read

Haki za Watoto.

797. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 31, Uk. 290:

“Ewe Ali ! Allah swt huwalaani wazazi wale wanao wafanya watoto wao wasiwe watiifu kwao kwa sababu ya kuwalaani kwao.”

798. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia mmoja ya wafuasi wake, Nahjul Balagha Uk. 536, Msemo, No. 352:

“Usiupitishe wakati wakati wako mwingi pamoja na mke wako na watoto wako waliokuwa wakubwa, kwa sababu kama mke wako na watoto wako ni wampendao Allah swt, basi Allah swt hatawaacha wapenzi wake bila ya kuwajali, iwapo watakuwa ni maadui wa Allah swt, basi kwa nini wewe uwe na wasiwasi na ujiweke mashughuli kwa ajili ya maadui wa Allah swt.

Na mambo mawili yanayoweza kuchukuliwa katika wanaume katika kuhusiana na kuwapatiapo familia zao. Moja ni kutokutimiza wajibu wake kwao, na pili kinachotajwa hapa ni kulimbikiza kupita kiasi kwa mali kwa ajili yao.”

799. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 6, Uk. 47:

“Chukueni hatua za kuwafundisha watoto wenu riwaya na ahadith za Ahlul Bayt a.s. kabla watoto wenu hawajaharibika na hawajachafuliwa akili zao.”

800. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 483:

“Heri ya mtu kwa mtoto wake ni kule kwa mtoto wake kuwa heri kwa wazazi wake.”

801. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Nahjul Balagha, Msemo 399:

“Haki ya mtoto kwa wazazi wake ni kwamba apewe jina1 zuri kabisa, afundishwe adabu njema na afundishwe Qur'an kwa kanuni zake.”

802. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi J. 6, Uk. 47:

“Wafundisheni watoto wenu kuogelea na kulenga shabaha.”

803. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-'Ummal, J. 16, No. 45, 330:

“Watoto wenu wanapokua kufikia umri wa miaka saba, wafundisheni sala, wanapokuwa na umri wa miaka kumi, muwalazimishe kusimamisha sala; na mutenganishe vitanda vyao vya kulalia.”

804. Amesema Al Imam Zaynul 'Abediin a.s. : Man la Yahdharul Faqih, J. 2, Uk. 622:

“Haki ya mtoto wako ni kwamba wewe utambue wazi kuwa yeye amekuja humu duniani kwa kukupitia wewe, kwa hiyo yaliyo sahihi na yaliyo mabaya yanatokana na wewe. Wewe unawajibika kumpa mafunzo na elimu bora, kumwelekeza kwa Allah swt, na kumsaidia katika kumtii Allah swt. Kwa hivyo iwapo utamsaidia utamfanyia hisani mtoto wako, basi utaweza kufikia malengo hayo; na kama wewe utamwia kiovu, basi hayo yatakurejea wewe mwenyewe.”

805. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 104, Uk. 95:

“Muwaheshimu watoto wenu na muwafundishe kuwa wema, mtasamehewa na Allah swt.”

  • 1. Nimekikusanya na kukitarjumu kitabu kiitwacho Majina kwa ajili ya Watoto Waislamu.