read

Khums

1339. Allah swt anavyotuelezea katika Qur'an Tukufu, Surah al-Anfaal, 8, Ayah 41 :

وَاعْلَمُوا أَنَّمَا غَنِمْتُمْ مِنْ شَيْءٍ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَىٰ وَالْمَسَاكِينِ وَابْنِ السَّبِيلِ إِنْ كُنْتُمْ آمَنْتُمْ بِاللَّهِ وَمَا أَنْزَلْنَا عَلَىٰ عَبْدِنَا يَوْمَ الْفُرْقَانِ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ ۗ وَاللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

NA JUENI ya kwamba ngawira mnayoipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Allah swt na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Allah swt na tuliyoteremsha kwa mja wetu(Muhammad) siku ya kipambanuo (katika Vita vya Badr), siku ( Waislamu na Makafiri ) yalipokutana majeshi mawili. Na Allah swt ni Muweza wa kila kitu.

1340. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Man la yahdhurul Faqih, J.2, uk.41

“Kwa kuwa Allah swt ametuharamishia Zaka sisi Ahlul-Bayt a.s.hivyo ametuwekea Khums kwa ajili yetu na hivyo Sadaka pia ni haram kwetu na zawadi imeruhusiwa kwa ajili yetu.”

1341. Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Usuli Kafi, J. 1, Uk.545 :

“Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kununulia chochote kutoka kifungu ambacho Khums haijalipwa na hadi pale wasipoifikisha kwa wanaostahiki kwetu.”

1342. Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Al-Kafi, J.1, Uk. 546 :

“Siku ya Qiyamah wakati ule utakuwa mgumu kabisa pale wanaostahiki Khums watakapotokezea kudai haki zao kutoka wale wasioilipa.”

1343. Miongoni mwa marafiki tajiri mmoja kutokea Uajemi alimwandikia barua Al-Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. na alimwomba Imam a.s. ruhusa ya kuitumia ile mali ambayo khums haijatolewa. Basi Imam a.s. alimwandikia majibu kama ifuatavyo : Imenakiliwa kutoka Al-Wafi, Al-Kafi na Tahdhib

“Bila shaka Allah swt ni Wasi’ na Mkarimu na amechukua dhamana ya kumlipa thawabu na malipo mema yule mtu ambaye atatekeleza hukumu zake na ameweka adhabu kwa yeyote atakayekwenda kinyume ya hayo. Bila shaka mali iliyo halali kwa ajili ya mtu ni ile ambayo Allah swt ameihalalisha na kwa hakika Khums ni dharura yetu na ni hukumu ya Dini yetu na ni njia ya kujipatia kipato kwa jili ya riziki sisi na wenzetu na imewekwa kwa ajili ya kulinda hishima zetu dhidi ya wapinzani wetu. Hivyo kamwe musiache kutoa na kulipa Khums. Na kila inapowezekana kusijikoseshe Du’a zetu na kwa hakika kwa kutoa Khums kunazidisha riziki yenu na kutoharisha na ni hazina kubwa kwa ajili ya Siku ile ambayo kutakuwa na taabu tupu na mateso (Siku ya Qiyamah). Na kwa hakika Mwislamu sahihi ni yule ambaye amemwahidi Allah swt kwa ahadi na ‘ibada, basi atimize kwa ukamilifu. Na iwapo atakubali kwa mdomo tu ilhali moyoni anakataa na kupinga basi atambue kuwa yeye si Mwislamu.

1344. Imeripotiwa kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. katika Al-Kafi J.5, Uk. 144 kuwa :

“Iwapo mimi nitapenda kumpatia kitu rafiki yangu basi mimi nitampa zawadi kwani ninaipenda zaidi kuliko Sadaka.”

1345. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kwa muda wa siku saba hakupata mgeni nyumbani kwake basi alisema huku akilia :

“Nasikitika mno na ninakhofu kuwa isije Allah swt akaniondolea rehema na baraka zake.”

1346. Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu Surah al- Ma’arij,70, Ayah 24 – 25 :

وَالَّذِينَ فِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ مَعْلُومٌ

لِلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ

Na ambao katika mali yao iko haki maalumu.
Na mwenye kuomba na anaye jizuilia kuomba…

1347. Al Imam Musa bin Ja’afer a.s. amepokelewa riwaya kuwa :

“Katika ukoo wa Bani Israil kulikuwa na mtu mwema ambaye alikuwa na mke aliye mwema pia. Siku moja aliota ndoto ambamo aliambiwa kuwa Allah swt amempangia kiasi fulani cha umri wake ambapo nusu ya umri huo utapita katika raha na mustarehe wakati nusu ya umri uliobakia utapita katika shida na dhiki na umasikini.

Hivyo Allah swt amekupa fursa wewe kuchagua iwapo utapenda kupitisha umri wako wa nusu ya awali ya raha na mustarehe na baadaye dhiki na umasikini ? Hivyo chagua mojawapo. Kwa hayo mtu huyo alijibu kuwa : ‘Mimi ninaye mke wangu aliye mwema na hushirikiana naye katika maswala yote, hivyo nitapenda kupewa muda wa kuweza kuongea naye kabla sijatoa uamuzi wa chaguo langu.’

Mke wake alimshauri mumewe kuukubalia umri ule wenye neema uwe ndio wa kuanzia kwani: ‘Inawezekana Allah swt anataka kututeremshia neema na baraka zake hivyo tukaongoka.’

Hivyo usiku uliofuatia, bwana huyo aliulizwa jibu alilolifikia katika uamuzi wake. Naye akajibu : ‘Mimi ninataka kuupitisha nusu ya umri wangu katika neema, raha na mustarehe.’ Kwa hayo akajibiwa kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mujibu wa chaguo lake.

Kuanzia hapo yeye alijaaliwa kila aina ya raha na akawa tajiri mkubwa mwenye mali na milki nyingi.

Katika kutajirika huku, mke wake akamwambia, ‘Ewe Bwanangu! Usiwasahau kuwasaidia na kukidhi haja za majamaa zetu na mafukara na masikini na uwe na uhusiano mwema pamoja nao. Na uwazawadie watu fulani fulani wakiwemo majirani na marafiki, zawadi mbalimbali.’

Mtu huyo alizingatia na kutekeleza ushauri uliokuwa umetolewa na mke wake. Na hivyo alifungua milango ya kugawa mali yake katika masuala hayo hadi ulipofika wakati wa kuisha kwa nusu ya umri wake wa awali.

Kuisha huku kwa nusu ya kwanza ya umri wake, aliota ndoto tena ambamo aliambiwa kuwa : ‘Kwa kutokana na uwema wako wa kuwasaidia wenye shida na dhiki imekuwa kipaumbele kwako, basi Allah swt amekubadilishia sehemu hii ya pili kuwa katika raha na mustarehe kama ilivyo sasa.’”

1348. Wakati wa mavuno kwa kiwango kile ambacho bado Zaka haijapigiwa hisabu, inagawiwa kwa kuchota mkono moja kwa wapita njia kama vile alivyosema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah al –Al-An-‘Aam 6, Ayah 141 :

وَهُوَ الَّذِي أَنْشَأَ جَنَّاتٍ مَعْرُوشَاتٍ وَغَيْرَ مَعْرُوشَاتٍ وَالنَّخْلَ وَالزَّرْعَ مُخْتَلِفًا أُكُلُهُ وَالزَّيْتُونَ وَالرُّمَّانَ مُتَشَابِهًا وَغَيْرَ مُتَشَابِهٍ ۚ كُلُوا مِنْ ثَمَرِهِ إِذَا أَثْمَرَ وَآتُوا حَقَّهُ يَوْمَ حَصَادِهِ ۖ وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisiyo tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana. Kileni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo.

1349. Yaani kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi :

“Katika mlango wa Jannah kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaka na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.’”

1350. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Wafi :

“Wakati Mumin mmoja anapomkopesha Mumin mwenzake deni kwa ajili ya kutaka ridhaa ya Allah swt , basi Allah swt anamhisabia deni hilo katika Sadaka hadi kuja kulipwa kwake.”

1351. Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa akisema kuwa :

“Kwa kupuuzia ‘Ma’un’ (mambo ya nyumbani ) ambayo Allah swt ameahidi katika Qur'an Tukufu adhabu, basi si Zaka inayozungumziwa, bali ni kuwasaidia kwa kuwakopa wale wenye shida na wenye shida wanapokuja kuazima vitu vya nyumbani, basi inabidi kuwa azima vitu vya nyumbani.”

1352. Abu Basir amemwambia Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa

“Majirani zetu wanapokuja kuazima vyombo au vitu vingine vya nyumbani, na tunapo waazima basi huvunja vunja na kuviharibu vitu vyetu na hivyo sisi tunalazimika kuwakatalia kwa misingi hiyo, sasa je kuwakatalia huku ni dhambi ?”

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. alimjibu :
“Iwapo watu hao wanatabia kama hiyo, basi si dhambi kuwanyima.”

1353. Inabidi kuwapa muda au kuwasamehe madeni wale ambao hawana uwezo wa kuyalipa madeni hayo. Na kuhusiana na swala hili Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Iwapo mtu anataka asidhalilishwe Siku ambayo hakuna mwingine wa kuwaokoa isipokuwa Allah swt , basi inambidi awape muda wa kulipa madeni wadaiwa wake au kuwasamehe madeni yao.”

1354. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema :

“Yeyote yule atakayempa muda wa kulipa madeni ambaye hana uwezo wa kulipa ( basi kwa ajili yake ) thawabu zake mbele ya Allah swt ni sawa na thawabu za kutoa Sadaka kila siku kwa kiasi hicho hadi atakapolipwa.”

1355. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. aliambiwa kuwa :

“Abdur Rahmaan bin Sababah anamdai deni marehemu mmoja, nasi twamwambia yeye kuwa amsamehe lakini yeye anakataa kata kata kumsamehe deni lake.”

Kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. akasema :
“Ole wake, je haelewi kuwa iwapo atamsamehe marehemu deni lake basi Allah swt atamlipa Dirham kumi kwa kila Dirham yake moja. Na iwapo hatamsamehe basi atalipwa Dirham moja kwa Dirham yake moja.”

1356. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Al-Kafi, J.2,Uk. 204 :

“Mtu yeyote atakayemsaidia Mumin kwa mavazi wakati wa baridi au joto basi Allah swt atamjaalia mavazi ya Jannah (Peponi au Paradiso ) na atampunguzia shida kali wakati wa kutoa roho yake (wakati anapokufa ) na atampanulia kaburi lake na Siku ya Qiyamah atakapotoka nje ya kaburi lake atakuwa akitoka katika hali ya furaha kwa kuonana na Malaika.”

1357. Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J.2, Uk.205 :

“Iwapo Mwislamu yeyote atamsaidia mtu asiye na mavazi kwa mavazi au aliye na dhiki ya mali, akasaidiwa ( nyumba,mali n.k ) basi Allah swt anamwekea Malaika elfu saba hadi Siku ya Qiyama kwa ajili ya kumwombea maghfirah kwa kila dhambi lake.”

1358. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Wafi, al-Kafi na kunakiliwa pia katika Tahdhiib :

“Baada ya kufariki kwa mtu, huongoka kwa mambo matatu
Sadaka ambayo aliitoa humu duniani na ambayo inaendelea baada yake,

Sunnah ambayo aliitekeleza kwa mfano Adhan ambayo baada ya kifo chake ingali ikiendelea,

Kuacha mtoto mwenye tabia na mienendo mizuri ambaye atakuwa akimwombea dua na usamehevu kwa ajili yake (na akifanya mema kwa niaba ya baba yake, kama inavyoelezwa katika vitabu vingine.