read

Kuwapa Hima kwa Ajili ya Kuoa.

814. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi J. 5, Uk. 328 :

“Mtu anayeoa hujipatia nusu ya imani yake, na nusu ya imani inayobakia lazima awe na Taqwa.”

815. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema: Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 384:

“Wengi wa watu wa Jahannam watakuwa wale wasioolewa (bila kujali mwanamme au mwanamke).”

816. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., At-Tahdhib,J. 7, Uk. 239:

“Wengi wa wapotofu na walio haribika katika wale walio kufa miongoni mwenu ni wale wasioolewa na wasiooa.”

817. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Man la Yahdharul Faqih, J. 3, Uk. 385:

“Yeyote yule anayetaka awe msafi na aliye takasika wakati atakapo onana na Allah swt, basi aoe na awe na mke.”

818. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. : Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Oeni, ama sivyo mtahesabiwa miongoni mwa Rahbani au ndugu wa mashaytani.”

Ndoa ni Ufunguo wa Rehema za Allah SWT na Bashara Njema.

819. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Milango ya Jannah kwa rehema inafunguliwa katika nyakati nne:
1. Pale inaponyesha mvua,

2. wakati mtoto anapoangalia kwa huruma nyuso za wazazi wake,

3. pale wakati mlango wa Al Ka’aba tukufu unapofunguliwa, na

4. pale ndoa inapofanyika.”

820. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema: Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 222:

“Waunganisheni watoto wenu wavulana kwa wasichana kwa ndoa kwa sababu, humo Allah swt huwajaalia tabia njema, na huwazidishia katika riziki na heshima zao.”

821. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Al-Kafi J. 5, Uk. 328:

“Muolewe na muwaoze mabinti zenu, kwa sababu ni bahati nzuri kwa Mwislamu mwanamme kumtoa au kuwapa mtoto wake aliyekua au dada yake kwa ajili ya ndoa.”

822. Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi J. 5, Uk. 328:

“Hakuna kilicho kipenzi mbele ya Allah swt kuliko ile nyumba ambayo kuna maamrisho ya Islam yanatekelezwa kwa ndoa; na hakuna kitu chochote kinacho mghadhabisha Allah swt kuliko nyumba ile ambamo kunatokea talaka na ufarakano na utengano kati ya bibi na bwana.”