read

Dini na Kusomea Mambo Yake.

991. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 1, Uk. 176:

“Ole wake yule Mwislam ambaye habakizi siku moja katika juma zima kwa ajili ya kujifunza masuala ya dini yake na wala kujaribu kufanya uchunguzi na utafiti wa dini yake.”

992. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Muhajjat-ul-Baidha, J. 1, Uk. 15:

“Yeyote yule anayesomea dini ya Allah swt, basi kwa hakika ana uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yake na kumpatia yeye riziki kutokea mahala ambapo yeye alikuwa hata hajaweza kuwazia.”

993. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Bihar al-Anwaar, J. 1, Uk. 214:

“(Vijana wa Kish’ia lazima wawe na program au utaratibu wa kujifunza masuala ya dini). Mimi ninapomwona kijana wa Kishi’a ambaye hana program au utaratibu kama huu basi mimi nitamfundisha somo.”

994. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 2, Uk. 29:

“Wajulishe wafuasi wetu kuwa kwa hakika bila shaka wao watakuwa miongoni mwa wale watakao okoka siku ya Qiyamah kwa masharti iwapo wao watakuwa watimizaji wa yale wanayo amrishwa.”

995. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 2, Uk. 153:

“Yeyote yule kutokea Ummah wangu atakaye hifadhi (kariri) hadithi arobaini ambazo zinahitajiwa na watu katika maisha yao ya kidini (kwa ajili ya Tabligh na muongozo), basi Allah swt atamwinua akiwa mwenye hekima kutoka waliokufa Siku ya Qiyamah.”