read

Kuomba Tawba ya Allah Swt.

1008. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 22 :

“Mjipake manukato ya Istighfar ili hata tone na mabaki ya madhambi yenu yasiwadhalilishe nyie.”

1009. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimfundisha mtu mmoja kwa kumwomba Allah swt dua kwa kumwambia, Bihar al-Anwaar,J. 94, Uk. 242 :

“Sifa zote ni za Allah swt kwa kila neema; na mimi ninamwomba kila la kheri na kila la wema; na naomba Allah swt aniepushe na kila aina ya shari; na ninamwomba Allah swt msamaha kwa madhambi yote.”

1010. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema kuwa, Khisal-i-Sadduq, Uk. 317:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliulizwa kuwa bora wa waja ni nani, naye alijibu: Wao ni:
1. Wanapofanya mema wanafurahia hayo;

2. wanapofanya mabaya basi wanaomba Tawba na Istighfar ;

3. wanapojaaliwa chochote wanashukuru;

4. wanapokuwa katika hali ngumu, wanaonyesha subira;

5. wao wanapo mghadhabikia mtu, humsamehe.”

1011. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Makarim-ul-Akhlaq, Uk. 313:

“Anapozidisha muumin Mwislam kwa kuomba Istighfar ya Allah swt, basi rikodi ya matendo yake mema yataongezeka na yatakuwa yaking’ara.”