read

Fadhail za Imam Ali a.s.

1460. Kutokea ‘Ala, amesema yeye: “Mimi nilimwuliza ‘Aysha kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib. Mimi nilimwuliza Mtume s.a.w.w. kuhusu yeye. ‘Ayesha alijibu, naye akasema kuwa ‘Ali ni mtu bora kabisa katika Wanadamu, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa ni mpagani tu.

1461. Na kutoka ‘Ali ibn Abi Talib a.s., kasema: “Aliniambia Mtume Muhammad s.a.w.w. ‘Wewe ni bora wa viumbe vya Allah swt, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa atakuwa ni kafiri’

1462. Na kutoka kwa Hudhaifa: “Alisema Mtume Muhammad s.a.w.w. kuwa ‘ ‘Ali ni bora wa Wanaadamu. Yeyote yule anayekataa haya kwa hakika ni kafiri.’

1463. Kutokea kwa Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: “Alisema Mtume Muhammad s.a.w.w. , ‘uadui, chuki na bughudha dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib ni ukafiri na uadui dhidi ya Bani Hashim ni unafiki.’”

1464. Na kutokea kwake, kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w. akasema: “Hakuna ampendaye ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa ni mumiin halisi, na hakuna amchukiaye ‘Ali isipokuwa ni kafiri.”

1465. Na kutokea Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. , alisema: “Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. kuwa yeyote yule atakaye msema vibaya ‘Ali ibn Abi Talib, basi ajue kuwa amenisema mimi vibaya hivyo, na yeyote yule anisemaye mimi vibaya, basi amemsema hivyo Allah swt (na hilo ni dhambi kuu ).”

1466. Amesema Al-Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “Kwa hakika Allah swt alitazama kuelekea dunia hii na akanichagua mimi kutoka watu wa dunia; na kwa mara nyingine tena aliangalia duniani na kukuchagua wewe kutoka watu wa dunia; na kwa mara ya tatu alipoangalia akawachagua Maimamu a.s. kutokea vizazi vyako miongoni mwa watu wote wa dunia hii; na kwa mara ya nne alipoangalia akamchagua binti yangu Fatimah kutokea wanawake wote wa dunia hii.”

1467. Kutokea Ja’abir, anasema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “Ali ibn Abi Talib a.s. ni bora miongoni mwa watu wa dunia. Yeyote yule aliye na shaka, basi ni kafiri.”

1468. Amesema Ibn ‘Abbas kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “ ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni mlango wa Hitta 1 Yeyote yule atakayeingia ndani mwake basi kwa hakika ndiye mumiin wa kweli, na yeyote atakayetoka kutoka humo ni kafiri.”

1469. Al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. kutokea baba yake amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. aliulizwa kuhusu hali ya watu, naye akajibu “ bora kabisa na Mcha Mungu halisi na ambaye aliye karibu kabisa nao ambaye yuko karibu nami ni Ali ibn Abi Talib a.s. , na hakuna Mcha-Mungu halisi miongoni mwenu, na ambaye yupo karibu nami kuliko Ali ibn Abi Talib a.s.”

1470. Jami’ bin ‘Omair, alisema kuwa yeye alimwuliza ‘Ayesha kuhusu daraja la ‘Ali ibn Abi Talib a.s. mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. ? Yeye alijibu: “ Kwa hakika ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w.”

Yeye alimwuliza tena kuhusu nafasi ya Ali ibn Abi Talib a.s. katika macho ya Mtume Muhammad s.a.w.w. . Alijibiwa kuwa “Ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. .”

1471. Na kutokea Ibn ‘Umar amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Bora wa mtu miongoni mwenu ni ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na bora wa vijana wenu ni Al - Hassan na Al -Husayn

1472. ‘Urwah anaripoti kutoka ‘Ayesha kuwa: Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. “Kwa hakika nimeahidiwa na Allah swt kuwa yeyote yule atakayeinuka dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi kwa hakika ni kafiri na kwa hakika ataingia Jahannam aunguzwe na moto. ‘Aisha akasema kuwa “Mimi niliisahau hadith hii siku ya(vita vya) Jamal, hadi hapo nilipoikumbuka au nilipokumbushwa tukiwa Basra (Iraq), nami namwomba Allah swt anisamehe, na sitegemei kuwa miongoni mwao.”

1473. Abu Salim bin Abu al-Jaada amesema kuwa yeye alimwomba Ja’abir azungumze chochote kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. Ja’abir kasema: “’Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa bora miongoni mwa wanadamu.” Mimi nilimwuliza tena “Je unasemaje kuhusu mtu atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s.” Yeye alinijibu: “Hakuna atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa kafiri.”

1474. Hashim bin Barid alisema kuwa ‘Abdullah ibn Mas’ud alisema : “Mimi nilijifunza Sura 70 za Qur’an Tukufu kutokea kinywani mwa Mtume Muhammad s.a.w.w. na Surah za Qur’an zilizobakia nilijifunza kutokea mbora wa Ummah wetu yaani Ali ibn Abi Talib a.s.”

1475. Muhammad bin Salim al-Bazzar anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Said bin al-Musayyib katika Masjid-i-Nabi, siku ya Ijumaa, ndipo alipotokezea mhubiri kutoka kabila la Banu Omayyah (laana za Allah swt ziwafikie juu yao) na akapanda juu ya mimbar na akaanza kumtusi Ali ibn Abi Talib a.s. kwa kusema: “Kwa hakika, Allah swt hakumtukuza Ali ibn Abi Talib a.s. kwa mapenzi yake badala yake amefanya hivyo kwa kuhofu uchochezi wake.” Kwa hayo Said bin Al-Musayyib alimlaani na kumwambia: “Kwa hakika wewe unasema uongo mtupu” 2 Na hapo alimtupia nguo aliyokuwa akijifunika juu ya mdomo wa mhubiri huyo. Hapo watu walipomwambia kuwa itakuwaje iwapo Abu Muhammad wakati Imam huyo anatokana na Banu Omayyah ? Hapo Said alijibu: “Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi sijui nilichokisema, lakini mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema haya kutokea makbara haya nami ndipo nilipoyarudia kuyasema.”

1476. Ummi Hani binti Abu Talib a.s. kasema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. kasema kuwa: “Bora wa viumbe vya Allah swt katika mtazamo wake Allah swt, ni yule anayelala kaburini mwake na kamwe hakumshuku 'Ali ibn Abi Talib a.s. na kizazi chake ni bora wa vizazi katika viumbe vyote.”

1477. Ja’abir anasema kuwa “Hakuna anayeshuku fadhail za ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa ni kafiri na kasema kuwa “Kwa kiapo cha Allah swt sisi kamwe tulikuwa hatuwajui wanafiki, katika zama za Mtume Muhammad s.a.w.w. isipokuwa kwa yule mwenye chuki dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”

1478. Said bin Ja’abir alisema kuwa yeye alikuwa akimwongoza Ibn ‘Abbas baada ya yeye kupoteza nuru ya macho yake, kutokea Msikitini, na aliwapita kundi la watu waliokuwa wakimtukana ‘Ali ibn Abi Talib a.s. na aliniambia kuwa nimchukue hapo.

Hivyo mimi nilimfikisha kwao. Kufika hapo alisema “Ni nani miongoni mwenu anayemkashifu Allah swt?! Kwa hakika yeyote yule anayemkashifu Allah swt amekuwa kafiri. Na ni yupi yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ? Na kwa hakika hili limetokea” Ndipo alipoendelea kusema: “Nashuhudia Allah swt, kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema ‘Yeyote yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi amenikashifu mimi na kwa hakika anayenikashifu mimi basi ajue kuwa amemkashifu Allah swt na yule anayemkashifu Allah swt, Mtume wake basi watatakiwa kutoa maelezo yake.” Na hapo ndipo Ibn ‘Abbas aligeuka.

1479. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. : “Muzirembeshe vikao vyenu kwa mazungumzo na makumbusho ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s. kwa dhikr ya ni dhikr zangu na dhikr zangu ndizo dhikr za Allah swt na dhikr za Allah swt ni ‘ibadah. Na mwenye kufanya ‘ibadah huingia Peponi.”

  • 1. Rejea al-Qur’an Sura 2 : 55 na 7 : 161
  • 2. Rejea Al-Qur’an Sura 18 : 35