read

Kuwajali Ndugu na Majama’a.

787. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 89:

“Yeyote yule anayetaka kuongezewa riziki na baraka na siku yake ya mauti icheleweshwa, basi inambidi awajali ndugu na majama’a zake.”

788. Amesema Al Imam 'Ali ar-Ridha a.s., Bihar al-Anwaar, J. 7, Uk. 138:

“Mali haiwezi kulimbikana kupita kiasi isipokuwa kwa njia tano:
1. Ubahili kupita kiasi,

2. matarajio makubwa sana,

3. uroho kupita kiasi,

4. kuvunja uhusiano pamoja na ndugu na majama’a ya mtu mwenyewe, na

5. kuijali na kuipenda dunia hii kuliko Akhera.”

789. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Amesema, Al-Usul-i- Kafi , J. 2, Uk. 150:

“Kuwajali Jama’a na ndugu kunaleta faida tano:
1. Kutakasika na kukubalika kwa matendo ya mtu

2. Kuongezeka katika utajiri na mali

3. Kuondoa balaa na shida mbalimbali

4. Kurahisisha maswala yake katika Akhera

5. Umri kuwa mrefu.”

790. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Khisal Uk. 179:

“Kuna makundi matatu ya watu ambao hawataruhusiwa kuingia Jannah:
1. Wanywaji wa pombe,

2. Wachawi 1, na

3. wale wanaokana Jama’a na ndugu zao.

  • 1. Ninajiandaa kukitarjumu kitabu juu ya maudhui haya.