read

Harakisheni Kuoa

823. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi J. 5, Uk. 337:

“Kwa hakika bikira ni kama matunda ya mtini; matunda hayo yanapokomaa na kama hayakuchumwa, basi mwanga wa jua una yaharibu na upepo unayatawanya. Hivyo bikira wapo katika hali hiyo hiyo. Na pale wanapo tambua kile anachohisi mwanamke, basi hakuna dawa yao yoyote isipokuwa kuolewa na bwana. Iwapo wao hawataozwa, basi hawataweza kuepukana na uchafuzi, kwa sababu wao ni binaadamu, vile vile. (kwa sababu wao pia wanahisia na matakwa kama binaadamu wengineo).”

824. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Kijana yeyote anayeoa mwanzoni mwa ujana wake, Shaytani wake analia na kujuta kabisa kuwa yeye ameikomboa sehemu mbili ya tatu ya imani yake kutoka kwa Shaytani.”

825. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w, Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 14, Uk. 153:

“Ewe kijana ! Iwapo kuna yeyote miongoni mwenu anayeweza kuoa, basi afanye hivyo, kwa sababu ni vizuri kwa macho yenu (msiwachungulie wanawake wengine) na inahifadhi sehemu zenu za siri (ili muendelee kubakia wacha Allah swt).”

826. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w, Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 14, Uk. 248:

“Allah swt ameharamisha hali ya kutokuoa, na amewaharamishia wanawake kutokujitenga bila kuolewa (hivyo lazima na wanawake pamoja na kuwa wacha Allah swt lazima waolewe).”