read

Maadili ya Islam:

Nafs aina na sifa zake

Masomo ya akhlaq- maadili katika Islam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyewe ambayo Islam inaamini kuwa ni faradhi. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: “Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi kwa hakika ametambua Allah.”

Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amebainisha kuwa: “Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo:

Hapana shaka kuwa mwanadamu hana nafs zaidi ya moja, lakini hii nafsi au inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama ‘nafsi ya kujilaumu’ ‘au nafsi ya kuamrisha’ ‘nafsi inayotosheka’ (kama vile vielezwavyo katika Qu’rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

1484. Nafsi Safi au Thabiti (thabit.)

Katika Qur’an Tukufu, Surah Ash Shua’raa, 26, Ayah 89, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:-

“Isipokuwa mwenye kuja kwa Allah swt na moyo safi”

Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.

Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa: “Moyo ulio msafi- halisi ni ule ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt tu”

Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allah swt tu.

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo twaambiwa:
“Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake.”

Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah swt na wale wapendwao kwa ajili ya Allah swt (Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ahali yake a.s.)

1485. Nafsi Yenye Kutubu (al-Nafs al- Muniib).

Sharti lingine la moyo au Nafsi ni kutubu na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Allah swt, Qur’an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33:

“Anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu), na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt).”

Kuwa na khofu ya Allah swt pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah swt kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah swt imo ndani yake thabiti.

Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Allah swt yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah swt na wala haitorudi kamwe kwa Allah swt.

1486. Nafsi Mwongozi (al- Nafs al- Muhtadi).

Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur’an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11, inatuambia:

“Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah swt. Na anayemuamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu.”

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah swt, yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

1487. Nafsi Iliyo Ridhika (al-Nafs al- Mutmai’na)

Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni kuridhika. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Ar-Raa’d, 13, Ayah 28

“ Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia.”

Na vile vile mwishoni mwa Qur’an Tukufu, Surah al-Fajr, 89, Ayah 28, twaambiwa:

“Ewe nafsi yenye kutua”!
“Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika na umemridhisha.”

Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah swt tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza kumghalibu na kumpotosha yeye.

Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ma - Imamu a.s. waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

1488. Nafsi Ya Tahadhari Ya Uadilifu (al-nafs Al

Muttaqi ):

Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu.
Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 32 :

“Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayezihishimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo.”

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha Taqwa kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allah swt na yale yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, shariah, waumini wake, Makkah, Al-Ka’abah Tukufu n.k. Kwa ufupi chochote kile kinachohusika na Allah swt huwa kina kuwa na umuhimu na ta‘adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya taqwa

1489. Nafsi Nyenyekevu (Al- nafs Al- mukhbit)

Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu na uvumilivu, yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah swt

Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Qur’an Tukufu, Surah al Hajj, 22, Ayah 54:

“Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Allah swt anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia iliyo nyooka.”

Kwa sababu nyoyo hizi hujiinamisha chini mbele ya Allah swt na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allah swt nao kamwe hawavunji maamrisho ya Allah swt na wala hawazisaliti au kuzipinga.

1490. Nafsi Halisi (AL-nafs AL-zakiyyah):

Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au iliyo mtakatifu. Katika Qur’an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 9-10, Allah swt anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akiisemea nafsi, anatuambia:

“Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)”

Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwa kuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele.

1491. Nafsi ya Kukaripia - Laumu (al-nafs al- lawwama).

Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa.
Qur’an Tukufu, Surah Al Qiyamah, 75, Ayah 1-2, inatuelezea:

“Naapa kwa siku ya Qiyamah. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)”.

Ni dhahiri kuwa iwapo Allah swt akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.

1492. Nafsi iliyofunguliwa heri (Al-nafs Al-mulham):

Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Allah swt. Twaambiwa katika Qur’an Tukufu, Surah Ash-Shams, 91, Ayah 8

“ Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake”

Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- Nafsi halisi si ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah swt yatafikia kikomo chake.

Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.

1493. Nafsi Yenye Madhambi (Alo-nafs Al-aathima):

Iwapo nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi.
Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 283 inazungumzia kulipa kwa amana:

“Na mkiwa safarini na hamkupata mwandishi, yatosha kukabidhiwa rahani. Na mmoja wenu akimwekea amana mwenziwe basi aliye aminiwa airudishe amana ya mwenzake, na amche Allah swt, Mola wake Mlezi. Wala msifiche ushahidi. Na atakaye ficha basi hakika moyo wake ni wenye kutenda dhambi. Na Allah swt ni Mjuzi wa mnayo yatenda.”

Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.

1494. Nafsi iliyo sinzia (Al-nafsal-ghafil)

Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah swt. Anaelezea Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Kahf, 18, Ayah 28:

“Na isubirishe nafsi yako pamoja na wanao muomba Mola wao Mlezi asubuhi na jioni, hali ya kuwa wanataka radhi yake. Wala macho yako yasiwaruke kwa kutaka pambo la maisha ya dunia. Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata matamanio yao yakawa yamepita mpaka”

1495. Nafsi Zilizotiwa Muhuri (Al-nafs Al- matbu’)

Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho, Amesema Allah swt katika Quran: :
“Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao kwa sababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu.”

Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allah swt hadi kudharau na kutokubali ujumbe Wake na maamrisho ya Allah swt ambayo amemwekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo nafsi yake inaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athari yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimia kwa nafsi na kushindwa kwake.

1496. Nafsi Iliyo Pofuka ( Al-nafs Al- amya):

Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka.
Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 46:
“Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikia? Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka.”

Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah swt na hazimwoni Allah swt. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah swt na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.

1497. Nafsi Yenye Maradhi (Al-nafs Al-maridha):

Qur’an Tukufu, Surah Al Baqara, 2, Ayah 10:

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah swt amewazidishia maradhi. basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uongo.”

Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa (na Allah swt) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na Aakhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno. Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa anavutiwa navyo kama kwamba ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi iliyokwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia.

Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Allah swt katika sala na kutii Sharia Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa hiyo nafsi wake imeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kusita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur’an Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga wa moyo, wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., ili waweze kuitibu nafsi ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.

1498. Nafsi Inayokwenda Upande (al-nafs al-za’igha):

Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu.

Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakumbwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Allah swt. i.e njia iliyonyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu

Katika Qur’an Tukufu, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu, Surah Al I’mran, 3, Ayah 7:

“Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi. Na wale wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. lakini hawakumbuki hayo isipokuwa wenye akili.”

Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih) wa aya za Qur’an Tukufu ili kuitumia Qur’an Tukufu kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.

1499. Nafsi ya Moyo Mgumu (al-nafs al-qasiya)

Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili. Katika Qur’an Tukufu, Surah Al Maida, 5, Ayah 13

“Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao tuliwalaani, na tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyo kumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipo kuwa wachache miongoni mwao. Basi wasamehe na waache. Hakika Allah swt huwapenda wafanyao wema.”

Allah swt anatuambia katika Qur’an Tukufu Surah Al H’adiid, 57, Ayah 16:

“Je! Wakati haujafika bado kwa walio amini zikanyenyekea nyoyo zao kwa kumkumbuka Allah swt na haki iliyo teremka? Wala wasiwe kama walio pewa Kitabu kabla yao, muda wao ukawa mrefu, Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu na wengine wao wakawa wapotovu.”

Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!

1500. Nafsi Wasiwasi (al-nafs al-murtaba):

Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu ipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya Dini ya Islam kama vile kushuku kuwapo kwa Allah swt, Aakhera, Utume wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na vile vile Uimamu (wa ma-Imamu a.s.), na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi.

Katika Qur’an Tukufu, Surah Tawba, 9, Ayah 45:

“ Wasio muamini Allah swt na Siku ya Mwisho na nyoyo zao zina shaka, hao tu ndio wanao kutaka ruhusa. Basi hao wanataradadi katika shaka zao.”

Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza katika Ayah za Qur'an Tukufu na Ahadith Tufuku za Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na Ma-Imamu a.s. na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).

1501. Nafsi Iliyopata Kutu (al-nafs-al-ra’ina):

Kutu ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha nafsi ambavyo ni sehemu umuhimu kwa ajili ya Allah swt utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza kurudishwa iwapo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Allah swt.

Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Allah swt kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Allah swt, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia kutokana kwa Allah swt, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa maana yake. Qur’an Tukufu, Surah Al Mut’affifiin, 83, Ayah 14, ikiwa inatukumbusha kuwa:

“Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma.”

Katika aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba (Kipo kitabu nilichokitarjumu katika lugha ya kiswahili kinachozungumzia swala hili kwa marefu na mapana ) mara moja kwa ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadith Tukufu kuwa:
“Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Qiyama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka ‘naomba msamaha wa Allah swt’ chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa hivyo inambidi kila Mwislam miongoni wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Allah swt azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

1502. Nafsi Amuru (al-nafs al- ‘ammara):

Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matendo ya madhambi bila kiasi. Katika Qur’an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53 , kuhusu kisa cha Mtume Yussuf a.s., inazungumziwa Nafsi :

“Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.”

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Mtume Yussuf a.s.. Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Mtume Yussuf a.s. alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile dhidi ya Mtume Yussuf a.s.. Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Mtume Yussuf a.s. au ni wote vyovyote vile, Qur’an Tukufu, Surah Yusuf, 12, Ayah 53, inatuambia kuwa:

“Nami sijitoi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu isipokuwa ile ambayo Mola wangu Mlezi aliyo irehemu. Hakika Mola wangu Mlezi ni Msamehevu na Mwenye kurehemu.”

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na ma’asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, ilimradi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na maana yake; na ile nafsi iliyo ilimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.