read

Kuwasaidia na Kuingilia kati Katika Ndoa Zilizo Halali

827. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Bihar al-Anwaar, J. 103, Uk. 221:

“Yeyote yule anayefanya jitihada za kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa iliyo halali ili waweze kuoana kwa sheria takatifu za Allah swt, basi Allah swt atamjaalia kwa ndoa hiyo Hur ul-‘Ain mwenye macho meusi katika Jannah, na atamjaalia thawabu za ibada za mwaka mmoja kwa kila hatua atakayochukua au neno atakalolizungumza.”

828. Amesema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., At-Tahdhib, J. 7, Uk. 415 na Al-Kafi J. 5, Uk. 331:

“Ibada bora kabisa ni kule wewe kuingilia kati ya watu wawili kwa ajili kuoana ki halali kwa mujibu wa amri za Allah swt.”

829. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 356:

“Katika siku ya Qiyamah, ambapo hakutakuwa na kivuli chochote isipokuwa kivuli cha rehema za Allah swt, basi kutakuwa na aina tatu ya watu ambao watapewa kivuli hicho cha ‘Arish ya Allah swt:
1. Mtu yule aliye sababisha kusaidia kufunga ndoa ya Mwislamu mwenzake, au

2. yule ambaye amemhudumia, au

3. yule ambaye amemfichia siri zake kwa ajili ya suala lake hilo.”

830. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema, At-Tahdhib, J. 7, Uk. 404:

“Yeyote yule anayewaunganisha wasioolewa katika ndoa basi wao watakuwa miongoni mwa wale watu ambao Allah swt atawatazama kwa rehema Zake siku ya Qiyamah.”

831. Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Bihar al-Anwaar, J. 74, Uk. 356:

“Katika siku ya Qiyamah, kutakuwa na kivuli maalum cha Allah swt ambamo hakutakuwapo na wengine isipokuwa
1. Mitume a.s au vizazi vyao, au

2. Muumin anayemfanya huru mtumwa, au

3. Muumin anayelipa deni la muumin mwingine, au

4. Muumin ambaye anawaunganisha waumini ambao katika ndoa (waumini ambao hawajaoana).”

832. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. Amesema, Wasa'il ush-Shi'ah, J. 20, Uk. 46:

“Yeyote yule anayejaribu kuwaunganisha Waislam wawili katika ndoa kwa mujibu wa sheria za Allah swt, basi Allah swt atampatia Hur ul-‘Ain elfu moja (wahudumu wanaokaa Jannah wakiwa na macho meusi makubwa) katika ndoa na ambapo kila mmoja wao atakuwa katika ngome ya malulu na almas na yakuti.”