read

Kuwaheshimu Wake Zenu.

864. Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s. amenakili kutoka kwa baba yake hadi kufikia kwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 8,Uk. 310:

“Amelaaniwa mwanamke yule ambaye anamfanya mme wake akasirike, na mwanamke mwenye furaha ni yule ambaye humridhisha bwana wake kwa furaha.”

865. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 7, Uk. 214:

“Yeyote yule aliye na wanawake wawili na kama hawawii kwa haki kwa nafsi na mali yake miongoni mwao, basi siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa amefungwa kwa minyororo na nusu ya mwili wake hautakuwa wima hadi kule atakapo tumbukizwa Jahannam.”

866. Imam Muhammad al-Baqir a.s. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 224:

“Yeyote yule anayeoa mwanamke lazima amheshimu kwa heshima zote, kwa sababu mwanamke kwa mtu yeyote anamaanisha raha na mustarehe, kwa hiyo yeyote anayemwoa mwanamke asimharibu wala kumdhalilisha yeye (Kwa kutojali haki zake zinazostahili).”

869. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 223:
“Kwa hali yoyote ile na katika sura yoyote ile lazima mpatane na wake zenu, na muongee nao vyema kwa kutumia maneno mema mazuri, na hivyo matendo yao yatakuwa mema na watabadilika kuwa wake wema na wazuri kwa ajili yenu.”

867. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s. kwa kumnakili baba a.s. yake ambao wamemnakili Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akisema, Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 228:

“Kiasi chochote cha imani cha mtu kitakachoongezeka basi na kumjali kwa mke wake pia kutaongezeka.”

868. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kuwa, Al Khisal, Uk. 183 na Bihar al-Anwaar, J. 76, Uk. 141:

“Kutokana na vitu vya duniani, mimi huwajali wanawake na manukato zaidi, lakini ibada ni nuru ya macho yangu, (mapenzi na ibada ya Allah swt).”