read

Azma ya Mwanamme Katika Ndoa.

847. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, At-Tahdhib, J. 7, Uk. 399:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa urembo wake tu (bila ya kujali imani yake), basi yeye hataambulia kile alichokitaka; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya mali na utajiri wake (basi Allah swt atampa hiyo mali na utajiri tu peke yake.) Kwa hivyo ni juu yenu nyie kutafuta mwanamke aliye katika dini na mcha Allah swt.”

848. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi J. 5, Uk. 333:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa matarajio ya utajiri, basi Allah swt anampa utajiri na mali peke yake.”

849. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, At-Tahdhib, J. 7, Uk. 399:

“Yeyote anayeoa mwanamka kwa utajiri wake, Allah swt humwachia hayo tu; na yeyote anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake na uzuri wake, basi yeye atayaona yale ndani ya mwanamke yale asiyoyapenda; lakini yule anayeoa mwanamke kwa misingi ya imani na dini yake, basi Allah swt atamjazia kila aina ya sifa ya mambo hayo kwa ajili yake.”

850. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Wasa'il ush-Shi'ah, J. 20, Uk. 53:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya urembo wake tu, basi Allah swt atamjaalia uzuri wake na uzuri wa mwanamke huyo utamdhuru na kumletea matatizo huyo mwanamme.”

851. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin a.s., Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 385:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke kwa ajili ya ridhaa ya Allah swt, na kuungana naye kwa wema basi Allah swt atamjaalia taji la heshima na ufanisi.”

852. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al-Muhajjat-ul-Baidha, J. 3, Uk. 85:

“Msioe wanawake kwa ajili ya urembo wao tu kwa sababu urembo wao unaweza kusababisha wasiwe wacha Allah swt wala si kwa ajili ya mali yao kwa sababu mali yao inaweza ikawasababisha wakose utiifu; lakini muwaoe kwa misingi ya imani ya dini yao.”