read

Majivuno na Kiburi.

949. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Tasnif-i-Ghurar-ul-Hikam,Uk. 443:

“Msiwe wakaidi (na msing’ang’anie kufuata vile mfikiriavyo nyie wenyewe), kwa sababu watu kama hawa hukumbana na maangamizo.”

950. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Tasnif-i-Ghurar-ul-Hikam,Uk. 308 na Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 91:

“Yeyote yule ajionaye kuwa yeye ndiye mkubwa kabisa (hana mfano mwingine) basi si kitu chochote kile mbele ya Allah swt.”

951. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Bihar al-Anwaar, J. 72, Uk. 39:

“Mambo mawili yanasababisha watu kuangamia (na kutumbukizwa katika Jahannam):
Kuogopa umaskini, na

Kutaka ukubwa kwa kupitia majivuno.”

952. Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Ghurar-ul-Hikam, Uk. 298:

“Mjiepushe na kujifakharisha wenyewe, kwa kutegemea yale muyaonayo mazuri ndani mwenu na kwa kupenda kuzidishiwa sifa kwa sababu hayo ndiyo majukumu makubwa yakutegemewa na Shaytani.”

953. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Kafi, J. 2, Uk. 310:

“Yeyote yule aliye na kiburi hata kidogo moyoni mwake basi hataruhusiwa kuingia Jannah.”