read

Biashara na Uhusiano wa Kijamii.

919. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Amesema Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 89:

“Iwapo mtu atanunua bidhaa katika vyakula ambavyo ni muhimu katika jamii na akakificha kwa siku arobaini kwa matumaini kuwa bei yake itapanda miongoni mwa Waislam, na kama atafanikiwa kukiuza kwa bei ya juu hicho chakula basi kama fedha zote atazigawa katika sadaka kwa na wenye kuhitaji misaada maskini, basi hiyo haitapunguza adhabu yoyote mbele ya Allah swt kwa kile alicho kitenda (kuhujumu uchumi).”

920. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 93:

“Yeyote yule anayefanya biashara bila ya kuzingatia sheria na kanuni za Islam, basi kwa hakika ataingia katika riba, (bila ya yeye mwenyewe kujijua).”

921. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ananakili kutoka Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa Amesema, Khisal-i-Sadduq, J. 1, Uk. 286:

“Yeyote yule aliye katika biashara na anayenunua na kuuza vitu lazima ajiepushe mambo matano, ama sivyo asinunue wala asiuze kitu chochote:
1. Riba,

2. Kula kiapo,

3. Kuficha ubaya na kasoro za mali,

4. Kusifu kitu kama hakistahili hivyo wakati wa kuuza; na

5. kutafuta kasoro au ubaya wakati wa kununua.1

922. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Amesema, Al-Kafi, J. 5, Uk. 78:

“Yeyote yule anayetafuta riziki humu duniani ili aondokane na shida za kutegemea watu katika mahitaji yake, na ili kuwalisha na kuwasaidia wananyumba wake, na kueneza mapenzi yake kwa majirani zake basi atakutana na Allah swt siku ya Qiyamah huku uso wake ukiwa uking’ara kama mwezi.”

  • 1. Tunaona mara nyingi sisi katika biashara tunaapa kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu hiki kitu bwana hivi…………. tunaapa uongo na ukweli ‘mimi naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu fulani alinunua angalia wakati yeye hakununua kwako. Na mara nyingi tunajua hiki kitu ni kibaya lakini tunamwambia mtu uongo ili anunue kwa hiyo ndiyo uongo huo umeharamishwa katika Uislam na hata kitu kibaya sisi tutakisifu kweli kiasi kwamba mnunuzi anaweza kutuamini akanunua

    Lakini tunapotaka kununua sisi tunaanza kutafuta kasoro aah kitu hiki hivi na kitu hiki vile Wallahi nakuapia Mungu niliwahi kutumia kitu hiki ikawa hivi kumbe hayo yote ni uongo kwa sababu tunataka yule mtu mwisho atuuzie kwa bei iliyo ya chini kabisa.

    Allah swt swala kama hili pia amelikemea katika Qur'an Tukufu Sura Mutaffifina anasema ole wao wale watu wanapopimiwa vitu wanataka wapimiwe kamili ukinunua kilo moja ya sukari upate kilo moja kamili lakini unapouza unataka uuze ikiwa kasoro upunguze hata gram kidogo lakini uuze kitu ambacho kiko kasoro, kwa watu kama hawa kwa hakika wanalaaniwa.