read

Kufanya Kazi na Kukaa Bure.

962. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema At-Tahdhib, J. 6, Uk. 324:

“Ibada imegawanyika katika matawi sabini, na bora ni kule mtu kujitafutia riziki halali.”

963. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam Uk. 197:

“Kamwe, Kamwe hakutapatikana raha na starehe za maisha kwa kubakia bila kazi au kuwa mvivu.”

964. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 175:

“Jiepusheni uvivu na kutokuridhika. Na haya mawili ndio ufunguo wa kila aina ya maovu.”

965. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliambiwa na Sa’ad Ansari kuwa mikono yake imekufa ganzi au imekuwa ngozi ngumu ni kwa sababu ya kufanya kazi kwa kutumia kamba na koleo kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kutumia yeye, mke na watoto wake.

Kwa kusikia hayo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliibusu mikono yake (akionyesha heshima) na akasema, Usd-ul-Ghabah, J. 2, Uk. 269:
“Kwa hakika huu ndio mkono ambao moto wa Jahannam kamwe hautaugusa.”