read

Kunyoyesha Maziwa

806. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 561:

“Naam malipo ya mwanamke wakati wa mimba yake hadi kuzaa mtoto, na wakati pale anapolea mtoto ni sawa na kuwekwa askari katika kituo cha kulinda mipaka ya Waislam dhidi ya hujuma za makafiri, kwa ajli ya Allah swt. Kwa hivyo iwapo atakufa katika kipindi hiki, basi mwanamke huyo atakuwa katika daraja la mashahidi.”

807. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il ush-Shi'ah, J. 21, Uk. 452:

“Hakuna maziwa yenye faida zaidi kwa mtoto isipokuwa maziwa anayonyonya kutoka kwa mama yake.”

808. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 104, Uk. 106:

“Wakati mwanamke anaposhika mimba basi atakuwa ni kama mpiganaji ambaye anafunga saumu wakati wa mchana na anakesha usiku kucha katika ‘ibada, na amejitolea mhanga maisha yake na mali yake katika njia ya Allah swt. Hivyo anapozaa anapata malipo makubwa sana ambayo hakuna mtu anayeelewa isipokuwa Allah swt mwenyewe. Na pale anaponyonyesha mtoto maziwa basi atapata thawabu za kumfanya mtoto mmoja kuwa huru kutoka katika kizazi cha Mtume Ismail a.s. kwa kila mara atakapo nyonyesha.

Na wakati ufikapo kipindi cha kumuachisha mtoto kunyonya, basi malaika aliyekaribu naye humwambia kuanza matendo kwa mara nyingine tena kwani kwa hakika yeye sasa hivi alipo ni katika hali ya kusamehewa kikamilifu (yaani ashike mimba na kuzaa na kunyonyesha tena kwa mara nyingine).”

809. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Mustadrak-ul-Wasa'il, sehemu ya 48:

“Hakuna maziwa yaliyo bora kabisa kwa mtoto isipokuwa maziwa ya mama yake.”