read

Kuwahurumia Wazazi.

791. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Mustadrak Al-Wasa'il-ush-Shiah, J. 15, Uk. 176:

“Furaha ya Allah swt ipo katika furaha ya wazazi wa mtu (kama ndio hivyo ni kweli, basi adhabu na ghadhabu zake pia zipo katika ghadhabu za wazazi wa mtu).”

792. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 85:

“Bora ya matendo ni:
1. Kusali kwa wakati wake,

2. kuwa mwema na mwenye huruma na mwenye mapenzi kwa wazazi wake, na

3. kuchangia katika vita vitakatifu vya Jihad (dhidi ya Mapagani) katika njia ya Allah swt.”

793. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Safinat-ul-Bihar,J. 2, Uk. 553:

“Iwapo mtu anataka Allah swt ampunguzie makali ya mauti, basi lazima awajali Jama’a na ndugu zake, na awawie wema wazazi wake. Na pale mtu anapofanya hivyo, basi Allah swt atampunguzia makali ya mauti na kamwe hatapata umaskini katika maisha yake.”

794. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Usul-i- Kafi, J. 2, Uk. 349:

“Yeyote yule anayewatazama wazazi wake kwa macho ya ghadhabu, hata kama wao hawakuwa waadilifu kwake, basi Allah swt hatazikubalia ibada za mtu huyo (hadi hapo atakapofanya Tawba).”

795. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 5, Uk. 554:

“Watendee wazazi wako kwa huruma ili na watoto wako waje wakutendee vivyo hivyo; na uwe mcha Allah swt kwa wake wa watu wengine ili wake zako wabakie wacha Allah swt.”

796. Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi J. 2, Uk. 162:

“Safari moja mtu alimwijia Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na kumwuliza namna ya kuwashughulikia wazazi. Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimjibu
1. uwe mwenye huruma kwa mama yako:

2. uwe mwenye huruma kwa mama yako na

3. uwe mwenye huruma kwa mama yako;

4. Uwe mwenye huruma kwa baba yako

5. uwe mwenye huruma kwa baba yako; na

6. uwe mwenye huruma kwa baba yako lakini huruma hiyo uianzie kwa mama yako kabla ya baba yako.”