007. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Al-Kafi, J. 2, Uk. 303:

“Ghadhabu ni kitu kinacho teketeza moyo wa mwenye hekima; kwani yeyote yule asiyeweza kudhibiti vyema ghadhabu yake basi kamwe hawezi kuitumia busara yake.”